Fahamu madhara ya utoaji mimba

 


Kutokana kuongezeka kwa idadi ya mahusiano duniani na kutotumia njia za uzazi wa mpango wasichana wengi kwa sasa wanatoa mimba. Asilimia tisini ya wasichana wanaokua kwenye mahusiano na wanaume zaidi ya mwaka mmoja kabla ya ndoa hutoa mimba na asilimia tano tu ya wote ndio wanaamua kuzaa. Sio ajabu kusikia mtu ameolewa akiwa ametoa mimba nne mpaka tano.

Madhara ya kutoa mimba kama ifuatavyo…

Kuna uwezekano mkubwa wa kufa (kupoteza maisha):

Utafiti uliofanywa na madaktari wa finland mwaka 1997 umegundua kwamba wanawake wanaotoa mimba wanauwezekano mkubwa wa kupoteza maisha, hii ni kwa sababu wanapoteza damu nyingi sana, vile vile wengine hutumia njia zisizo rasmi kutoa mimba hali inayoweza kusababisha kutokwa na mabonge ya damu. Utafiti pia uliongeza kutoa mimba moja uwezekano wa kufa unakua 45%, mimba mbili 114%, mimba tatu 192%.

Kuzaa watoto wenye upungufu wa akili:

Utoaji wa mimba kuharibu mlango wa mfuko uzazi na kufanya kushindwa kushika vizuri na matokeo yake mwanamke hujikuta akizaa kabla ya muda husika. Lakini pia watoto hawa wanaozaliwa kabla ya muda maalumu na viungo ambavyo havijakomaa hupata shida ya ubongo na kua wagonjwa wa akili maisha yao yote.

Kansa ya mlango wa uzazi:

Kitendo cha kutoa mimba kina aslimia kubwa ya kusababisha kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba. Hii ni kwa sababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi.

KUMBUKA:
Kila mwaka wanawake 70000 wanakufa kwa kutoa mimbA.

Comments