AKWELINA - 5

 

AKWELINA - 5

  


Simulizi : Akwelina

Sehemu Ya Tano (5)


Kakinga aliingia ndani baada ya kuzungumza maneno hayo akamuacha akwelina katika mshangao mkali sana. Baada ya wiki moja kupita ndani ya kampuni Julius aliwatuma walinzi wakamlete Patrick , walinzi walimleta patrick mbele ya kiongozi wao ( julius ) Julius akamwambia patrick :-


JULIUS ?? Nakupa nafasi nyingine Patrick nenda kamtafute akwelina na uniletee hapa akiwa hai au amekufa nenda kaungane na mdogo wako Warda Chukua wanajeshi unaowataka kwa sababu usiporudi na akwelina hapa utanijua mimi ni nani pia mchukue huyo mke wa Kakinga ( Monna ) mtumie kama chambo ili kumpata Kakinga sawa?


PATRICK ?? Sawa kiongozi wangu ahsante kwa nafasi hii nakuahidi sitokuangusha tena.


JULIUS ?? Good unaweza kuondoka.


Patrick aliondoka hadi katika chumba chake akaoga alafu akachukua simu akampigia mdogo wake ( warda ), walizungumza kwa muda mrefu wakati huo akiwa anavaa nguo. Patrick alipomaliza kuvaa nguo zake aliondoka moja kwa moja hadi katika Chumba alichokuwepo monna akamchukua kama mzigo hali iliyompatia mashaka sana monna na kumfanya ajiulize maswali mengi bila kupata majibu, Patrick alimpeleka monna ndani ya Chumba chake walipofika alimwambia :-


PATRICK?? Kesho tunaenda mjini kumtafuta Kakinga lakini lengo sio mume wako tunamtaka akwelina na nawashangaa sana mnapoteza muda angalia leo hii wewe na mume wako mmetengana na kujenga chuki kubwa Baina yako na mume wako kwa sasa mume wako hana mapenzi na wewe kwa sababu ya mtoto ambaye sio wako duuh poleni sana lakini usijali Monna Mimi nakueleza ukweli toka moyoni sijui utaniamini au hautaniamini NAKUPENDA , Nakupenda monna amini hivyo na ndio maana nimekutoa leo ili tushirikiane kumtafuta mume wako tukimpata nitamuuliza kuhusu wewe alafu utaamini haya ninayokwambia kwa sasa Mimi ndio nakupenda lakini sio mume wako tena, Chaguo lipo kwako mwenyewe. Nenda kajiandae chakula kipo tayari na hiki ndio Chumba chako kuanzia leo .


Patrick alitumia maneno mazuri kumpoteza monna ili atimize lengo lake kwakua monna alikuwa ameshakata tamaa kuhusu Kakinga aliamini maneno ya Patrick. Siku ya pili asubuhi na mapema waliondoka hadi kwa warda walipofika Warda alitia mashaka uwepo wa monna pale lakini Patrick alimtuliza. Kwakua walifika majira ya mchana Patrick alimchukua monna wakaenda ziwani kupunga upepo ( kupumzika ) walipofika ziwani walitembea huku na huko kwakua jua kali lilikuwa kali ilibidi watafute sehemu yenye kimvuli kwa mbali waliona kibanda wakakisogelea walipofika karibu Patrick alimuona Kakinga alistuka sana akampigia simu warda baada ya muda mchache wanajeshi wengi walikizunguka kile kibanda wakati huo kakinga alikuwa hajui chochote.


Monna akamwita Kakinga , sauti ya monna ilimstua Kakinga kwakua alikuwa anaitambua, Kakinga alipogeuka alimuona monna akiwa na Patrick kakinga alipotaka kuingia ndani alipigwa sindano ya madawa. Sindano hiyo ilimvunja nguvu ( kupoteza nguvu ) kakinga akadondoka chini wale wanajeshi wakamchukua Kakinga wakamfunga kamba walipotaka kuondoka mbele yao walimuona akwelina …….


Walipotaka kuondoka mbele yao walimuona akwelina wanajeshi wote walinyanyua silaha zao juu wakajiandaa kumshambulia akwelina kabla ya kufyatua risasi Patrick aliwaziwia wanajeshi wake akasema kwa dharau :-


PATRICK ?? Hatuwezi kupoteza risasi zetu kwa binti kama huyu sisi ni wanaume mfungeni kamba na yeye kwa sababu lengo letu lilikuwa ni huyu binti .. Oooh hahaha akwelina ama kweli wewe ni mali ya pekee katika kampuni yetu yenye jina kama lako nikikuangalia nakosa jibu hivi Steven baba yako alifikiria nini kuweka ufunguo wenye thamani ndani ya mwili wako, Sijui alifikiria nini na ndio maana alikufa mapema alikuwa mjinga sana.


AKWELINA ?? Weee baba yangu hakuwa mjinga wewe chunga kauli yako hiyo ??


PATRICK ?? Mjinga tu sasa leo hii upo katika mikono yangu sasa ndio nini, alifanya ujinga pia alisahau kwamba siku zote mwanamke atabaki kuwa mwanamke tu, askari wangu fanyeni kazi yenu.


Maneno ya kejeli kutoka kwa patrick yaliutesa moyo wa akwelina mapigo ya moyo yalibadirika ghafla kutokana na hasira zilizomvamia akwelina, Wanajeshi ( askari ) walimfikia akwelina walipomgusa akwelina aliwashambulia kwa muda mfupi na hakuna aliyekuwa mzima, kitendo hicho kiliwastua wanajeshi wote hakuna aliamini kama akwelina anauwezo mkubwa kiasi kile , Wanajeshi walipoona wenzao wamepoteza maisha walishikwa na hasira wakatupa silaha chini wote wakamvamia akwelina, Kwa uwezo aliokuwa nao akwelina alitumia dakika kadhaa akawamaliza wote akabaki Patrick na monna wanatazamana, Patrick alikuwa anameza mate kwa hofu na woga.


Akwelina aliwasogelea Patrick pamoja na monna kabla hajawafikia alisikia sauti ya kike ikisema :-


“” Tulia hapo hapo binti kakinga kwa usalama wa baba yako piga magoti alafu weka mikono juu haraka “” Yalikuwa maneno ya warda .


Akwelina aligeuka akamuona msichana aliyetaka kumfanyia unyama mwaka mmoja uliopita ameweka kisu katika shingo la baba yake kipenzi na tegemeo la maisha yake, ilibidi akwelina afanye kama alivyoambiwa na warda Patrick alitumia nafasi hiyo hiyo akamfuata akwelina akamfunga kamba, Baada ya kumfunga kamba walimchukua akwelina pamoja na kakinga wakaondoka nao hadi ndani ya msitu mnene na wenye kutisha. Kakinga akiwa na akwelina walipata mateso makali sana kutoka kwa watu waliojifunika nyuso zao.


Ulipita mwezi mmoja , mwezi huo ulikuwa wenye mateso ndani yake kwa mateso waliyokuwa wanayapata Kakinga na akwelina walitamani kufa, Siku hiyo majira ya usiku monna alijitokeza mbele yao ?? Ilikuwa vigumu kwa kakinga kumuona monna mbele yake :-


“” Habari kakinga mume wangu kipenzi daah muda mrefu sijakuona mume wangu “” yalikuwa maneno ya monna.


“” Samahani dada baba yangu hana mke .Baba huyu mwanamke ni nani ?

Akwelina alimjibu monna na kumuuliza baba yake ( kakinga )


“” Akwelina binti yangu jaribu kuwa mtulivu huyo alikuwa mke wangu kipindi cha nyuma kabla hajaniacha pia unatakiwa umuheshimu sana kwa sababu yeye ndio aliyeokoa maisha yako kipindi ukiwa mdogo mama yako mzazi kabla hajapoteza maisha alimkabizi mtoto ambaye ndio wewe “” Kakinga alimjibu akwelina.


Majibu ya kakinga yalimshangaza sana akwelina na kutokuamini kama mwanamke aliyembele yake ndio aliyesaidia maisha yake, Kakinga akaendelea kusema :-


“” Jina lake anaitwa monna ni msichana aliyekupenda kipindi cha nyuma wakati huo alikuwa yupo tayari kupoteza maisha yake kwa ajili yako hakika alikuwa zaidi ya mama kwako na sio kwako pekee msichana huyo alikuwa ananipenda kuliko msichana yeyote hapa dunia lakini alichonifanyia siwezi kumsahau hadi siku nitayokufa Mimi.


Kakinga alimaliza kuzungumza maneno hayo, Monna akiwa analia sana. Monna alilia kwa muda mrefu mwisho akasema :-


MONNA ?? Akwelina mama yako mzazi bado yupo hai ni mzima wa afya japo yupo sehemu mbaya .


AKWELINA ?? Unasemaje ? ?? Mama yangu yupo wapi …..



AKWELINA ?? Unasemaje ? ?? Mama yangu yupo wapi ?


MONNA ?? Mama yako akwelina yupo usijali nitakuelekeza sehemu anapopatikana lakini muda hautoshi nimekuja hapa kuwasaidia mtoke sehemu hii kwa sababu kesho daktari bingwa anafika hapa Tanzania kutoka nje ya nchi. Najua kakinga unanichukia na huniamini tena kutokana na vitu nilivyokutendea. Mimi nakubali endelea kunichukia lakini tambua nakupenda sana na ndio maana nafanya yote haya mipango yao yote naifahamu sina mengi ya kuzungumza eneo hili.


Monna aliwafungua kamba haraka haraka kisha wakaondoka eneo hilo. Usiku ulizidi kukomaa monna na wenzake waliendelea kukimbia ndani ya msitu huo japo msitu huo ulikuwa unatisha mno, kakinga akiwa anakimbia alisimama ghafla. Kitendo hicho kiliwashangaza monna na akwelina ikabidi wasimame pia.


“” Kuna nini baba mbona umesimama ? akwelina alimuuliza baba .


“” Nimechoka kukimbia kila siku narudi eneo lile nahitaji kuanza kazi yangu kwa sasa sina hofu tena binti yangu umeshakuwa mkubwa ninaamini Unaweza kuishi maisha yeyote hata kama nikiwa nimekufa sasa Kwanini niendelee kukimbia hovyo hapana narudi kupambana nao wamenitesa sana washenzi hawa “”… Kakinga alimjibu akwelina akiwa na hasira zilizopiliza hadi kupelekea mwili wake kutetemeka.


Monna na akwelina walijaribu kumshawishi kakinga ili waendelee na safari lakini ilikuwa ngumu sana kakinga kukubali kuendelea na safari. Kakinga hakuzungumza tena aligeuka alipotoka akarudi kwa kukimbia kwa kasi sana, ilibidi akwelina na monna wamfuate nyuma. Walipokaribia eneo lile kakinga alisimama akasogea katika kichaka akatulia, akwelina alimsogelea kakinga akamwambia:-


AKWELINA ?? Kuna nini baba sijakuelewa kabisa japo umesema hauhitaji kuendelea kukimbia ?


MONNA ?? Jamani narudia tena muda hautoshi Patrick atafika hapa muda wowote na hatokuwa peke yake atakuja na askari wa kutosha na lengo lao wanataka kuupata ufunguo uliopo ndani ya mwili wa binti huyu akwelina mshauri baba yako kwa sababu wewe ndiyo anakusikia sana tuondoke jamani .


KAKINGA ?? Nisikilize monna kwanza tunashukuru kwa msaada wako lakini leo nahitaji kuonesha kitu kwa hawa wajinga najua lazima watakuja eneo hili lengo langu namtaka Patrick ili anipeleke huko katika kampuni yao leo.


MONNA ?? Njia hiyo hata mimi naifahamu nitawapeleka kakinga hebu jaribu kuelewa hapa sio sehemu salama na…


Kabla monna hajamaliza kuzungumza ulisikika mlio wa risasi , mlio huo uliwastua wote ghafla monna akadondoka chini, Kakinga na akwelina wakiwa katika mshangao mkali walizungukwa na askari wengi. Patrick akajitokeza akiwa na kisu hakuzungumza kitu alimfuata Monna wakati huo monna alikuwa chini akitokwa na damu nyingi akashika shingo lake akasema :-


PATRICK ?? Sikiliza wewe binti unatupatia ufunguo ulionao au nichukue maisha ya huyu mshenzi aliyetusaliti kweli unampenda sana mume wako huyu wa zamani , Binti unatupatia ufunguo au hutupatii zungumza haraka.


Patrick alipoona kimya kimezidi alipitisha kisu katika shingo la monna, monna alipiga kelele kali sana kelele zilizojaa simanzi , akwelina alimuonea huruma monna akasema ;-


AKWELINA?? Muache , Muache tafadhali nipo tayari kuwapa ufunguo alisaidia maisha yangu siwezi kukubali apoteze maisha kwa ajili ya ufunguo .


KAKINGA ?? Hapana akwelina hapana usikubali kutoa ufunguo .


PATRICK ?? Nilikueleza monna Kakinga hakupendi tena umeona , Sikia binti ufunguo upo wapi ?


AKWELINA ?? Upo ndani katika tako langu .


Patrick na wenzake walicheka sana walihisi akwelina anawatania..


“” Kweli siwatanii ufunguo upo ndani ya tako langu “”.. akwelina alimjibu Patrick .


Patrick alimsogelea akwelina akamvua suruali aliyokuwa ameivaa, Kakinga aligeuka pembeni hakuhitaji kuona mwili wa binti yake. Akwelina hakuleta kipingamizi chochote kwa sababu alihitaji kusaidia maisha ya monna, Patrick alifanikiwa kutoa ufunguo ndani ya tako la akw Chakwelina cha ajabu kilichotokea mbele ya macho ya Kakinga alimuona monna anasimama akiwa mzima, monna alimsogelea Akwelina akacheka sana :-

“” Pole sana binti yangu huruma yako imekuponza huu ulikuwa ni mtego pia nilihitaji kujua kitu kweli Kakinga hunipendi lakini ahsante tumefanikiwa kupata ufunguo huu.. Yalikuwa maneno ya monna .


Monna akiwa anajisifia na kuzungumza maneno ya dharau kwa akwelina, Monna alistuka amewekewa bastola kichwani alipogeuka alimuona Patrick akasema :-


“””” Hahahha hata wewe nilikutumia tu huna thamani tena mbele yangu unahitajika kufa monna …. Patrick alimwambia monna.


Wakati Patrick anazungumza na monna Kakinga ali……


____Leo imekuwa fupi kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu kesho tutakuwa pamoja mungu akipenda.




Wakati Patrick anazungumza na monna Kakinga alisimama kwa kasi sana akamvamia patrick kwakua patrick alikuwa hajajipanga ilikuwa rahisi kakinga kumshinda patrick. Wanajeshi waliokuja na patrick walipotaka kumsaidia kiongozi wao walimuona Patrick amenyanyua mikono juu akiwa amewekewa bastola kichwani kakinga akasema :-


KAKINGA ?? Wekeni silaha zenu chini haraka kabla sijafumua ubongo wa kiongozi wenu .


Wale wanajeshi walitaka kupinga kauli ya kakinga , Patrick akasema kwa nguvu akiwa anatetemeka mwili mzima kwa hofu ya kupoteza maisha yake :-


PATRICK ?? Weka silaha chini harakaaaaaa pumbafu ninyi ??


Wanajeshi wote waliweka silaha chini kakinga hakupoteza muda alimnyanganya ufunguo Patrick alafu akampatia akwelina kisha akasema:-


“”” Binti yangu ondoka haraka eneo hili kimbia nenda mbali, Usiwe na wasiwasi kuhusu maisha yangu hata kama nikipoteza maisha leo hii usijali nenda kasaidie dunia binti, Kuna watu wengi wanahitaji msaada kutoka kwako usipoteza muda nenda kawasaidie ??.


Maneno ya kakinga yalimtoa machozi akwelina aliondoka japo nafsi yake ilikuwa inatamani imsaidie kakinga ( baba yake mlezi ) akwelina aliondoka kwa kukimbia hali ya kuwa alikuwa na maumivu makali sana katika tako lake. Kakinga alizidi kumtazama akwelina anavyo ondoka mwanajeshi mmoja aliyekuwa nyuma ya kakinga alisimama kimya kimya akamnyanganya bastola kakinga, baada ya kumnyanganya bastola wanajeshi wote walisimama wakaanza kumpiga kakinga.


Akwelina alizidi kukimbia ndani ya msitu huo wenye kutisha bila kutambua kama kakinga yupo kwenye matatizo, safari ya akwelina ndani ya Msitu huo ilikuwa ndefu sana hatimae akatoka nje ya msitu huo, Akwelina alianza kupata faraja baada ya kuona makazi ya watu ( miji ).Patrick na wenzake waliendelea kumpiga kakinga bila huruma, kipigo kilipozidi kakinga alipoteza fahamu wakamchukua kisha wakaondoka nae.


Yalipofika majira ya asubuhi akwelina alikuwa amelala ndani ya mtaro mkubwa ulikuwa unapitisha maji machafu katika mtaa aliokuwepo, Milio ya magari mbalimbali katika eneo lile ilimstua akwelina alisimama baada ya kuamka akatazama eneo hilo eneo hilo lilikuwa geni kwake ikabidi amulize mwanaume mmoja mpita njia akatajiwa jina la eneo hilo :-


“” Duuh sipajua hapa kaka yangu “” akwelina alimjibu yule mpita njia.


“” Wewe umetoka wapi “” mpita njia alimuuliza akwelina …


Akwelina alimjibu yule mpita njia sehemu anapoishi .


“” Pole sana dada huko unapotoka na hapa ni mbali sana unaweza kutumia masaa sita kufika eneo hilo kama ukipanda gari nauli ni shilingi elfu arobaini ( 40,000/= ) .”” yalikuwa maneno ya mpita njia akimueleza akwelina. Baada ya maelezo hayo mpita njia aliondoka akwelina alikaa chini kichwa kikamuuma sana kwa sababu alikuwa hana pesa yeyote na lile jeraha lilizidi kumtesa kwa kumpatia maumivu makali sana. Baada ya masaa matatu kakinga alirudisha fahamu akajikuta yupo kwenye gari ilionesha kuna sehemu anapelekwa ingawa alikuwa hajui wapi anapelekwa. Ilichukua muda mrefu kufika sehemu walipokuwa wanakwenda, Walipofika kakinga aliona neno kubwa limeandikwa AKWELINA ilimshangaza sana kuona jina la binti yake katika sehemu hiyo .


Hali ilizidi kuwa mbaya kwa akwelina kutokana na kutokwa na damu nyingi ghafla alishikwa na kizunguzungu akaondoka chini, watu walimpita kama hawamuoni japo eneo hilo watu walikuwa wengi wanaopita, akwelina alijaribu kujivuta kwa kutumia mikono yake lakini alishindwa akachukua ufunguo ambao alikuwa ameushika akauweka akaumeza bila maji kwa hofu ya kuupoteza. Katika watu waliokuwa wanapita Kijana mmoja mdogo alimuona binti anaomba msaada yule kijana alimwita kaka yake, Kaka alipofika alimbeba akwelina wakampandisha kwenye gari wakaondoka kuelekea hospital kwa sababu hali yake haikuwa nzuri.


Patrick na wenzake walipofika ndani ya kampuni walimfuata Julius wakamweleza yote yaliyowakuta Julius alichukia sana akachukua kipande cha chuma akamfuata kakinga akampiga nacho, Julius alitumia chuma hicho kama fimbo katika mwili wa kakinga. Kakinga alipasuka sehemu mbalimbali katika mwili wake damu zilimtoka kama maji, Julius hakuridhika akachukua kisu kilichokuwa katika kiuno cha Patrick akamfuata kakinga akasema:


“””Leo ndio mwisho wako umenisumbua kijana wewe “”


Julius alishika kisu vizuri alipotaka kumchoma kakinga , Monna alijitokeza mbele ya kakinga kile kisu kika…….



Kile kisu kikamchoma monna katika kiganja cha mkono kwa kasi ya kisu kile kilitoboa kiganja cha monna na kumuachia maumivu makali yalimfanya monna apige kelele kali:


“” Wewe msichana umetumwa au ndio mapenzi ya kweli , unabahati sana kisu hiki kuchoma katika kiganja cha mkono wako laiti kama kingefika katika tumbo lako hakika usingepona leo mpumbafu kabisa, Patrick mtoe mbele yangu huyu mwanamke mjinga anapiga fujo , Kakinga leo umepona kesho hautapona ninyi wawili peleka chumba cha giza hii takataka..””


Yalikuwa maneno ya Julius baada ya kumchoma kisu Monna. Patrick alimchukua Monna kisha akaondoka nae kama alivyoambiwa na Julius , Wanajeshi wawili walimpeleka kakinga ndani ya chumba cha giza walipofika ndani ya chumba hicho walimfungua pingu alafu wakaondoka. Baada ya masaa kadhaa kupita akwelina aliamka toka katika usingizi mzito baada ya kufumbua macho yake alimuona kijana mmoja mzuri akimtazama akwelina alizidi kuzungusha macho huku na huko akagundua yupo hospital.


“”” Nesiiii tafadhali njoo Mgonjwa wangu kafumbua macho “”” Yule kijana alimwita nesi .


Nesi alikuja akamfanyia vipimo akwelina alipogundua hali yake ipo vizuri alichukua karatasi nyeupe akaandika kisha akampatia yule kijana akasemwambia :-


NESI ?? Hakikisha unanunua dawa hizo zilizoandikwa hapo.


Yule nesi alimgeukia akwelina akaendelea kusema :-


NESI ?? Pole sana binti kwa sasa upo sawa hali yako sio mbaya hakikisha unasafisha donda lako ili liwahi kupona pole sana mungu atakusaidia utapona .


Akwelina alimshukuru sana yule kijana kwa msaada aliompatia, yule kijana alimpatia nguo Mpya akwelina kwakua hali haikuwa mbaya sana kwake alisimama akaenda chooni akabadirisha nguo kwa sababu nguo zake zilikuwa chafu sana, alipotoka chooni akwelina alisimama mbele ya yule kijana akasema :


AKWELINA __ ahsante sana kaka kwa msaada wako naomba nirudi nyumbani kwa sababu ninamengi ya kufanya japo naishi mbali eneo hili .


KIJANA__ Pole sana dada yangu naomba chukua business card yangu hii kama hautajali ukifika unapokwenda utanitafuta siku moja tunaweza kuonana yamungu mengi pia chukua pesa hizi zinaweza kukusaidia huko uendapo usizikatae pesa hizi nimependa kukupa toa wasiwasi dada yangu pia subiri nikuletee dawa zako sawa.


Pesa zilikuwa nyingi sana akwelina alizipokea zile pesa akiwa haamini kama angeweza kupata pesa kama zile , akwelina alimshukuru sana mungu akachukua zile pesa. Yule kijana hakuchelewa alirudi haraka akampatia dawa, Akwelina alimshukuru sana yule kijana akaondoka hadi stenti ya magari akapanda gari ili arudi nyumbani, akiwa ndani ya gari akwelina alikuwa na mawazo sana hadi machozi yalimtoka kwa uchungu na hasira alizokuwa nazo, Gari hilo lilichukua muda mrefu kufika jijini alipokuwa anaishi akwelina, Kwa bahati nzuri walifika salama njia ilikuwa moja kwa akwelina alienda nyumbani kwao. Mazingira ya nyumbani kwao yalikuwa machafu kutokana na kutokuwepo kwao kwa muda mrefu.


Akwelina aliweka mazingira sawa kisha akaingia ndani. Yalipofika majira ya usiku akwelina alitoka nje akiwa na mawazo sana, akwelina akiwa ndani ya timbwi hilo la mawazo alistuka kumuona kakinga mbele yake ilibidi asimame kwa furaha alimkumbatia lakini cha ajabu alikumbatia hewa, Akwelina alicheka sana peke yake kama kichaa akajipiga makofi kichwani kwake ili kuondoa mawazo. Majira ya asubuhi yalipofika akwelina aliingia ndani akavaa nguo zake za mazoezi akaanza kupiga mazoezi japo kidonda chake kilikuwa bado kibichi , Siku hadi siku akwelina aliendelea kufanya mazoezi kwa bidii. Akwelina alifanya mazoezi kwa miezi mitatu bila kupumzika usiku na mchana , Mazoezi hayo yaliujenga mwili wa akwelina na kuupatia nguvu za kutosha. Siku moja majira ya jioni akwelina alikuwa barabarani akifanya mazoezi ya kukimbia kwa mbali alimuona msichana anakuja mbele yake nae akiwa anakimbia kwa muonekano alikuwa anafanya mazoezi , alipomkaribia aligundua yule msichana ni warda Akwelina ali.



Akwelina alihamia upande wa pili wa barabara Warda akiwa hajui chochote alizidi kumsogelea akwelina alipofika karibu zaidi akwelina alimshika mkono, Warda alishangaa sana akautazama mkono uliomshika , Mkono huo ulizidi kumshangaza warda kwa sababu ulikuwa unatetemeka mno, warda alipoitazama sura ya aliyemshika hakuamini kama ni akwelina. Kutokana na hasira alizokuwa nazo akwelina alimpiga sana warda, kipigo hicho kilimfanya warda apoteza fahamu akwelina akambeba warda kisha akaondoka nae na kuwaacha wapita njia midomo wazi.


Baada ya masaa manne kupita warda alirudisha fahamu akajikuta yupo kwenye kiti amefungwa kamba sehemu aliyokuwepo kulikuwa na giza nene lenye kutisha , warda alianza kutetemeka mapigo ya moyo wake yalizidi kwenda mbio.. Ghaflaaaa akatokea akwelina mbele yake akiwa ameshika nyundo warda alipiga kelele Akwelina akasema:-


“” Shiiiiiiiiiiiiii ‘ kimya hakuna atayeweza kukusaidia eneo hili hata upige kelele kiasi gani. Bado Sijasahau unyama wako siku ile kama ungefanikiwa leo hii nisingekuwa akwelina huyu wa sasa hivi, Kwanza ungeniathiri kisaikologia, Pili nisingekuwa bikra tena sasa leo nalipa unyama wote ulionitendea Mimi na baba yangu kipenzi “””


Maneno ya akwelina yalizidi kumzidishia wasiwasi warda, akwelina alisimama akaanza kumzunguka warda akiwa na nyundo mkononi akwelina alitumia nyundo hiyo kama fimbo katika mwili wa warda, Warda alipata maumivu makali sana baadhi ya viungo vya Warda viliteguka na kuvunjika kutokana na hasira alizokuwa nazo akwelina hakuchagua sehemu ya kupiga na hakuwa na huruma tena.


“”” Usiniue akwelina nisamehe nipo tayari kukupeleka sehemu ambayo baba yako yupo aaaaah … Ooooh mama nakufa mimi leo oooh mungu nisaidie nakufa mimi nisamehe akwelina mama nisamehe ????


Yalikuwa maneno ya warda akilalamika kutokana na kipigo alichokuwa anakipata. Pamoja na kulalamika kiasi hicho bado haikusaidia kitu akwelina aliendelea kushusha kipigo bila huruma :-


“”” Nisamehe binti yangu sina kosa mimi yote amesababisha kaka yangu patrick alimchukua mtoto wangu akiwa bado mdogo sana mtoto niliyempata katika ndoa yangu Mimi na kakinga baba yako japokuwa kakinga hadi sasa anatambua siku ile hospital wakati wewe ulipokuwa mdogo nilitoa mimba sio kweli sikutoa mimba mdogo wako yupo akwelina “”


Baada ya maneno hayo akwelina aliacha kumpiga warda akamuuliza :-


AKWELINA __ Unasema mdogo wangu mtoto wa baba yangu ! nieleze yupo wapi muda huu na ukinidanganya hutoki salama leo.


Hapana siwezi kukudanganya akwelina nakumbuka miaka mingi imepita nilipewa kazi na kaka yangu ambaye ndio huyo patrick , Tulitengeneza ajali na tukafanikiwa lakini ndani ya kazi hiyo nilimpenda baba yako ( kakinga ) nilitokea kumpenda sana nikaamua kufunga nae ndoa, nilipofunga ndoa nae Patrick pamoja na Julius walichukia sana wakaniambia nivunje ndoa yangu kipindi hicho tayari nilikuwa mjamzito nilipinga walichotaka , wakaniambia nimdanganye kakinga kwamba ujauzito wake nimeutoa. Kwa bahati nzuri nikasikia kakinga ametoroka kipindi hicho wewe ulikuwa mdogo sana, nilitunza mimba ile hadi nilipojifungua mtoto wa kiume walimchukua Mtoto wangu siku hiyo hiyo daah ?? inaniuma sana baada ya kumchukua waliniambia siku nikikupeleka wewe ndio watanipatia Mtoto wangu na siku ile nilipovaa ngozi ya bandia nilifanya vile ili nikupate lengo nikupeleke ili nikamchukue Mtoto wangu ningefanyaje Mimi akwelin ? Ukweli sikupenda kukufanyia unyama wote huo lakini Mimi ni mzazi nilihitaji kumsaidia mtoto wangu lakini hadi leo siitambui sura ya mtoto wangu ??


Warda alimaliza kumsimulia akwelina maisha yake kwa ufupi akiwa analia sana, Japokuwa akwelina alikuwa na hasira lakini alishikwa na hudhuni mno, roho ya huruma ilichukua nafasi yake ndani ya moyo wa akwelina akadondosha ile nyundo chini akalia kwa uchungu ghafla akaacha kulia akasimama akamfuta warda akamwambia :-


AKWELINA __ Nipeleke sehemu baba yangu yupo nahitaji kumsaidia kakinga baba yangu kipenzi ..


Akwelina akamfungua kamba warda akampeleka katika kitanda kwakua warda alikuwa ameumia sana akwelina alimpatia huduma ya kwanza Warda akamshukuru akwelina kwa kumsamehe. Usiku huo huo akwelina alienda duka la madawa ( pharmacy ) akanunua dawa nyingi kisha akamuuliza mtoa huduma :-


AKWELINA __ Samahani dada leo imepita miezi kadhaa niliwahi kumeza ufunguo kwa bahati mbaya na kila nikienda chooni kwenye kinyesi siiuoni tatizo ni nini au daah hata sielewi ?


MTOA HUDUMA __ Ni kweli inawezekana kutokana na mmeng’enyo wa chakula lakini usijali nitakupatia dawa itayolainisha kinyesi tumboni kwako nahisi ufunguo huo unaweza ukatoka.


Akwelina alinunua dawa hiyo, alipofika nyumbani alitumia dawa aliyopewa baada ya dakika tatu tumbo lilianza kuuma akaenda chooni na wavu wake ambao alikuwa anautumia kila siku . Siku hiyo aliharisha sana kwa bahati nzuri akauona ufunguo ule alifurahi mno.


Yalipofika majira ya asubuhi na mapema ndani ya kampuni kakinga alikuwa bado yupo katika mateso makali sana , siku hiyo Julius aliingia katika chumba alipokuwepo kakinga akiwa na kijana mwenye miaka kumi na tano, Yule kijana alipomuona kakinga ametapakaa damu mwili mzima na akiwa amefungwa kamba alimuuliza Julius :-


“”” Huyo ni nani ambaye ametapaa damu mwilini mwake ?


JULIUS ___ Huyo ni baba yako mzazi



JULIUS ___ Huyo ni baba yako mzazi ..


Julius alitambua kijana bado hajamuelewa akaendelea kusema :-


JULIUS ___Natambua hujanielewa #BILALI huyo unaemuona mbele yako ni baba yako mzazi, Kwanini nasema ni baba yako ? Kwa sababu mama yako asingeweza kukuzaa wewe bila kubakwa na baba yako ambaye ndio huyo hapo .


BILALI ___ Mimi nimepatikana kwa kubakwa!! ?? hapana sio kweli alafu kwanini miaka yote nipo eneo hili na siku zote nambua wewe ndio baba yangu inakuaje leo unaniambia mambo kama haya ?


JULIUS ___ Upo sahihi bilali niliamua kukuchukua wewe kutokana na hali ya mama yako , Mama yako alikuwa anamaisha magumu sana lakini baba yako huyo hakuwa na huruma alimbaka na kumpatia ujauzito alafu akamkimbia , Mama yako aliishi kwa tabu sana hadi alipojifungua katika hospital ambapo nilikuwa nafanya kazi miaka ya nyuma.


BILALI ___ Mama yangu yupo wapi ?


JULIUS___ Mama yako alifariki siku ambayo anakuzaa wewe ( kujifungua ) kwakua Mimi ndio nilimsaidia kujifungua niliumia sana nikaamua kukuchukua wewe ili nikutunze na niliweka ahadi kwamba nitamtafuta huyo mshenzi alimsababishia kifo mama yako kwa bahati nzuri mama yako alinisimulia na picha ya huyu mjinga alinipatia, Nilimtafuta na nikampata leo hii yupo mbele yako utajua wewe utamfanyaje kwa ajili ya kifo cha mama yako …


Bilali alihisi kizunguzungu kwa kusikia maisha ya mama yake kabla hajapoteza maisha kama Julius alivyomueleza, Alishikwa na hasira mno bilali akamsogelea kakinga , Akautazama mwili wa kakinga akaona vidonda vipo vingi sehemu kubwa ya mwili wa kakinga , Bilali alisimama akatazama huku na kule akaona kipande cha chuma ambacho kipo ndani ya chumba hicho kwa ajili ya kumpatia adhabu kakinga, Bilali aliokota kile kipande cha chuma akarudi akachukua kile chuma akachoma katika kidonda kikubwa katika mwili wa kakinga. Kakinga alilia sana na kupiga kelele zenye maumivu makali ndani yake , Bilali hakuridhika akatupa chuma akatumia mikono yake kuendelea kufinya vidonda vya kakinga bila huruma kwakua vidonda vilikuwa vibichi maumivu yalikuwa makali sana ????????

__ “”” Kufa mshenzi wewe umembaka mama yangu na kumsababishia kifo sikuachi salama kufa kufa kufaaaaaaaaaa “””

Bilali alisema maneno hayo kwa hasira akiendelea kufinya ( kubinya ) vidonda vya kakinga, Bilali bado hakuridhika alisimama akamfuata Julius akachomoa bastola iliyokuwa kiunoni akahitaji kumpiga risasi kakinga Julius akamziwia kisha akamwambia :-


JULIUS __Tulia kijana wangu mtu kama huyu unatakiwa umpige risasi mbele ya macho ya watu ili kila mwenye tabia kama yake ajifunze kupitia yeye.


Julius alimchukua bilali akaondoka nae, Kakinga akiwa bado anamaumivu alisema moyoni kwake akiwa analia :-

“”” Ewe mungu nimekukosea nini Mimi ni bora unichukue kuliko mateso ninayopata ????.


Baada ya mwezi mmoja kupita warda alipata nafuu viungo vilivyovunjika vilirudi katika hali yake kama mwanzo. Siku hiyo akwelina hakuwepo nyumbani alikuwa ameenda mbali na nyumbani kwa ajili ya kufanya mazoezi ya kutuliza akili, Akwelina alitumia muda mrefu sana katika mazoezi hayo jioni ilipofika akwelina alirudi nyumbani alipoingia ndani cha ajabu hakumuona warda, akwelina alimtafuta warda sehemu zote lakini hakumuona, Wakati huo warda alikuwa njiani anarudi nyumbani kwake japo hali yake haikuwa nzuri lakini alijitahidi kutembea hivyo hivyo ilimchukua muda mrefu sana kufika nyumbani kwake. Alipofika nyumbani alichukua silaha pamoja na vitu vyenye thamani kwake kisha akaondoka ili kurudi kwa akwelina. Usiku ulipotanda akwelina alikuwa yupo nje akiwa na mawazo sana ghafla akamuona warda akiwa na begi kubwa akwelina alifurahi kwa sababu alitambua bila warda hawezi kutambua sehemu Kakinga alipopelekwa, Akwelina alimsaidia warda wakaingia ndani .


Siku ya pili majira ya asubuhi wanajeshi walimchukua kakinga wakamfunga katikati ya uwanja mkubwa ndani ya kampuni hiyo , wakamchapa fimbo nyingi mbele ya watu wote wanaoishi ndani ya kampuni hiyo baada ya kumchapa sana alikuja Julius akiwa na bilali walipofika Julius alisimama akachukua kipaza sauti akasema :-


JULIUS ___ Leo ni siku muhimu sana kijana mnaemuona hapo alifanya unyama kwa msichana mmoja na kusababisha kifo chake na huyu ndio mtoto wa msichana huyo ambaye ni marehemu, Leo kijana huyu anataka kulipa kisasi BILALI kijana wangu muda ndio huu unesha upendo kwa mama yako hata huko alipo afurahi.


BILALI alichukua panga akamfuata kakinga alipo akaweka panga katika shingo la kakinga, Kakinga alifumba macho akiwa anatabasamu :-

“” Ahsante mungu kwa kusikia kilio changu “”” yalikuwa maneno ya kakinga. Bilali alinyanyua panga juu kisha aka….



Bilali alinyanyua panga juu kisha akashindwa kushusha panga lile katika shingo la kakinga baada ya kumuona Kakinga anatokwa na machozi, Julius alishindwa kumuelewa bilali kwa kumuona anashindwa kukata kichwa cha Kakinga :-


“” Maliza kazi bilali unafikiri nini “”


Julius alizidi kumpatia ujasili bilali lakini pamoja na Julius kumlazimisha bado nafsi ya bilali iligoma kukata kichwa cha Kakinga ilimchukua muda mrefu sana kufanya maamuzi ghafla alikaza mikono yake akashusha panga kwa kutumia nguvu nyingi watu wengi waliokuwa eneo hilo walifumba macho kwa muda walitambua bilali amekata kichwa cha kakinga, Julius alifurahi mno Julius alicheka zaidi kwa furaha cha ajabu alimuona bilali anamshika mkono kakinga akasimama nae kakinga akiwa hai bilali akamsogelea Julius akiwa amemshika mkono Kakinga alipofika karibu yake akamwambia :-


BILALI ?? Huyu ndiye baba yangu haijalishi nimepatikana kwa njia gani lakini bado atabaki kuwa baba yangu , Mama yangu hayupo duniani nikimpoteza na baba nitakosa furaha ya milele nimeamua kumsamehe baba yangu kwa sababu katika upatikanaji wangu alipanga mungu baba yangu hanakosa katika hilo .


JULIUS ?? Mtoto mjinga sana wewe pumbafu sikutegemea kama utakuwa mjinga kiasi hiki .


KAKINGA ?? Jina lako unaitwa bilali ? Sikia kijana Mimi sina mtoto japo nina mtoto wa kumlea maisha yangu yote sikubahatika kupata Mtoto huyu Julius anakudanganya muulize baba na mama yako wapo wapi lakini sio mimi, Sikutaka kukuambia haya yote kwa sababu nilikuwa nahitaji kufa kwakua umeshindwa kuniua ndio maana nakueleza haya Mimi sio baba yako.


JULIUS ?? Baba mjinga kama mtoto wake bilali ni mtoto wako aliyemzaa warda. Warda alikudanganya kwamba mimba waliitoa lakini sio kweli warda alijifungua mtoto nikamchukua na nilimpatia adhabu kwamba ili nimpatie Mtoto wake lazima aniletee akwelina mbele yangu na una bahati sana nilitaka damu yako leo ichukue maisha yako.


Julius alijisahau akaendelea kutoa siri mbele ya bilali kutokana na hasira alizokuwa nazo baada ya Bilali kushindwa kumkata kichwa Kakinga. Bilali hakuamini kama alikuwa anadanganywa bilali alichukia sana akamuuliza Julius akiwa jaziba:


BILALI ?? Bado sijaamini kama ulikuwa unanidanganya kwanini umenifanyia hivi kwaniniiiii !!!??


JULIUS ?? Weee tuliza kichwa chako hicho unamkaripia nani hapa ? mwenye umri kama wako pumbafu , sikia wewe bilali nilitaka leo umalize maisha ya baba yako ili nitimize malengo yangu ya kukulea ni kweli mama yako yupo hai pia kakinga hakumbaka mama yako. Umetambua ukweli utanifanya nini sasa ??


Mwili wa bilali ulisisimka kwa hasira hali iliyomfanya bilali amvamie Julius na kumshushia kipigo , Julius alipoona anapigwa na jabar alimwita mwanajeshi wake mkuu kwa sauti ya juu “”””” MTAWALAAAAAA “”” sauti hiyo ilimfikia mtawala alipokuwepo na kumfanya afike eneo husika haraka sana, Mtawala alipofika alimshika mguu bilali akamtupa mbali, bilali alipogeuka kumtazama aliyemtupa Alimuona mwanajeshi mmoja mwenye mwili mkubwa mno , Bilali alisimama japo alikuwa mdogo lakini alikuwa anajiamini na jasili sana, bilali alikimbia kwa kasi akamvamia mtawala bado haikusaidia kitu kutokana na nguvu alizokuwa nazo mtawala. Bilali alipigwa sana, mtawala alishika shingo la bilali alipotaka kumnyonga kakinga alisimama akampiga mtawala ngumi moja ambayo iliwashangaza macho ya watu , Mtawala alishuka chini na kupoteza maisha papo hapo. Julius hakuamini kama kakinga anauwezo mkubwa kama ule wanajeshi walipoona balaa hilo walimpiga kakinga sindano ya sumu akadondoka chini akapoteza fahamu wakamchukua kakinga pamoja na bilali wakawapeleka katika chumba cha giza .


Usiku wa siku hiyo akwelina na warda waliendelea kufanya mazoezi kwa bidii , baada ya kufanya mazoezi walisafisha miili yao wakatulia warda akamwambia akwelina


WARDA ?? Kesho inatakiwa tuanze safari ya kwenda katika kampuni yenye jina lako ili tukamalize ushetani uliopo ndani ya kampuni ile daah natamani nimuone mwanangu ????


AKWELINA ?? Pole sana usijali utamuona mtoto wako kesho tunaenda kumsaidia mtoto wako mimi nahitaji kumsaidia baba yangu kipenzi kakinga nimemkumbuka sana baba yangu .


Walilala baada ya kuzungumza mambo mengi kuhusu safari yao. Yalipofika majira ya saa tisa usiku warda alikuwa bado hajalala alisimama akachukua sindano ya madawa ya kulevya akamchoma akwelina , Akwelina alistuka ghafla akalala tena warda alisimama akautafuta ufunguo kwa muda mrefu kwa bahati nzuri aliupata ufunguo ule akachukua begi lake akaondoka moyoni mwake alisema :-

“” Nisamehe sana akwelina kwa hiki nilichokutendea inabidi nimpelekee ufunguo Julius ili nimpate mtoto wangu ”’


Warda aliondoka alipofika barabarani alipanda gari moja kwa moja hadi gest ( nyumba ya wageni ). Asubuhi palipopambazuka warda alichukua gari akaanza safari kuelekea katika kampuni, Safari ilikuwa ndefu sana warda akiwa ndani ya gari alisikia gari linasimama ghafla dereva wa gari hilo alishuka na kukimbia warda alishindwa kuelewa akatoka kwenye gari alipotazama mbele ya gari alimuona akwelina akiwa ameshika bunduki Warda ali……



Warda alipatwa na mshangao mkali sana kwa kile alichokiona mbele yake alianza kurudi nyuma huku akiwa anatetemeka , Akwelina alimfuata akiwa na hasira zilizojaa moyoni mwake, Warda alipiga magoti akasema :-


WARDA__ Nisamehe akwelina najua nimekosa sana lakini nilifanya kitendo kile kwa ajili ya maisha yako , sikia akwelina kwa hali yeyote pamoja na uwezo ulionao hauwezi kupambana na askari waliopo ndani ya kampuni ile kifupi kuna askari wengi wenye nguvu na uwezo wa juu sana na ndio maana niliamua kuchukua ufunguo huu ili nikamsaidie mtoto wangu nafahamu Julius anahitaji ufunguo huu pekee na ningekueleza haya usinge kubali akwelina binti yangu Mimi ningefanyaje Mimi akwelina ?


AKWELINA ___ Siku zote baba yangu aliniambia kwamba “” Binti yangu akwelina katika maisha yako usimuamini binadamu yeyote hata Mimi japo nimekulea lakini usije ukaniamini kwa sababu nafsi zetu huwa zinabadirika muda wowote ishi maisha yako yote lakini kumbuka binadamu sio wa kumuamini”” Kupitia maneno ya baba niliishi na wewe kwa akili sana na sindano ile niliibadirisha ili bila wewe kujua na ndio maana leo hii unaniona hapa. Sitaki kuzungumza mengi kwanza naomba ufunguo pili utaendesha gari hili hadi katika kampuni hiyo najua kwa uwezo wa mungu nitashinda tu.


Akwelina alichukua ufunguo toka kwa warda kisha akampandisha kwenye gari kwa nguvu , Warda akaendesha gari kuelekea katika kampuni hiyo. Monna alishindwa kuvumilia utumwa katika mikono ya Patrick kutokana na kukosa uhuru, Monna aliishi maisha ya mateso katika mikono ya patrick, siku zote monna aliishi akiwa anajuta kwa vitendo alivyomfanyia kakinga monna alikumbuka siku moja walipokuwa wanaishi kijiji kabla monna hajampokea akwelina, kakinga alimwambia monna :-


“” Mke wangu naomba nikueleze maneno haya kwa sababu nakupenda sana mbali na kukupenda sisi ni yatima wewe na mimi sote hatuna wazazi katika dunia hii, Wewe ndio mama yangu hali kadhalika na Mimi ndio baba yako kwahiyo nakuomba mke wangu nipende kama nilivyo katika maisha yako yote kwani ninaamini katika dunia hii hakuna mwanaume anaekupenda kama Mimi chunga sana tamaa, Dunia hii kuna wanaume wengi lakini wengi wao ni waongo na wenye mapenzi ya dhati kama Mimi tupo wachache sana mke wangu __????


Monna alilia sana kwa kumbukumbu hizo alijuta sana kwa kuruhusu kumpoteza mwanaume aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwake , Wakati huo upande wa kakinga alikuwa na mawazo sana kwa kwa kumwamini sana monna , kakinga akiwa katika mawazo hayo alimtazama mtoto wake bilali akamuona bilali analia sana Kakinga alipojaribu kumgusa bilali alimuona bilali anapiga magoti mbele yake bilali akasema :-


BILALI__ Nisamehe sana baba yangu sikutambua kama Julius alikuwa ananidanganya nimekutesa baba yangu daaah najilaumu sana nisamehe sana baba yangu nisamehe baba .


KAKINGA ___ Usijali kijana wangu yote haya sio makosa yako ni mipango yake mungu pekee sisi wanadamu siku zote ni wakosaji mwanangu usijali nimekusamehe .


Bilali alimkumbatia baba yake akiwa anatokwa na machozi kwa wingi sana Kakinga alimtuliza bilali. Baada ya siku mbili Akwelina na warda walikuwa bado wapo njiani akwelina alimuuliza warda baada ya kukaa ndani ya gari kwa muda mrefu :-


AKWELINA __ Bado muda gani tufike ?


WARDA ___ Bado kama siku tatu tufike binti yangu .


AKWELINA __ Ongeza mwendo .


Usiku wa siku hiyo mama mzazi wa akwelina alikuwa ndani ya chumba chenye kutisha , Chumba ambacho kilikuwa na wadudu wengi na chenye kutoa harufu mbaya sana mama wa akwelina aliteswa mno na wadudu waliokuwa ndani ya chumba hicho. Mama wa akwelina akiwa ndani ya mateso hayo kwa mbali alisikia sauti yenye huzuni ya mwanaume ikiomba maji ya kunywa, Mtu huyu aliomba maji kwa muda mrefu ilibidi mama wa akwelina aifute ile sauti alipofika karibu alimuona mtu amechakaa kama chizi amekaa chini akiendelea kuomba maji mama akwelina alipomtazama vizuri alistuka kumuona mtu yule ni STEVEN mume wake kipenzi ….



Mama akwelina alipomtazama vizuri alistuka kumuona mtu yule ni STEVEN mume wake kipenzi, ilikuwa vigumu sana moyo kuamini kile macho ilichokuwa inakitazama, Miguu ilikuwa mizito na kusababisha mama wa akwelina kushinda kupiga hatua zaidi akaondoka chini. Steven alistuka baada ya kusikia kishindo karibu yake.


“” Nani wewe nisaidie maji nahitaji maji ya kunywa ninakiu cha maji pia nina njaa siku ya pili leo sijala chochote njaa inaniuma mwambie Julius mdogo nahisi njaa tafadhali” Maneno hayo ya Steven yalimuumiza sana mama akwelina na kushindwa kuvumilia akaruhusu mvua ya machozi katika macho yake. Kilio kikali kilichotoka kwa mama akwelina kilizidi kumshangaza Steven na kumfanya ajiulize maswali mengi sana :-


“” Kwanini unalia wewe ni nani ? Steven alimuuliza mama akwelina, Kwa sauti yenye huzuni ndani yake mama akwelina alimjibu Steven:


“” Ni Mimi mume wangu ??

“” Wewe nani mbona hujibu unalia tu?

“” Mimi daaah ?? ni Mimi JAMILA ..

“” Jamila !! jamila yupi acha kulia niambie ili nikufahamu binti .


Jamila ( mama wa akwelina ) alizidi kupata maumivu baada ya kutambua mume wake amemsahau hadi sauti yake , Jamila alijikaza akamjibu :


“”_ Ni mimi mke wako jamila mume wangu .

“”_ Niniiii !! mke wangu jamila ni wewe kweli hapana niliambiwa umekufa mke wangu kumbe upo hai siamini.

“”_ Nipo hai mume wangu umesahau hadi sura yangu jamani niangalie vizuri mume wangu .

“” _Daah sioni Mimi mume wangu Julius shemeji yako alinipulizia dawa na kusababisha leo hii nimepoteza nuru katika macho yangu sioni mimi mke wangu .


Jamila alizidi kulia akasimama japo alikuwa hana nguvu akamsogelea Steven ( mume wake ) akamkumbatia , walikumbatiana kwa muda mrefu sana Steven alimwaga machozi kwa wingi katika mgongo wa jamila japo machozi ya steven yalikuwa ya furaha ndani yake.


Yalipofika majira ya asubuhi na mapema askari waliingia katika chumba alichokuwepo bilali na baba yake wakawachukua wote wakaondoka nao moja kwa moja hadi katika uwanja mkubwa uliokuwepo ndani ya kampuni hiyo, Bilali na baba yake walipofika katika uwanja huo waliona watu wengi wapo katika mateso makali upande wa pili katika uwanja huo kulikuwa na watu wengi waliokuwa wanakatwa vichwa, hali hiyo ilimpatia wasiwasi bilali ghafla Julius alitokea akamshika bega bilali akamwambia :


“” _ Kijana unajua kwanini upo hapa ? Hahaha acha kuogopa nimekuleta hapa ili utambue kama Mimi sio mtu wa mchezo na huwa sipendi dharau kipigo ulichonipatia sijakisahau kabisa leo nahitaji nikupatie adhabu kali ili nijue kama wewe kweli ni jasili huu ndio unaitwa UWANJA WA KIFO.


Baada ya maongezi hayo askari walimchukua bilali wakamfunga kamba katika mikono yake alafu wakamtupa ndani ya kisima chenye maji mengi, Kakinga alihitaji kumsaidia bilali askari walimchukua wakaenda nae katikati ya uwanja alafu wakaanza kumpiga, Kakinga aliwashambulia askari wote waliokuwa wanampiga Julius akachukua bunduki akampiga Kakinga risasi ya kifua, kakinga alidondoka chini papo hapo.


Majira hayo hayo monna akiwa na Patrick alipatwa na wasiwasi mkubwa katika moyo wake akasema kwa nguvu “” KAKINGA “” moyo wake ulizidi kwenda mbio hofu iliutawala mwili wake wote monna anamtazama sana Patrick akasema:-


“” Kakinga yupo wapi ?

“” hahaha wewe hujui kakinga yupo uwanja wa kifo leo hawezi kupona .

“” Hapana hapana haiwezekani


Alimaliza kwa maneno hayo monna akasimama akatoka nje akiwa anakimbia kuelekea uwanja wa kifo. Bilali alisumbuka sana ndani ya maji hayo baada ya kukaa kwa muda mrefu kidogo pumzi ilimuisha bilali akajitahidi kamba zikafunguka akaongelea kwenda juu kwa bahati nzuri alifika juu akatoka nje ya kisima akatazama mbele yake akamuona mwanajeshi mmoja anauvuta mwili wa kakinga kwa sababu kisima kilikuwa karibu na sehemu ambayo kakinga alipopingwa risasi, Bilali hakuamini akamtazama Julius akamuona Julius anacheka sana akiwa ameshika bunduki bilali alishikwa na hasira aka……



Bilali alishikwa na hasira akasimama japo alikuwa amechoka sana kutokana na kupambana na maji kwa muda mrefu, Kakinga alimnyoshea mkono bilali kuashiria anahitaji msaada toka kwake wakati huo yule mwanajeshi alizidi kumvuta kakinga bila huruma hali iliyozidi kumpatia hasira bilali aliondoka kwa mwendo wa kasi sana akamuua yule mwanajeshi aliyekuwa anamvuta baba yake baadaa kumuua yule mwanajeshi bilali akamtazama Julius kwa muda mrefu sana .


Julius akaweka vizuri bunduki yake akamlenga kichwani bilali alipotaka kufyatua risasi alimuona monna kasimama mbele ya bilali ikabidi Julius ashushe bunduki yake alafu akashuka chini akamsogelea monna akamshika nywele akaanza kumvuta huku na kule katika uwanja huo , Monna aliumia sana akaanza kulia na kuomba msaada hali iliyomfanya kakinga japo alikuwa kapigwa risasi alisimama akamfuata Julius akamshika mkono akapiga magoti mbele yake akiwa anatokwa na damu nyingi katika kifua akasema :-


“” _Tafadhali muache huyu binti hana makosa mwenye makosa ni Mimi na sio yeye Mimi ndio nahitaji kupata adhabu na kufanyiwa chochote lakini sio hawa tafadhali waache waende .


“” _Hahaha kumbe unajua kuomba eee, Sawa nitawaacha lakini kwa sharti moja unatakiwa uwe mbwa wangu leo na ubweke kama mbwa anavyobweka ukifanya hivyo nitawaacha wakiwa wazima .


Julius aliomba mnyororo akapewa akamfunga shingoni Kakinga kitendo hicho kilimuuma bilali akahitaji kumshambulia Julius, kakinga akamziwia “” Bilali mtoto wangu tuli hatuna uwezo wa kupambana nao angalia baba yako sina nguvu tena nani atakusaidia kijana wangu tulia acha nifanye hivi kwa ajili ya maisha yenu “” yalikuwa maneno ya kakinga akimweleza bilali. Julius alimvuta mnyororo ule Kwa nguvu Kakinga akadondoka chini bilali alishindwa kuvumilia akamvamia Julius wanajeshi walikuja wakamshika bilali, Julius alitoa amri kwa hasira :-


“””” Maliza mbwa wote hao “””

Wanajeshi walichukua bunduki zao walipotaka kuwapiga risasi mama mdogo wa monna ( Madame ) alitokeza akawaziwia wanajeshi wale kwa kusema :-


“”_ Julius mume wangu kwanini upo dhaifu hivyo hawa hawastahili kupigwa risasi wanatakiwa wafe kifo chenye mateso sana au unasemaje ?


“”_ Ni kweli mke wangu umesema neno lenye umuhimu mkubwa hakuna haja ya risasi, Askari wapeleke gerezani hawa panya baada ya siku mbili nitawauwa kwa mikono yangu mwenyewe na kifo chao kila raia aliyopo ndani ya kampuni hii atashuhudia kifo hicho.


Wanajeshi waliwachukua na kuwapeleka gerezani monna hakuamini kama mama yake mdogo amekuwa katili kiasi kile. Walipofika gerezani hali ya kakinga ilizidi kuwa mbaya sana jaraha la kakinga lilizidi kutoa damu kwa wingi , Monna alilia sana akamueka katika katika miguu yake machozi kutoka kwa monna yalikuwa yanadondoka katika sura ya kakinga taratibu mkono wa kakinga ulishika shavu la monna kwa sauti ya chini kakinga alimwambia monna:-


“”_Acha kulia monna unalia nini ?


“”_Nisamehe sana mume wangu bado najuta kwa niliyofanya kwako nafsi inaniuma sana mume wangu japo niliomba taraka lakini bado nakupenda usiniache peke yangu .


“”_Ni ngumu kuivumilia hali hii naumia sana naomba nisikilize monna huyo kijana unaemuona ni mtoto wangu anaitwa bilali ni mtoto wa warda naomba kama nilipoteza maisha leo nitunzie kijana wangu tafadhali.


“”_Haiwezekani ufe baba haiwezekani


Bilali alitazama huku na kule ndani ya gereza hilo kwa bahati nzuri aliona mfupa wa mnyama aliyefia ndani ya gereza hilo , bilali aliutumia mfupa huo kutoa risasi ndani ya kifua cha kakinga, Ilimchukua muda mrefu sana kutoa risasi ile, kakinga alipiga kelele kali kwa maumivu aliyopata kwa bahati njema bilali akafanikiwa kutoa ile risasi kisha akavua shati lake akaziwia damu ili zisiendelee kutoka.


Usiku wa saa tisa Patrick alikwenda gerezani akamkuta monna ametapakaa damu katika mikono yake Patrick alistuka sana akamtuma mwanajeshi mmoja akalete dawa ya vidonda yule mwanajeshi hakuchelewa akaleta dawa hiyo Patrick akampa monna dawa ile alafu akaondoka Monna alimshukuru mungu sana waliitumia dawa ile kumtibu kakinga katika majeraha yake.


Baada ya wiki mbili kupita kakinga alipona kabisa akaanza kupiga mazoezi ndani ya gereza hilo akiwa na kijana wake bilali, Siku hadi siku kakinga na bilali walizidi kuwa imara. Siku hiyo majira ya usiku Julius akiwa kitandani pamoja na Madame alisema


“” Nimemuacha sana kakinga kesho ndio siku yao ya mwisho lazima wafe”


Kama kawaida ya wanajeshi asubuhi ilipofika waliandaa vizuri uwanja wakawapatia taarifa watu wote waliokuwa wanaishi ndani ya kampuni hiyo kuhusu mauaji yatayofanyika siku hiyo baada ya muda kidogo watu walikusanyika kwa wingi sana katika uwanja huo. Kakinga, Monna pamoja na bilali walifungwa kamba katikati ya uwanja huo , Julius alikuwa amekaa juu akicheka sana panga ziliandaliwa kwa ajili ya kukata vichwa vyao. Mwanajeshi mmoja alimfuata monna akaweka panga katika shingo lake akamtazama Julius , Julius akaruhu monna akatwe kichwa yule mwanajeshi kabla hajashusha panga alipigwa risasi akadondoka chini Julius pamoja na watu wote katika uwanja huo walipata mshangao mkali kakinga alipotazama mbele katika mlango mkuu alimuona akwelina …



Kakinga alipotazama mbele katika mlango mkuu alimuona akwelina anakuja baada ya mwanajeshi huyo kupigwa risasi wanajeshi wote waligeuka wakaanza kumshambulia Akwelina , Akwelina alikuwa zaidi ya mnyama aliteketeza wanajeshi kwa wingi kakinga akatumia nafasi hiyo akakata kamba akachukua bunduki akamfuata bilali akamfungua kamba akambeba Monna begani kisha akaondoka hadi katika chumba kilichokuwa wazi katika uwanja huo , kakinga alipofika alimuweka monna chini akamfungua kamba, alafu akampatia bunduki bilali :-


“” Sikia monna hii sehemu sio salama kwako baki hapa hakikisha hauondoki eneo hili umenielewa ?


“” Sawa lakini hakikisha unarudi salama mungu akusaidie .


“” Bilali mwanangu baki eneo hili uwanja wa vita sio salama kwako pia


“” Hapana baba nitakufa na wewe siwezi kubaki hapa siwezi baba.


Bilali hakujali chochote kibaya kinachoweza kutokea mbele yake ilibidi Kakinga amkubalie wakarudi kupambana, Milio ya risasi iliwapa tabu sana raia na kuwafanya baadhi ya raia kupoteza fahamu kutokana na milio hiyo, Pamoja na kuwauwa wanajeshi wengi lakini bado walizidi kuongezeka kwa kasi , Akwelina nae hakuchoka alizidi kuwaangamiza wanajeshi bila huruma. Giza lilitanda bado pambano lilikuwa linaendelea taratibu taratibu wanajeshi waliaanza kupungua hali iliyompatia wasiwasi Julius wakati huo Patrick alikuwa amejifungia ndani kwa hofu.


Madame alimtuliza Julius baada ya kumuona anawasiwasi mkubwa :-


“” Mtoto wa kiume hupaswi kuwa na wasiwasi lazima ujiamini mume wangu acha kuogopa sawa.


“” Daah sawa mke wangu lakini huyu msichana aliyevamia kampuni yangu sijui ni nani na anataka nini kwangu .


“” Kumbuka wewe ni tajiri lazima utawindwa na wengi cha kufanya ni kuwateketeza hawa wafungwa na raia wote huenda itasaidia kumtuliza huyo msichana .


“” Wazo zuri mke wangu vizuri sana.


Yalipofika majira ya asubuhi bado pambano lilikuwa linaendelea katika uwanja ule ghafla wanajeshi waliacha kupiga risasi wakarudi nyuma akwelina alipopata nafasi hiyo alimfuata baba yake mlezi ( kakinga ) akamkumbatia kwa furaha akasahau yupo eneo hatari :


“”” Nilikukumbuka sana baba yangu nilimuomba sana mungu nikukute salama nimekuja kukusaidia baba yangu nakupenda sana baba nakupenda.


“” Sikia binti yangu hapa sio sehemu salama tupambanie maisha yetu kwanza hayo mengine baadae.


Akwelina alimsikiliza baba yake akaokota silaha yake wakajificha nyuma ya jiwe kubwa lililokuwa ndani ya uwanja huo baada ya kuona wanajeshi wanarudi nyuma. Ulipita muda mchache akwelina na wenzake waliona raia wengi wanaletwa uwanjani na kuuwawa ovyo ovyo wanajeshi walizidi kuua raia kwa wingi. Hali hiyo iliwashangaza sana kakinga na watoto wake, Julius akachukua kipaza sauti akasema:-


“” Kakinga najua unanisikia naomba weka silaha chini pamoja na huyo msichana haijalishi unamfahamu au laa ili kusaidia maisha ya raia hawa vinginevyo nitaendelea kuwauwa kwa sababu yenu .


Julius alitoa ruhusu kwa wanajeshi wake baada ya kuzungumza maneno hayo wakaendelea kuuwa raia kakinga alishindwa kuvumilia akatoka nyuma ya jiwe akatupa silaha chini, Bilali na akwelina nao wakatupa silaha chini Julius alifurahi mno wanajeshi waliwazunguka Kakinga na watoto wake kwa lengo la kuwateka, Wanajeshi walipotaka kuwagusa walipigwa risasi wote Julius alizungusha macho huku na huko kumtafuta aliyewauwa wanajeshi wake ghafla warda akajitokeza akiwa anapiga risasi , Julius akarudi ndani haraka.


Kakinga na watoto wake waliokota silaha zao wakaungana na warda wakawashambulia wanajeshi. Raia walichukia sana wakaokota mawe na kuwapiga wanajeshi, Kutokana na wingi wa raia wanajeshi waliuwawa wote kwa muda mfupi kisha wakatawanyika sehemu zote na kuwafungulia wenzao, Julius alipofika chumbani kwake alimkuta Madame anachukua ufunguo wa gari lake pamoja na pesa zote:-


“” Unataka kwenda wapi na pesa zangu wewe mwanamke ?


“” Kila mtu afe na chake Julius baki na balaa lako Mimi naondoka .


“” Nipatie ufunguo wa gari langu pamoja na pesa zangu .


“” Sikupi pia sahau hilo.


Julius alichukia sana akachomoa bastola akampiga risasi Madame ya kichwa , Madamu akapoteza maisha papo hapo Julius akachukua pesa zake pamoja na ufunguo wa gari akatoka nje akiwa makini sana njiani akakutana na patrick wakaungana, Wakatafuta njia ili watoroke lakini kila sehemu walipokwenda walikutana na raia wakiwa na hasira kali Patrick akamwambia kakinga :-


“” Kaka njia sahihi hapa ni kumchukua kaka yako na mke wake jamila ili tuwatumie kuondoka hapa kwa sababu raia hawa wanawatambua wataogopa na njia tutapa kaka au unasemaje ?


“” Ni kweli kabisa wazo zuri nifuate.


Julius na Patrick waliondoka hadi katika chumba alichokuwepo Steven na mke wake ( Jamila ) Julius aliwachukua kama uchafu bila kujali Steven ni kaka yake, Walitoka nao nje walipofika nje Julius alipiga risasi juu raia walisogea mbali warda akamwambia akwelina :-


“” Wale waliotekwa ndio wazazi wako halali wale ndio waliokuzaa wewe .


Akwelina hakuamini alichokisia kutoka kwa warda, Akwelina akiwa katika mshangao mkali huo Julius alipanda kwenye gari akiwa na wazazi wa akwelina pamoja na patrick wakaondoka, Akwelina alitazama huku na kule akaona pikipiki ya kijeshi akaifuata akapanda kisha akalifuata gari ……



Akwelina alitazama huku na kule akaona pikipiki ya kijeshi akaifuata akapanda kisha akalifuata gari akwelina alikimbiza pikipiki ile kwa mwendo wa kasi sana japokuwa gari lilikuwa na uwezo mkubwa lakini akwelina alijitahidi akalifikia, Patrick akiwa ndani ya gari aliona pikipiki ikiwafuata kwa kasi sana akapata mashaka alipoangalia vizuri alimuona akwelina Patrick alistuka sana akamwambia Julius ambaye alikuwa anaendesha gari hilo :-


“” Nahisi kuna mtu anatufuata nyuma kaka ongeza mwendo .


“” Unasemaje !! nani huyo tena ?


Julius hakupoteza muda aliongeza mwendo taratibu taratibu walianza kumuacha akwelina , Akwelina akiwa juu ya pikipiki alichomoa bunduki yake akarenga taili la gari kisha akapiga risasi, Risasi ilipasua taili lile na kulifanya gari lipate ajali likadondoka nje ya barabarani kwa bahati nzuri patrick na wenzake wote walitoka ndani ya gari wakiwa wazima japokuwa Julius alivunjika mkono. Akwelina alisimama akawafuata Patrick alijaribu kupambana na akwelina lakini ilikuwa ngumu sana kutokana na uwezo wa akwelina katika mapambano, Akwelina aliwafunga kamba Julius pamoja na patrick kisha akawafuata wazazi wake akawakumbatia akiwa analia sana:-


“” Mama na baba siamini kama ningewaona tena kwa kuwa mbali na ninyi hadi sasa nimekubwa binti mkubwa lakini kwa uwezo wa mungu leo nimewaona siamini.


“” Jamila mke wangu huyo nani anayelia na kuzungumza maneno hayo ?

“” Mume wangu hata Mimi sijamtambua bado , Sikia binti yangu wewe nani mbona sikutambui acha kulia nieleze ili nielewe binti ?


“” Mama na baba ni mimi mtoto wenu HASMA mwenye jina mgongoni kwangu lililoandikwa AKWELINA wazazi wangu ????


“” Hapana sio kweli hapana mume wangu hii sio kweli siamini .


“” Twende kwa msichana uliyenikabidhi kwake nilipokuwa mdogo sana mama nahisi ukimuona utaamini.


Akwelina aliwachukua wazazi wake pamoja na wafungwa wake ambao ni Patrick na Julius akakodisha gari likawapeleka hadi ndani ya kampuni ile. Kakinga , Monna, Bilali , Warda pamoja na raia walimuona akwelina akiingia ndani ya uwanja akiwa na wazazi wake mkononi ameshika kamba iliyomfunga Julius na Patrick, Raia walikuwa na hasira kali sana waliwafuata Patrick na Julius wakawapiga sana kipigo kilipozidi Julius na Patrick walipoteza fahamu raia walichukua kuni na mafuta wakawachoma moto , Warda alilia sana kumuona kaka yake ( Patrick ) anachomwa moto.


Monna alimfuata akwelina akamshika mkono akamsogeza karibu ya jamila alafu akasema :-


“” Dada naomba nikurudishie mtoto wako uliyenikabizi miaka ya nyuma sana Akwelina huyu ndio mama yako mzazi .


Steven hakuamini alichokuwa anasikia ikabidi amwite akwelina ( HASMA ) akapitisha mkono mgongoni kwake akagusa lile jina aliyomwandika akiwa mdogo sana ndipo alipoamini kama kweli ni mtoto wake Steven alimkumbatia Akwelina akiwa anatokwa na machozi mengi sana, Wakati huo kakinga alikuwa mbali kidogo, nae machozi ya furaha yalimtoka :-


“” Mtoto wangu hasma umekuwa binti mkubwa sioni Mimi ningekuona leo mwanangu daah alafu unaufunguo katika mwili wako mwanangu unajua hilo ?


“” Ndio baba na niliutoa kwa sababu watu wengi walikuwa wanautaka ufunguo huo ninao hapa hapa baba.


“” Mungu wangu afadhali naomba ufunguo huo .


Akwelina ( HASMA ) alimpatia baba yake ufunguo , Steven alibonyeza ufunguo ule ardhi yote katika kampuni hiyo ilitetemeka ghafla kilitokea chumba kikubwa chini ya ardhi katika uwanja huo , Steven aligeuka akampatia Akwelina ufunguo kisha akamwambia :-


” Fungua chumba hicho mwanangu ”


Akwelina alifungua chumba kile akashangaa sana kuona chumba chote kimejaa Mali mbalimbali zikiwemo almasi na dhahabu pia kulikuwa na masanduku mengi sana akwelina alipoyafungua aliona pesa zimejazwa ndani ya masanduku yale akwelina alizidi kushangaa na kugeuza macho huku na huko aliona karatasi moja ipo juu ya sanduku akaichukua akaisoma akagundua ile ilikuwa hati miliki ya kampuni hiyo.


Akwelina alitoka nje akiwa na furaha sana cha ajabu alimuona kakinga anaondoka akiwa na bilali Akwelina alimfuata akamziwia akamuuliza :-


“” Unakwenda wapi baba yangu ?


“” Naenda mbali akwelina samahani kwa kukuita jina hilo nimezoea hivyo , Nisikilize Hasma kwa sasa upo salama pia umekuwa binti mkubwa na wazazi wako wale pale wanakuhitaji nenda ukawalinde .


“” Mimi bila wewe hata wao wasingeniona leo, popote utapokwenda nitakuwa nawe pia kampuni hii pamoja na mali zote nakupa wewe bado nitaendelea kuwa chini yako baba yangu tafadhali kubali suala hili .


Kakinga hakuamini kama anaenda kuwa tajiri mkubwa sana duniani alifurahi mno moyoni mwake alisema “” Hakika #WEMA huwa hauozi ahsante mungu “” Kakinga aliingia ndani ya chumba kile akachukua Mali nusu akawapatia raia walikuwa wanateseka ndani ya kampuni hiyo. Baada ya mwaka mmoja kupita kakinga alikuwa tajiri mkubwa sana akaiboresha kampuni ile ikawa kituo cha watoto #YATIMA , Kakinga alitumia Mali nyingi kuyatibu macho ya Steven kwa uwezo wa mungu Steven alipona na akaona tena Akwelina alifurahi sana.


Monna pamoja na warda nao walikuwa matajiri wakubwa japokuwa moyo wa monna ulikosa furaha kwa kumpoteza kakinga katika maisha yake, Kakinga hakuhitaji kuwa na mke kutokana na umri wake kuwa mkubwa, Kakinga aliendelea kuwa tajiri siku hadi siku hadi leo kakinga ni tajiri mkubwa.


#ZINGATIO

Ndugu msomaji kumbuka siku zote katika maisha yako ukiona shida zinakuelemea tambua mafanikio hayapo mbali , Usikate tamaa hata kama upo katika wakati mgumu kiasi gani huwezijua mungu kapanga nini kwako .Tenda WEMA kwa yeyote hata kama humfahamu malipo yake yapo japo yatachelewa.

___ Shukrani kwa kuwa nami mwanzo hadi mwisho



*MWISHO*

Comments