Donald Trump kurejea mtandaoni hivi karibuni, asema mshauri wake
Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump hivi karibu atarejea katika mtandao wa kijamii "mtandao wake mwenyewe", mshauri wake amesema.
"Nafikiri tutamuona Rais Donald Trump akirejea kwenye mtandao wa kijamii katika kipindi cha karibu miezi miwili au mitatu," Jason Miller amezungumza na Fox News.
Alisema mtandao huo "utakuwa unaovuma kati ya mitandao ya kijamii" na "utabadilisha kabisa mitandao".
Bwana Trump alikatishwa kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter na Facebook baada ya kutokea kwa ghasia mbaya za mwezi Januari katika Bunge la Capitol Washington DC.
Shambulio hilo lilitekelezwa Januari 6 na wafuasi wa Trump na kusababisha mauaji ya watu 5 akiwemo afisa wa polisi na kutikisa misingi ya demokrasia ya Marekani.
Siku kadhaa baadaye, mtandao wa Twitter ulisema kuwa akaunti ya Bwana Trump ya - @realDonaldTrump - "imekatishwa kabisa… kwasababu ya hatari ya kusababisha ghasia zaidi.
Bwana Trump alitumia mtandao wa Twitter kwa zaidi ya miaka 10 kuepuka vyombo vya habari vya zamani na aliweza kuzungumza na wapiga kura moja kwa moja.
Donald Trump alikuwa na karibu wafuasi milioni 90 katika mtandao wa kijamii.
Je tunajua ni mtandao gani ambao Bwana Trump atautumia?
Hapana. Siyo kweli.
Bwana Miller alitoa taarifa akisema kwa hilo "kila mmoja atasubiri kuona hasa ni kipi kitakachokuwa kinatekelezwa na Rais Trump".
Mshauri alisema Bwana Trump alikuwa akifanya "mikutano ya ngazi ya juu" huku timu kadhaa zikifikiria mradi wake katika eneo la Mar-a-Lago fukwe ya Florida.
"Kampuni kadhaa" tayari zimewasiliana na aliyekuwa rais, Bwana Miller amesema.
"Mtandao huu mpya utakuwa mkubwa," aliongeza, akitabiri kuwa Bwana Trump atavutia "makumi ya mamilioni ya watu".
Kwanini Trump alipigwa marufuku?
Mara ya kwanza, Bwana Trump alifungiwa mtandao wa Twitter kwa saa 12 mnamo mwezi Januari baada ya kuita watu waliovamia Bunge na kusababisha "ghasia".
Mamia ya wafuasi walivamia Bunge wakati linajaribu kuidhinisha ushindi wa Joe Biden katika uchaguzi wa urais mwaka jana.
Wakati huo, mtandao wa Twitter ulionya kuwa utamfungia Bwana Trump "kabisa" kuutumia ikiwa atakiuka tena sheria za mtandao huo.
Na baada ya kuruhusiwa kuanza tena kutumia Twitter, Bwana Trump alituma ujumbe mara mbili ambazo kampuni hiyo ilisema ndio ulikuwa wa mwisho kuvumilika.
Kampuni hiyo ya mtandao wa kijamii ilisema kuwa ujumbe wake huo aliotuma, zote mbili "ulikuwa sheria ya kusababisha ghasia".
Akaunti za Bwana Trump katika Facebook pia zilisitishwa, mtandao wa Twitch pamoja na Snapchat.
Comments
Post a Comment