Bibi yake Barack Obama afariki Kenya

 


Bibi wa Kambo wa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, Sarah Obama amefariki katika hospitali nchini Kenya akiwa na umri wa miaka 99, familia yake imenukuliwa na vyombo vya habari vya nchini humo.

Mama Sarah amekuwa mgonjwa kwa muda na amefariki alipokuwa akipokea matibabu.

Familia yake inafanya mipango ya kufanya mazishi yake Jumatatu katika makaburi ya umma mjini, kulingana na ripoti.

Rais Obama alikuwa akimuita Granny Sarah.

Bi Obama alimtetea mjukuu wake wakati wa uchaguzi wa Marekani iliposemekana ni Muislamu na hakuzaliwa Marekani.

Comments