AKWELINA - 2 Simulizi : Akwelina Sehemu Ya Pili (2) Sauti ya Monna ilimstua Kakinga pamoja na Dereva wakaanza kumtafuta Monna huku na huko Dereva akawasha tochi lake wakati anamoreka tochi lilimdondoka yule dereva alipoinama ili achukue tochi alihisi kuna kitu kitu upande wake wa kushoto yule dereva alisogea taratibu akiwa makini sana akaona pango dogo akamoreka ndani ya lile pango akamuona msichana mmoja akiwa ameshikwa na wanaume zaidi wanne yule dereva alimuita Kakinga, kakinga alipofika alimuona mke wake ameshikwa na wanaume wengi. Kakinga alishikwa na hasira akaingia ndani ya pango hilo akawapiga sana wale wahuni kwa hasira alizokuwa nazo kakinga alifunja mikono ya vijana hao na kuhitaji kuwauwa kabisa , yule Dereva akamziwia Kakinga Vijana hao wakakimbia . Kakinga akamtoa mke wake ndani ya pango , Monna hakuamini kama amepata msaada monna alimkumbatia mume wake yule dereva akawapatia msaada hadi nyumbani kwake, yule Dereva alikuwa amepanga chunga kimoja na sebure, kwakua yalikuwa ni majira ya usiku Kakinga na Monna walilala sebuleni. Asubuhi palipokucha yule Dereva aliamka mapema sana akawapa pesa ya chakula akaondoka kwenda katika shughuli zake, Monna alimshukuru mungu kwa kumpata kijana mwenye roho nzuri . Baada ya wiki mbili kakinga aliiamka asubuhi sana akaingia mtaani kutafuta kazi siku hiyo kakinga alizunguka mji mzima lakini hakupata kazi, Kakinga hakukata tamaa aliendelea kupambana kutafuta kazi mungu akamjalia kakinga akapata kazi ya kubeba mizigo stenti ya magari , kakinga alifanya kazi bila kuchoka kuanzia asubuhi hadi majira ya saa mbili usiku akapata shilingi 10000 Kakinga akarudi nyumbani akiwa hoi Mwili wote unamuuma kama donda . Wakati huo njaa ilikuwa inamuuma kwa sababu alikuwa hajala toka asubuhi Kakinga alitamani anunue chakula ale lakini alishindwa kwa sababu alitambua Monna atakuwa hajala kama yeye, Kakinga alitumia zile fedha akanunua vyakula vya kutosha akiwa njiani anarudi nyumbani alimuona mtoto mdogo anataka kuingia kwenye moto Kakinga akashangaa sana akatazama eneo lote akaona kimya ikabidi Kakinga akimbie haraka akamchukua yule mtoto kabla hajaufikia Moto , Kakinga akiwa amembeba mtoto alisikia mtu mmoja ikisema : "" Jamani yule Mwizi wa mtoto huyu hapa njooni njooni .. Watu wa mtaa ule walitoka nje na silaha mbalimbali wakamva............. Watu wa mtaa ule walitoka nje na silaha mbalimbali wakamvamia kakinga wakamshambulia kakinga , kakinga alijaribu kuwaelezea ukweli kuhusu mtoto lakini wananchi hawakumuelewa kabisa, waliendelea kumpiga kwa bahati nzuri askari wa lindo la usiku walitokea eneo lile wakamchukua kakinga wakaenda nae kutuo cha police walipofika kituoni askari hawakutaka kumsikiliza kakinga wakamueka mahabusu. Siku hiyo monna alikuwa anawasiwasi mkubwa sana, muda ulizidi kwenda monna alitoka nje na mtoto akamtazama sana mtoto akasema kwa sauti ya chini sana :- “”* Akwelina mtoto wangu najua unahisi njaa unahitaji kula masikini tangu asubuhi hadi muda huu hujala kitu chochote nitafanyaje mimi ndani hakuna kitu, pesa hakuna baba yako tangu aondoke hajarudi hadi muda sasa sijui kapatwa na tatizo gani daaah matiti ninayo lakini hayana maziwa ndani yake hayatoi kitu vumilia mtoto wangu *”””” Monna alipomaliza kuzungumza aliimba wimbo mzuri akiwa anambembeleza akwelina taratibu taratibu akwelina alilala, Monna akaingia ndani akamlaza mtoto alafu akatoka nje akakaa karibu na mlango monna alizungumza mouoni :- “”** Upo wapi mume wangu , umepatwa na nini mbona wanifanya nikose amani rudi mume wangu *””” Muda ulizidi kwenda hadi saa saba usiku monna alikuwa bado yupo nje anamsubiri mume wake, Yule dereva alikuja amelewa sana akamkuta monna yupo nje akasema :- DEREVA ??Wewe mwanamke unawanga nini mbona upo nje hadi muda huu unafanya nini anhaaaa kumbe wewe ndio unakujaga usiku chumbani kwangu unanichapa bakora weeee nikiamka asubuhi nakuwa nimechoka sanaaa sasa nasema ondokeni wewe na mume wako siwezi kuwalea watu wazima kama ninyi nasema ondokeni pumbafu “” MONNA ?? Shemeji mimi nitaenda wapi usiku huu jamani mume wangu hajarudi pia ninamtoto mdogo jamani najua umelewa nenda kalale shemeji tutazungumza kesho . DEREVA ?? Mimi nimelewa ? Haaaah !! Mimi sijawahi kulewa toka nizaliwe nasema toka hunijui eeh subiri sasa nimewachoka nawalisha kila siku kama watoto ondokeni . Yule dereva aliingia ndani akatoa nguo za monna akawa anazitupa nje monna alimuomba sana lakini yule dereva hakusikia kilio cha Monna, monna aliingia ndani akachukua mizigo yake akambeba akwelina mgongoni akatoka nje akaenda hadi stenti ya magari iliyokuwa karibu na nyumba waliyokuwa wanaishi, Monna alifika stenti akamtoa akwelina mgongoni akakaa kwenye kiti. Kakinga alikuwa na mawazo sana mahabusu , kakinga akiwa na mawazo alisema :- “” Eee mungu kwanini kila siku napata matatizo mimi tu au kuna binadamu mwingine anapata matatizo kama mimi , hivi nimekosa nini mimi? Wema wangu wa kumsadia yule mtoto leo hii napata shida kiasi hiki nyumba yangu imechomwa kisa mtoto , nimenusurika kufa kisa mtoto leo nimekuja kuja humu mahabusu kwa ajili yake kwa sababu moyoni niliweka nia natafuta kazi ili nimnunulie maziwa au huyu mtoto sio binadamu ni jini, shetani au ni pepo, Nimechoka sasa nikifanikiwa kurudi nyumbani nitamchukua mtoto nitaenda kumtupa bila kujali kama mke wangu atapenda au hatopenda. Hayo ni maneno aliyokuwa anazungumza kakinga baada ya kuona matatizo yanamuandana kila siku. Kakinga alikesha usiku kucha bila kulala yalipofika majira ya asubuhi wale askari waligundua kakinga hana makosa wakamtoa mahabusu kakinga alitoka mahabusu akiwa na hasira sana, kakinga alipofika nyumbani hakumkuta monna akawauliza majirani wakamwambia yote yaliyotokea Jana , kakinga alipata maumivu makali sana , wakati kakinga amesimama anahasira zilizopitiliza alisikia sauti ya monna ikimwita, kakinga alipogeuka alimuona mke wake akamfuata akamchukua akwelina akaondoka nae akiwa anakimbia , kitendo kile kilimshangaza sana monna , Kakinga alimbia hadi sokoni akasimama akapiga magoti akamtazama sana akwelina akasema :- “”” Utanisamehe sana kwa unyama huu lakini nitafanyaje unanitesa sana akwelina nakuacha hapa atapita mtu mwema mwingine atakuchukua kwaheri sana akwelina nakupenda. Kakinga alizungumza maneno hayo machozi yakimtoka , kakinga akamuweka chini akwelina akahitaji kuondoka kakinga alishangaa kuona akwelina amemshika kidole chake kwa nguvu kakinga aka…….. Kakinga akatoa mkono wa akwelina katika kidole chake akasimama akaondoka akwelina alianza kulia, kilio cha akwelina kilitesa nafsi ya kakinga, Kakinga alitamani kurudi lakini akajitahidi akaondoka, Akwelina aliendelea kulia masikini Kakinga hakujali aliendelea kuondoka kurudi kwa Monna, Kakinga alikutana na monna njiani, monna alimuona Kakinga hana mtoto monna alichanganyikiwa sana alimuuliza Kakinga :- MONNA ?? Mume wangu akwelina yupo wapi ? KAKINGA ?? aaaah achana na habari hizo nimempeleka kwa wengine watusaidie kumlea kama wema tumeufanya sana yule mtoto katuletea matatizo ya ajabu sana Wewe angalia tulipotoka na hapa tulipo yote ni mikosi kwahiyo ndio hivyo nimewapelekea wengine. MONNA ?? Unasemaje wewe sikuelewi mume wangu namtaka akwelina wangu sikuelewi Mimi siwezi kuishi bila yeye tafadhali nenda kaniletee akwelina wangu . KAKINGA ?? Nakwambia hivi sahau kuhusu akwelina turudi nyumbani . MONNA ?? Nyumbani wapi mume wangu rafiki yako ametufukuza amesema ametuchoka siwezi kukuelewa bila kumuona akwelina niambie yupo wapi nimfuate Mimi jamani . Monna alilia sana katika mikono ya mume. Kakinga aliishiwa nguvu baada ya kuambiwa rafiki yake aliyemsaidia amewafukuza katika nyumba yake kakinga alikaa chini akashika kichwa, monna alipomuona mume wake amechanganyikiwa ghafla monna alijaribu kumfariji japo walikuwa na ugomvi kuhusu mtoto , Monna alikuwa hapendi kumuona mume wake akose furaha hata siku moja mbele yake, Kakinga alisema kwa uchungu :- KAKINGA ?? Umeona mke wangu sijui sisi tumemkosea nini mungu kila siku matatizo yapo kwetu tu daah na kwa hali hii tutaenda wapi ? Na akwelina tungemleaje kwa hali kama hii mke wangu ? Ni bora nimewapelekea wenye uwezo wamlee mke wangu ama kweli jasho lako ndio lako lakini jasho la mwingine mke wangu ni sumu liokope kabisa . MONNA ?? Usijali mume wangu maisha ni kokote nipo tayari kulala nje ndani ya jiji hili kwa ajili yako nakupenda mume wangu sihitaji kingine katika maisha haya zaidi ya furaha yako. Monna alimshika mkono mume wake wakasimama wakaondoka, Monna na mume wake walipita katika migahawa wakiomba kazi kwa bahati nzuri monna alipata kazi ya kuosha vyombo, Monna alipopata kazi alifurahi sana Kakinga akamwambia monna :- “””””* Mke wangu kwakua Wewe umepata kazi endelea kufanya kazi Mimi naenda kutafuta kazi kwenye viwanda nitarudi jioni kama nikipata kazi na ukimaliza kazi nikukute stenti pale usitoke hadi nifike hapo pia usisahau kule chakula tangu jana hujala kitu mke wangu sawa *””” Kakinga aliondoka akaenda kutafuta kazi. Muda ulizidi kwenda akwelina alizidi kulia katika eneo lile aliloachwa na Kakinga watu walimvuka na kumruka bila kumsaidia wala kumuokota, jua lilizidi kuwa kali likamchoma akwelina, akwelina alilia zaidi lakini hakupata msaada wowote. Baada ya muda mfupi kiongozi wa wanajeshi anayemtafuta sana mtoto akwelina alikuja na wanajeshi wake katika ofisi moja iliyokuwepo eneo hilo , Akwelina baada ya kulia sana akajitokeza msalia mwema mmoja bibi kizee akamuokota akwelina , yule bibi aliuliza kila mtu aliyekutana naye njiani lakini kila aliyemuuliza alimjibu hamtambui mtoto yule. Bibi kizee alitembea sana bila mafanikio kwa bahati nzuri akamuona yule kiongozi amevaa nguo za kijeshi bibi alifurahi sana akasema :- “”””* Ahsante mungu kwa maana hii ni kesi kubwa ngoja nimpelekee yule askari wa kijeshi ili mtoto awe kwenye mikono salama *”””” Bibi alimfuata yule kiongozi alipomkaribia bibi alim…. Bibi alimfuata yule kiongozi alipomkaribia bibi alimpatia mtoto yule kiongozi yule kiongozi alishangaa sana baada ya kumuona bibi kizee anamletea mtoto kiongozi alimuuliza bibi :- KIONGOZI ?? Samahani bibi kwanini umenipatia huyu mtoto wewe wanitambua Mimi ? BIBI ?? Hapana Mjukuu wangu sikufahamu na hata huyu mtoto simtambui pia, Mimi nimemuokota huyu mtoto na nimejaribu kuwauliza watu wengi katika eneo hili, wote wananijibu hawamtambui ndio nilipokuona wewe umevaa nguo za jeshi la nchi nimekuletea nahisi atakuwa Sehemu salama akiwa kwako Mjukuu wangu dunia imeisha KIONGOZI ?? Sawa upo sahihi bibi lakini sheria ni ngumu sana nakushauri nenda kituo chochote cha police kilichopo karibu yako ukawakabidhi wao hiyo ndio njia salama bibi . Wakati kiongozi anaendelea kuzungumza na bibi alikuja mwanajeshi mmoja akasema :- “”* Mkuu tumepata taarifa kuhusu yule mtoto kuna sehemu yupo *””” Kiongozi hakutaka kuzungumza na bibi tena akaondoka haraka haraka kuelekea sehemu hiyo, bibi alianza kujilaum kwa kitendo alichofanya cha kumuokota akwelina. Yule kiongozi na kundi lake walifika katika eneo lililosemekana akwelina alikuwepo hapo wale wanajeshi waliwauliza watu wa eneo lile “** Kuna bibi mmoja ndio alikuwa na huyo mtoto mnamzungumzia nilimuona huyo mtoto hapa toka majira ya asubuhi *””””” Ilikuwa ni sauti ya muuza matunda maarufu wa eneo hilo akiwapatia Maelezo wale wanajeshi kuhusu mtoto, Kiongozi alimuuliza yule muuza matunda kuhusu huyo bibi , muuza matunda alimueleza kiongozi yule bibi alivyokuwa , kiongozi akamkumba huyo bibi ndio yule aliyemletea mtoto , kiongozi akaingia kwenye gari akarudi maeneo yale aliyemuona bibi huyo. Bibi alizidi kutembea huku na huko akiwa na mtoto mkononi ndani ya mji huo baada ya kutembea sana bibi alikutana na Kakinga akamwambia :- “””* Kijana wangu nisaidie kumshika huyu Mjukuu wangu nataka nifunge nguo vizuri nimechoka sana *””” Kakinga alitua mfuko wa Cement chini akamshika mtoto, bibi akaondoka zake , Kakinga akiwa amemshika mtoto alimuona bibi anaondoka kakinga akamfuata yule bibi akamziwia :- KAKINGA ?? Bibi unakwenda wapi unaniachia Mjukuu wako ? BIBI ?? Wala sio Mjukuu wangu huyo nimemuokota tu na nimetembea nae sana lakini sijamuona mwenye mtoto huyo na unavyoniona umri wangu huu huyo mtoto nitampeleka wapi lakini wewe bado Kijana unaweza kufanya kitu ili umsaidie mtoto huyo . Bibi aliondoka kakinga alizidi kumsumbua bibi ili amchukue mtoto , bibi hakujali hilo akazidi kuondoka kakinga alikuwa bado hajamtazama vizuri mtoto yule kakinga akasema :- “””” Jamani sasa hili ni balaa akwelina nilimuacha kule ili wasalia Wema wanjsaidie kumlea yaani leo leo hii tena nimeletewa mtoto mwingine hivi hii ni mikosi gani jamani mungu nimekukosea nini Mimi daaaah sijui nijiue aaaaah ?? Kakinga alilalamika sana akamtazama vizuri mtoto aliyepewa Kakinga alistuka sana kumuona mtoto yule ni akwelina aliyemtupa mbali, Kakinga alishindwa kuamini macho yake , Kipindi kakinga akiwa bado yupo katika mshangao mkali alisikia magari yamesimama mbele yake, alipotazama alimuona yule bibi aliyempatia akwelina akiwa na kiongozi wa wanajeshi, Kiongozi wa wanajeshi alisema :- “”** Kijana ulidhani unaweza kunikwepa kamwe hautaweza katika maisha yako na vita hii umeyoinunua itakuponza naomba kwa wema tu niapatie huyo mtoto kabla sijakupiga risasi na huwezi kunikimbia leo *””” Yule kiongozi akachomoa bastola yake akaweka risasi akamwambia kakinga amlete mtoto, Kakinga alimsogelea yule kiongozi aliyekuwa ndani ya gari kakinga alikuwa makini sana kipindi anamsogelea yule kiongozi kakinga alipofika karibu ya gari aliona njia upande wa kushoto kakinga alitimua mbio akiwa na akwelina mikononi mwake, Yule kiongozi akampiga kakinga risasi ya mgongo , kakinga akadondoka chini kakinga alijitahidi akasimama tena japo alikuwa na maumivu makali sana akaendelea kukimbia kakinga alijikongoja hadi kwa mke wake monna , Monna alikuwa anaendelea na kazi katika mgahawa ule alimuona mume wake kakinga anakuja akiwa anachechemea damu nyingi zinamtoka monna alimkimbilia mume wake Kakinga akamuona akwelina , Kakinga alimpatia monna mtoto akasema :- “””* Kimbia na akwelina mke wangu watu wabaya wanakuja kumchukua usipate tabu kuhusu Mimi okoa maisha ya akwelina kwanza haraka ondoka mke wangu *””””” Monna hakukubali kumuacha mume wake akajaribu kumnyanyua ili waondoke pamoja baada ya hatua chache monna na Kakinga walizungukwa na wanajeshi , Yule kiongozi alishuka kwenye gari akachomoa kisu akamfuata kakinga akamch……… Yule kiongozi alishuka kwenye gari akachomoa kisu akamfuata kakinga akamchoma kisu cha tumbo, Monna alitetemeka sana baada ya kumuona mume wake kakinga amechomwa kisu na yule kiongozi. Yule kiongozi alimvuta kakinga akamsogelea katika sikio akamwambia :- KIONGOZI ?? Nilikwambia kijana huwezi kunikimbia ulijifanya wewe mjanja sana sasa mwisho wako ndio huu kufa mjinga wewe . Kakinga akiwa amechomwa kisu tumboni aliona bastola katika mkanda wa yule kiongozi kakinga akachomoa ile bastola akamteka yule kiongozi wa wanajeshi, Wanajeshi walipoona kiongozi wao ametekwa waliweka silaha zao chini wakapiga magoti, kakinga japo alikuwa na maumivu makali sana alimshikilia vizuri yule kiongozi akaondoka nae, Kakinga akiwa na mke wake monna pamoja na yule kiongozi wa wanajeshi walizidi kuondoka walipofika mbali kakinga alimwambia yule kiongozi alale chini , yule kiongozi alilala chini kakinga akaweka ile bastola chini taratibu , Monna akamshika vizuri mume wake wakaondoka. Baada ya masaa matatu kupita wale wanajeshi walifuata njia ile aliyopita Kakinga wakamkuta kiongozi wao bado amelala chini wakamwita, kiongozi wao akasimama wanarudi kwenye magari yao wakapanda wakaondoka. Kakinga na monna walienda mbali sana wakatokezea ufukweni mwa bahari , kakinga alishindwa kuendelea na safari kutokana na kutokwa na damu nyingi sana, kakinga alindoka chini akapoteza fahamu, Monna alilia sana baada ya kumuona mume wake amepoteza fahamu , Monna alimshusha akwelina akamuweka chini akaondoka kwenda kutafuta msaada, Monna alizunguka sehemu kubwa lakini hakupata msaada monna hakukata tamaa aliendelea kutafuta msaada kwa bahati nzuri akakutana na babu mmoja aliyekuwa anaishi hapo ufukweni mwa bahari monna alimuomba msaada yule babu , Yule babu alikubali kumsaidia monna akachukua baadhi ya dawa kutokana na Maelezo ya monna akaondoka nae walipofika yule babu alikuwa mtaalamu alimtoa risasi kakinga akamchoma kile kisu alafu akamshona sehemu zote alizopata majeraha baada ya tiba yule babu pamoja na monna walimnyanyua kakinga wakaondoka kuelekea katika nyumba ya huyo babu, kipindi wanaondoka babu alisema :- BABU ?? Mbona mtoto umemuacha ? hujui sehemu hii sio nzuri kuna baridi Kali . MONNA ?? Tuondoke tu babu huyo mtoto sio wangu nilimuokota tu na huyo mtoto katuletea matatizo makubwa sana Mimi na mume wangu huyu bila wewe mume wangu angepoteza maisha kwa sababu ya huyu mtoto nimegundua kile alichonieleza mume wangu ni sahihi. Monna akaenda bila kujali kile babu alichomwambia kuhusu mtoto ( akwelina ) Nyumba ya babu haikuwa mbali na bahari, walipofika walimlaza kakinga nje ili apate hewa safi. Kakinga alilala nje hapo hadi majira ya usiku akarudisha fahamu , Monna alifurahi sana kumuona mume wake alirudisha fahamu monna alimkumbatia mume wake kwa furaha, babu akatoka nje kakinga akamsalimia babu alafu akamuuliza monna :- KAKINGA ?? Mke wangu tupo wapi hapa na huyu babu ni nani ? MONNA ?? Huyu babu ndiye aliyesaidia maisha yako na hapa ni nyumbani kwake mume wangu . KAKINGA ?? Ahsante sana babu kwa msaada wako mungu atakulipa kwa Wema uliyonifanyia alafu Akwelina yupo wapi au amelala ? MONNA ?? Aaaaah sahau kuhusu akwelina nilishindwa kukusikia mwanzo leo hii kidogo nikupoteze mume wangu kwa ajili ya mtoto yule nimemtupa mbali sana huko . KAKINGA ?? Weeee Unasemaje siwezi kukuelewa nasema hivi ili tuelewane nenda sehemu uliyomtupa akwelina uniletee hapa sasa hivi. Kakinga na monna waligombana kwa muda mrefu mwisho monna akakubali akamfuata akwelina akamkuta amefunikwa na uchafu wa bahari nguo alizokuwa amevaa akwelina zote zilikuwa zimerowa na maji, Monna japo alikuwa ameanza kumchukia akwelina lakini alimuonea huruma sana kwa sababu akwelina alikuwa anatetemeka sana, Monna alimtoa akwelina zile nguo mbichi akamfunika kanga aliyokuwa nayo. Monna akarudi nyumbani akiwa na akwelina , Alipofika nyumbani kakinga alifurahi sana kakinga akambusu akwelina kwa furaha. Baada ya wiki moja kupita majira ya usiku kakinga alimwita mke wake akamwambia :- “”* Mke wangu hebu niletee vile vitu tulivyomkuta navyo akwelina *””” Monna alimletea Kakinga vitu alivyohitaji alafu akaenda jikoni kupika , Kakinga aliona kitabu kidogo akakiweka pembeni , akaona mfuko mweusi umefungwa vizuri Kakinga alihitaji kuufungua ule mfuko lakini akasita akauweka pembeni mwisho akaona bahasha juu ya bahasha ile kulikuwa na michirizi ya damu, kakinga akaifungua ile bahasha akaona picha nyingi zipo ndani ya ile bahasha kakinga alipoziangalia zile picha aliona sura mbalimbali ikiwepo na sura ya yule kiongozi, Kakinga alizidi kuzitazama zile picha, picha ya mwisho kakinga alimuona Madam ( mama yake mdomo monna ) kakinga alistuka sana akajiuliza Kwanini zile picha awekewe akwelina , Kakinga alishindwa kuelewa kabisa akazirudisha zile picha ndani ya bahasha akashika uke mfuko mdogo mweusi akaufungua ndani ya mfuko aliona vitu kama mawe mdogo madogo yanang’aa sana Kakinga alipotazama vizuri akagundua yale sio mawe ya kawaida ni ….. Kakinga alipotazama vizuri akagundua yale sio mawe ya kawaida ni mawe yenye madini ndani yake , kakinga alizidi kuyashangaa yale mawe yale mawe yalikuwa mengi sana kakinga aliyageuza geuza akagundua mawe yale yalikuwa ni almasi Kakinga japo aligundua kuwa zile ni almasi lakini hakuwa na uhakika wa kutosha kakinga alichukua jiwe moja akamfuata yule babu , Babu alikuwa kandokando ya bahari anavua samaki babu alikuwa anapenda kufanya hivyo kila siku majira ya usiku Kakinga alipofika kwa babu alikaa karibu yake kakinga akamuuliza babu :- KAKINGA ?? Hivi babu kwanini unaishi huku ufukweni peke yako wewe hauna familia ? BABU ?? ???? Unanifanya nifurahi sana kijana wangu , Unazungumzia familia Mimi nilikuwa na familia yangu na nilikuwa na pesa za kutosha nakumbuka mwaka 1943 Nilipokuwa kijana mwenye umri kama wako Maisha yangu yalikuwa magumu sana kwa sababu nilikuwa sina baba wala mama Mimi nimelelewa katika vituo vya watoto yatima tu, Nilipokuwa kijana ninayejitambua niliwafuata wale walezi wa kituo cha watoto yatima nikawauliza historia ya maisha yangu daaah walinijibu kwamba hawajui Mimi nilitoka wapi kwa sababu walinikuta nje ya kituo chao nikiwa mtoto mdogo sana. Ukweli sikuridhika na majibu ya wale walezi wetu ikanibidi nimfuate mkuu wa kituo kile nilipofika kwa mkuu wa kituo alinikaribisha vizuri nikamuomba historia ya maisha yangu nilipewa majibu yale yale kama niliyopewa mwanzo lakini akaenda chumba cha kuhifadhi kumbukumbu za watoto wote wanaoishi pale akarudi na mfuko akanipatia akaniambia waliniokota na mfuko ule labda nikague naweza kugundua kitu niliuchukua ule mfuko nikarudi chumbani kwangu, Nilipoufungua ule mfuko nilikuta kuna picha mbili ya mwanamke na mwanaume nyuma ya zile picha zilikuwa zimeandikwa MAMA na BABA , Kwa haraka haraka niligundua wale watakuwa ni wazazi wangu nilitokwa na machozi mengi sana kwa kuwaona wazazi wangu kwa kupitia picha , niliendelea kukagua vitu ndani ya mfuko ule nikaona mfuko mweusi umefungwa vizuri nilipoufungua ule mfuko mweusi nikakuta kuna almasi nyingi sana nilitetemeka sana nikaficha ule mfuko japo nilikuwa nipo peke yangu chumbani, nikaurudisha ule mfuko kwa hofu kipindi naurudisha niliona kitabu kidogo nilichukua kile kitabu nilipokifungua nilikutana na historia nzima ya maisha yangu , kitabu kile alikiandika baba kabla hajapoteza maisha nililia sana daaah unanikumbusha machungu niliyoyapata kijana wangu ??????. KAKINGA ?? Pole sana babu Nisamehe kwa kukumbusha mambo yaliyopita . BABU ?? Usijali kijana wangu nili…niliii… Daah niligundua wazazi wangu waliuwawa kutokana na Mali walizokuwa nazo kuna kundi limejitengeneza na lina nguvu sana hadi ndani ya serikali yetu wapo watu hao kila sehemu wapo watu hao kazi yao ni kuwanyanganya watu Mali zao ardhi na kuwapoteza duniani, Niliumia sana nilitamani kulipa kisasi kwa watu hao lakini nilishindwa niliamua kuuza zile almasi nikafunga ndoa na nikajaliwa watoto watatu. Siku moja nikiwa na familia yangu nilivamiwa na watu nisiowajua wakambaka mke wangu alafu wakamchinja mke wangu pamoja na watoto wangu mbele ya macho yangu niliumia wakaninyanga Mali zangu zote. Wakanipiga risasi wakajua nimekufa wakanitupa baharini nilisaidiwa na mtu nisiyemjua maisha yangu yakaishia hivyo hadi leo na walikuwa wananitafuta kwa kutumia alama hii. Yule babu alivua shati lake akamuonesha Kakinga alama ile kakinga alistuka kumuona babu ameandikwa neno AKWELINA katika mgongo wake kama alivyo andikwa mtoto waliyenaye hadi leo. Kakinga akiwa na hofu kubwa alimuuliza babu :- KAKINGA ?? Hiyo alama inamaana gani babu ? BABU ?? Hii sio alama ni jina la huyo mshenzi anayeendesha kundi la hao watu na niliandikwa na wazazi wangu walitambua siku moja nitaweza kulipa kisasi lakini siwezi kutokana umri wangu huu lakini ninaamini ipo siku mungu ataleta mtu wa kuja kuwatoa hao mashetani kwa sababu kila siku wanazidi kuwatesa watu wasio na hatia na niligundua waliniwekea kifaa maalumu kilichokuwa kinawapatia taarifa sehemu yeyote nilipokuwepo walikiweka hapa katika mkono wa kulia kwamba huwezi kuwakimbia . Kakinga aliposikia maneno yale toka kwa babu alikimbia haraka kumfuata akwelina ndani akamkuta amelala kakinga akamfunua nguo akwelina akamkagua katika mikono yote miwili akaona kovu katika mkono wa kushoto kakinga alipotazama vizuri akaona kuna kitu kinatoa mwanga mwekundu ndani ya kovu lile. Kipindi kakinga anashangaa kile kitu alisikia mlio wa risasi nje kakinga akatoka nje akamuona babu amedondoka ndani ya maji kwa mbali akaona meli ndogo inakuja ikiwa na wanajeshi kakinga ali……… Kakinga alirudi ndani haraka haraka akambeba akwelina akamweleza mke wake wapo katika hatari kubwa sana, Monna alianza kutetemeka , mapigo ya moyo walimwenda mbio Monna , Kakinga alitoka nje tena baada ya kukumbuka vitu walivyomkuta navyo Monna alivisahau nje. Wale wanajeshi walizidi kusogea sehemu alipokuwa kakinga na mke wake Monna , Kakinga alikaza moyo akamshika mkono mke wake. “”” Kuwa jasiri mke wangu tupo sehemu hatari maisha yetu yapo hatarini lazima uwe na nguvu ili tumsaidie akwelina “”” Yamekuwa maneno ya kakinga akimwambia mke wake Monna ili kumpatia nguvu na faraja kwa sababu kakinga aligundua mke wake anatetemeka sana baada ya kumshika mkono, Maneno ya kakinga yaliupatia nguvu ya kutosha moyo wa Monna, Kakinga hakuhitaji kupoteza muda akatoka nje akiwa amemshika mkono Monna mke wake walitoka taratibu kakinga akachukua vile vitu walivyomkuta navyo akwelina kwakua kakinga alikuwa na wasiwasi sana alidondosha mfuko uliokuwa na almasi ndani yake, Walifanikiwa kutoka sehemu hiyo hatari kakinga na monna walipofika mbali wakajificha wakawaona wale wanajeshi wanauchukua mwili wa babu wakauchoma moto pamoja na nyumba yake masikini kitendo kile kilimuuma sana kakinga, Kakinga na monna wakiwa wamejificha eneo hilo walisikia sauti kali ikilia karibu yao kakinga alijaribu kuitafuta sauti ile ilipokuwa inatoka akagundua ilikuwa inatoka katika mkono wa akwelina. Walipotazama mbele yao waliwaona wale wanajeshi wanakuja eneo walilokuwepo wakiwa na kitu chenye mfano wa simu katika mikono yao kakinga akamshika mkono mke wake wakakimbia. Safari yao ilikuwa ndefu sana Kwa bahati nzuri walifanikiwa kuwakimbia wale wanajeshi na ule mlio ulikuwa unatoka katika mkono wa akwelina uliacha kulia. Walimshukuru mungu kisha wakaendelea na safari japo walikuwa hawajui wapi wanapoelekea walitembea Kwa muda mrefu monna alikuwa amechoka sana akamuomba mume wake watafute sehemu wapumzike , kakinga alimsikiliza mke wake wakapumzika , Walipokuwa wamepumzika kakinga alimsimulia mke wake yote aliyozungumza na babu kule ufukweni, Monna alishangaa sana akamwangalia akwelina katika mkono wake akagundua ni kweli alichoambiwa na mume wake. Monna alimuomba mume wake kakinga wampeleke akwelina hospital wakamtoe hicho kitu katika mkono, Kwakua walikuwa hawana pesa Monna alichukua cheni aliyopewa na marehemu mama yake akauza pesa walizopata wakaenda hospital walipofika daktari alimfanyia vipimo akwelina alafu akawaambia : DAKTARI?? Ni kweli mtoto wenu anakifaa mkononi na hiyo ni GBS kifaa maalumu kinachotoa taarifa popote mtoto huyu atapokuwepo hiyo ni Moja , Mbili kifaa hicho kimewekwa kitaalamu sana kimeungwa kupitia mifipa ya fahamu sasa katika upasuaji wa mtoto huyu kuna matukio mawili KUFA au KUPONA kama mpo tayari niwaletee mkataba tunahitaji sahihi ( sign ) zenu . Kakinga na monna walitazamana sana kakinga akasema ….. Kakinga na monna walitazamana sana kakinga akasema :- KAKINGA ?? Fanya upasuaji dakatari naomba huo mkataba niweke sahihi . MONNA?? ?? Hapana mume wangu hapana mtoto akifa ? KAKINGA ?? Huwezi kuiziwia roho ya mtu kama muda wake umefika mke wangu tumuachie mungu kwa hili. Daktari Fanya kazi yako . DAKTARI ?? Sawa nisubirini . Daktari alitoka nje dakika kadhaa alafu akarudi ndani ya chumba chake akiwa na karatasi mkononi alipofika akampatia karatasi ile kakinga , Kakinga bila hofu alichukua kalamu alipotaka kuweka sahihi Monna alishika mkono wa mume wangu, kakinga alipomtazama mke wake alimuona amejawa na wasiwasi mkubwa, Kijasho chembamba kilikuwa kinamteremka Monna. Kakinga aliweka chini ile kalamu akamtazama Monna kwa muda mrefu sana alafu akamwambia :- “””* Mke wangu wewe ndio mama wa mtoto huyu na siku zote mama huwa hakubali kumpoteza mtoto wake, Mama yupo tayari kuyapoteza maisha yake kwa ajili ya kupambania maisha ya mtoto wake na siku zote tiba ya kweli ya mtoto ni nafsi ya mama kama mama hujaridhia kwa mtoto kamwe kitu hicho hakiwezi kufanikiwa , samahani daktari kwakua mama amepinga jambo hili basi naomba tuondoke . Kakinga alisimama akampatia Monna mkono ili waondoke Monna alifikiria sana akachukua ile kalamu akampatia kakinga, kitendo hicho kilimpatia faraja kakinga akaweka sahihi katika karatasi zile. Daktari alichukua zile karatasi akaziweka pembeni , akamchukua akwelina akaenda nae maabara. Daktari alichukua muda mwingi sana katika upasuaji huo , hali hiyo ilimpatia wasiwasi mkubwa Monna , Monna alikuwa anazunguka huku na huko ndani ya chumba cha daktari. Baada ya masaa sita kupita daktari alirudi :- “””* Ndugu zangu tumshukuru mungu nimefanikiwa kufanya upasuaji salama wa mtoto wenu kwahiyo kuna dawa mnazotakiwa kununua. Kakinga alimshukuru sana dakatri yule. Akwelina alitumia muda mrefu sana kupona hali iliyowatesa sana kakinga na mke wake Monna kutokana na kipato chao. Baada ya miezi mitatu akwelina alipona daktari aliwaruhusu warudi nyumbani lakini daktari alikuwa anamtazama sana Monna walipokuwa wanataka kuondoka daktari alimuuliza Monna : DAKTARI ?? Samahani mnaishi sehemu gani ? MONNA ?? Ni historia ndefu sana kifupi Mimi na mume wangu hatuna sehemu ya kuishi maisha yetu ni magumu sana . DAKTARI ?? Ooh poleni sana na kwa hali ya mtoto anatakiwa apate chakula kizuri na sehemu safi kwakua umesema hamna sehemu ya kwenda basi Mimi nitawasaidia tutaenda sote kwangu mtaishi kwangu hadi mtapopata makazi yenu jina langu naitwa PATRICK . Hakika ilikuwa ni furaha kwa kakinga na mke wake monna, waliendelea kumsubiri Dr Patrick katika chumba chake hadi alipomaliza kazi zake, Patrick alipomaliza kazi aliwachukua wakaenda hadi nyumbani kwake, Maisha yalianza kuwa matam na mazuri kwa kakinga na monna. Wanasema mapenzi ni kitu cha ajabu sana hiyo ilimkuta Patrick baada ya kuishi na familia ya kakinga taratibu taratibu Patrick alianza kuvutiwa na monna kutokana na uzuri aliokuwa nao , Monna alikuwa Mrembo sana baada ya kupata matunzo hali iliyosababisha Patrick kushindwa kuziwia hisia zake. Kwakua Patrick alishindwa kumwambia ukweli monna , Patrick alikuwa anamletea zawadi mbalimbali zenye thamani mno, kakinga alianza kuwa na mashaka kwa mke wake. Siku moja Patrick hakwenda kazini siku hiyo ilikuwa ni siku ya mapumziko. Monna alimka mapema sana siku hiyo kwakua alitambua Patrick yupo nyumbani , monna akiwa jikoni akiandaa chai Patrick alimfuata monna jikoni wakati huo monna alikuwa hajatambua kama Patrick yupo nyuma yake , Patrick alimshika kiuno monna , Monna alisisimka sana akageuka kumwangalia aliyemshika kiuno ni nani akashangaa kumuona ni Patrick monna ali………. Monna alishikwa na aibu ya ajabu sana monna akabaki kutazama chini muda wote, Patrick alijisogeza karibu zaidi kwa monna akamshika mkono , Mapigo ya moyo ndani ya mwili wa monna yalikuwa yanakwenda mbio zaidi ya siku zote, Patrick alipogundua monna anatetemeka alitumia nafasi hiyo hiyo akamsogeza mdomo wake karibu ya sikio la monna akasema :- ?? Monna unajua wewe ni mrembo sana na hakika nimeshindwa kuziwia hisia zangu juu yako, kweli natambua umeolewa na pengine mume wako unampenda sana lakini nami ni binadamu pia naomba usinifikirie vibaya hizi ni hisia zangu kwako nipo tayari kufanya chochote utachohitaji katika dunia hii nakupenda monna naomba nipe nafasi japo theluthi nikuoneshe jinsi gani ninavyokupenda nakutakia asubuhi njema andaa chai vizuri nakupenda monna ?? Patrick baada ya kumwambia maneno hayo monna alimsogelea zaidi monna , monna hakuwa jasili akafumba macho , Patrick alitumia nafasi hiyo akahitaji kumpiga busu monna lakini kabla hajaufikia mdomo wa monna walisikia sauti ya kakinga akimwita mke wake , Patrick akaondoka jikoni haraka alitumia mlango wa nyuma kwa sababu jiko hilo lilikuwa na milango miwili tofauti , Kakinga alipoingia jikoni alimuona mke wake monna ana wasiwasi uliopitiliza kakinga alijaribu kjmuuliza monna lakini monna hakuzungumza kitu. Siku zilizidi kwenda tabia ya Patrick kumletea zawadi monna haikuisha kila kukicha Patrick alizidi kumjali monna Kwa kumpatia fedha na vitu vikubwa zaidi. Siku iliyofuata kakinga alikuwa na monna sebuleni wanacheza na akwelina Patrick aliingia akiwa na boksi mbali za simu mkononi mwake kakinga aliwapatia simu wote, Daah kakinga alifurahi mno Kwa sababu katika maisha yake yote hakuwahi kumiliki simu. Yalipofika majira ya usiku simu ya monna iliita monna alipoitazama aliona namba mpya , Monna akapokea simu ?? Monna ni mimi Patrick kuna zawadi nimekununulia ipo nyuma yako ichukue hiyo kesho naomba kutoka na wewe peke yake kuna sehemu nahitaji twende kama hautojali *”” Monna aligeuka akaona mfuko alipofungua alikuta nguo nzuri sana , Monna alifurahi sana akamkubalia Patrick ombi lake . Siku iliyofuata asubuhi na mapema kakinga alimuaga mke wake kuna sehemu alituma maombi ya kazi, Monna kwakua hakuhitaji mume wake ajue safari yake na Patrick alifurahi. Muda ulizidi kwenda yalipofika majira ya mchana Patrick alichukua gari lake akamchukua monna , wakamuacha akwelina ndani peke yake akiwa amelala , Safari yao ilichukua muda kiasi hatimae wakafika sehemu husika hakika eneo lile lilikuwa linavutia sana , wakati monna anashangaa eneo lile Patrick alimkumbatia monna akamwambia :- “”” NAKUPENDA MONNA nipe nafasi tafadhali “” Monna alimgeukia Patrick Kwa macho ya kimahaba aka…. Monna alimgeukia Patrick Kwa macho ya kimahaba akajaribu kuzungumza maneno ambayo Patrick hakuyaelewa kabisa : ~~ Patrick mmmh unajua mimi daah sijui nifanyaje mimi Patrick unanipatia wakati mgumu daah . Yalikuwa ni maneno ya monna akijing’atang’ata mbele ya Patrick, wakati wote huo Patrick alikuwa anamsoma monna aligundua monna hawezi kumkubalia kile alichohitaji kwa sababu monna alikuwa hajiamini pia monna alikuwa na wasiwasi uliotawala mwili na akili yake , Patrick hakuchoka akamvuta monna , monna alikuwa laini zaidi ya bamia monna alijikuta yupo katika kifua cha Patrick , Monna akiwa kifuani kwa Patrick, Patrick alisema :- “”* Mungu kweli fundi muda aliopoteza wakati anakuumba wewe ninaamini hakujutia, Monna moyo wangu unaomba kuzungumza na wewe tafadhali zungumza na moyo wangu “” Patrick alishika kichwa cha monna akamgeuza sikio la monna lilituwa upande wa kushoto mwa kifua cha Patrick monna aliyasikia mapigo ya moyo wa Patrick yanapiga kwa kasi sana Patrick alishika kichwa cha monna kwa Mara ya pili alafu akayatazama macho ya monna kwa muda mrefu sana, monna alishindwa kumtazama Patrick , Patrick akatumia nafasi hiyo akasogelea midomo ya monna alipoigusa tu monna akamsukuma Patrick , Patrick alidondoka chini monna aliogopa sana akamfuata Patrick akamuomba msamaha, Patrick alimwambia monna asijali lakini bado Patrick alikuwa analilia penzi kwa monna. Monna alisema :- MONNA ?? Nisamehe Patrick kwa kukusukuma nimesikia ombi lako na usijali nipatie muda nitakujibu tafadhali vuta subira . Patrick alifurahi sana kusikia maneno yale kutoka kwa monna, Patrick akamchukua monna wakapanda kwenye gari wakaenda sehemu nyingine. Kakinga alitoka katika ile kampuni aliyoomba kazi alitamani sana kumnunulia mke wake zawadi lakini kakinga hakuwa na pesa yeyote , kakinga alifikiria njia rahisi inayoweza kumpatia pesa kwa muda ule kwa ajili ya kumnunulia zawadi mke wake kipenzi, kakinga akaona bora aigize kama mlemavu ili apate pesa za kumnunulia zawadi mke wake baada ya kupata wazo hilo kakinga alifanikiwa kupata pesa kwa muda mfupi akachukua zile fedha akaenda kununua viatu kwa ajili ya mke wake, Kakinga aliporudi nyumbani alikuta nyumba imefungwa cha ajabu alisikia sauti ya mtoto ndani analia kakinga alichungulia dirishani akamuona akwelina analia akiwa chini , Kakinga alichanganyikiwa sana kakinga alitafuta njia ya kuingia ndani akaikosa ikabidi avunje dirisha akaingia ndani akamkuta akwelina amedondoka chini damu zinamtoka puani. Kakinga alishikwa na hasira sana akampatia huduma ya kwanza akwelina alafu akatoka nje ya nyumbani ile akakaa chini . Muda ulikwenda sana hatimae usiku ukaingia kakinga akiwa ndani ya giza nene kwa sababu hakuwasha taa lolote katika nyumba ile alimuona Patrick anafungua geti akiwa na monna, Patrick akiwa amemshika kiuno monna waliingia ndani monna akiwa na furaha sana , walipoona giza monna akasema : MONNA ?? Mbona giza hivi au mume wangu hajarudi ? PATRICK ?? Aaah yule ni mwanaume buana atarudi tu kwani mimi sio mume wako ? MONNA ?? Usijali nawe siku moja utakuwa mume wangu hata sio mbali washa taa ya simu tuingie ndani basi . PATRICK ?? Subiri kidogo monna kwani unawahi nini huko ndani sasa siingii ndani hadi unipige busu la nguvu kama sivyo nalala nje hapahapa . MONNA ?? Jamani Patrick sawa sogea nahofu mume wangu asije nikuta lakini si nilikuambia nipe muda ila usijali busu tu sawa. Patrick alifurahi akamvuta karibu monna akamshika kiuno kimahaba alafu akambusu kwenye shavu , baada ya hapo wakasogea karibu ya nyumba Patrick akawasha taa ya simu yake ule mwanga wa taa ulipowaka walimuona kakinga amekaa karibu na mlango monna ali…….. Ule mwanga wa taa ulipowaka walimuona kakinga amekaa karibu na mlango, monna alistuka sana: “”* Mume wangu kumbe upo jamani nisamehe mume wangu tulikuwa mbali kwenye vikao , Patrick aliniomba nikamsaidie kazi Kwa sababu wewe uliondoka mapema sana . Yalikuwa ni maneno ya monna akijaribu kumuelezea mume wake kakinga, Kakinga alimtazama sana monna hali iliyomfanya monna atetemeke kakinga akasema : KAKINGA ??Na huko kushikana viuno na kupigana mabusu ni moja ya kazi za ofisini huko mlipokuwa ? MONNA ?? Jamani mbona wanifikiria vibaya lakini nakuomba mume wangu tuliza hasira nisamehe kwa nilichofanya mbele yako najua umenitafsiri vibaya lakini sio kweli hicho unachofikiria kwa sasa. KAKINGA ?? Sawa na vipi kuhusu mtoto kwanini usiondoke nae je kama ungemkuta kapoteza maisha unamuona alivyopata majeraha yote kwa ujinga wako. PATRICK ?? Nisamehe mimi kaka kwa sababu mimi ndio nilimuomba niondoke nae na nilifahamu tutawahi kurudi lakini kwa bahati mbaya tumechelewa nisamehe mimi. Siku zote kakinga huwa ni mwelewa sana japo alihisi kuna kitu kinaendelea baina ya Patrick na mke wake monna, kakinga alicheka sana akasema :- KAKINGA ?? Hahaha ?? acha uoga mke wangu mimi nakuamini siwezi kuweka hofu kwako japo umeniudhi kwa kumuacha mtoto ndani si unajua nampenda sana mtoto wangu . Monna na Patrick walishusha pumzi nzito baada ya kusikia maneno hayo toka kwa kakinga, Kakinga akamshika mkono mke wake wakaingia ndani walipofika ndani walisha taa Patrick aliona dirisha limevunja kakinga akamueleza hali iliyokuwepo. Siku baada ya siku ukarimu wa monna na Patrick ulizidi kuwa karibu zaidi, Kakinga alikuwa anaona yote hayo lakini alikuwa mkimya sana, Patrick hakuchoka kumletea monna zawadi mbalimbali kama kawaida yake kutokana na ukaribu huo, Monna alianza kumpenda Patrick. Siku baada ya siku monna alijikuta yupo busy sana na Patrick kuliko mume wake . Kakinga hakuchoka kumchunguza mke wake, Baada ya siku mbili kupita monna alijikuwa nyumbani anafanya usafi siku hiyo Patrick alirudi nyumbani mapema akamkuta monna anafanya usafi monna alipomuona Patrick aliacha kufanya usafi akamkumbatia Patrick cha ajabu monna akambusu Patrick alafu akaondoka, Patrick alifurahi sana akasema :- “”* Kazi imekwisha kilichobaki ni kufanya kitu ambacho nakihitaji toka kwake wooooooooh hahaha. Patrick akaingia ndani kwake yote yalikuwa yanatendeka kakinga alikuwa anayaona akiwa nyuma ya ukuta, Roho ilitaka kupasuka kwa maumivu aliyokuwa nayo kakinga kwa sababu kakinga alikuwa anampenda sana mke wake. Usiku ulipofika wakawi katika meza ya chakula monna macho yake yote yalikuwa kwa Patrick bila kujali kakinga yupo nae eneo hili kitendo hicho kilimfnya kakinga aache chakula akaondoka , Monna alipoona kakinga kaondoka alifurahi sana akamsogelea Patrick akawa anamtania kwa kumtekenya tekenya yote hayo kakinga alikuwa anayashuhudia, Kiukweli kakinga alishindwa kuvumilia maumivu hayo. Yalipofika majira ya asubuhi kakinga aliamka mapema sana akakusanya nguo zote akazifunga vizuri kakinga akamuamsha monna , monna alipoamka alimshangaa mume wake kakinga akamshika mkono monna wakatoka nje japo monna alikuwa hataki walipofika sebuleni wakammuta Patrick monna akamshika mkono Patrick kakinga akasimama akamuuliza monna :- KAKINGA ?? Chagua Mona monna kuondoka na mimi au kubaki na Patrick ? Cha ajabu monna ali… Cha ajabu monna alitoa mkono kwa kakinga alafu akasogea kwa Patrick, Kakinga aliishiwa nguvu akadondosha begi la nguo alilokuwa ameshika , Ilikuwa ni ngumu sana kuamini kile anachoona mbele yake ! “”””””*” Nisamehe sana kakinga “”””* Moyo wa kakinga ulizidi kwenda mbio kwa kusikia leo Monna kwa Mara ya kwanza anataja jina hilo , kakinga alizoea kuitwa mume , mpenzi na baba watoto hasira alizokuwa nazo kakinga zilimfanya ashikwe na kizunguzungu , kakinga alishika kichwa chake kwa muda mrefu kiasi Monna hakumuonea huruma kakinga akaendelea kusema: MONNA???? Naomba msamaha tena mbele yako kwa kufanya hiki ninachofanya katika maisha yako , Najua nimetoka mbali na wewe na umenivumilia kwa mambo mengi sana, Kakinga hadi sasa nimeishi na wewe kwa miaka mingi zaidi ya sita bado hali yako sio nzuri kimaisha nimekuvumilia sana kakinga lakini bado unahali mbaya ya kimaisha , kula kwetu tabu , kuvaa tabu hatuna sehemu ya kuishi daah nimechoka kakinga naomba taraka yangu leo hii hii na nitakurudishia pesa yako ya mahari. Mimi nahitaji mwanaume mwenye pesa miaka zaidi ya sita hata mtoto sina na sijapata hata kichefuchefu sasa hebu niambie napata faida gani kwako ? PATRICK ?? Heeeeh !!?? yule mtoto sio wako ? MONNA ?? Nizae wapi huyo mtoto nimemuokota tu hata sio wangu pia huyu mwanaume nikiwa nae ndani anakuwa mvi… KAKINGA ?? Basiiiiiiiiii monna ?? unapokwenda sipo ni kweli upo sahihi Mimi sio mzima siwezi kuzalisha si ndiyo ? Na pia Mimi masikini sana lakini tatizo kwanini haukuniambia mapema laiti ungeniambia mapema nisingeruhusu moyo wangu ukupende kiasi hiki , Monna nakupenda mke wangu mtoe shetani kichwani naomba shika mkono wangu huu twende tukatafute maisha nakupenda monna siwezi kupinga hili kweli nakupenda. Pamoja na kakinga kutetea penzi lake haikusaidia kitu monna aliingia ndani baada ya muda alitoka nje akiwa ameshika karatasi pamoja na kalamu akampatia kakinga, Monna akaomba taraka . Kakinga alifikiria sana mwisho akaamua kuchukua maamuzi magumu akaandika taraka wakati anampatia taraka kakinga alimwangalia sana monna machozi yakiwa yanamteremka alisema :- “” Monna kwa sasa upo huru nimefanya hivi kwa sababu wewe umetaka hivyo nilikuahidi kwamba nitafanya chochote ili uwe na furaha hata kama kitaniumiza Mimi lakini wewe uwe na furaha milele chukua taraka yako monna lakini kumbuka “” Kimvuli chako ndio rafiki yako kipenzi popote utapokuwepo hakiwezi kukuacha lakini ukiwa gizani kamwe hautakiona , Patrick ndugu yangu nakukabidhi binti huyu naomba mpende kweli usimdanganye kwa sababu maumivu ya mapenzi leo nimeyafahamu hakika mapenzi yanauma sana kwaheri monna. Kakinga alirudi ndani akatoka na akwelina akiwa amelala akamtazama tena monna masikini kisha akaondoka. Maneno aliyosema kakinga yalimpatia mawazo sana monna lakini, Patrick akamshika mkono monna wakarudi ndani. Kakinga akiwa na akwelina mgongoni hakutambua aende wapi masikini , Kakinga alitembea huku na huko akiwa na mawazo yaliyotawala fikra zake, Kakinga alijikuta yupo barabarani hadi majira ya usiku kutokana na kutembea sana akwelina alikuwa amechoka sana akaanza kulia hali iliyomfanya kakinga atambue akwelina atakuwa anataka kula kakinga alienda kuuza simu aliyonunuliwa na Patrick akapata pesa akamnunulia chakula akwelina. Majira hayo hayo monna akiwa ndani pamoja Patrick, Patrick alikuwa huru katika mwili wa monna usiku huo Patrick aliutawala mwili wa monna atakavyo , Monna nae hakuwa mchoyo alimpatia chochote alichohitaji Patrick wakiwa katika mambo hayo maneno ya kakinga yalijirudia katika masikio ya monna , monna akabadirika ghafla hali iliyomfanya Patrick alazimishe kufanya mapenzi na monna , Monna hakukubali kufanya mapenzi kwa nguvu Patrick akachukia akatoka kitandani akafungua kabati akachukua bastola akamnyoshea monna kisha …….. ITAENDELEA Email ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook Leave a comment Simulizi Za Kusisimua Newer Post Older Post Home 0 comments: Post a comment Umependezwa Na Makala Uliyoisoma? Tuachie Maoni yako Hapa Chini. Endelea Kufurahia Makala Zingine Zinazotolewa Na Blog Hii. Subscribe to: Post Comments (Atom) Promoted Content Mgid Mgid Drink This Before Bed, Watch Your Body Fat Melt Like Crazy Black Latte Kuwa na tumbo la tambarare kwa wiki moja, sasa inawezekana! Black Latte Fanya mbinu hii rahisi kupunguza mafuta ya tumbo wakati umelala Black Latte 10 Most Expensive Things In The World Brainberries 9 Movies Brad Pitt Ruined Brainberries Where Are Tiger & Elin's Kids 11 Years After The Drama Unfolded Brainberries Celebs Who Stopped Eating Meat And Why They Did It Brainberries 9 Kids’ Movies That Are More Than Just A Little Scary Brainberries The Curse Of Tutankhamun: The Real Deal Or Nah? Brainberries Maddie Ziegler Has Changed So Much Since ‘Dance Moms’ Brainberries This Inventor Creates Things That Nobody Literally Needs Brainberries 8 Interesting Unknown Facts Of Sasha Obama Brainberries Why Does My Dog Always Get Between Me And My Girlfriend? Brainberries Quimera The Two-Faced Cat Became Viral Sensation Brainberries Another Hilarious Christmas Movies Except Home Alone (1990) Brainberries Effects Of Love On Your Brain And Body Brainberries Most Attractive President's Daughters During Their Prime Beauty Brainberries Biggest Misconceptions About The Body You Should Stop Believing Brainberries PopAds.net - The Best Popunder Adnetwork PopAds.net - The Best Popunder Adnetwork Tengeneza Pesa Mtandaoni / Make Money Online PopAds.net - The Best Popunder Adnetwork PopAds.net - The Best Popunder Adnetwork PopAds.net - The Best Popunder Adnetwork PopAds.net - The Best Popunder Adnetwork PopAds.net - The Best Popunder Adnetwork PopAds.net - The Best Popunder Adnetwork Search Search Here Donate now Blog Rafiki Based on True Story Novel DM Gospel Music Kenya Stories Tanzania Tourism Tanzania Petroleum and Mining Geology Mgodi Wa Maarifa Donate now Page Za Ndani Home WASAFI STORY BOOK WAKUBWA TU 18+ WAANDISHI WA SIMULIZI SIMULIZI ZA SAUTI UCHAWI UPO SHUHUDA ZA KWELI SIMULIZI FUPI NA STORY ZA MAPENZI SIMULIZI ZA MAISHA SIMULIZI ZA KUSISIMUA CHOMBEZO SIMULIZI ZA KICHAWI CHOMBEZO PLUS+ SIMULIZI ZA KIJASUSI WASILIANA NASI/CONTACT US MWALIMU WA KISWAHILI SALIM MSANGI NA ELIMU YA FREEMASON AFYA NA JAMII UFAHAMU NA MAARIFA WANAWAKE NA UREMBO NDOA UCHUMBA NA MAHUSIANO MAPISHI MBALIMBALI JUISI, MATUNDA NA MBOGAMBOGA TANZANIA COMPUTER TECHNOLOGY HISTORIA KILIMO UFUGAJI NA UVUVI DOCTOR LOVE FADHILI PAULO TABIBU WA TIBA ZA ASILI MZIZI MKAVU DAWA ZA TIBA MBADALA ZA MITISHAMBA Donate now Page Za Nje KUTOA MIMBA NA USHAURI SIMULIZI NA HADITHI MIMBA NA UZAZI AFRICA SCHOLARSHIPS BIASHARA NA UJASIRIAMALI MIRADI YA KIJAMII UONGOZI NA UTAWALA STADI ZA MAISHA Registered and Accredited Institutions by Nacte TANZANIA COLLEGES AND INSTITUTIONS MASUALA MTAMBUKA TEHAMA NA UTANDAWAZI MAMBO MENGINE Blog archive ► 2019 (5411) ► 2020 (4458) ▼ 2021 (860) ► January (253) ▼ February (363) ► Feb 04 (6) ▼ Feb 06 (90) BWANA HARUSI ALIYEJERUHIWA - 1 BWANA HARUSI ALIYEJERUHIWA - 2 BWANA HARUSI ALIYEJERUHIWA - 3 BWANA HARUSI ALIYEJERUHIWA - 4 BWANA HARUSI ALIYEJERUHIWA - 5 SOKA LILIVYONIKUTANISHA NA SHETANI - 1 SOKA LILIVYONIKUTANISHA NA SHETANI - 2 SOKA LILIVYONIKUTANISHA NA SHETANI - 3 SOKA LILIVYONIKUTANISHA NA SHETANI - 4 SOKA LILIVYONIKUTANISHA NA SHETANI - 5 WIVU - 1 WIVU - 2 WIVU - 3 WIVU - 4 WIVU - 5 UPEPO WA USIKU - 1 UPEPO WA USIKU - 2 UPEPO WA USIKU - 3 UPEPO WA USIKU - 4 UPEPO WA USIKU - 5 KIFO SIKU YA HARUSI YANGU - 1 KIFO SIKU YA HARUSI YANGU - 2 KIFO SIKU YA HARUSI YANGU - 3 KIFO SIKU YA HARUSI YANGU - 4 KIFO SIKU YA HARUSI YANGU - 5 ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU - 1 ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU - 2 ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU - 3 ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU - 4 ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU - 5 MAMBO YA AJABU YALIYOMPATA ALLAN QUATERMAIN NA WEN... MAMBO YA AJABU YALIYOMPATA ALLAN QUATERMAIN NA WEN... MAMBO YA AJABU YALIYOMPATA ALLAN QUATERMAIN NA WEN... MAMBO YA AJABU YALIYOMPATA ALLAN QUATERMAIN NA WEN... MAMBO YA AJABU YALIYOMPATA ALLAN QUATERMAIN NA WEN... MASHIMO YA MFALME SULEMANI - 1 MASHIMO YA MFALME SULEMANI - 2 MASHIMO YA MFALME SULEMANI - 3 MASHIMO YA MFALME SULEMANI - 4 MASHIMO YA MFALME SULEMANI - 5 BIASHARA YA KIFO - 1 BIASHARA YA KIFO - 2 BIASHARA YA KIFO - 3 BIASHARA YA KIFO - 4 BIASHARA YA KIFO - 5 ULINISALITI JULIET - 1 ULINISALITI JULIET - 2 ULINISALITI JULIET - 3 ULINISALITI JULIET - 4 ULINISALITI JULIET - 5 MOYO ULIOONJA MAUMIVU - 1 MOYO ULIOONJA MAUMIVU - 2 MOYO ULIOONJA MAUMIVU - 3 MOYO ULIOONJA MAUMIVU - 4 MOYO ULIOONJA MAUMIVU - 5 MZIMU UNAOTABASAMU - 1 MZIMU UNAOTABASAMU - 2 MZIMU UNAOTABASAMU - 3 MZIMU UNAOTABASAMU - 4 MZIMU UNAOTABASAMU - 5 PENZI LISILO NA MWISHO - 1 PENZI LISILO NA MWISHO - 2 PENZI LISILO NA MWISHO - 3 PENZI LISILO NA MWISHO - 4 PENZI LISILO NA MWISHO - 5 SCAILA MICHAEL - 1 SCAILA MICHAEL - 2 SCAILA MICHAEL - 3 SCAILA MICHAEL - 4 SCAILA MICHAEL - 5 UTAJIRI WENYE UCHUNGU - 1 UTAJIRI WENYE UCHUNGU - 2 UTAJIRI WENYE UCHUNGU - 3 UTAJIRI WENYE UCHUNGU - 4 UTAJIRI WENYE UCHUNGU - 5 AKWELINA - 1 AKWELINA - 2 AKWELINA - 3 AKWELINA - 4 AKWELINA - 5 ADILI NA NDUGUZE - 1 ADILI NA NDUGUZE - 2 ADILI NA NDUGUZE - 3 ADILI NA NDUGUZE - 4 ADILI NA NDUGUZE - 5 MAISHA YANGU NYUMA YA PAZIA JEUSI - 1 MAISHA YANGU NYUMA YA PAZIA JEUSI - 2 MAISHA YANGU NYUMA YA PAZIA JEUSI - 3 MAISHA YANGU NYUMA YA PAZIA JEUSI - 4 MAISHA YANGU NYUMA YA PAZIA JEUSI - 5 ► Feb 07 (181) ► Feb 19 (20) ► Feb 20 (22) ► Feb 28 (44) ► March (244) Labels AFYA NA JAMII BEST 1 Chemsha Bongo Chombezo Chombezo Plus+ DOCTOR LOVE Fadhili Paulo FEDHA HELA PESA ZA MTANDAONI Gospel Lyrics Hekaya HISTORIA Huduma Ya Kwanza Imani Injili Jamiiforums JUISI MATUNDA NA MBOGAMBOGA Kenyan Palace Kenyan Stories KILIMO UFUGAJI NA UVUVI Maarifa Ya Maisha Magonjwa Mapishi MATANGAZO Mifugo Motivational And Inspirational Short Stories MWALIMU WA KISWAHILI MZIZI MKAVU NDOA UCHUMBA NA MAHUSIANO PANDORA Saikolojia SALIM MSANGI Simulizi Fupi Na Story Za Mapenzi Simulizi Za Kichawi Simulizi Za Kijasusi Simulizi Za Kusisimua Simulizi Za Kweli Simulizi Za Maisha Simulizi Za Sauti Swahili English Dictionary TANZANIA COMPUTER TECHNOLOGY Ufahamu na Maarifa Ujasiriamali USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI Utabiri Wa Maisha Waandishi Wa Simulizi Wadudu Wakubwa Tu 18+ WANAWAKE NA UREMBO Wepigraphas
AKWELINA - 2
Simulizi : Akwelina
Sehemu Ya Pili (2)
Sauti ya Monna ilimstua Kakinga pamoja na Dereva wakaanza kumtafuta Monna huku na huko Dereva akawasha tochi lake wakati anamoreka tochi lilimdondoka yule dereva alipoinama ili achukue tochi alihisi kuna kitu kitu upande wake wa kushoto yule dereva alisogea taratibu akiwa makini sana akaona pango dogo akamoreka ndani ya lile pango akamuona msichana mmoja akiwa ameshikwa na wanaume zaidi wanne yule dereva alimuita Kakinga, kakinga alipofika alimuona mke wake ameshikwa na wanaume wengi. Kakinga alishikwa na hasira akaingia ndani ya pango hilo akawapiga sana wale wahuni kwa hasira alizokuwa nazo kakinga alifunja mikono ya vijana hao na kuhitaji kuwauwa kabisa , yule Dereva akamziwia Kakinga Vijana hao wakakimbia .
Kakinga akamtoa mke wake ndani ya pango , Monna hakuamini kama amepata msaada monna alimkumbatia mume wake yule dereva akawapatia msaada hadi nyumbani kwake, yule Dereva alikuwa amepanga chunga kimoja na sebure, kwakua yalikuwa ni majira ya usiku Kakinga na Monna walilala sebuleni. Asubuhi palipokucha yule Dereva aliamka mapema sana akawapa pesa ya chakula akaondoka kwenda katika shughuli zake, Monna alimshukuru mungu kwa kumpata kijana mwenye roho nzuri .
Baada ya wiki mbili kakinga aliiamka asubuhi sana akaingia mtaani kutafuta kazi siku hiyo kakinga alizunguka mji mzima lakini hakupata kazi, Kakinga hakukata tamaa aliendelea kupambana kutafuta kazi mungu akamjalia kakinga akapata kazi ya kubeba mizigo stenti ya magari , kakinga alifanya kazi bila kuchoka kuanzia asubuhi hadi majira ya saa mbili usiku akapata shilingi 10000 Kakinga akarudi nyumbani akiwa hoi Mwili wote unamuuma kama donda .
Wakati huo njaa ilikuwa inamuuma kwa sababu alikuwa hajala toka asubuhi Kakinga alitamani anunue chakula ale lakini alishindwa kwa sababu alitambua Monna atakuwa hajala kama yeye, Kakinga alitumia zile fedha akanunua vyakula vya kutosha akiwa njiani anarudi nyumbani alimuona mtoto mdogo anataka kuingia kwenye moto Kakinga akashangaa sana akatazama eneo lote akaona kimya ikabidi Kakinga akimbie haraka akamchukua yule mtoto kabla hajaufikia Moto , Kakinga akiwa amembeba mtoto alisikia mtu mmoja ikisema :
"" Jamani yule Mwizi wa mtoto huyu hapa njooni njooni ..
Watu wa mtaa ule walitoka nje na silaha mbalimbali wakamva.............
Watu wa mtaa ule walitoka nje na silaha mbalimbali wakamvamia kakinga wakamshambulia kakinga , kakinga alijaribu kuwaelezea ukweli kuhusu mtoto lakini wananchi hawakumuelewa kabisa, waliendelea kumpiga kwa bahati nzuri askari wa lindo la usiku walitokea eneo lile wakamchukua kakinga wakaenda nae kutuo cha police walipofika kituoni askari hawakutaka kumsikiliza kakinga wakamueka mahabusu. Siku hiyo monna alikuwa anawasiwasi mkubwa sana, muda ulizidi kwenda monna alitoka nje na mtoto akamtazama sana mtoto akasema kwa sauti ya chini sana :-
“”* Akwelina mtoto wangu najua unahisi njaa unahitaji kula masikini tangu asubuhi hadi muda huu hujala kitu chochote nitafanyaje mimi ndani hakuna kitu, pesa hakuna baba yako tangu aondoke hajarudi hadi muda sasa sijui kapatwa na tatizo gani daaah matiti ninayo lakini hayana maziwa ndani yake hayatoi kitu vumilia mtoto wangu *””””
Monna alipomaliza kuzungumza aliimba wimbo mzuri akiwa anambembeleza akwelina taratibu taratibu akwelina alilala, Monna akaingia ndani akamlaza mtoto alafu akatoka nje akakaa karibu na mlango monna alizungumza mouoni :-
“”** Upo wapi mume wangu , umepatwa na nini mbona wanifanya nikose amani rudi mume wangu *”””
Muda ulizidi kwenda hadi saa saba usiku monna alikuwa bado yupo nje anamsubiri mume wake, Yule dereva alikuja amelewa sana akamkuta monna yupo nje akasema :-
DEREVA ??Wewe mwanamke unawanga nini mbona upo nje hadi muda huu unafanya nini anhaaaa kumbe wewe ndio unakujaga usiku chumbani kwangu unanichapa bakora weeee nikiamka asubuhi nakuwa nimechoka sanaaa sasa nasema ondokeni wewe na mume wako siwezi kuwalea watu wazima kama ninyi nasema ondokeni pumbafu “”
MONNA ?? Shemeji mimi nitaenda wapi usiku huu jamani mume wangu hajarudi pia ninamtoto mdogo jamani najua umelewa nenda kalale shemeji tutazungumza kesho .
DEREVA ?? Mimi nimelewa ? Haaaah !! Mimi sijawahi kulewa toka nizaliwe nasema toka hunijui eeh subiri sasa nimewachoka nawalisha kila siku kama watoto ondokeni .
Yule dereva aliingia ndani akatoa nguo za monna akawa anazitupa nje monna alimuomba sana lakini yule dereva hakusikia kilio cha Monna, monna aliingia ndani akachukua mizigo yake akambeba akwelina mgongoni akatoka nje akaenda hadi stenti ya magari iliyokuwa karibu na nyumba waliyokuwa wanaishi, Monna alifika stenti akamtoa akwelina mgongoni akakaa kwenye kiti. Kakinga alikuwa na mawazo sana mahabusu , kakinga akiwa na mawazo alisema :-
“” Eee mungu kwanini kila siku napata matatizo mimi tu au kuna binadamu mwingine anapata matatizo kama mimi , hivi nimekosa nini mimi? Wema wangu wa kumsadia yule mtoto leo hii napata shida kiasi hiki nyumba yangu imechomwa kisa mtoto , nimenusurika kufa kisa mtoto leo nimekuja kuja humu mahabusu kwa ajili yake kwa sababu moyoni niliweka nia natafuta kazi ili nimnunulie maziwa au huyu mtoto sio binadamu ni jini, shetani au ni pepo, Nimechoka sasa nikifanikiwa kurudi nyumbani nitamchukua mtoto nitaenda kumtupa bila kujali kama mke wangu atapenda au hatopenda.
Hayo ni maneno aliyokuwa anazungumza kakinga baada ya kuona matatizo yanamuandana kila siku. Kakinga alikesha usiku kucha bila kulala yalipofika majira ya asubuhi wale askari waligundua kakinga hana makosa wakamtoa mahabusu kakinga alitoka mahabusu akiwa na hasira sana, kakinga alipofika nyumbani hakumkuta monna akawauliza majirani wakamwambia yote yaliyotokea Jana , kakinga alipata maumivu makali sana , wakati kakinga amesimama anahasira zilizopitiliza alisikia sauti ya monna ikimwita, kakinga alipogeuka alimuona mke wake akamfuata akamchukua akwelina akaondoka nae akiwa anakimbia , kitendo kile kilimshangaza sana monna , Kakinga alimbia hadi sokoni akasimama akapiga magoti akamtazama sana akwelina akasema :-
“”” Utanisamehe sana kwa unyama huu lakini nitafanyaje unanitesa sana akwelina nakuacha hapa atapita mtu mwema mwingine atakuchukua kwaheri sana akwelina nakupenda.
Kakinga alizungumza maneno hayo machozi yakimtoka , kakinga akamuweka chini akwelina akahitaji kuondoka kakinga alishangaa kuona akwelina amemshika kidole chake kwa nguvu kakinga aka……..
Kakinga akatoa mkono wa akwelina katika kidole chake akasimama akaondoka akwelina alianza kulia, kilio cha akwelina kilitesa nafsi ya kakinga, Kakinga alitamani kurudi lakini akajitahidi akaondoka, Akwelina aliendelea kulia masikini Kakinga hakujali aliendelea kuondoka kurudi kwa Monna, Kakinga alikutana na monna njiani, monna alimuona Kakinga hana mtoto monna alichanganyikiwa sana alimuuliza Kakinga :-
MONNA ?? Mume wangu akwelina yupo wapi ?
KAKINGA ?? aaaah achana na habari hizo nimempeleka kwa wengine watusaidie kumlea kama wema tumeufanya sana yule mtoto katuletea matatizo ya ajabu sana Wewe angalia tulipotoka na hapa tulipo yote ni mikosi kwahiyo ndio hivyo nimewapelekea wengine.
MONNA ?? Unasemaje wewe sikuelewi mume wangu namtaka akwelina wangu sikuelewi Mimi siwezi kuishi bila yeye tafadhali nenda kaniletee akwelina wangu .
KAKINGA ?? Nakwambia hivi sahau kuhusu akwelina turudi nyumbani .
MONNA ?? Nyumbani wapi mume wangu rafiki yako ametufukuza amesema ametuchoka siwezi kukuelewa bila kumuona akwelina niambie yupo wapi nimfuate Mimi jamani .
Monna alilia sana katika mikono ya mume. Kakinga aliishiwa nguvu baada ya kuambiwa rafiki yake aliyemsaidia amewafukuza katika nyumba yake kakinga alikaa chini akashika kichwa, monna alipomuona mume wake amechanganyikiwa ghafla monna alijaribu kumfariji japo walikuwa na ugomvi kuhusu mtoto , Monna alikuwa hapendi kumuona mume wake akose furaha hata siku moja mbele yake, Kakinga alisema kwa uchungu :-
KAKINGA ?? Umeona mke wangu sijui sisi tumemkosea nini mungu kila siku matatizo yapo kwetu tu daah na kwa hali hii tutaenda wapi ? Na akwelina tungemleaje kwa hali kama hii mke wangu ? Ni bora nimewapelekea wenye uwezo wamlee mke wangu ama kweli jasho lako ndio lako lakini jasho la mwingine mke wangu ni sumu liokope kabisa .
MONNA ?? Usijali mume wangu maisha ni kokote nipo tayari kulala nje ndani ya jiji hili kwa ajili yako nakupenda mume wangu sihitaji kingine katika maisha haya zaidi ya furaha yako.
Monna alimshika mkono mume wake wakasimama wakaondoka, Monna na mume wake walipita katika migahawa wakiomba kazi kwa bahati nzuri monna alipata kazi ya kuosha vyombo, Monna alipopata kazi alifurahi sana Kakinga akamwambia monna :-
“””””* Mke wangu kwakua Wewe umepata kazi endelea kufanya kazi Mimi naenda kutafuta kazi kwenye viwanda nitarudi jioni kama nikipata kazi na ukimaliza kazi nikukute stenti pale usitoke hadi nifike hapo pia usisahau kule chakula tangu jana hujala kitu mke wangu sawa *”””
Kakinga aliondoka akaenda kutafuta kazi. Muda ulizidi kwenda akwelina alizidi kulia katika eneo lile aliloachwa na Kakinga watu walimvuka na kumruka bila kumsaidia wala kumuokota, jua lilizidi kuwa kali likamchoma akwelina, akwelina alilia zaidi lakini hakupata msaada wowote. Baada ya muda mfupi kiongozi wa wanajeshi anayemtafuta sana mtoto akwelina alikuja na wanajeshi wake katika ofisi moja iliyokuwepo eneo hilo , Akwelina baada ya kulia sana akajitokeza msalia mwema mmoja bibi kizee akamuokota akwelina , yule bibi aliuliza kila mtu aliyekutana naye njiani lakini kila aliyemuuliza alimjibu hamtambui mtoto yule. Bibi kizee alitembea sana bila mafanikio kwa bahati nzuri akamuona yule kiongozi amevaa nguo za kijeshi bibi alifurahi sana akasema :-
“”””* Ahsante mungu kwa maana hii ni kesi kubwa ngoja nimpelekee yule askari wa kijeshi ili mtoto awe kwenye mikono salama *””””
Bibi alimfuata yule kiongozi alipomkaribia bibi alim….
Bibi alimfuata yule kiongozi alipomkaribia bibi alimpatia mtoto yule kiongozi yule kiongozi alishangaa sana baada ya kumuona bibi kizee anamletea mtoto kiongozi alimuuliza bibi :-
KIONGOZI ?? Samahani bibi kwanini umenipatia huyu mtoto wewe wanitambua Mimi ?
BIBI ?? Hapana Mjukuu wangu sikufahamu na hata huyu mtoto simtambui pia, Mimi nimemuokota huyu mtoto na nimejaribu kuwauliza watu wengi katika eneo hili, wote wananijibu hawamtambui ndio nilipokuona wewe umevaa nguo za jeshi la nchi nimekuletea nahisi atakuwa Sehemu salama akiwa kwako Mjukuu wangu dunia imeisha
KIONGOZI ?? Sawa upo sahihi bibi lakini sheria ni ngumu sana nakushauri nenda kituo chochote cha police kilichopo karibu yako ukawakabidhi wao hiyo ndio njia salama bibi .
Wakati kiongozi anaendelea kuzungumza na bibi alikuja mwanajeshi mmoja akasema :-
“”* Mkuu tumepata taarifa kuhusu yule mtoto kuna sehemu yupo *”””
Kiongozi hakutaka kuzungumza na bibi tena akaondoka haraka haraka kuelekea sehemu hiyo, bibi alianza kujilaum kwa kitendo alichofanya cha kumuokota akwelina. Yule kiongozi na kundi lake walifika katika eneo lililosemekana akwelina alikuwepo hapo wale wanajeshi waliwauliza watu wa eneo lile
“** Kuna bibi mmoja ndio alikuwa na huyo mtoto mnamzungumzia nilimuona huyo mtoto hapa toka majira ya asubuhi *”””””
Ilikuwa ni sauti ya muuza matunda maarufu wa eneo hilo akiwapatia Maelezo wale wanajeshi kuhusu mtoto, Kiongozi alimuuliza yule muuza matunda kuhusu huyo bibi , muuza matunda alimueleza kiongozi yule bibi alivyokuwa , kiongozi akamkumba huyo bibi ndio yule aliyemletea mtoto , kiongozi akaingia kwenye gari akarudi maeneo yale aliyemuona bibi huyo. Bibi alizidi kutembea huku na huko akiwa na mtoto mkononi ndani ya mji huo baada ya kutembea sana bibi alikutana na Kakinga akamwambia :-
“””* Kijana wangu nisaidie kumshika huyu Mjukuu wangu nataka nifunge nguo vizuri nimechoka sana *”””
Kakinga alitua mfuko wa Cement chini akamshika mtoto, bibi akaondoka zake , Kakinga akiwa amemshika mtoto alimuona bibi anaondoka kakinga akamfuata yule bibi akamziwia :-
KAKINGA ?? Bibi unakwenda wapi unaniachia Mjukuu wako ?
BIBI ?? Wala sio Mjukuu wangu huyo nimemuokota tu na nimetembea nae sana lakini sijamuona mwenye mtoto huyo na unavyoniona umri wangu huu huyo mtoto nitampeleka wapi lakini wewe bado Kijana unaweza kufanya kitu ili umsaidie mtoto huyo .
Bibi aliondoka kakinga alizidi kumsumbua bibi ili amchukue mtoto , bibi hakujali hilo akazidi kuondoka kakinga alikuwa bado hajamtazama vizuri mtoto yule kakinga akasema :-
“””” Jamani sasa hili ni balaa akwelina nilimuacha kule ili wasalia Wema wanjsaidie kumlea yaani leo leo hii tena nimeletewa mtoto mwingine hivi hii ni mikosi gani jamani mungu nimekukosea nini Mimi daaaah sijui nijiue aaaaah ??
Kakinga alilalamika sana akamtazama vizuri mtoto aliyepewa Kakinga alistuka sana kumuona mtoto yule ni akwelina aliyemtupa mbali, Kakinga alishindwa kuamini macho yake , Kipindi kakinga akiwa bado yupo katika mshangao mkali alisikia magari yamesimama mbele yake, alipotazama alimuona yule bibi aliyempatia akwelina akiwa na kiongozi wa wanajeshi, Kiongozi wa wanajeshi alisema :-
“”** Kijana ulidhani unaweza kunikwepa kamwe hautaweza katika maisha yako na vita hii umeyoinunua itakuponza naomba kwa wema tu niapatie huyo mtoto kabla sijakupiga risasi na huwezi kunikimbia leo *”””
Yule kiongozi akachomoa bastola yake akaweka risasi akamwambia kakinga amlete mtoto, Kakinga alimsogelea yule kiongozi aliyekuwa ndani ya gari kakinga alikuwa makini sana kipindi anamsogelea yule kiongozi kakinga alipofika karibu ya gari aliona njia upande wa kushoto kakinga alitimua mbio akiwa na akwelina mikononi mwake, Yule kiongozi akampiga kakinga risasi ya mgongo , kakinga akadondoka chini kakinga alijitahidi akasimama tena japo alikuwa na maumivu makali sana akaendelea kukimbia kakinga alijikongoja hadi kwa mke wake monna , Monna alikuwa anaendelea na kazi katika mgahawa ule alimuona mume wake kakinga anakuja akiwa anachechemea damu nyingi zinamtoka monna alimkimbilia mume wake Kakinga akamuona akwelina , Kakinga alimpatia monna mtoto akasema :-
“””* Kimbia na akwelina mke wangu watu wabaya wanakuja kumchukua usipate tabu kuhusu Mimi okoa maisha ya akwelina kwanza haraka ondoka mke wangu *”””””
Monna hakukubali kumuacha mume wake akajaribu kumnyanyua ili waondoke pamoja baada ya hatua chache monna na Kakinga walizungukwa na wanajeshi , Yule kiongozi alishuka kwenye gari akachomoa kisu akamfuata kakinga akamch………
Yule kiongozi alishuka kwenye gari akachomoa kisu akamfuata kakinga akamchoma kisu cha tumbo, Monna alitetemeka sana baada ya kumuona mume wake kakinga amechomwa kisu na yule kiongozi. Yule kiongozi alimvuta kakinga akamsogelea katika sikio akamwambia :-
KIONGOZI ?? Nilikwambia kijana huwezi kunikimbia ulijifanya wewe mjanja sana sasa mwisho wako ndio huu kufa mjinga wewe .
Kakinga akiwa amechomwa kisu tumboni aliona bastola katika mkanda wa yule kiongozi kakinga akachomoa ile bastola akamteka yule kiongozi wa wanajeshi, Wanajeshi walipoona kiongozi wao ametekwa waliweka silaha zao chini wakapiga magoti, kakinga japo alikuwa na maumivu makali sana alimshikilia vizuri yule kiongozi akaondoka nae, Kakinga akiwa na mke wake monna pamoja na yule kiongozi wa wanajeshi walizidi kuondoka walipofika mbali kakinga alimwambia yule kiongozi alale chini , yule kiongozi alilala chini kakinga akaweka ile bastola chini taratibu , Monna akamshika vizuri mume wake wakaondoka. Baada ya masaa matatu kupita wale wanajeshi walifuata njia ile aliyopita Kakinga wakamkuta kiongozi wao bado amelala chini wakamwita, kiongozi wao akasimama wanarudi kwenye magari yao wakapanda wakaondoka.
Kakinga na monna walienda mbali sana wakatokezea ufukweni mwa bahari , kakinga alishindwa kuendelea na safari kutokana na kutokwa na damu nyingi sana, kakinga alindoka chini akapoteza fahamu, Monna alilia sana baada ya kumuona mume wake amepoteza fahamu , Monna alimshusha akwelina akamuweka chini akaondoka kwenda kutafuta msaada, Monna alizunguka sehemu kubwa lakini hakupata msaada monna hakukata tamaa aliendelea kutafuta msaada kwa bahati nzuri akakutana na babu mmoja aliyekuwa anaishi hapo ufukweni mwa bahari monna alimuomba msaada yule babu , Yule babu alikubali kumsaidia monna akachukua baadhi ya dawa kutokana na Maelezo ya monna akaondoka nae walipofika yule babu alikuwa mtaalamu alimtoa risasi kakinga akamchoma kile kisu alafu akamshona sehemu zote alizopata majeraha baada ya tiba yule babu pamoja na monna walimnyanyua kakinga wakaondoka kuelekea katika nyumba ya huyo babu, kipindi wanaondoka babu alisema :-
BABU ?? Mbona mtoto umemuacha ? hujui sehemu hii sio nzuri kuna baridi Kali .
MONNA ?? Tuondoke tu babu huyo mtoto sio wangu nilimuokota tu na huyo mtoto katuletea matatizo makubwa sana Mimi na mume wangu huyu bila wewe mume wangu angepoteza maisha kwa sababu ya huyu mtoto nimegundua kile alichonieleza mume wangu ni sahihi.
Monna akaenda bila kujali kile babu alichomwambia kuhusu mtoto ( akwelina ) Nyumba ya babu haikuwa mbali na bahari, walipofika walimlaza kakinga nje ili apate hewa safi. Kakinga alilala nje hapo hadi majira ya usiku akarudisha fahamu , Monna alifurahi sana kumuona mume wake alirudisha fahamu monna alimkumbatia mume wake kwa furaha, babu akatoka nje kakinga akamsalimia babu alafu akamuuliza monna :-
KAKINGA ?? Mke wangu tupo wapi hapa na huyu babu ni nani ?
MONNA ?? Huyu babu ndiye aliyesaidia maisha yako na hapa ni nyumbani kwake mume wangu .
KAKINGA ?? Ahsante sana babu kwa msaada wako mungu atakulipa kwa Wema uliyonifanyia alafu Akwelina yupo wapi au amelala ?
MONNA ?? Aaaaah sahau kuhusu akwelina nilishindwa kukusikia mwanzo leo hii kidogo nikupoteze mume wangu kwa ajili ya mtoto yule nimemtupa mbali sana huko .
KAKINGA ?? Weeee Unasemaje siwezi kukuelewa nasema hivi ili tuelewane nenda sehemu uliyomtupa akwelina uniletee hapa sasa hivi.
Kakinga na monna waligombana kwa muda mrefu mwisho monna akakubali akamfuata akwelina akamkuta amefunikwa na uchafu wa bahari nguo alizokuwa amevaa akwelina zote zilikuwa zimerowa na maji, Monna japo alikuwa ameanza kumchukia akwelina lakini alimuonea huruma sana kwa sababu akwelina alikuwa anatetemeka sana, Monna alimtoa akwelina zile nguo mbichi akamfunika kanga aliyokuwa nayo. Monna akarudi nyumbani akiwa na akwelina , Alipofika nyumbani kakinga alifurahi sana kakinga akambusu akwelina kwa furaha. Baada ya wiki moja kupita majira ya usiku kakinga alimwita mke wake akamwambia :-
“”* Mke wangu hebu niletee vile vitu tulivyomkuta navyo akwelina *”””
Monna alimletea Kakinga vitu alivyohitaji alafu akaenda jikoni kupika , Kakinga aliona kitabu kidogo akakiweka pembeni , akaona mfuko mweusi umefungwa vizuri Kakinga alihitaji kuufungua ule mfuko lakini akasita akauweka pembeni mwisho akaona bahasha juu ya bahasha ile kulikuwa na michirizi ya damu, kakinga akaifungua ile bahasha akaona picha nyingi zipo ndani ya ile bahasha kakinga alipoziangalia zile picha aliona sura mbalimbali ikiwepo na sura ya yule kiongozi, Kakinga alizidi kuzitazama zile picha, picha ya mwisho kakinga alimuona Madam ( mama yake mdomo monna ) kakinga alistuka sana akajiuliza Kwanini zile picha awekewe akwelina , Kakinga alishindwa kuelewa kabisa akazirudisha zile picha ndani ya bahasha akashika uke mfuko mdogo mweusi akaufungua ndani ya mfuko aliona vitu kama mawe mdogo madogo yanang’aa sana Kakinga alipotazama vizuri akagundua yale sio mawe ya kawaida ni …..
Kakinga alipotazama vizuri akagundua yale sio mawe ya kawaida ni mawe yenye madini ndani yake , kakinga alizidi kuyashangaa yale mawe yale mawe yalikuwa mengi sana kakinga aliyageuza geuza akagundua mawe yale yalikuwa ni almasi Kakinga japo aligundua kuwa zile ni almasi lakini hakuwa na uhakika wa kutosha kakinga alichukua jiwe moja akamfuata yule babu , Babu alikuwa kandokando ya bahari anavua samaki babu alikuwa anapenda kufanya hivyo kila siku majira ya usiku Kakinga alipofika kwa babu alikaa karibu yake kakinga akamuuliza babu :-
KAKINGA ?? Hivi babu kwanini unaishi huku ufukweni peke yako wewe hauna familia ?
BABU ?? ???? Unanifanya nifurahi sana kijana wangu , Unazungumzia familia Mimi nilikuwa na familia yangu na nilikuwa na pesa za kutosha nakumbuka mwaka 1943 Nilipokuwa kijana mwenye umri kama wako Maisha yangu yalikuwa magumu sana kwa sababu nilikuwa sina baba wala mama Mimi nimelelewa katika vituo vya watoto yatima tu, Nilipokuwa kijana ninayejitambua niliwafuata wale walezi wa kituo cha watoto yatima nikawauliza historia ya maisha yangu daaah walinijibu kwamba hawajui Mimi nilitoka wapi kwa sababu walinikuta nje ya kituo chao nikiwa mtoto mdogo sana. Ukweli sikuridhika na majibu ya wale walezi wetu ikanibidi nimfuate mkuu wa kituo kile nilipofika kwa mkuu wa kituo alinikaribisha vizuri nikamuomba historia ya maisha yangu nilipewa majibu yale yale kama niliyopewa mwanzo lakini akaenda chumba cha kuhifadhi kumbukumbu za watoto wote wanaoishi pale akarudi na mfuko akanipatia akaniambia waliniokota na mfuko ule labda nikague naweza kugundua kitu niliuchukua ule mfuko nikarudi chumbani kwangu, Nilipoufungua ule mfuko nilikuta kuna picha mbili ya mwanamke na mwanaume nyuma ya zile picha zilikuwa zimeandikwa MAMA na BABA , Kwa haraka haraka niligundua wale watakuwa ni wazazi wangu nilitokwa na machozi mengi sana kwa kuwaona wazazi wangu kwa kupitia picha , niliendelea kukagua vitu ndani ya mfuko ule nikaona mfuko mweusi umefungwa vizuri nilipoufungua ule mfuko mweusi nikakuta kuna almasi nyingi sana nilitetemeka sana nikaficha ule mfuko japo nilikuwa nipo peke yangu chumbani, nikaurudisha ule mfuko kwa hofu kipindi naurudisha niliona kitabu kidogo nilichukua kile kitabu nilipokifungua nilikutana na historia nzima ya maisha yangu , kitabu kile alikiandika baba kabla hajapoteza maisha nililia sana daaah unanikumbusha machungu niliyoyapata kijana wangu ??????.
KAKINGA ?? Pole sana babu Nisamehe kwa kukumbusha mambo yaliyopita .
BABU ?? Usijali kijana wangu nili…niliii… Daah niligundua wazazi wangu waliuwawa kutokana na Mali walizokuwa nazo kuna kundi limejitengeneza na lina nguvu sana hadi ndani ya serikali yetu wapo watu hao kila sehemu wapo watu hao kazi yao ni kuwanyanganya watu Mali zao ardhi na kuwapoteza duniani, Niliumia sana nilitamani kulipa kisasi kwa watu hao lakini nilishindwa niliamua kuuza zile almasi nikafunga ndoa na nikajaliwa watoto watatu. Siku moja nikiwa na familia yangu nilivamiwa na watu nisiowajua wakambaka mke wangu alafu wakamchinja mke wangu pamoja na watoto wangu mbele ya macho yangu niliumia wakaninyanga Mali zangu zote. Wakanipiga risasi wakajua nimekufa wakanitupa baharini nilisaidiwa na mtu nisiyemjua maisha yangu yakaishia hivyo hadi leo na walikuwa wananitafuta kwa kutumia alama hii.
Yule babu alivua shati lake akamuonesha Kakinga alama ile kakinga alistuka kumuona babu ameandikwa neno AKWELINA katika mgongo wake kama alivyo andikwa mtoto waliyenaye hadi leo. Kakinga akiwa na hofu kubwa alimuuliza babu :-
KAKINGA ?? Hiyo alama inamaana gani babu ?
BABU ?? Hii sio alama ni jina la huyo mshenzi anayeendesha kundi la hao watu na niliandikwa na wazazi wangu walitambua siku moja nitaweza kulipa kisasi lakini siwezi kutokana umri wangu huu lakini ninaamini ipo siku mungu ataleta mtu wa kuja kuwatoa hao mashetani kwa sababu kila siku wanazidi kuwatesa watu wasio na hatia na niligundua waliniwekea kifaa maalumu kilichokuwa kinawapatia taarifa sehemu yeyote nilipokuwepo walikiweka hapa katika mkono wa kulia kwamba huwezi kuwakimbia .
Kakinga aliposikia maneno yale toka kwa babu alikimbia haraka kumfuata akwelina ndani akamkuta amelala kakinga akamfunua nguo akwelina akamkagua katika mikono yote miwili akaona kovu katika mkono wa kushoto kakinga alipotazama vizuri akaona kuna kitu kinatoa mwanga mwekundu ndani ya kovu lile. Kipindi kakinga anashangaa kile kitu alisikia mlio wa risasi nje kakinga akatoka nje akamuona babu amedondoka ndani ya maji kwa mbali akaona meli ndogo inakuja ikiwa na wanajeshi kakinga ali………
Kakinga alirudi ndani haraka haraka akambeba akwelina akamweleza mke wake wapo katika hatari kubwa sana, Monna alianza kutetemeka , mapigo ya moyo walimwenda mbio Monna , Kakinga alitoka nje tena baada ya kukumbuka vitu walivyomkuta navyo Monna alivisahau nje. Wale wanajeshi walizidi kusogea sehemu alipokuwa kakinga na mke wake Monna , Kakinga alikaza moyo akamshika mkono mke wake.
“”” Kuwa jasiri mke wangu tupo sehemu hatari maisha yetu yapo hatarini lazima uwe na nguvu ili tumsaidie akwelina “””
Yamekuwa maneno ya kakinga akimwambia mke wake Monna ili kumpatia nguvu na faraja kwa sababu kakinga aligundua mke wake anatetemeka sana baada ya kumshika mkono, Maneno ya kakinga yaliupatia nguvu ya kutosha moyo wa Monna, Kakinga hakuhitaji kupoteza muda akatoka nje akiwa amemshika mkono Monna mke wake walitoka taratibu kakinga akachukua vile vitu walivyomkuta navyo akwelina kwakua kakinga alikuwa na wasiwasi sana alidondosha mfuko uliokuwa na almasi ndani yake, Walifanikiwa kutoka sehemu hiyo hatari kakinga na monna walipofika mbali wakajificha wakawaona wale wanajeshi wanauchukua mwili wa babu wakauchoma moto pamoja na nyumba yake masikini kitendo kile kilimuuma sana kakinga, Kakinga na monna wakiwa wamejificha eneo hilo walisikia sauti kali ikilia karibu yao kakinga alijaribu kuitafuta sauti ile ilipokuwa inatoka akagundua ilikuwa inatoka katika mkono wa akwelina.
Walipotazama mbele yao waliwaona wale wanajeshi wanakuja eneo walilokuwepo wakiwa na kitu chenye mfano wa simu katika mikono yao kakinga akamshika mkono mke wake wakakimbia. Safari yao ilikuwa ndefu sana Kwa bahati nzuri walifanikiwa kuwakimbia wale wanajeshi na ule mlio ulikuwa unatoka katika mkono wa akwelina uliacha kulia. Walimshukuru mungu kisha wakaendelea na safari japo walikuwa hawajui wapi wanapoelekea walitembea Kwa muda mrefu monna alikuwa amechoka sana akamuomba mume wake watafute sehemu wapumzike , kakinga alimsikiliza mke wake wakapumzika , Walipokuwa wamepumzika kakinga alimsimulia mke wake yote aliyozungumza na babu kule ufukweni, Monna alishangaa sana akamwangalia akwelina katika mkono wake akagundua ni kweli alichoambiwa na mume wake.
Monna alimuomba mume wake kakinga wampeleke akwelina hospital wakamtoe hicho kitu katika mkono, Kwakua walikuwa hawana pesa Monna alichukua cheni aliyopewa na marehemu mama yake akauza pesa walizopata wakaenda hospital walipofika daktari alimfanyia vipimo akwelina alafu akawaambia :
DAKTARI?? Ni kweli mtoto wenu anakifaa mkononi na hiyo ni GBS kifaa maalumu kinachotoa taarifa popote mtoto huyu atapokuwepo hiyo ni Moja , Mbili kifaa hicho kimewekwa kitaalamu sana kimeungwa kupitia mifipa ya fahamu sasa katika upasuaji wa mtoto huyu kuna matukio mawili KUFA au KUPONA kama mpo tayari niwaletee mkataba tunahitaji sahihi ( sign ) zenu .
Kakinga na monna walitazamana sana kakinga akasema …..
Kakinga na monna walitazamana sana kakinga akasema :-
KAKINGA ?? Fanya upasuaji dakatari naomba huo mkataba niweke sahihi .
MONNA?? ?? Hapana mume wangu hapana mtoto akifa ?
KAKINGA ?? Huwezi kuiziwia roho ya mtu kama muda wake umefika mke wangu tumuachie mungu kwa hili. Daktari Fanya kazi yako .
DAKTARI ?? Sawa nisubirini .
Daktari alitoka nje dakika kadhaa alafu akarudi ndani ya chumba chake akiwa na karatasi mkononi alipofika akampatia karatasi ile kakinga , Kakinga bila hofu alichukua kalamu alipotaka kuweka sahihi Monna alishika mkono wa mume wangu, kakinga alipomtazama mke wake alimuona amejawa na wasiwasi mkubwa, Kijasho chembamba kilikuwa kinamteremka Monna. Kakinga aliweka chini ile kalamu akamtazama Monna kwa muda mrefu sana alafu akamwambia :-
“””* Mke wangu wewe ndio mama wa mtoto huyu na siku zote mama huwa hakubali kumpoteza mtoto wake, Mama yupo tayari kuyapoteza maisha yake kwa ajili ya kupambania maisha ya mtoto wake na siku zote tiba ya kweli ya mtoto ni nafsi ya mama kama mama hujaridhia kwa mtoto kamwe kitu hicho hakiwezi kufanikiwa , samahani daktari kwakua mama amepinga jambo hili basi naomba tuondoke .
Kakinga alisimama akampatia Monna mkono ili waondoke Monna alifikiria sana akachukua ile kalamu akampatia kakinga, kitendo hicho kilimpatia faraja kakinga akaweka sahihi katika karatasi zile. Daktari alichukua zile karatasi akaziweka pembeni , akamchukua akwelina akaenda nae maabara. Daktari alichukua muda mwingi sana katika upasuaji huo , hali hiyo ilimpatia wasiwasi mkubwa Monna , Monna alikuwa anazunguka huku na huko ndani ya chumba cha daktari. Baada ya masaa sita kupita daktari alirudi :-
“””* Ndugu zangu tumshukuru mungu nimefanikiwa kufanya upasuaji salama wa mtoto wenu kwahiyo kuna dawa mnazotakiwa kununua.
Kakinga alimshukuru sana dakatri yule. Akwelina alitumia muda mrefu sana kupona hali iliyowatesa sana kakinga na mke wake Monna kutokana na kipato chao. Baada ya miezi mitatu akwelina alipona daktari aliwaruhusu warudi nyumbani lakini daktari alikuwa anamtazama sana Monna walipokuwa wanataka kuondoka daktari alimuuliza Monna :
DAKTARI ?? Samahani mnaishi sehemu gani ?
MONNA ?? Ni historia ndefu sana kifupi Mimi na mume wangu hatuna sehemu ya kuishi maisha yetu ni magumu sana .
DAKTARI ?? Ooh poleni sana na kwa hali ya mtoto anatakiwa apate chakula kizuri na sehemu safi kwakua umesema hamna sehemu ya kwenda basi Mimi nitawasaidia tutaenda sote kwangu mtaishi kwangu hadi mtapopata makazi yenu jina langu naitwa PATRICK .
Hakika ilikuwa ni furaha kwa kakinga na mke wake monna, waliendelea kumsubiri Dr Patrick katika chumba chake hadi alipomaliza kazi zake, Patrick alipomaliza kazi aliwachukua wakaenda hadi nyumbani kwake, Maisha yalianza kuwa matam na mazuri kwa kakinga na monna. Wanasema mapenzi ni kitu cha ajabu sana hiyo ilimkuta Patrick baada ya kuishi na familia ya kakinga taratibu taratibu Patrick alianza kuvutiwa na monna kutokana na uzuri aliokuwa nao , Monna alikuwa Mrembo sana baada ya kupata matunzo hali iliyosababisha Patrick kushindwa kuziwia hisia zake. Kwakua Patrick alishindwa kumwambia ukweli monna , Patrick alikuwa anamletea zawadi mbalimbali zenye thamani mno, kakinga alianza kuwa na mashaka kwa mke wake. Siku moja Patrick hakwenda kazini siku hiyo ilikuwa ni siku ya mapumziko. Monna alimka mapema sana siku hiyo kwakua alitambua Patrick yupo nyumbani , monna akiwa jikoni akiandaa chai Patrick alimfuata monna jikoni wakati huo monna alikuwa hajatambua kama Patrick yupo nyuma yake , Patrick alimshika kiuno monna , Monna alisisimka sana akageuka kumwangalia aliyemshika kiuno ni nani akashangaa kumuona ni Patrick monna ali……….
Monna alishikwa na aibu ya ajabu sana monna akabaki kutazama chini muda wote, Patrick alijisogeza karibu zaidi kwa monna akamshika mkono , Mapigo ya moyo ndani ya mwili wa monna yalikuwa yanakwenda mbio zaidi ya siku zote, Patrick alipogundua monna anatetemeka alitumia nafasi hiyo hiyo akamsogeza mdomo wake karibu ya sikio la monna akasema :-
?? Monna unajua wewe ni mrembo sana na hakika nimeshindwa kuziwia hisia zangu juu yako, kweli natambua umeolewa na pengine mume wako unampenda sana lakini nami ni binadamu pia naomba usinifikirie vibaya hizi ni hisia zangu kwako nipo tayari kufanya chochote utachohitaji katika dunia hii nakupenda monna naomba nipe nafasi japo theluthi nikuoneshe jinsi gani ninavyokupenda nakutakia asubuhi njema andaa chai vizuri nakupenda monna ??
Patrick baada ya kumwambia maneno hayo monna alimsogelea zaidi monna , monna hakuwa jasili akafumba macho , Patrick alitumia nafasi hiyo akahitaji kumpiga busu monna lakini kabla hajaufikia mdomo wa monna walisikia sauti ya kakinga akimwita mke wake , Patrick akaondoka jikoni haraka alitumia mlango wa nyuma kwa sababu jiko hilo lilikuwa na milango miwili tofauti , Kakinga alipoingia jikoni alimuona mke wake monna ana wasiwasi uliopitiliza kakinga alijaribu kjmuuliza monna lakini monna hakuzungumza kitu.
Siku zilizidi kwenda tabia ya Patrick kumletea zawadi monna haikuisha kila kukicha Patrick alizidi kumjali monna Kwa kumpatia fedha na vitu vikubwa zaidi. Siku iliyofuata kakinga alikuwa na monna sebuleni wanacheza na akwelina Patrick aliingia akiwa na boksi mbali za simu mkononi mwake kakinga aliwapatia simu wote, Daah kakinga alifurahi mno Kwa sababu katika maisha yake yote hakuwahi kumiliki simu. Yalipofika majira ya usiku simu ya monna iliita monna alipoitazama aliona namba mpya , Monna akapokea simu
?? Monna ni mimi Patrick kuna zawadi nimekununulia ipo nyuma yako ichukue hiyo kesho naomba kutoka na wewe peke yake kuna sehemu nahitaji twende kama hautojali *””
Monna aligeuka akaona mfuko alipofungua alikuta nguo nzuri sana , Monna alifurahi sana akamkubalia Patrick ombi lake . Siku iliyofuata asubuhi na mapema kakinga alimuaga mke wake kuna sehemu alituma maombi ya kazi, Monna kwakua hakuhitaji mume wake ajue safari yake na Patrick alifurahi. Muda ulizidi kwenda yalipofika majira ya mchana Patrick alichukua gari lake akamchukua monna , wakamuacha akwelina ndani peke yake akiwa amelala , Safari yao ilichukua muda kiasi hatimae wakafika sehemu husika hakika eneo lile lilikuwa linavutia sana , wakati monna anashangaa eneo lile Patrick alimkumbatia monna akamwambia :-
“”” NAKUPENDA MONNA nipe nafasi tafadhali “”
Monna alimgeukia Patrick Kwa macho ya kimahaba aka….
Monna alimgeukia Patrick Kwa macho ya kimahaba akajaribu kuzungumza maneno ambayo Patrick hakuyaelewa kabisa :
~~ Patrick mmmh unajua mimi daah sijui nifanyaje mimi Patrick unanipatia wakati mgumu daah .
Yalikuwa ni maneno ya monna akijing’atang’ata mbele ya Patrick, wakati wote huo Patrick alikuwa anamsoma monna aligundua monna hawezi kumkubalia kile alichohitaji kwa sababu monna alikuwa hajiamini pia monna alikuwa na wasiwasi uliotawala mwili na akili yake , Patrick hakuchoka akamvuta monna , monna alikuwa laini zaidi ya bamia monna alijikuta yupo katika kifua cha Patrick , Monna akiwa kifuani kwa Patrick, Patrick alisema :-
“”* Mungu kweli fundi muda aliopoteza wakati anakuumba wewe ninaamini hakujutia, Monna moyo wangu unaomba kuzungumza na wewe tafadhali zungumza na moyo wangu “”
Patrick alishika kichwa cha monna akamgeuza sikio la monna lilituwa upande wa kushoto mwa kifua cha Patrick monna aliyasikia mapigo ya moyo wa Patrick yanapiga kwa kasi sana Patrick alishika kichwa cha monna kwa Mara ya pili alafu akayatazama macho ya monna kwa muda mrefu sana, monna alishindwa kumtazama Patrick , Patrick akatumia nafasi hiyo akasogelea midomo ya monna alipoigusa tu monna akamsukuma Patrick , Patrick alidondoka chini monna aliogopa sana akamfuata Patrick akamuomba msamaha, Patrick alimwambia monna asijali lakini bado Patrick alikuwa analilia penzi kwa monna. Monna alisema :-
MONNA ?? Nisamehe Patrick kwa kukusukuma nimesikia ombi lako na usijali nipatie muda nitakujibu tafadhali vuta subira .
Patrick alifurahi sana kusikia maneno yale kutoka kwa monna, Patrick akamchukua monna wakapanda kwenye gari wakaenda sehemu nyingine. Kakinga alitoka katika ile kampuni aliyoomba kazi alitamani sana kumnunulia mke wake zawadi lakini kakinga hakuwa na pesa yeyote , kakinga alifikiria njia rahisi inayoweza kumpatia pesa kwa muda ule kwa ajili ya kumnunulia zawadi mke wake kipenzi, kakinga akaona bora aigize kama mlemavu ili apate pesa za kumnunulia zawadi mke wake baada ya kupata wazo hilo kakinga alifanikiwa kupata pesa kwa muda mfupi akachukua zile fedha akaenda kununua viatu kwa ajili ya mke wake, Kakinga aliporudi nyumbani alikuta nyumba imefungwa cha ajabu alisikia sauti ya mtoto ndani analia kakinga alichungulia dirishani akamuona akwelina analia akiwa chini , Kakinga alichanganyikiwa sana kakinga alitafuta njia ya kuingia ndani akaikosa ikabidi avunje dirisha akaingia ndani akamkuta akwelina amedondoka chini damu zinamtoka puani.
Kakinga alishikwa na hasira sana akampatia huduma ya kwanza akwelina alafu akatoka nje ya nyumbani ile akakaa chini . Muda ulikwenda sana hatimae usiku ukaingia kakinga akiwa ndani ya giza nene kwa sababu hakuwasha taa lolote katika nyumba ile alimuona Patrick anafungua geti akiwa na monna, Patrick akiwa amemshika kiuno monna waliingia ndani monna akiwa na furaha sana , walipoona giza monna akasema :
MONNA ?? Mbona giza hivi au mume wangu hajarudi ?
PATRICK ?? Aaah yule ni mwanaume buana atarudi tu kwani mimi sio mume wako ?
MONNA ?? Usijali nawe siku moja utakuwa mume wangu hata sio mbali washa taa ya simu tuingie ndani basi .
PATRICK ?? Subiri kidogo monna kwani unawahi nini huko ndani sasa siingii ndani hadi unipige busu la nguvu kama sivyo nalala nje hapahapa .
MONNA ?? Jamani Patrick sawa sogea nahofu mume wangu asije nikuta lakini si nilikuambia nipe muda ila usijali busu tu sawa.
Patrick alifurahi akamvuta karibu monna akamshika kiuno kimahaba alafu akambusu kwenye shavu , baada ya hapo wakasogea karibu ya nyumba Patrick akawasha taa ya simu yake ule mwanga wa taa ulipowaka walimuona kakinga amekaa karibu na mlango monna ali……..
Ule mwanga wa taa ulipowaka walimuona kakinga amekaa karibu na mlango, monna alistuka sana:
“”* Mume wangu kumbe upo jamani nisamehe mume wangu tulikuwa mbali kwenye vikao , Patrick aliniomba nikamsaidie kazi Kwa sababu wewe uliondoka mapema sana .
Yalikuwa ni maneno ya monna akijaribu kumuelezea mume wake kakinga, Kakinga alimtazama sana monna hali iliyomfanya monna atetemeke kakinga akasema :
KAKINGA ??Na huko kushikana viuno na kupigana mabusu ni moja ya kazi za ofisini huko mlipokuwa ?
MONNA ?? Jamani mbona wanifikiria vibaya lakini nakuomba mume wangu tuliza hasira nisamehe kwa nilichofanya mbele yako najua umenitafsiri vibaya lakini sio kweli hicho unachofikiria kwa sasa.
KAKINGA ?? Sawa na vipi kuhusu mtoto kwanini usiondoke nae je kama ungemkuta kapoteza maisha unamuona alivyopata majeraha yote kwa ujinga wako.
PATRICK ?? Nisamehe mimi kaka kwa sababu mimi ndio nilimuomba niondoke nae na nilifahamu tutawahi kurudi lakini kwa bahati mbaya tumechelewa nisamehe mimi.
Siku zote kakinga huwa ni mwelewa sana japo alihisi kuna kitu kinaendelea baina ya Patrick na mke wake monna, kakinga alicheka sana akasema :-
KAKINGA ?? Hahaha ?? acha uoga mke wangu mimi nakuamini siwezi kuweka hofu kwako japo umeniudhi kwa kumuacha mtoto ndani si unajua nampenda sana mtoto wangu .
Monna na Patrick walishusha pumzi nzito baada ya kusikia maneno hayo toka kwa kakinga, Kakinga akamshika mkono mke wake wakaingia ndani walipofika ndani walisha taa Patrick aliona dirisha limevunja kakinga akamueleza hali iliyokuwepo. Siku baada ya siku ukarimu wa monna na Patrick ulizidi kuwa karibu zaidi, Kakinga alikuwa anaona yote hayo lakini alikuwa mkimya sana, Patrick hakuchoka kumletea monna zawadi mbalimbali kama kawaida yake kutokana na ukaribu huo, Monna alianza kumpenda Patrick. Siku baada ya siku monna alijikuta yupo busy sana na Patrick kuliko mume wake .
Kakinga hakuchoka kumchunguza mke wake, Baada ya siku mbili kupita monna alijikuwa nyumbani anafanya usafi siku hiyo Patrick alirudi nyumbani mapema akamkuta monna anafanya usafi monna alipomuona Patrick aliacha kufanya usafi akamkumbatia Patrick cha ajabu monna akambusu Patrick alafu akaondoka, Patrick alifurahi sana akasema :-
“”* Kazi imekwisha kilichobaki ni kufanya kitu ambacho nakihitaji toka kwake wooooooooh hahaha.
Patrick akaingia ndani kwake yote yalikuwa yanatendeka kakinga alikuwa anayaona akiwa nyuma ya ukuta, Roho ilitaka kupasuka kwa maumivu aliyokuwa nayo kakinga kwa sababu kakinga alikuwa anampenda sana mke wake. Usiku ulipofika wakawi katika meza ya chakula monna macho yake yote yalikuwa kwa Patrick bila kujali kakinga yupo nae eneo hili kitendo hicho kilimfnya kakinga aache chakula akaondoka , Monna alipoona kakinga kaondoka alifurahi sana akamsogelea Patrick akawa anamtania kwa kumtekenya tekenya yote hayo kakinga alikuwa anayashuhudia, Kiukweli kakinga alishindwa kuvumilia maumivu hayo.
Yalipofika majira ya asubuhi kakinga aliamka mapema sana akakusanya nguo zote akazifunga vizuri kakinga akamuamsha monna , monna alipoamka alimshangaa mume wake kakinga akamshika mkono monna wakatoka nje japo monna alikuwa hataki walipofika sebuleni wakammuta Patrick monna akamshika mkono Patrick kakinga akasimama akamuuliza monna :-
KAKINGA ?? Chagua Mona monna kuondoka na mimi au kubaki na Patrick ?
Cha ajabu monna ali…
Cha ajabu monna alitoa mkono kwa kakinga alafu akasogea kwa Patrick, Kakinga aliishiwa nguvu akadondosha begi la nguo alilokuwa ameshika , Ilikuwa ni ngumu sana kuamini kile anachoona mbele yake !
“”””””*” Nisamehe sana kakinga “”””*
Moyo wa kakinga ulizidi kwenda mbio kwa kusikia leo Monna kwa Mara ya kwanza anataja jina hilo , kakinga alizoea kuitwa mume , mpenzi na baba watoto hasira alizokuwa nazo kakinga zilimfanya ashikwe na kizunguzungu , kakinga alishika kichwa chake kwa muda mrefu kiasi Monna hakumuonea huruma kakinga akaendelea kusema:
MONNA???? Naomba msamaha tena mbele yako kwa kufanya hiki ninachofanya katika maisha yako , Najua nimetoka mbali na wewe na umenivumilia kwa mambo mengi sana, Kakinga hadi sasa nimeishi na wewe kwa miaka mingi zaidi ya sita bado hali yako sio nzuri kimaisha nimekuvumilia sana kakinga lakini bado unahali mbaya ya kimaisha , kula kwetu tabu , kuvaa tabu hatuna sehemu ya kuishi daah nimechoka kakinga naomba taraka yangu leo hii hii na nitakurudishia pesa yako ya mahari. Mimi nahitaji mwanaume mwenye pesa miaka zaidi ya sita hata mtoto sina na sijapata hata kichefuchefu sasa hebu niambie napata faida gani kwako ?
PATRICK ?? Heeeeh !!?? yule mtoto sio wako ?
MONNA ?? Nizae wapi huyo mtoto nimemuokota tu hata sio wangu pia huyu mwanaume nikiwa nae ndani anakuwa mvi…
KAKINGA ?? Basiiiiiiiiii monna ?? unapokwenda sipo ni kweli upo sahihi Mimi sio mzima siwezi kuzalisha si ndiyo ? Na pia Mimi masikini sana lakini tatizo kwanini haukuniambia mapema laiti ungeniambia mapema nisingeruhusu moyo wangu ukupende kiasi hiki , Monna nakupenda mke wangu mtoe shetani kichwani naomba shika mkono wangu huu twende tukatafute maisha nakupenda monna siwezi kupinga hili kweli nakupenda.
Pamoja na kakinga kutetea penzi lake haikusaidia kitu monna aliingia ndani baada ya muda alitoka nje akiwa ameshika karatasi pamoja na kalamu akampatia kakinga, Monna akaomba taraka . Kakinga alifikiria sana mwisho akaamua kuchukua maamuzi magumu akaandika taraka wakati anampatia taraka kakinga alimwangalia sana monna machozi yakiwa yanamteremka alisema :-
“” Monna kwa sasa upo huru nimefanya hivi kwa sababu wewe umetaka hivyo nilikuahidi kwamba nitafanya chochote ili uwe na furaha hata kama kitaniumiza Mimi lakini wewe uwe na furaha milele chukua taraka yako monna lakini kumbuka “” Kimvuli chako ndio rafiki yako kipenzi popote utapokuwepo hakiwezi kukuacha lakini ukiwa gizani kamwe hautakiona , Patrick ndugu yangu nakukabidhi binti huyu naomba mpende kweli usimdanganye kwa sababu maumivu ya mapenzi leo nimeyafahamu hakika mapenzi yanauma sana kwaheri monna.
Kakinga alirudi ndani akatoka na akwelina akiwa amelala akamtazama tena monna masikini kisha akaondoka. Maneno aliyosema kakinga yalimpatia mawazo sana monna lakini, Patrick akamshika mkono monna wakarudi ndani. Kakinga akiwa na akwelina mgongoni hakutambua aende wapi masikini , Kakinga alitembea huku na huko akiwa na mawazo yaliyotawala fikra zake, Kakinga alijikuta yupo barabarani hadi majira ya usiku kutokana na kutembea sana akwelina alikuwa amechoka sana akaanza kulia hali iliyomfanya kakinga atambue akwelina atakuwa anataka kula kakinga alienda kuuza simu aliyonunuliwa na Patrick akapata pesa akamnunulia chakula akwelina.
Majira hayo hayo monna akiwa ndani pamoja Patrick, Patrick alikuwa huru katika mwili wa monna usiku huo Patrick aliutawala mwili wa monna atakavyo , Monna nae hakuwa mchoyo alimpatia chochote alichohitaji Patrick wakiwa katika mambo hayo maneno ya kakinga yalijirudia katika masikio ya monna , monna akabadirika ghafla hali iliyomfanya Patrick alazimishe kufanya mapenzi na monna , Monna hakukubali kufanya mapenzi kwa nguvu Patrick akachukia akatoka kitandani akafungua kabati akachukua bastola akamnyoshea monna kisha ……..
ITAENDELEA
0 comments:
Post a comment
Umependezwa Na Makala Uliyoisoma? Tuachie Maoni yako Hapa Chini. Endelea Kufurahia Makala Zingine Zinazotolewa Na Blog Hii.