AKWELINA - 4
Simulizi : Akwelina
Sehemu Ya Nne (4)
KAKINGA: Sawa Daktari naomba linda uhai wa mke wangu narudi sasa hivi Kaka yangu .
DAKTARI: Sawa jitahidi kuwahi .
Kakinga alipanda kwenye gari lake moja kwa moja hadi nyumbani akamkuta Monna anampatia Akwelina chakula Kakinga alipitiliza hadi chumbani kwake, Monna alisimama akafunga mlango mkubwa alafu ufunguo akauchomoa akauficha ndani ya sidilia yake , Kakinga alichukua pesa za kutosha haraka haraka akatoka nje ili kuwahisha fedha Hospital, Kakinga alipoufikia mlango cha ajabu mlango ulikuwa umefungwa Kakinga alijaribu kufungua mlango kwa pupa lakini mlango haukufunguka Monna akamsogelea Kakinga akamwambia: Kakinga leo huondoki ufunguo ninao Mimi nina maongezi na wewe Kakinga na nahitaji majibu mazuri laaa sivyo sikupi ufunguo .
Kakinga aligeuka kwa hasira kisha akasema: ?? Unasemaje wewe naomba nipatie ufunguo haraka , huu sio muda wa matani Monna hali ya Warda sio nzuri na ninahitajika nipeleke pesa kwa matibabu yake nipatie ufunguo haraka Monna .
MONNA : Mimi sijali hilo Kakinga na bora afe tu ili nikupate kijana ninaekupenda kuliko unavyofikiria, siwezi kukubali Kukupoteza kwa hali yeyote Kakinga wangu nakupenda .
Kakinga alizidi kushikwa na hasira akasema kwa sauti ya juu : Nipatie ufunguo monnaaaaaaa sina muda wa kupoteza mjinga wewe ??
Monna hakujali akajibu : Sikupi Ufunguo na fanya utakavyo lakini sikupi ufunguo hadi ufanye nitakacho usinitishe ufunguo hauta upata na nikuambie ukweli ufunguo upo katika nguo zangu nimeuficha lakini ndio huwezi kuupata Kakinga wangu .
Kakinga alishikwa na hasira zaidi akamfuata Monna akampiga kibao alafu akamkagua katika nguo zake ili achukue ufunguo, Monna nae hakukubali kukaguliwa, Vurugu iliendelea kwa muda mrefu sana , wakati vurugu zinaendelea Akwelina hakuwa mbali nao , Kakinga alishindwa kuvumilia akamsukuma Monna kwa nguvu Monna akampamia Akwelina kwa bahati mbaya Akwelina akajigonga kwenye ukuta akapoteza fahamu papo hapo.
Monna hakuamini kama ujinga wake ungeweza kuleta madhara kama hayo, Kakinga akambeba Akwelina Monna akafungua mlango haraka wakapanda kwenye gari wakaondoka hadi hospital. Kakinga akiwa amembeba Akwelina alikwenda katika chumba alichomuacha Warda kwa ajili ya kumfuata Daktari aliyempatia karatasi ya malipo, Walipofika katika chumba hicho Kakinga alisukuma mlango kwa haraka walipofika ndani Kakinga alimuona Warda anazungumza na Daktari, Daktari huyo aliposikia mlango umefunguliwa kwa kasi alistuka na kugeuka, Kakinga na Monna hawakuamini kumuona Daktari huyo ni PATRICK ?? Monna ali ..........
Monna na Kakinga hawakuamini kama daktari yule ni PATRICK ?? Monna aliogopa mithiri ya kudondoka chini , moyo wake ulipata mstuko wa ajabu sana kwa kumuona Patrick akiwa hai , kakinga alishikwa na hasira sana kwa kumuona Patrick mbele yake :
"__Mmeambiana mkutane ndani ya hospital hii sio ?
Kakinga alimuuliza monna akiwa na hasira mno , hasira zilichanganya kichwa chake hadi akasahau kama akwelina anahitaji tiba japo alikuwa katika mikono yake
"__Hapana hapana huyu sio mtu Kakinga, Patrick alishakufa muda mrefu huyu sio yeye " Monna alimjibu Kakinga akiwa anatetemeka sana na kujificha nyuma ya mgongo wa Kakinga. Kakinga alishindwa kuelewa alichokuwa anasema monna .
""*__Usiogope monna Mimi bado nipo hai sijafa japo unajua nilikufa na labda nikueleze kitu monna serikali ipo mikononi mwangu. Unajua kwanini nilikuhitaji kipindi kile? Nilikuhitaji kwa sababu nilihitaji kupata ladha ya mapenzi yako tu na kutokana na tamaa zako nilifanikiwa hilo. Siku uliyotoroka ndio ingekuwa siku ya mwisho kwako kuishi katika hii dunia, unahabati sana kutoroka siku ile. Kakinga huyu warda ni mdogo wangu na ajali ile Mimi ndio niliyoitengeneza nikiwa na mdogo wangu warda tulipanga suala hilo **
Yalikuwa maneno ya Patrick akimueleza monna , ilikuwa ngumu upande wa Kakinga kuamini kama warda mke wake ni mdogo wa adui yake aliyemnyanganya mke wa zamani ( monna ) patrick hakuishia hapo aliendelea kusema :-
**" Haha najua huwezi kuamini Kakinga lakini ukweli ndio huo kipindi ukiwa na mawazo nilikuwa upande wa pili wa barabara nikamtuma njiwa wa bandia kwa kutumia remote control nilifanikiwa kumvuta mtoto katikati ya barabara hatimae ajali ikatimia, Nilimtumia mdogo wangu kwa kutumia mapenzi ili iwe rahisi kukupata na kingine umechelewa sana Kakinga mimba uliyompatia mdogo wangu tumeshaitoa kwa sababu kazi yake imeshaisha. Ooooh kakinga najua inakuuma sana pole hahaha, pia unajua lengo la kufanya yote hayo ni nini .. Lengo ni mtoto huyo kwa bahati nzuri umemleta mwenyewe kwa maana tulitaka tumfuate huko hotelini .
Bado akili ya kakinga ilikuwa inapinga ukweli huo , Ghafla akatokea Julius ( kiongozi wa wanajeshi ) akiwa na wanajeshi wengi akamchukua mtoto katika mikono ya kakinga alafu akamfunga pingu , Warda alisimama akamfuata Kakinga baada ya kuona amefungwa pingu akamwambia :-
"" Najua huwezi kuamini Kakinga mume wangu hiki kilichotokea mbele yako amini huu ndio ukweli pamoja na yote nakupenda sana kakinga wangu japo hii ilikuwa ni kazi ""
Warda alipomaliza kumwambia kakinga maneno hayo alishika mikono ya kakinga akampatia ufunguo wa pingu alafu akaondoka.
Julius alitoa amri kwa wanajeshi wake wakamchukua Kakinga na monna wakatoka nje moja kwa moja hadi kwenye gari safari ikaanza japo kakinga na monna hawakutambua wapi wanaelekea wakiwa ndani ya gari Patrick alimpatia tiba akwelina baada ya muda mfupi akwelina alirudisha fahamu akaanza kumlilia Kakinga , Patrick ikabidi ampatie mtoto Kakinga , Akwelina alipofika katika mikono ya kakinga alitulia.
Safari ilizidi kusonga mbele Kakinga akiwa na akwelina alishusha mikono chini akafungua zile pingu alizofungwa alafu akatulia . Gari zilikuwa zinaondoka kwa mwendo wa kasi sana zikafika katika daraja kubwa ambalo chini ya daraja hilo lilikuwa na mto , zile gari zilipunguza mwendo ili kuvuka daraja hilo. Gari zilipofika katikati ya daraja Kakinga alifungua mlango wa gari akatoka nje ya gari akajirusha akiwa na akwelina katika mikono yake
a ndani ya gari baada ya kumuona kakinga amejirusha hawakuamini kama kakinga angekuwa jasili kiasi hicho, monna alilia sana alipohitaji kujirusha kujirusha ili amfuate kakinga Patrick alimzuwia akamrudisha ndani ya gari wakaendelea na safari Julius alikuwa na hasira sana akiwa ndani ya gari.
Kakinga akiwa na mtoto mikononi mwake alisukumwa na maji ya mto ule akiwa anajipigiza katika mawe mbalimbali yaliyokuwepo ndani ya mto huo , Maji yalizidi kumsukuma Kakinga hali iliyompatia wakati mgumu sana kupambana na maji hayo ili kusaidia maisha ya akwelina. Pamoja na kupambana na maji hayo lakini maji yalikuwa na nguvu sana walimzidi nguvu Kakinga akapoteza fahamu akiwa ndani ya mto huo baada ya kakinga kupoteza fahamu maji yalimsukuma hadi nje ya mto katika msitu mkubwa. Baada ya muda mrefu kupita alikuja Mzee mmoja ambaye alikuwa mvuvi alipofika sehemu aliyokuwa anaitumia kuvua samaki alishangaa sana kumuona kijana mmoja akiwa amemshikilia mtoto kifuani kwake, Yule mvuvi alimsogelea Kakinga akamvuta ili kumtoa ndani ya maji yale ya mto , Mvuvi alifanikiwa kumtoa nje Kakinga kwakua yule mvuvi alikuwa anayatambua maji vizuri alimsaidia Kakinga kumtoa maji yalikuwa ndani ya kifua chake kwa uwezo mkubwa aliokuwa nao mvivu huyo alifanikiwa kurudisha fahamu kwa Kakinga .
Kakinga alipopata fahamu yule mvuvi alimchukua akaondoka nae hadi nyumbani kwake, Hali ya akwelina ilikuwa mbaya japo yule mvuvi alijitahidi sana kumpatia tiba mtoto lakini bado haikusaidia kitu, Siku zilizidi kusonga mbele bado hali ya akwelina ilizidi kuwa mbaya. Usiku mmoja Kakinga akiwa nje ya nyumba ya mvuvi yule alikuwa amembeba akwelina machozi yakimteremka , Yule mvuvi aliporudi nyumbani alimkuta Kakinga analia .
"" Kwanini unalia kijana wangu ? Mvuvi alimuuliza Kakinga baada ya kumuona analia sana .
"" Daah nafsi inaniuma sana babu binti huyu ndio tumaini langu la mwisho kwanini anataka kuniacha peke yangu kama akifa bora na Mimi nife sioni sababu ya kuishi tena sina familia nyingine zaidi yake huyu mtoto ndio familia yangu.
Yalikuwa maneno ya kakinga akimjibu mvuvi huyo. Baada ya wiki mbili akwelina alionesha dalili ya kupoteza maisha Kakinga alilia sana alitambua akwelina amepoteza maisha yule mvuvi alichimba kaburi kwa ajili ya maziko ya akwelina, Kakinga alibeba mwili wa akwelina akaenda nao hadi katika kaburi lile alipotaka kumzika akwelina cha ajabu akwelina alipiga chafya alafu akaanza kulia Kakinga hakuamini kama akwelina hakupoteza maisha. Maisha ya monna yalikuwa magumu sana ndani ya utawala wa Julius , Monna akiwa ndani ya mateso hayo alimuona warda anakuja mbele yake akiwa na msichana mmoja amefungwa kitambaa usoni alipofika karibu yake warda alifungua kitambaa kile monna alistuka sana kumuona mama aliyempatia AKWELINA siku ya kwanza ndani ya msitu , Warda akasema :-
WARDA ?? Unamkumbuka huyu mama ? Najua unamkumbuka huyu ndio mama yake na akwelina aliyekupatia mtoto wake wewe . Unafikiri alikufa hapana bado yupo hai na kama ulikuwa hufahamu huyu ni mke wa Julius , Unajiuliza nimejuaje yote haya usijali kwakua upo hapa utafahamu kila kitu.
Monna alishikwa na butwaa kwa maneno aliyosikia toka kwa warda. Baada ya miaka sita kupita akwelina alianza kukua akiwa na afya njema siku zote akwelina alikuwa anapenda kuwa karibu na Kakinga kutokana na upendo wa juu sana aliokuwa nao akwelina kwa kakinga. Japokuwa hali ilikuwa mbaya na maisha ya chini waliyokuwa wanaishi lakini furaha zilitawala mioyo , Siku moja majira ya asubuhi akwelina alimfuata kakinga ( baba mlezi ) akamuuliza :
"" Baba hivi Mimi nina mama kweli ?
.......
Kakinga alitulia kimya kwa muda mrefu sana bila kujibu chochote , Akwelina akamuuliza Kakinga kwa mara nyingine : Baba mbona hunijibu nataka kumuona Mama yangu .
Kakinga alimgeukia Akwelina kisha akamwambia : Binti yangu siku natamani sana kukueleza kitu muhimu lakini kwa sasa muda haujafika kuwa na amani sawa ?
Akwelina alipoteza furaha akasema : Marafiki zangu wote wana Mama na Baba kila siku wanacheza na Mama zao kwanini Mimi sina Mama ?
KAKINGA : Mtoto wangu usijisikie vibaya inatakiwa uishi na kukubaliana na hali iliyopo kwa sababu leo nipo na wewe vipi kama kesho na mimi nikiwa sipo wewe utafanyaje ?
Maneno hayo yalimfanya Akwelina aogope akajikuta anasema : Baba unataka kunikimbia na wewe ?
Kakinga alimbeba Akwelina na kumwambia : Binti yangu sote niwapitaji katika hii Dunia, kila kitu kitaondoka na hakuna ataebaki mzima sote tutakufa Mtoto wangu .
Akwelina alimkumbatia Kakinga akaanza kulia Kakinga akamuuliza : Unalia nini binti yangu ?
Akwelina alijibu : Sihitaji uondoke Baba tafadhali usiniache peke yangu Nakupenda sana Baba yangu kipenzi
Kakinga alimtuliza Akwelina moyoni mwake akasema : Akwelina upo sahihi binti yangu una haki ya kupata mapenzi toka kwa Mama yako ili nawe uwe na furaha kama watoto wengine lakini simjui Mama yako Binti yangu na sijui nifanyaje ili nawe umuone Mama yako daah ?? Lakini usijali mtoto wangu nitakulea hadi mwisho wa maisha yangu Mimi ndio Mama na ndio Baba yako pia .
Siku hiyo iliisha Akwelina akiwa hana furaha na alikuwa mnyonge sana, Usiku ulipotanda Akwelina alimfuata Babu ( mvuvi ) alimkuta Babu yupo anaimba wimbo nzuri wa kilugha, Wimbo aliyokuwa anaimba Babu ulimvutia sana Akwelina japo alikuwa hana furaha wimbo ule ulimpatia faraja moyoni mwake, Akwelina alipofika karibu ya Babu alikaa karibu yake kisha akamuuliza Babu : Babu unaimba wimbo mzuri sana huo wimbo una maana gani ?
Babu alicheka mno kisha akajibu : Haha Akwelina mjukuu wangu wimbo huu ni wa asili ya kwetu nakumbuka nilikuwa namwimbia marehemu mke wangu ambaye ni Bibi yako , kwahiyo siku nikimkumbuka basi huwa naimba wimbo huu kama ulivyosikia .
Akwelina akauliza tena : Hivi Babu Mama yangu yupo wapi ?
Babu alishanga mno kisha akajibu : Mmnh swali hilo gumu sana mjukuu wangu nenda kamuulize baba yako, lakini usijali siku moja Mama atarudi na utamuona sawa mjukuu wangu kwahiyo ondoa wasiwasi .
Maneno ya Babu yalimpatia faraja Akwelina kwa kiasi kikubwa. Usiku ulizidi kukomaa siku hiyo Kakinga alichelewa sana kurudi nyumbani, Babu alipoona usiku unazidi kukomaa alimwambia Akwelina aingie ndani akalale lakini Akwelina alikataa kwa sababu alikuwa hajamuona Baba yake, Babu alijaribu kumshawishi Akwelina ili aingie ndani kutokana na baridi kuwa kali bado haikusaidia kitu. Baada ya masaa mawili kupita Kakinga alifika nyumbani akiwa amechoka sana siku hiyo , Akwelina alipomuona Kakinga alimkimbilia akamkumbatia , Kakinga akamuuliza Akwelina : Umekula binti yangu ?
Akwelina alijibu : Mama yangu yupo wapi Baba niruhusu kidogo tu nikamuone tafadhali nakuomba .
Kakinga alichukia sana akamjibu Akwelina kwa jazba na kwa sauti ya juu : Mimi ndio MAMA na BABA yako hakuna mwingine sihitaji uniulize tena hilo swali umenielewa ? Nenda ndani haraka ukalale kila mda Mama , Mama sasa kama hayupo Mimi nifanyaje ? Nenda ndaniii ??
Akwelina alilia sana baada kuona Baba yake anamkaripia, Kakinga alimuonea huruma Akwelina akambembeleza na kusema : Usijali mtoto wangu Mama yako atakuja siku moja sawa , Nisamehe kwa kukuogopesha mtoto wangu acha kulia Mama angu futa machozi .
Akwelina alimsikiliza baba yake akaacha kulia wakaingia ndani pamoja na Babu. Asubuhi na mapema palipo pambazuka Monna alikuwa katika Chumba alichofungiwa , Chumba hicho kilikuwa na mateso makali sana , Monna akiwa amechoka walikuja wanajeshi watatu wakamfunga kitambaa Monna kwenye macho alafu wakaondoka nae, baada ya hatua kadhaa walimfungua kitambaa kile Monna alijikuta yupo katikati ya watu wengi sana mfano wa Gereza, Monna akiwa bado anashangaa mazingira hayo alishikwa mkono alipogeuka alimuona Mama wa Akwelina , Mama huyo alimvuta Monna pembeni kisha akasema : Samahani mdogo wangu mtoto wangu niliyekupatia yupo hai na kama yupo hai ni mzima ? Daah masikini mtoto wangu ??
Monna alijibu : Yupo hai mtoto wako na anaitwa AKWELINA .
Mama alitokwa na machozi ya furaha akasema : Daah ahsante Mungu kumbe mtoto wangu mzima jamani ??
MONNA : Acha kulia mwanao ni mzima kabisa naomba nikuulize kwani ilikuaje na kwanini nilikukuta msituni na ukaamua kunipatia mtoto wako na hapa ni wapi ?
Mama alifuta machozi kisha akasema : Daah ni stori ndefu sana nakumbuka miaka kumi iliyopita nilikuwa ......
MAMA ?? Daah ni stori ndefu sana nakumbuka miaka 10 ( kumi ) iliyopita nilikuwa naishi na mume wangu #Steven maisha yetu yalikuwa yenye furaha na amani mume wangu alikuwa anapesa sana japo sikutambua anafanya kazi gani inayompatia pesa nyingi kama alizokuwa nazo, sikuhitaji sikuhitaji kumfatilia sana kwakua nilimuamini sana mume wangu. Siku moja mume wangu alikuja na Julius huyu ambaye ndio mmiliki wa eneo hili kwa sasa, Julius alikuwa mdogo wa mume wangu siku hiyo nilikuwa chumbani nikasikia wanatupiana maneno makali , baada ya muda mfupi nilisikia mlango unafungwa kwa nguvu nikatoka nje nikamkuta mume wangu peke yake akiwa na mawazo sana nilipomuuliza alinijibu “” Amechoka kufanya unyama kwa watu wasio na hatia “” ukweli sikuelewa anamanisha nini ikabidi nimuulize akasimama akaniambia
“” Leo mke wangu nahitaji utambue ukweli kuhusu Mimi lakini naomba usinichukie kwa ukweli wangu “”
Mume wangu alisimama akavua shati lake akanionesha alama iliyokuwa kwenye bega lake alikuwa ameandikwa neno #AKWELINA sikutambua neno lile lilikuwa na maana gani na kwanini alinionesha ile alama , Baada ya kunionesha aliniambia nikae chini kisha akasema
“” Mke wangu hili neno ni jina la…
“””” Nani monna hapa “” Monna na mama wa akwelina Walistuka baada ya askari mmoja aliyekuja akauliza jina la monna .
“” Ni Mimi hapa “” Monna alimjibu yule askari , yule askari alimchukua monna akaondoka nae. Monna alikasirika sana kwa sababu alitamani kujua mengi toka kwa mama wa Akwelina. Monna aliondoka na yule askari hadi ndani ya Chumba kimoja katika eneo hilo, Monna alipofika aliwakuta watu wengi sana wakiwa busy na computer ( kompyuta ) wakati anatazama huku na huko alimuona Patrick mbele yake hakutambua amekujaje mbele yake , Patrick akasema :
PATRICK ?? Oooh mrembo kipenzi changu wa zamani najua hujui kwanini upo hapa sio ?
MONNA ?? Ndio sijui hilo alafu samahani Mimi sio mpenzi wako bora kifo kuliko kuniita hivyo nakuchukia sana wewe mshenzi .
PATRICK ?? Hahaha tuliza hasira binti nimekuita hapa kuna kitu nahitaji kukuonesha muda huu upo tayari hebu tazama hapa katika computer hii unaona nini ?
Moyo wa monna ulipatwa na mshituko wa ajabu sana baada ya kumuona Kakinga akiwa anacheza na binti mdogo bila shaka monna alitambua yule ni akwelina monna alianza kutetemeka na kujiuliza maswali mengi kakinga yupo wapi hapo na wamewezaje kumuona. Kipindi monna anajiuliza maswali mengi ndani ya kichwa chake Patrick alimsogelea akamwambia :-
PATRICK ?? Ndani ya mwili wa mtoto huyo kuna kitu cha thamani sana na popote alipo tukiamua kumtafuta tunampata na muda huu nazungumza na wewe tumeshatuma askari katika eneo hilo muda sio mrefu Kakinga na Akwelina wataletwa hapa na utawaona haha askari mrudisheni sehemu yake.
Askari walimrudisha monna sehemu alipokuwepo. Baada ya siku mbili majira ya mchana katika nyumba ya mvuvi akwelina alikuwa anang’oa majani akiwa anafanya shughuli hiyo alihisi kitu kibaya mbele yake , Akwelina akasimama akatazama mbele yake kwa umakini sana aka…
Akwelina akasimama akatazama mbele yake kwa umakini sana akaona nyasi zinatikisika kisha zinatulia, akwelina alikuwa binti jasili sana aliingia ndani akachukua panga alafu akaenda sehemu ile ambayo nyasi zilikuwa zinatikisika na kutulia, Kwa umakini wa kutosha bila woga alifika eneo hilo kabla hajafika sehemu husika ghafla alitokea mbwa wao akiwa na sungura mdomo kwake akwelina alistuka akapuuzia akageuka akarudi , Wakati huo wanajeshi waliotumwa na Patrick walikuwa wameshafika eneo hilo walimuona mtoto kwa mbali akiwa na mbwa pembeni kiongozi wao alifungua laptop akatazama picha ya mtoto walioagizwa ikabidi atumie bunduki yake aka zoom ( kukuza ) sura ya akwelina alipohakikisha ndio yeye alipiga sindano ya kifua. Sindano ile ilikuwa na madawa ikamfanya akwelina apoteze fahamu walipomsogelea ili wamchukue mbwa alijaribu kuwaziwia wakampiga risasi kisha wakaondoka na akwelina.
Muda ulisonga mbele hadi majira ya saa moja usiku majira hayo hayo kakinga na babu walifika nyumbani walishangaa giza limetawala nyumba nzima na haijawahi kutokea hofu ilitanda zaidi baada ya kimya kikubwa kilichotawala eneo hilo kakinga alianza kupata wasiwasi mkubwa sana akaingia ndani akachukua tochi akaanza kutembea huku na kule katika eneo hilo akiwa anamwita akwelina , Kakinga aliita sana bila mafanikio yeyote hali hiyo iliongeza hofu kwa kakinga. Katika kuzunguka huku na huko Kakinga alimkuta mbwa wao kafariki alipomchunguza aligundua yule mbwa alipigwa risasi Kakinga alitupa tochi chini akashika kichwa aligundua Akwelina atakuwa amechukuliwa na watu wabaya mvua ya machozi alianza kumwagika katika macho ya Kakinga.
Akwelina akiwa ndani ya gari pamoja na wale wanajeshi walitembea kwa muda mrefu kwa mwendo mkali kipindi chote hicho Akwelina alikuwa amefungwa kitambaa usoni ili asitambue sehemu alipokuwa anaelekea. Usiku huo huo kakinga alianza kutembea mtaa kwa mtaa akimuuliza yeyote aliyekutana nae , Baadhi ya watu katika eneo hilo walijua kakinga amechanganyikiwa. Asubuhi palipokucha wale wanajeshi walifika sehemu wakasimama wakamfungua akwelina kile kitambaa Akwelina alishangaa yupo sehemu ambayo ni tofauti na nyumbani kwao ( Mjini ) Akwelina akiwa anashangaa alishikwa mkono na msichana ambaye hamtambui, Muda huo huo simu ya huyo msichana ilipigwa akapokea :-
“””” Hellow who are you ( Habari wewe ni nani ) ?
?? ___ ?? Acha bwebwe zako hizo unaongea na kaka yako hapa Patrick , sikia warda huyo ni akwelina mtunze kesho kutwa unatakiwa uje nae huku makao makuu tumalize mchezo , Kakinga yupo mbali hawezi kujua kama mtoto yupo kwako na anaweza juaje kama yupo kwako sio rahisi hakikisha hatoroki sawa ?
WARDA ?? Sawa kaka nimekuelewa.
?? __ ?? Asubuhi njema .
Warda alimchukua akwelina akaingia nae ndani wale wanajeshi wakaondoka. Muda huo wa asubuhi kakinga alikuwa bado yupo mtaani akimtafuta akwelina, Alizidi kumtafuta bila kuchoka ghafla akasikia mtu anasema :-
“”” Kijana weka mikono juu ya kichwa chako alafu piga magoti kisha lala chini “”
Siku zote Kakinga alikuwa mbishi na anaejimini sana pamoja na kuambiwa hivyo aligeuka akamkuta mwanajeshi mmoja amemnyoshea bunduki, Hasira alizokuwa nazo kakinga zilimuongezea ujasili Kakinga akamvamia yule mwanajeshi bila kujali silaha aliyokuwa nayo , Kakinga alimzidi nguvu yule mwanajeshi akampiga sana akiwa anamuuliza mtoto alipo, kipigo kilivyozidi yule mwanajeshi alizungumza ukweli bila kupoteza muda Kakinga alimchukua huyo mwanajeshi akampakiza kwenye gari moja kwa hadi mjini. Walipofika mjini yule mwanajeshi alimpeleka sehemu mtoto alipokuwepo , Yule mwanajeshi alimwita , Warda alipokuwa ndani alichungulia mlangoni akamuona mwanajeshi wao akafungua mlango akatoka nje alipotazama upande wa kulia akakutana macho kwa macho na kakinga warda al…….
Warda alistuka sana baada ya kumuona kakinga mbele yake , yule mwanajeshi alipopata nafsi alikimbia , warda alipotaka kukimbilia ndani Kakinga aliziwia mlango akamshika shati akamsukuma hadi ndani kutokana na hasira alizokuwa nazo Kakinga alikunja ngumi ili ampige warda lakini kabla ya kitendo hicho akwelina alishika mkono wa baba yake akiwa anatokwa na machozi .
??”” Baba usimpige utamuumiza baba ” yalikuwa maneno ya akwelina akimuomba baba yake .
??__ Acha nimfundishe adabu huyu sio mtu mzuri kwako binti yangu huoni kwamba alitaka kukuchukua bila ruhusa yangu nahitaji nimfunze adabu huyu mwanamke ili siku nyingine akuogope “” Kakinga alimjibu akwelina akiwa ana hasira.
Akwelina alijitahidi sana kumziwia baba yake, Kwa muda mrefu kakinga akakubali ombi la akwelina akamuachia warda akamshika mkono akwelina wakaondoka baada ya hatua kadhaa wakiwa wanaelekea nje ilisikika sauti ya warda ikisema:
??__ Naomba nikusaidie Kakinga mume wangu ili ufanikiwe hicho unachohitaji tafadhali.
??__ Funga mdomo wako kamwe siwezi kuwa na mke kama wewe usinifanye nibadili uamuzi huu “” yalikuwa ni majibu ya Kakinga akimjibu warda.
??__ Sawa sikatai lakini bila Mimi huwezi kumpata mama wa mtoto huyo “” Warda alimjibu kakinga .
Majibu ya warda yalimvunja nguvu kakinga akamtazama akwelina akaona dalili ambazo sio nzuri ikabidi aondoke. Warda alitumia njia zote lakini kakinga hakumsikiliza.
Baada ya kutoka kwa warda Kakinga aliamua kwenda sehemu aliyokuwa anaishi mwanzo kipindi cha nyuma sana wakati akwelina alipokuwa mdogo sana japo palikuwa mbali sana lakini walijitahidi wakafanikiwa kufika eneo kwa bahati nzuri kakinga alimkuta yule mwenyeji wake, Yule mwenyeji aliwapokea bila matatizo yeyote.
Yalipofika majira ya usiku monna akiwa ndani eneo lile alijitahidi akafika kwa yule mama wa Akwelina , monna alipofika alimkuta mama yule, Yule mama alipomuona monna cha ajabu alifurahi akasema:-
MAMA ?? Afadhali umekuja mdogo wangu .
MONNA ?? Kwanini Dada yangu ?
MAMA ?? Kesho ninahamishwa hapa napelekwa wapi masikini lakini namuachia mungu nilikuwa namuomba mungu utokeze ili nikuone Mara ya mwisho naweza hata kufa huko daah , Pia nilihitaji kukumalizia historia ya maisha yangu hadi nilipokutana na wewe sasa naomba unisikilize mume wangu aliponionesha ile alama akaniambia hivi :-
“”” Mke wangu hili neno ni jina la kampuni ya baba yetu alituachia Mimi na mdogo wangu Julius kabla baba hajafariki alituchora alama hizi kama kiapo ili tushirikiane , Kampuni hii ilikuwa mbaya sana ilikuwa inafanya mauaji , inanyanganya Mali za watu pia tulikuwa tunauza watu nje ya nchi kifupi kampuni hiyo ilikuwa mbaya sana na ilianzishwa na babu kabla baba yetu hajazaliwa nilikuepo ndani ya kampuni hiyo lakini ukweli sikupenda matendo ya kampuni hiyo. Baba alipofariki mama aliendeleza kusimamia kampuni yetu. Siku ya masiba wa mama kama unakumbuka sikuepo huku tanzania, Nilipofika hapa Tanzania nilifanya uchunguzi wangu nimegundua Julius ndio kafanya mauaji kwa mama ??
Mume wangu aliishia hapo nikamuona anasimama akachukua ufunguo wa gari akaondoka , Nilisubiri sana hadi majira ya usiku uchungu ukanishika mfanya kazi wangu wa ndani alinisaidia kupiga simu kwa daktari wetu akaja akanizalisha mtoto wa kike ambaye ndio niliyokupatia. Baada ya masaa mawili mume wangu akaja akiwa amechoka sana akanikuta nina mtoto cha ajabu akachukua kisu na na sindano ya nguo akaweka Uzi ndani ya sindano akamchukua mtoto akamchana katika tako lake la kesho akaweka ufunguo mdogo sana akamshona bila huruma Mtoto wangu alilia sana nilishindwa kuvumilia ikabidi nimfuate mume wangu akaniambia nimuache kwanza, kwakua nilikuwa namuamini nikamuacha alipomaliza kumshona aliondoka na mtoto hadi chumbani akafunga mlango. Nikasikia mtoto wangu analia sana muda kidogo akatoka nje akiwa na begi lenye vitu ndani yake pamoja na mtoto mkononi kwake alikuwa ametapakaa damu nyingi sana akaniambia nikimbie haraka pamoja nilikuwa na maumivu lakini nilijitahidi kukimbia nikiwa mbali na nyumba yetu nilisikia sauti ya mume wangu ikilalamika nilitamani kurudi lakini nikajikaza nikaendele kukimbia ndio nikakutana na wewe nikakupatia mtoto wangu sijui ule ufunguo ulikuwa na nini daah ….
Mama wa akwelina alishimdwa kuziwia hisia zake alianza kulia kwa uchungu pindi alipokumbuka maumivu aliyoyapata siku za nyuma , Moyo wa monna ulipatwa na huruma baada ya kufahamu ukweli kuhusu maisha ya akwelina pamoja na familia yake, Kilio kutoka kwa mama wa akwelina kilizidi kuiteka nafsi ya monna hali iliyomfanya monna ashushe mvua ya machozi katika macho yake, wakiwa katika majonzi hayo alikuja askari mmoja akamchukua mama wa akwelina kisha akaondoka nae japo mama huyo hakutambua wapi anapelekwa.
Siku iliyofuata asubuhi na mapema kakinga alijiandaa akaenda katika shule iliyokuwa karibu na sehemu wanapoishi alipofika shuleni hapo alizungumza na mwalimu mkuu kwa muda mrefu sana mwisho mwalimu mkuu alisema :-
”’ Kijana mlete mtoto wako apate elimu bora katika shule hii kwakua umenieleza maisha yako yalivyo nakupa nafasi ya pekee utalipa ada ya mtoto chochote utachokuwa nacho hata usijali kijana wangu nimeamua kukusaidia ili binti yako apate elimu bora nitakusaidia kila utapokwama katika ada ya mtoto.
Majibu ya mwl / mkuu yalimpatia matumaini makubwa sana kakinga hali iliyomfanya aondoke hadi sokoni akanunua nguo za shule kwa maandalizi ya akwelina mtoto wa pekee anayempenda sana, Mapenzi aliyokuwanayo kakinga kwa akwelina yalikuwa ya juu sana hadi watu wote waliokaribu yao waliamini akwelina ni mtoto wa kakinga aliyemzaa mwenyewe kwa upendo aliokuwa nao kakinga .
Asubuhi ya siku ya pili kakinga alimpeka akwelina shule kwa bahati nzuri alifanikiwa kumwandikisha katika shule ile, furaha haikuwa kwa kakinga pekee hata akwelina alifurahi kuanza shule. Maisha ya akwelina alipoanza kusoma yalikuwa mazuri sana, akwelina alikuwa mtoto mwenye uwezo mkubwa katika masomo kwa uwezo huo aliokuwa nao akwelina alipendwa na wengi sana ndani ya shule ile. Miaka ilizidi kwenda mbele nae akwelina alizidi kukuwa siku hadi siku hatimae akwelina akawa msichana mwenye miaka kumi na sita ( Miaka 16 ) Miaka yote hiyo Julius na Patrick waliendelea kumsubiri warda na walipozungumza nae warda aliwambia :-
“” Kaka yangu patrick ondoa shaka akwelina yupo mikononi mwangu acheni kumtafuta na nimeondoka kidogo muda sio mrefu nitarudi ondoeni wasiwasi “” Maneno hayo yaliwafanya waache suala la akwelina kwa muda wakaendelea na kazi yao ya unyanganyi.
Katika ukuaji wa akwelina alikumbana na vikwazo vingi vilivyomlenga mama, Vikwazo hivyo vilikuwa vinampatia maumivu makali lakini hakuhitaji kumwambia baba yake ( kakinga ) kwakua siku zote alipojaribu kuuliza suala kuhusu mama yake baba alikuwa mkali sana na siku zote akwelina hakuhitaji kumfanya baba yake akose furaha. Siku moja katika siku za uhai majira ya usiku akwelina alikuwa nje akitazama juu , kakinga alipomtazama akwelina aligundua hana furaha ikabidi amsogelee kabla hajamgusa alisikia akwelina anasema :-
“”__ MAMA upo wapi __ “”
Maneno hayo yalimuumiza sana kakinga akarudi ndani akatafakari sana kisha akachukua begi alilohifadhi vitu vyote alivyopewa monna kipindi anakabidhiwa mtoto, kakinga akarudi nje akampa akwelina lile begi akasema :-
“”_ Binti yangu ndani ya begi hilo ndio kuna ukweli wote kuhusu mama yako kwahiyo fungua begi hilo ndani yake utafahamu ukweli wote **
Kakinga akarudi ndani akamuacha akwelina njia panda , ilimchukua muda sana lakini akajitahidi akafungua lile begi akakuta vitu sio vingi akapekua pekua akaona kitabu kidogo akakifunua kile kitabu, Ndani ya kitabu kile kiliandikwa _??
??_Leo tarehe 16 mimi Steven nimeamua kuandika maneno hayo ndani ya kitabu hiki kidogo kwa sababu maisha yangu na mke wangu JAMILA pamoja na mtoto wangu yapo hatarini …..
JAMILA pamoja na mtoto wangu yapo hatarini, Ndani ya mwili wa binti yangu katika tako lake la upande wa kushoto nimeweka ufunguo wa dhahabu. Najua mdogo wangu Julius lazima atakuja kufuata ufunguo huu kwa sababu ndani ya kampuni ya marehemu baba ambao inaitwa #AKWELINA kuna chumba kimoja chenye hazina zote na hati miliki ya kampuni hiyo.
Akwelina alisimama akafunika kile kitabu akaingia chumbani kwake akavua nguo akagusa tako lake akagundua kuna alama nyeusi, Akwelina hakuridhika akafinyafinya eneo hilo akaona kuna uvimbe ndani ya ngozi yake akagundua bila shaka huo uvimbe ndio ufunguo aliowekwa na baba yake. Akwelina alivaa nguo zake akaendelea kusoma kitabu kile .
??__ Leo hii hii nazungumza ukweli kuhusu kampuni ya baba hii ya akwelina, Kampuni hii imeanza muda mrefu sana kabla sijazaliwa kwa maana hata nilipozaliwa niliikuta hiyo kampuni. Siku nilipogundua matendo yanayofanyika ndani ya kampuni hiyo niliumia sana nikajaribu kuiteketeza kampuni hii lakini nilishindwa kwa sababu kuna viongozi wakubwa wapo katika kampuni hii ndio nikaamua kuiba ufunguo huu wanaoutegemea ili siku kitabu hiki kikiwafikia askari watenda haki naomba mkawasaidie watu waliomo ndani ya kampuni hiyo na naomba kwa ambaye ataemuokota binti yangu huyu akiwa bado ni mzima Naomba amlinde na amtunze binti yangu nampenda sana, Mimi sio wa kupona lazima Julius ataniua jina la mtoto wangu naomba aitwe HASMA , kuna picha nimeziweka ndani ya bahasha ndogo hao ndio washiriki wakuu wa kampuni hii, Kwaheri binti yangu nakupenda zaidi mungu akulinde daima.
Akwelina alimaliza kusoma kitabu hicho mikono ikimtetemeka kwa maumivu aliyokuwa anayapata ndani ya moyo wake. Kilio kisichokuwa na mfano kiliutawala moyo wa akwelina hali iliyomstua sana Kakinga alipokuwa chumbani kwake alisikia sauti ya akwelina ikilalamika kwa kulia sana. Ilimbidi kakinga amfuate Akwelina chumbani kwake akajaribu kumtuliza cha ajabu kwa Mara ya kwanza akwelina alimsukuma kakinga akadondoka chini. Ilikuwa kama ndoto kwa Kakinga akwelina akasimama akiwa na jaziba sana akamwambia Kakinga
?? Wewe sio mtu mzuri kwangu haiwezekani siku zote unanificha ukweli huu ambao nimeufahamu leo , Kumbe wewe sio baba yangu mzazi daah naumia sana kumbe baba yangu ameuwawa pamoja na mama yangu alafu umeendelea kunificha kweli maana yako ilikuwa ipi eeeh nakuuliza maana yako ilikuwa ipi ?
?? Akwelina binti yangu wewe leo hii unaweza kunisukuma Mimi !! ni kweli pengine Mimi sio baba yako mzazi lakini kwa shida nilizopata toka kwako kwa ajili ya kusaidia maisha yako mungu ndio anaejua lakini usijali haya ndio maisha, Sababu iliyonifanya nikufiche ukweli huu ulikuwa bado mdogo sana na ningekuaribu akili laiti kama ungetambua ukweli huu lakini bado hujachelewa unaweza kuondoka muda huu ili ukafanye hicho kilichopo akilini kwako umekuwa binti sasa na mwenye nguvu unaweza kuondoka Akwelina.
Majibu ya Kakinga yalimfanya akwelina ajione mkosaji sana mbele yake bila kupoteza muda akwelina alipiga magoti mbele ya Kakinga akaomba msamaha, Kakinga alimnyanyua akwelina akamwambia:
__ Anaestahili kupigiwa magoti ni mungu pekee sio binadamu kwa sasa sina nguvu siwezi kukulinda tena ondoka binti Julius nenda katafute nguvu ili kesho nguvu hizo zikusaidie Mimi muda huu nina umri mkubwa siwezi kukulinda tena lakini usijali lala kesho tutazungumza vizuri.
Kakinga aliondoka moja kwa moja hadi katika Chumba chake, Usiku ulikuwa mrefu sana kwa akwelina kwa kitendo alichofanya kwa kakinga. Asubuhi na mapema akwelina alitoka chumbani kwake akaondoka hadi katika Chumba cha Kakinga alistuka kuona mlango upo wazi bila kupiga hodi akwelina aliingia hadi chumbani akakuta chumbani hakuna mtu kitu kilichompatia wasiwasi zaidi hakuona nguo hata moja ya kakinga. Hofu na wasiwasi ulitanda katika moyo wa akwelina aka…….
Hofu na wasiwasi ulitanda katika moyo wa akwelina akaanza kumtafuta Kakinga huku na kule alitumia muda mrefu sana kumtafuta baba yake mlezi ( kakinga ) toka majira ya asubuhi hiyo hadi usiku ulipotanda, lakini hakufanikiwa kumuona baba yake ?? kwakua giza lilikuwa limeshakuwa nene ilibidi akwelina arudi nyumbani, Njiani akiwa anarudi nyumbani alikuwa analia kama mtoto hali iliyomshangaza yeyote aliyekutana nae, baadhi ya watu aliokuwa anakutana nao walijaribu kumuuliza akwelina kama anatatizo ili wamsaidie ila majibu yake yalikuwa ni kilio tu. Akwelina alifika nyumbani salama japokuwa alikuwa na mawazo sana alipohitaji kuingia chumbani kwake aliona karatasi chini ya mlango akaiokota akaingia ndani akaifunua ile karatasi akaisoma ilikuwa imeandikwa ??
??__ Akwelina binti yangu sijui unanichukia kiasi gani kwa kukuficha ukweli wa maisha yako naomba nisamehe sana kwa hilo , Pili naomba usinitafute nimeenda mbali sana sio rahisi kuniona nilipo kwa sasa lakini usivunjike moyo binti yangu kwa uamuzi huu niliofanya, kuanzia muda huu unatakiwa uwe na nguvu na tegemea ulichonacho , Tegemea unachokiona kwa macho, Tegemea ulichonacho ili kupata ambacho huna, Jitegemee akwelina tarajia msaada kwa watu lakini usiwategemee binadamu sio wazuri.
Akwelina binti yangu jifunze kupitia ndege ,Ndege siku zote anapotuwa kwenye tawi la mti huwa hana hofu kwa sababu matumaini yake hayapo kwenye tawi alilotuwa, bali yapo kwenye mbawa zake. Tegemea uwezo wako , Usitegemee kuwezeshwa kwa sababu yeyote anaekupandisha anauwezo wa kukushusha pambana binti yangu nakutakia maisha mema akwelina.
Karatasi aliyokuwa anasoma akwelina ilikuwa kama imemwagiwa maji kutokana na machozi yaliyokuwa yanamtoka _
??Nisamehe baba siwezi kuwa imara bila wewe rudi baba rudi bab yangu nakuhitaji binti yako wewe ndio udhaifu wangu baba ?? alisema akwelina akiwa analia mno.
Baada ya miezi mitano kupita maisha ya akwelina yalikuwa magumu sana, akwelina akawa hafanyi vizuri katika masomo yake, Mwili wake ulikuwa dhoofu kwa kutokula vizuri , hali iliyowapatia maswali mengi Majirani wengine walimuonea huruma na kutupa lawama kwa kakinga kwa kusema
” Kakinga kamterekeza mtoto wake “
Baadhi yao walisema
” Kakinga sio mtu ni zaidi ya mnyama hawezi kumfanyia hivi binti yake “”
Miezi ilizidi kukatika mwalimu mkuu alimfuata akwelina akamuuliza tatizo linalomsumbua, Akwelina hakumficha alimueleza ukweli wote, Mwalimu mkuu akaamua kumchukua akwelina akaenda kuishi nae nyumbani kwake. Siku hadi siku hali ilizidi kuwa mbaya kwa akwelina ilikuwa ngum kwa mwalimu mkuu kumuelewa akwelina anatatizo gani linalomsumbua ikabidi amulize vizuri, Akwelina alijibu kwa unyonge
?? Namtaka baba samahani mwalimu wangu unaweza kuniletea baba yangu mbele yangu siwezi kuishi bila yeye siwezi Mimi namtaka baba ??
Mwalimu mkuu alijisikia vibaya sana alijaribu kumliwaza na kumpatia faraja kwamba ipo siku baba ake atarudi kidogo akwelina alifarijika. Jioni ya siku hiyo Julius alishindwa kuvumilia akamfuata Patrick akamkuta Patrick yupo anawatesa baadhi ya wafungwa Julius akamwita pembeni akamwambia :-
JULIUS ?? Kesho unatakiwa uanze uchunguzi rasmi kuhusu Akwelina bila shaka warda atakuwa anatudanganya sio mkweli au unasemaje kwa sababu hadi leo miaka mingi imepita .
PATRICK ?? Ni kweli ndugu yangu huyu warda huyu anampenda sana yule kijana ( Kakinga ) ambaye yupo na akwelina lakini usijali kesho nitamtafuta kwa kupita mtandao alafu nitawatuma askari wetu tutafanikiwa tu usijali lakini hivi ni kweli akwelina ni mtoto wako ?
JULIUS ?? Hapana yule ni mtoto wa kaka yangu elewa hivyo tu na hii ni siri olewako umwambie mtu yeyote.
Asubuhi ilipofika Patrick aliingia katika Chumba cha computer akamtafuta akwelina muda mchache akampata, GPS ikamunesha hadi mtaa aliopo kwa sasa Patrick alifurahi sana kisha …
Patrick alifurahi sana kisha akaita askari wengi wakachukua magari , Patrick akapanda ndege aina ya helicopter kwa ajili ya msako huo. Safari hiyo haikuwa ndefu kwa sababu walitumia vyombo vyenye nguvu sana na vinavyotembea kwa kasi kubwa kutokana na vyombo hivyo kuwa imara walifika mapema sana katika nyumba ya mwalimu mkuu ambapo mitandao yao ya GPS kwa kupitia kifaa kilichopo ndani ya mwili wa akwelina ilionesha wanaomtafuta yupo ndani ya nyumba hiyo bila kupoteza muda wale wanajeshi walivunja mlango ( geti ) Mlio wa geti hilo uliwastua wote waliokuwepo ndani akiwemo akwelina na familia ya mwalimu mkuu. Wale wanajeshi waliingia ndani wakawateka watu wote waliokuwepo ndani wakatoka nao nje lakini hawakumtambua akwelina ni yupi katika watu waliowateka japo mtandao ulionesha yupo hapo hapo.
©_ Tumewakosea nini askari wetu ? Mwalimu mkuu aliwauliza .
®_ Shida yetu sisi ni msichana anaeitwa akwelina na yupo hapa hapa na kama hutaki matatizo mzee mtaje huyo msichana ni yupi lakini usipozungumza ukweli hakika utajuta mzee wangu… Patrick alimjibu mwalimu mkuu kwakua aliambiwa jina na mdogo wake ( warda ) .
Kimya kilitawala kwa muda mrefu akwelina alikuwa anatetemeka sana kwa hofu alitambua lazima mwalimu mkuu atamtaja japokuwa alikuwa anajiuliza kwanini wale wanajeshi wanamtaka. Baada ya kimya kirefu patrick aliwapa kazi askari wake, Wale askari walimvuta pembeni mwalimu mkuu wakaanza kumpiga. Kichapo kilikuwa kikubwa zaidi mwalimu hakusema kitu japo alikuwa anapata mateso na maumivu makali, sauti ya mwalimu mkuu akiwa analalamika ilimfanya akwelina asimama akasema :-
?? AKWELINA ni Mimi hapa kuna shida gani au nimekosa nini ? Naomba msimsumbue mzee wangu .
Patrick alicheka sana , akacheka zaidi alafu akamsogelea akwelina akamzunguka akiwa anamtazama,
“” Umekuwa binti mkubwa kiasi hiki ama kweli wanawake mnakuwa kwa kasi sana , Askari mchukueni huyu binti tuondoke “” yalikuwa maneno ya Patrick.
Askari walimchukua akwelina wakaondoka nae hadi kwenye gari, bado akwelina alikuwa hajaelewa kafanya nini , Patrick aliamua kumjibu akwelina Baada ya kumuona anahoji sana :-
PATRICK ?? Sikia binti usitusumbue lakini sababu ya kukufuata hapa leo hii ni kwamba unakitu chenye thamani ndani ya mwili wako ambacho kitaifanya kampuni yetu inayoitwa AKWELINA izidi kuwa bora.
Akwelina alistuka baada ya kusikia maneno hayo akatambua watu hao sio watu wazuri akakumbuka maelezo yaliyokuwepo katika kitabu alichosoma , Ghafla akakurupuka akaanza kukimbia patrick na askari wake alianza kumkimbiza kwa kutumia miguu walimkimbiza kwa muda mrefu sana akwelina akachoka mwendo ukapungua wale askari kwakua walikuwa na mazoezi walimkaribia akwelina, walipotaka kumshika alitokea mtu akiwa na baiskeli katika baiskeli hiyo alikuwa amefunga miti mirefu mingi mno. Cha ajabu akawaziwia kwa kukaa mbele ya wale askari wakiwa na Patrick, yule mwenye baiskeli akashuka akamfuata akwelina wakati huo akwelina aliamua kukaa chini kwa sababu aliishiwa pumzi akamshika mkono akwelina akaondoka nae, Patrick pamoja na askari wake walifanikiwa kuvuka eneo lile kwa muda mrefu hali iliyowafanya wampoteze akwelina pamoja na mtu aliyewaziwia njia .
Safari ilizidi kuwa ndefu ilifika hatua akwelina alishindwa kabisa kutembea yule mtu akambeba hadi walipofika sehemu salama muda wote huo akwelina alikuwa hajamtambua yule mtu ikabidi amvue kofia aliyokuwa amevaa , Akwelina hakuamini kumuona kakinga ( baba mlezi ) yupo mbele yake, moyo wa akwelina ulipatwa na furaha ya ajabu ambayo hakutambua imetokea wapi akamkumbatia baba yake. Kakinga akaendelea kumbeba akwelina hadi katika nyumba moja ambayo ilikuwa nje ya jiji hilo walipofika alimshusha Akwelina akasema :-
KAKINGA ?? Hapa tupo sehemu salama .
AKWELINA ?? Nisamehe baba yangu nakupenda naomba usiniche tena wewe ndio kila kitu kwangu.
KAKINGA ?? Hatuna muda wa kupoteza inabidi uvumilie nikutoa kifaa ulichonacho mwilini kwako vinginevyo bado wataendelea kukufuata popote ulipo najua Patrick hakutoa kifaa hicho wakati ukiwa mdogo haijalishi kipi kitatokea kwako lakini lazima tukitoe kifaa hicho .
Akwelina alikuwa hajui suala hilo Kakinga aliingia ndani akachukua wembe pamoja na mkasi kisha ….
Kakinga aliingia ndani akachukua wembe pamoja na mkasi kisha akamsogelea akwelina akamuuliza kama yupo tayari, akwelina alikuwa japo alikuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake. Macho ya kakinga yaliangaza huku na huko akasimama akaokota kipande cha mti ..
“” Akwelina ng’ata kipande cha mti huu kitakusaidia kupunguza maumivu najua utaumia sana lakini vumilia ili uwe salama sawa mama”” alisema kakinga akiwa anampatia kipande hicho cha mti.
Akwelina alifanya kama alivyoambiwa na baba yake, Upasuaji ulianza bila dawa yeyote ambayo ingeweza kusaidia kupunguza maumivu ( ganzi ) katika upasuaji huo ( operation ) Kakinga alishika mkono wa akwelina akasogeza kisu hadi katikati ngozi ya kwanza, Kisu kilipofika kwenye ngozi akwelina alisisimka mwili mzima akafumba macho na kuruhusu kisu kichane ngozi yake, Kakinga alichana ngozi akaifikia nyama akaichana pia bado hakufika sehemu ambayo kifaa kile kilikuwepo ikabidi ashindilie kisu kikazidi kuingia ndani zaidi, Akwelina alipata maumivu makali mno akapiga kelele kali ghafla akapoteza fahamu, Kakinga alitumia nafasi hiyo akafanikiwa kutoa kifaa ambacho kilikuwa kinamuonesha popote alipokuwepo, Kakinga alipomaliza kufanya kazi hiyo alimchukua akwelina moja kwa moja hadi kituo cha afya akamuomba daktari amshone akwelina katika jeraha lile daktari alitaka barua toka kituo cha polisi cha ajabu Kakinga alitoa pesa nyingi sana akampatia daktari ili amsaidie, Pesa ni kila kitu katika dunia yule daktari alitoa huduma haraka, Baada ya matibabu Kakinga alimchukua akwelina akarudi nae nyumbani muda wote huo akwelina alikuwa bado hajarudisha fahamu .
Baada ya kumkosa akwelina Patrick alirudi ndani ya kampuni yao akiwa amechoka sana walipofika Julius alimpatia adhabu Patrick pamoja na wenzake kwa kushindwa kumleta akwelina. Patrick aliwekwa katika Chumba alichokuwepo monna ghafla akasikia sauti ikicheka ndani ya chumba hicho , patrick alistuka sana akaanza kutembeza macho huku na huko akamuona monna mbele yake ;
“””Unaogopa nini Patrick mpenzi wangu hahaha kweli watu wanaopendena watakuwa pamoja kila sehemu umekuja hadi huku kunifuata Mimi jamani mpenzi??
Monna alimwambia patrick akiwa anacheka sana kwa dharau. Patrick alichukia sana baada ya kuona monna anamdharau, patrick alimpiga kibao Monna kisha akakaba shingoni akamwambia :-
PATRICK ?? Nitakuua monna sipendi mtu anidharau sipendi monnaaaa na hujui mtu anamatatizo gani ohoo .
MONNA ?? Mbona unachelewa niue sasa hivi utakuwa umenisaidia sana sina thamani katika maisha haya.
Patrick alimsukuma monna mbali, monna alidondoka chini lakini bado alikuwa anamcheka sana. Siku ya pili majira ya jioni akwelina alirudisha fahamu zake kitu cha kwanza alisema “” BABA UPO WAPI ‘” bahati nzuri baba hakuwepo mbali alisogea akwelina alizidi kufurahi furaha yake ilimfanya alie baba akamfuta machozi akamwambia :
KAKINGA ?? Kwanini unalia binti yangu ?
AKWELINA ?? Nimekukumbuka baba yangu leo hii furaha yangu imerejea tena nakupenda sana baba yangu.
KAKINGA ?? Usijali binti yangu kwa uwezo wa mungu nimenunua nyumba kubwa sana kwahiyo kesho asubuhi tutaenda nyumbani kwetu sawa mama ?
AKWELINA ?? Kweli baba woooh ?? kumbe uliponikimbia ulikwenda kutafuta pesa Mimi nilijua uliniacha kwa sababu nikikusukuma baba .
KAKINGA ?? Kukukimbia ?? !!
AKWELINA ?? Ndio baba umesahau kama ulinikimbia ?
KAKINGA ?? Ooooh ndio lakini usijali binti yangu nimeshasahau yaliyopita jiandae kesho safari.
Usiku wa siku hiyo ulikuwa mfupi sana kwa akwelina kwa sababu alikuwa na furaha sana siku hiyo. Asubuhi majira ya saa mbili akwelina alikuwa bado kalala akaamshwa na mlio mkali wa gari, akwelina alikurupuka hadi nje akamkuta Kakinga ndani ya gari zuri sana ikabidi arudi ndani akajiandaa haraka haraka alafu wakaondoka. Walitumia masaa kadhaa wakafika katika jumba zuri la kifahari bado ilikuwa ndoto kwa akwelina hakuamini alichokuwa anakiona, Lakini alishangaa kuona milango inafungwa yote baada ya kuingia ndani alafu Kakinga akacheka sana , kicheko kilizidi hadi kikampatia wasiwasi akwelina. Akwelina alimuuliza kakinga :-
AKWELINA ?? Kuna nini baba mbona unacheka sana ?
KAKINGA ?? Nimefanikiwa leo hahaha nimefanikiwa wooh. Unahitaji kujua kwanini nafurahi ?
AKWELINA ?? Ndio baba yangu .
Kakinga aligeuka upande wa pili , ambapo akwelina alikuwa anamuona kwa nyumba ( mgongoni ) akavua ngozi ya juu aliyokuwa amevaa, Ilikuwa kama maigizo mbele ya macho ya akwelina, Kakinga baada ya kuvua ngozi aliyokuwa ameivaa akwelina aliona umbile la mwanamke na sio mwanaume tena, Yule mwanamke alipogeuka akwelina alistuka kumuona yule dada ambaye kipindi alipokuwa mdogo Kakinga ( baba yake mlezi ) alitaka kumuua ambaye ni WARDA ????
Warda alipiga makofi wakatokea wanaume wanne wenye nguvu za kutosha alafu akasema :-
WARDA ?? Monna binti wa Kakinga hahaha kweli wewe ni kipofu nimeishi na wewe muda wote huo hujanitambua kama Mimi sio baba yako pole sana lakini usijali upo sehemu salama japo inamaumivu kwako nimekuokoa toka katika mikono ya kaka yangu kwa sababu ninataka kufanya kazi na wewe ila kazi hiyo haitakiwi uwe bikra na ndio maana nimewaleta wanaume hawa watoa bikra yako kabla kazi yetu haijaanza . Vijana fanyeni kazi yenu .
Wale vijana walimsogelea akwelina waka………
Wale vijana walimsogelea akwelina wakamshika wakamfunga kamba katika mikono yake ili iwe rahisi kufanya walichokusudia, akwelina alijitahidi kujiziwia ili asifanyiwe unyama huo Lakini kwakua wanaume hao walikuwa na nguvu za kutosha walifanikiwa kumdhibiti akwelina wakamlaza chini akwelina akiwa chini alifunga miguu yake ( kubana muguu ) hali iliyowafanya wale watu washindwe kumuingilia kimwili ( kumbaka ) Mmoja kati ya wale wanaume wanne alichukia sana baada ya kuona akwelina anawasumbua akampiga ngumi ya tumbo , ngumi hiyo ilimpatia maumivu makali akwelina akapiga kelele kali za kuomba msaada , kelele hizo zilimstua mtu mmoja aliyekuwa amefungwa kamba ndani ya chumba cha pili katika nyumba hiyo hiyo. Yule mtu alijitahidi akakata kamba alizokuwa amefungwa kisha akavunja mlango akawakuta wanaume wanne wanataka kumbaka binti mmoja aliyekuwa amelala chini katika mikono yake amefungwa kamba na nguo za binti huyo zilikuwa zimechanika chanika alipomtazama vizuri yule binti alistuka akasema :-
“”” Haaaah ?? !! Warda pamoja na kuniteka na kunifungia ndani bado unataka kumfanyia unyama binti yangu haiwezekani leo sikuachi salama umewaleta watu wambake binti yangu leo utajua mimi ni nani nani ? Ninyi washenzi mnataka kuniharibia binti yangu ??. “” Kakinga alisema maneno hayo akiwa na hasira sana.
Kakinga aliwamia wale wanaume akaanza kupambana nao, Warda alipoona balaa hilo akafungua mlango akakimbia, Pambano liliendelea kwa muda mrefu kakinga akafanikiwa kumuua mmoja kati ya wale wanne. Wengine walipoona mwenzao kapoteza maisha walikimbia wote, Kakinga alimnyanyua binti yake akamkumbatia akiwa analia kwa hasira, Kakinga alijilaumu sana kwa kuondoka nyumbani na kumuacha akwelina peke yake hadi kupelekea kupata matatizo hayo, Suala hilo lilimpatia maumivu makali sana. Kakinga aliokota ile ngozi bandia aliyokuwa amevaa warda pamoja na kifaa maalumu kinachotoa sauti ya kakinga akasema :-
KAKINGA ?? Huyu warda mshenzi sana aliniteka siku ya pili baada ya kutoka nyumbani, nilikutana nae mtaani akiwa na wenzake akaniambia niungane nae ili akachukue hiyo kampuni yao inaitwa AKWELINA sijui, Nikakaa ndio akanifungia ndani lakini Mara ya mwisho alikuja na daktari mmoja akanivisha kifaa hiki katika shingo langu sikufahamu wanataka nini kumbe lengo lao lilikuwa hili daah pole sana binti yangu .
AKWELINA ???? Huyu dada sio mtu mzuri mara ya mwisho alinisaidia nilipokaribia kushikwa na wanajeshi wengi nilipomuangalia usoni niligundua ni wewe alikuwa anafanana na wewe na sauti ni kama yako baba yangu kumbe haukuwa wewe mungu wangu mimi daah baba yangu niahidi kwamba hautanikimbia tena nisamehe baba yangu bila wewe nitakufa mimi na leo ningekuwa nimeshabakwa usiondoke tena baba.
KAKINGA ?? Ni kweli binti yangu na nahisi alitambua kama kaka yake ( Patrick ) amekuja kukufuata wewe kwa sababu anakifaa kinachompatia taarifa na siku ya mwisho alipokea ujumbe wa sauti ukimjukisha wewe upo eneo gani, Sasa kwakua wanataka vita nilikuwa mpole kwa muda mrefu sasa nataka wanitambue Mimi ni nani tuondoke binti yangu .
Kakinga alimchukua akwelina wakaondoka moja kwa moja hadi walipokuwa wanaishi mwanzo Kakinga akachukua vitu vyote vinavyomuhusu akwelina kisha wakaenda mbali sana nje ya mji ambapo palikuwa ufukweni mwa bahari katika nyumba ya mzee aliyewahi kuwasaidia kipindi cha nyuma. Nyumba hiyo ilikuwa imebomoka ,Kakinga akaitengeneza na kuiboresha akishirikiana na akwelina kazi ilikuwa ngumu sana mwisho wakafanikiwa kuifufua nyumba ile. Yalipofika majira ya usiku akwelina alimuona baba yake hana furaha akamuuliza :-
AKWELINA ?? Kwanini una mawazo baba yangu na huna furaha ? Mimi ni mzima umenisaidia baba yangu toka katika mikono ya wale watu wabaya.
KAKINGA ?? Nimekumbuka mbali binti yangu kuna mzee aliwahi kutusaidia ulipokuwa mdogo sana sisi ndio tulisababisha kifo chake kwa maana bila sisi pengine angekuwepo duniani hadi leo alafu kwenye mkono wako umefanya nini ?
AKWELINA ?? Yule dada alipokuwa amevaa ngozi ya bandia yenye sura yako aliniambia anataka kunitoa kifaa kilichopo katika mkono wangu nilimuamini nikajua ni wewe nilipata maumivu makali sana sijui alinidanganya au ni kweli alinitoa kifaa japo sijui ni kifaa gani .
KAKINGA ?? Usijali binti yangu yote anajua mungu kama alitoa au hakutoa nina hasira sana moyoni mwangu kwa mateso na manyanyaso haya hivi hawajui kama Mimi niliwahi kuwa mwanajeshi ? nilifukuzwa kazi kutokana na hasira nilikuwa mkorofi sana, nilipoacha kazi ndio niliamua kufunga ndoa sitaki kuzungumza mengi lakini nahitaji nikupatie mazoezi makali ya kijeshi najua moyoni mwako unatamani kulipa kisasi hiyo ndio sababu inayonifanya nikufundishe mazoezi makali ili upate nguvu za kutosha na nakuahidi katika kisasi chako nitakuwa nawe hadi mwisho.
AKWELINA ?? Daah ahsante baba yangu nakupenda sana nawachukia watu hao wamepoteza maisha ya wazazi wangu ipo siku nitalipa kisasi kwa ajili ya wazazi wangu nisamehe baba sitokukosea tena nakuahidi .
Akwelina alifurahi akamsogelea baba yake mlezi ( Kakinga ) akalala katika miguu yake, Baada ya nusu saa akwelina alipitiwa na usingizi katika miguu ya baba yake mlezi, Kakinga alimbeba hadi chumbani akamlaza taratibu ili asistuke na kupoteza usingizi wake. Majira ya alfajiri muda ambao usingizi unakuwa mtamu zaidi Kakinga alimwamsha akwelina , akwelina aliamka kiunyonge alipofika nje alimkuta Kakinga ame….
Akwelina aliamka kiunyonge alipofika nje alimkuta Kakinga ameshika karatasi za aina mbili , Karatasi ya kwanza ilikuwa inarangi nyeupe na nyingine ilikuwa inarangi nyeusi, Muonekano wa karatasi hizo zilimchanga akwelina kwa sababu hakutambua maana ya karatasi hizo.
“” Baba hizo karatasi zinaamana gani ? akwelina alimuuliza baba .
“” Vizuri sana binti yangu inaonesha wewe ni mchunguzi sana na kutokana na kuwa mchunguzi basi nakuahidi utafanikiwa sana katika maisha yako. Karatasi hizi ni mfano wa nafsi ya mwanadamu chochote tunachofanya sisi wanadamu kina faida na hasara ndani yake pia haya mazoezi ninayotaka kukufundisha usipokuwa makini nafsi yako itakuwa mbaya kama karatasi hii nyeusi lakini ukiwa makini nafsi yako itakuwa msaada mkubwa kwa watu wanaokuzunguka, Je upo tayari kuanza mazoezi haya ? Yalikuwa maneno ya Kakinga kwa akwelina.
Akwelina alifikiri sana maneno ya aliyoambiwa na baba yake mlezi .
“” Nipo tayari baba nakuahidi nitakuwa bora na makini katika mazoezi hayo ili niwe mwanadamu bora na mwenye nafsi nyeupe kama karatasi hiyo . Akwelina alimjibu baba akiwa anajiamini sana .
Baba ( Kakinga ) alifurahi sana. Mazoezi yalikuwa matamu katika majira hayo ya asubuhi kwa sababu yalikuwa mazoezi laini. Siku zilizofuata mazoezi yalianza kuwa magumu na yenye mateso ndani yake hali iliyosababisha akwelina aanze kuyachukia na kuyaogopa mazoezi hayo aliyokuwa anapewa na kakinga ( baba yake mlezi ) Furaha na shauku ilianza kutoweka ndani ya moyo wa akwelina kutokana na mateso aliyokuwa anayapata katika mazoezi. Baada ya mwaka mmoja kupita akwelina aliyazoea mazoezi ikapelekea akawa bingwa katika mapamba ilikuwa ngumu sana kwa kakinga kuamini uwezo aliyoupata binti yake kwa muda mfupi akasema:
KAKINGA ?? Hahaha binti yangu hakika wewe ni binti wa ajabu sana kwa uwezo ulionao kwa sasa sio rahisi kwa sababu kwa kawaida ili mwanafunzi afikie uwezo ulionao anatakiwa afanye mazoezi kwa miaka mitano ( 5 ) lakini wewe ndani ya mwaka mmoja umekuwa na uwezo mkubwa kiasi hicho duuh ajabu sana kwa uwezo wako kwa sasa inatakiwa wewe ndio unifundishe mimi sikuwezi katika mapambano hongera sana.
ITAENDELEA
Comments
Post a Comment