KILICHONITOKEA BAADA YA KUBAKWA NA KAKA YANGU - 2

 

KILICHONITOKEA BAADA YA KUBAKWA NA KAKA YANGU - 2

 



Simulizi : Kilichonitokea Baada Ya Kubakwa Na Kaka Yangu

Sehemu Ya Pili (2)


Wakati akina mama wanazungumza, nilikuwa makini kuwasikiliza kwani kila kilichojiri pale kilikuwa kigeni machoni pangu.


Wakati mganga huyo akimchinja yule kuku, yule kijana tuliyemkuta siku ya kwanza alitoka na kwenda upenuni palipokuwa na mtungi akachota maji na kuyaweka kwenye sufuria, alipotupia macho upande tuliokuwa tumekaa akatuona na kutusalimia.


Alipotusabahi aliingia ndani, mama mkubwa aliyekuwa akipenda sana kushadadia mambo akatuambia yale maji aliyochota yule kijana alikwenda kuyachemsha kwa ajili ya kumnyonyolea yule kuku, tukacheka.


“Mama mkubwa unaonekana unayaelewa sana mambo ya waganga?” Dorcas anasema mama yake alimwuliza.


Kufuatia kuulizwa hivyo, mama mkubwa alimwambia alikuwa na uzoefu wa waganga kwa vile huko kwao, marehemu babu yake mzaa baba alikuwa mganga.

Yule mganga alipomaliza kumchinja kuku, alimwita msaidizi wake ambaye alitoka na ungo mweusi akaenda kumweka kuku kisha wakaongozana na mganga kuingia ndani.


“Mpaka kuondoka hapa leo tutajionea makubwa,” mama mkubwa alituambia kwa sauti ya kunong’ona, tukacheka.

“Kwa nini unasema hivyo?” Dorcas anasema mama yake alimwuliza.


Alipoulizwa hivyo, alitaambia si tuliona tukio la kuku aliyechinjwa alivyowekwa kwenye ungo mweusi huku kichwa chake kikiwa kimewekwa juu ya kitambaa cheusi.


Ingawa katika hali ya kawaida lile tukio lilikuwa la kustaajabisha lakini tulijikuta tukicheka ndipo mama akasema kweli ukiwa na matatizo utakutana na mengi.


Baada ya kukaa kama saa moja na dakika kumi, msaidizi wa mganga alitufuta na kutuambia tuingie ndani, tulipoingia tulikuta kuna chungu cheusi kilichofunikwa kikiwa kilingeni, chupa ambayo ndani ilikuwa imejaa dawa.


Ukiacha chungu hicho, palikuwa na blanketi jeusi ambapo mganga akatuambia tayari aliandaa dawa, akaniambia nijongee karibu yake.


Nilipofanya hivyo akanielekeza kwamba baada ya kunichanja kwenye paji la uso wangu na kunipaka dawa, nitainama juu ya kile chungu ambacho kilikuwa na maji ya moto yenye dawa kisha atanifunika blanketi ili mvuke unifikie vizuri.


“Binti naomba fuata maelekezo yangu kwa umakini, hata kama utahisi unaungua usitoke kichwa juu ya chungu kwani dawa zitakuwa zinavuta vitu ulivyotupiwa ambavyo vinakutesa,” mganga aliniambia.


Mama aliyehofia ningeunguzwa na mvuke huo alipomuuliza mganga kama sitapata madhara, alicheka na kuniambia nisingeungua, ndipo alifunua mfuniko kikabaki kitambaa cheusi kilichokuwa juu ya kile chungu ambacho kilipitisha kwa mbali mvuke akaniambia niweke kichwa changu.


Baada ya kukiweka kichwa, alinifunika lile blanketi na kuniambia hata kama nitahisi naungua nisitoe paji la uso wangu juu ya kile chungu kwani nitakapohisi naungua ndipo vitu nilivyotupiwa kichawi vinatoka.


Nikiwa nimeinamisha kichwa ndani ya kile chungu, nilihisi kuungua nikawa nainua kichwa lakini mganga alinishika kichwani na kunizuia nisikitoe akanimbia nikiona naungua ndipo vitu nilivyotupiwa vilikuwa vikitoka.


Kila nilipojaribu kuinua kichwa, mganga alisisitiza nisikitoe na baada ya kufanya hivyo kwa dakika zisizopungua kumi, alifunua lile blanketi ambapo kila mmoja wetu alipigwa butwaa baada ya kuona vitu vya kutisha juu ya kile kitambaa cheusi kilichokuwa juu ya chungu.


Tukiwa tunashangaa, mganga alisogea na kuchukua kichwa cha jogoo kilichokuwa cheusi, mdomoni kikiwa na kitambaa chekundu na utosini kilikuwa na unyoa mrefu.


Baada ya kushika kichwa hicho, alisogea karibu yetu na kutuambia kichwa hicho na vitu vingine vilivyokuwa juu ya kile kitambaa juu ya chungu ndivyo nilivyotupiwa kichawi.


Alipotoa kauli hiyo alitaka kumpatia mama akishike, kwa uoga mama akakataa, mganga alipomwambia mama mkubwa akishike kwa vile hakikuwa na madhara naye alikataa.


“Msiogope kwani hivi sasa hakina madhara yoyote,” Dorcas ambaye huo ndiyo ulikuwa mwanzo kukumbwa na mikasa alimkariri mganga.


Kufuatia akina mama kugoma, mganga alikitupa kile kichwa sakafuni na kusonya akaenda kuchukua vitu vingine vilivyokuwa juu ya kile kitambaa cheusi.


Kwa kuwa tulikuwa tumeketi mbali kidogo, hatukuweza kuona vizuri kitu alichokichukua hadi alipotusogelea akatuonesha, kila mmoja wetu alishangaa alipoona hirizi ndogo iliyokuwa ikipumua.


Akatuambia kama asingeitoa hirizi hiyo siku ambayo ingeacha kupumua ambayo ilibaki kidogo kufika ungekuwa mwisho wa maisha yangu.


Kama alivyofanya awali, hakutaka kumkabidhi mtu aliitupa sakafuni kisha alikwenda kuchukua kitu kingine na kurejea nacho, kilikuwa kitambaa ambacho ndani yake hatukujua kilikuwa na nini.


Alipokifungua, zilimwagika punje za mchele, maharage, unga na vitambaa vilivyofanana na baadhi ya nguo zangu na za mama, tulishangaa sana.


Yule mganga alisema vitu hivyo ndivyo nilitupiwa kichawi mwilini mwangu, akafafanua kwamba zile punje za mchele, maharage, unga na vipande vya nguo zangu nilifanyiwa na mbaya wangu kwa sababu ya wivu.


Aliongeza kuwa, watu wake yaani mizimu ilimwambia mwanamke huyo mchawi alikuwa akiwaonea wivu akina mama waliokuwa wakiuza maharage, mchele, na unga ndiyo aliamua kunitengeneza uchawi wa vitu hivyo ili anitese.


Pua aliongeza kuwa alikuwa akikereka sana jinsi mama zangu walivuokuwa wakinijalia kuanzia kula na mavazi ndipo alichungua nguo zangu kichawi na kutengeneza uchawi na kunitupia ili anitese.


“Sasa hautaumwa tena, kila uchawi uliotupiwa nimeutoa, nafikiri kila mmoja wenu ameushuhudia kwa macho yake, pole sana mjukuu wangu…hii dunia ina watu wabaya sana,” Dorcas anasema yule mganga aliwaambia.


Baada ya kutuambia hivyo alikusanya vile vitu vya ajabu akachukua kipande cha gazeti na kuviweka na kusema mama aliyefanya ule uchawi huko alikokuwa alikuwa akijua kilichokuwa kikiendelea na alikuwa analia.


Mama mkubwa ambaye alikuwa na hasira alisema na ushenzi wake alionifanyia alikuwa kilia nini, mganga akacheka na kusema:


“Si nimeuharibu uchawi wake ambao alitumia fedha nyingi na muda mwingi kuutengeneza ndiyo maana analia.”


Kutokana na kauli hiyo, mama alimwuliza alikoutoa uchawi huo, mganga alimwambia alioneshwa kwamba aliufuata Mbozi kwa mzee mmoja ambaye licha ya kujifanya mganga alikuwa mchawi.


Mganga huyo aliwaliza akina mama walitaka yule mama apewe adhabu gani, mama mkubwa akasema ili kuwapunguza wachawi majumbani hata akimuua ilikuwa sawa.


“Eti mama, unakubaliana na ushauri wa mwenzako?” mganga alimwuliza mama.

Mama ambaye alikuwa na huruma sana alipinga na kusema kwa kuwa nilikuwa nimepona hakukuwa na sababu ya kumfanya jambo lolote yule mchawi, mama mkubwa akaguna!


“Huyo hafai kuendelea kuishi, hivi mama Dorcas kama angekuulia huyu mtoto wako wa pekee ungejisikiaje, mimi sioni kama kuna sababu ya kumuonea huruma,” mama mkubwa alimwambia mama.





Baada ya mama ambaye alikuwa mpole sana kusema mchawi huyo asamehewe kwa kuwa nilikuwa nimepona, mama mkubwa alimpinga na kusema:


“Huyo hafai kuendelea kuishi, hivi mama Dorcas kama angekuulia huyu mtoto wako wa pekee ungejisikiaje, mimi sioni kama kuna sababu ya kumuonea huruma.”


Kwa kuwa mama hakuwa tayari mchawi huyo aadhibiwe, mganga hakuwa na kusema akanipatia dawa kisha alitufahamisha kwamba baada ya kutumia zile dawa siku tatu turejee kwa ajili ya kunipa kinga.


“Itabidi akimaliza hizo dawa aje nimpe kinga sababu kwa ninavyowafahamu wachawi huwa hawakubali kushindwa, yule mama atarudi tena tena anaweza kuwaalika hata wenzake ili wamsaidie,” Dorcas alimkariri yule mganga.


Kufuatia mganga kutoa kauli hiyo, mama ambaye kama akumuelewa alimwuliza mganga kwamba yaani pamoja na kuharibu uchawi wake bado wangekuja tena!


“Kuja ni lazima ndiyo maana nimesema akimaliza hizo dawa siku ya tatu kuanzia leo aje nimkinge vinginevyo mnaweza kumpoteza mtoto,” Dorcas alimkariri yule mganga.


Baada ya mganga kumweleza hivyo mama, mama mkubwa alisema:

“Mdogo wangu unasikia anachokisema baba, huyo mchawi inatakiwa tummalize kabla hajammaliza mtoto, hivi ujue huo upo wako utakuponza.”


Hata baada ya mama mkubwa kutoa ushauri huo, mama hakuwa tayari kulipa kisasi ndipo mganga akasema cha muhimu siku ya tatu turudi kwake ili anipe kinga.


Baada ya kukabidhiwa dawa tulirudi nyumbani, tulipofika tu mama mkubwa alichemsha dawa na jioni nikaanza kunywa, usiku tukiwa tunapiga stori maongezi yetu yalikuwa ni juu ya vitu nilivyotupiwa na yule mchawi.


“Jamani hii dunia kuna watu wabaya sana, mtu anachukua maharage, mchele na nguo anazifanyia uchawi wa kumtesa mtu, Mungu atusaidie,” mama alituambia.


Baada ya mama kutoa kauli hiyo, mama mkubwa alimwambia tena wapo watu wanaweza kuwaua wenzao kwa dakika moja kutokana na uchawi wao.


Siku hiyo tulizungumza kwa muda mrefu ndipo mama akaniambia nikalale lakini kwa hofu niliyokuwanayo nilikataa kwenda kulala peke yangu wote tukalala chumbani kwao.


Kwa kuwa zile dawa nilitakiwa kunywa asuhubi, mchana na jioni, kabla sijaenda shuleni mama mkubwa aliniandalia na baada ya kunywa niliwaaga na kuelekea shuleni.


Asubuhi sikupita ile njia ya kutokea kwa yule mama tuliyehisi mchawi, niliamua kumpitia rafiki yangu Yasinta aliyekuwa akiishi mtaa mwingine kisha tukaelekea shuleni.


Siku hiyo mwili wangu ulikuwa mwepesi tofauti na kabla sijatolewa vitu vya ajabu kichwani mwangu ambapo sikuwa sawa kabisa, pia nilichangamka sana.


Kama tulivyoambiwa na mganga, siku ya tatu tulikwenda kwake ambapo alitueleza kwamba kupitia watu wake alimuona yule mama alivyokuwa akilalamika uchawi wake kuharibika.


Aliongeza kuwa licha ya kila siku kuja kuniwangia pale nyumbani hakuweza kufanikiwa kwa sababu ya zile dawa alizonipatia na kwamba kwa hasira alikwenda kichawi kwa yule mganga mchawi wa Mbozi kumweleza kilichotokea.


Mganga alitueleza kwamba tusihofu kwa sababu kinga atakayotupatia ni kiboko na kwamba yule mchawi akirudia angeweza kupatwa na balaa.


Tukiwa kwa yule mganga alinichanja chale sehemu mbalimbali za mwili wangu akanipaka dawa na kuniwiza kwamba mtu yeyote atakayekuja kunichezea asifanikiwi na uchawi wake umrudie mwenyewe.


“Wanangu, kwa kuwa nyinyi ndiyo wazazi wa huyu binti na mnaishi nyumba moja ni vizuri nanyi niwape kinga kwa sababu wachawi wanaposhindwa kumfikia mtu waliyemkusudia umalizia hasira zao kwa wengine,” mganga aliwaambia akina mama.


Baada ya kutoa kauli hiyo, mama mkubwa ambaye kwa sehemu alikuwa anaelewa mambo ya wachawi alikubali lakini mama alisita, mpaka leo nashindwa kuelewa sijui kwa nini marehemu mama hakupenda mambo ya kishirikina.


Hata hivyo, kwa ushawishi mkubwa wa mama mkubwa na yule mganga mama alikubalia ambapo nao walichanjwa na kupakwa dawa ya kinga.


“Wanangu kutokana na hii dawa ya kinga niliyowachanjia leo msioge mpaka kesho jioni,” mganga alituambia.


Mganga huyo aliongeza kuwa, usiku tukiwa tumelala yule mama mchawi akiwa na wenzake watakuja lakini tusiwe na hofu tutakaposikia upepo ukivuma juu ya bati ni kwamba kinga yake itakuwa ikifanya kazi kuwazuia.


Mama mkubwa alimshukuru kwa taarifa hiyo na kumuuliza kama ukizidi tufanye nini, akamwambia tutulie hadi watakapoondoka.


Kabla hatujaondoa kwa yule mganga, mama mkubwa aliuliza kiasi cha fedha alichohitaji ambapo mganga alisema hakuhitaji fedha isipokuwa kuna kitu alihitaji kama angekipata hicho ingekuwa malipo ya kazi yake.


Mama mkubwa alipomuuliza ni kitu gani akasema redio kwani aliyokuwanayo iliharibika na alipenda sana kusikiliza taarifa ya habari na vipindi vingine.


Mganga alipotoa ombi hilo, mama mkubwa ambaye pale nyumbani alikuwa na redio mbili alimwambia angempelekea, mganga alifurahi sana na kabla hatujaondoka alimwita mkewe na kumwambia atufungashie maharage pamoja na mahindi.


“Wanangu nimefurahi sana kunikubalia ombi langu kwani muda sasa nashindwa kusikiliza redio hapa nyumbani,” mganga aliwaambia akina mama.


Mama alimwambia asijali angepata redio hiyo ndipo tuliwaaga ambapo walitusindikiza kidogo kisha wakarudi nasi tukaenda kupanda gari la kwenda Mbeya mjini.


Tulipofika nyumbani kabla ya kufanya kitu chochote tuliketi sebuleni na kuanza kuzungumza mambo ya kwa yule mganga, mama mkubwa alimsifia kwamba alikuwa mganga mahiri na angetusaidia sana.


“Mimi nashukuru alivyoamua kutupa kinga hata sisi, amefanya jambo la muhimu sana,” mama mkubwa alituambia.

Wakati tunazungumza hakuna aliyejua kwamba huko mbele kungekuwa na vita kubwa dhidi yetu na wachawi ambayo ingesababisha mama kupoteza maisha katika mazingira tata.


Kwa upande wangu pia sikujua mikosi ambayo ningekutana nayo likiwemo balaa la kubakwa ambalo limeharibu kabisa maisha yangu.


Tulipopumzika, niliwasha jiko nikainjika maji kwenye sufuaria kubwa ambapo mama mkubwa aliniuliza yale maji yalikuwa ya nini, nikamwambia ya kuoga.

“Wewe Doracs kwani hukusikia alichotuambia mganga kwamba leo hatupaswi kuoga hadi kesho jioni,” mama mkubwa aliniambia.


Aliponieleza hivyo, nilikumbuka ni kweli mganga alitupa sharti hilo nikaishia kucheka na kumwambia nilisahau.

“Hapo kama ungekuwa peke yako ungeoga na kuharibu kinga yote, sisi wazee ndiyo tulitakiwa tusahau lakini siyo wewe,” mama mkubwa akaniambia nikaishia kucheka tu!


Wakati tukizungumza na mama mkubwa, mama alikuwa akiendelea kuchambua mchele name nilibadili ile sufuria na kuweka ambayo ilikuwa ikitumika kupikia wali.


Siku hiyo kila mmoja wetu alishirikia mapishi ya jioni na chakula kilipokuwa tayari saa mbili usiku mama mkubwa alikiandaa mezani, tukala na kwenda kulala.


Wote tukiwa tumelala kwenye kitanda cha futi sita kwa sita cha mama mkubwa, ilipotimu saa nane usiku nilisikia upepo mkali ukivuma na kutikisa bati la nyumba.

Hali hiyo pia ilisikiwa na akina mama lakini hakuna kati yetu aliyeshtuka sana kwa sababu tulikwishaambiwa na mganga kuhusu tukio hilo, tulitulia mpaka upepo ukatoweka.


“Mmeamini maneno ya mganga?” mama mkubwa alituuliza.

“Nimeamini dada yangu, kweli hii dunia ina mambo sasa nimeanza kuamini,” Dorcas anasema mama yake aliwaambia.


Kufuatia tukio hilo, tulitumia muda mrefu kulizungumzia hadi tulipotiwa na usingizi, niliposhtuka ilikuwa kwenye saa 12 alfajiri ambapo niliamka ndipo mama mkubwa aliniuliza nilitaka kwenda wapi, nikamwambia shuleni.


“Hapana mwanangu leo usiende utaenda kesho,” mama mkubwa aliniambia.

Nilipomuuliza sababu akaniambia nisiende tu nisubiri mpaka siku iliyofuata, kwa kuwa nilikuwa mtoto sikutaka kumbishia kwa sababu wakubwa wanaposhauri jambo ni vyema kuwasikiliza.


Kwa kuwa ratiba ya kwenda shule haikuwepo, sikutaka kurudi kulala nikataka kutoka nje nikafagie uwanja, kuosha vyombo na kufua nguo.

“Mwenzetu mbona umeduaa, kwa kuwa huendi shule rudi ulale,” Dorcas anasema mama yake mkubwa alimwambia.


Mama mkubwa aliponiambia hivyo nilimweleza kwa kuwa nilikuwa nimeamka ngoja nikafagie uwanja, kuosha vyombo na baada ya kupata kifungua kinywa ningefua nguo.


Licha ya kumwambia hivyo, mama mkubwa alinizuia kwenda kufangia na kunitaka nirudi kulala kwa sababu nje kulikuwa na baridi, nikaamua kurudi kulala.


Ilipofika saa moja, tuliamka na baada ya kupata kifungua kinywa, akina mama walinianga kwamba wanakwenda kwenye biashara wakaniachia hela za matumizi, nakumbuka mama aliniambia nikanunua nyama wangerejea na ndizi kwa sababu zilipita siku kadhaa bila kula chakula hicho.


Walipoondoka, niliosha vyombo kwenye saa tatu hivi na nusu niliamua kwenda sokoni kununua nyama pamoja na viungo, wakati narudi nikiwa nimepita kwenye uchochoro ghafla nilimuona paka mweusi akiwa amesimama mbele yangu, nywele zikanisisimka.


Nakumbuka siku moja tukiwa tunazungumza na akina mama, mama mkubwa aliwahi kusema ikitokea mtu anatembea usiku au mchana halafu akahisi nywele kumsisimka hali hiyo inaashiria hatari ipo mbele yake.


Kutokana na hali hiyo, nilihisi sikuwa sehemu salama, nikapa wazo la kurudi ili nipite njia nyingine, wakati nawaza hivyo yule paka alikuwa amesimama akiniangalia.


Jambo la kushangaza nilipogeuka nyuma ili nirudi kwa lengo la kupita njia nyingine nikashangaa kumuona paka aliyefanana na yule aliyekuwa mbele yangu akiwa amesimama ananiangalia, moyo ukapiga paa!


Kutokana na tukio hilo, niligeuka tena nyuma ili kumwangalia yule paka wa awali, sikumuona nikabaki nikijiuliza alihamaje na kuja kusimama nyuma yangu.


Kwa kuwa lengo langu lilikuwa ni kutoka pale uchochoroni niliamua kusonga mbele, cha ajabu nilipotembea hatua tatu ghala yule paka alitokea mbele yangu.


Tukio hilo ambalo ilikuwa mara yangu ya kwanza kukumbana nalo liliniogopesha sana, nilishindwa kuvumilia nikaanza kupiga mayowe ya kuomba msaada.


Cha kushangaza ni kwamba licha ya kupiga mayowe yule paka hakuondoka mbele yangu, wa kwanza kufika pale uchochoroni walikuwa akina mama wawili, mama Thabi, mama Elisha kisha walitokea vijana watatu na dada mmoja.


“Wewe Dorcas umepatwa na nini?” Dorcas anasema mama Thabi ambaye alikuwa akimfahamu vizuri alimwuliza.


Nikiwa mwenye hofu niliwaonesha paka ambaye bado alikuwa mbele yangu na kuwaeleza alikuwa akinizuia, wakashangaa na kuniuliza paka huyo alikuwa wapi!


Kwa kuwa mnyama huyo alikuwa amesimama karibu kabisa na mama Elisha, nikawaonesha lakini hawakumuona, mzee mmoja akasema huenda malaria ilinipanda kichwani.


Niliwahakikishia kwamba sikuwa na malaria na kusisitiza kuwauliza kama ni kweli hawakumuona yule paka, jambo la ajabu ni kwamba nilipoangalia sehemu aliyokuwepo yule paka sikumuona.

“Dorcas huyo paka mbona sisi hatumuoni,” mama Elisha aliniuliza.


Kwa kuwa paka alikuwa ametoweka niliwaambia aliondoka wakabaki wameduwaa ndipo yule mzee alisema kama kweli nilimuona paka muda ule anaweza kuwa wa miujiza.


Hata hivyo, mama Elisha alimpinga kwamba hapakuwa nap aka kwa sababu walipofika hawakumuona mnyama huyo, aliponiuliza tena kama nilimuona paka, niliwasisitizia kwamba nilimuona.


Mmoja wa wale vijana aliniuliza nilikuwa najisikiaje nikamwambia nilikuwa mzima, akasema kama sikuwa na tatizo basi niende nyumbani kisha wakaondoka.


Baada ya wale vijana kuondoka, yule mzee aliwaambia akina mama Elisha, yule dada na mama Thabi kwamba huenda ni kweli nilitokewa nap aka kwani isingekuwa rahisi katika hali ya kawaida kupiga mayowe na kusema nilimuona paka.


Mzee huyo alimuomba mama Thabi anisindike nyumbani kisha kila mmoja akaendelea na mambo yake nikaongozana na mama Thabi kwenda nyumbani.


Kwa kuwa sikuwa na tatizo, tulipofika aliniaga na kuniambia akina mama wakirudi niwasimulie nikamwambia sawa.

Mama Thabi alipoondoka, nilitoa kitoweo na vitu vingine nilivyotoka kuvinunua na kuanza mapishi kwa kuinjika nyama jikoni kisha kukatakata viungo.


Nyama ilipoiva niliipua na kwa kuwa sikuwa nahisi njaa, niliamua kujipumzisha kuwasubiri akina mama warejee ili tuandae chakula cha alasiri kwani walikuwa wanapenda sana kula nyumbani.


Wakati wanawasubiri niliingia chumbani kwangu nikajilaza kitandani, nikiwa sijapitiwa na usingizi ghafla nilishtukiwa nikikabwa shingoni na mtu.


Kwa kuwa mle chumbani nilikuwa peke yangu, kila nilipojaribu kupiga mayowe ya kuomba msaada sikuweza kwani aliendelea kunikaba huku akisema atahakikisha ananiondoa duniani.


Mtu huyo ambaye alikuwa amejitanda nguo nyeusi kila nilipojaribu kujinasua aliendelea kunikaba huku akikwepesha sira yake nisiione ndipo nikaanga kusema; ‘Mungu wangu niokoe, Mungu wangu niokoe ghafla alianiachia na kutoa msonyo wa nguvu na kuniambia nilikuwa nina bahati.


Alipotoa kauli hiyo, nikajikuta mle chumbani nimebaki peke yangu lakini nikasikia sauti ikiniambia nichungulie dirishani, nilipofanya hivyo nilimuona mama mmoja aliyekuwa kanipa mgongo akitembea.


Mama huyo aliyekuwa amejifunga nguo nyeusi, kwa muonekano wake wa nyuma na tembea yake alifanana na yule mama tuliyekuwa tukimhisi alikuwa akituchezea kichawi.


Nilimwangalia mpaka alipotoweka kwa kukata kona na kuingia kwenye uchochoro ndipo nilitoka pale dirishani na kwenda kukaa kitandani, nikashusha pumzi kwa nguvu.


Baada ya kufanya hivyo, ghafla nikaanza kulia mpaka nikaanza kukohoa huku ndipo nilishangaa nikiwa nimeshikwa na mama mkubwa akaanza kuniuliza nilipatwa na nini!


Nikiwa nalia mama aliingia akapigwa butwaa kuniona nikilia, baada ya kunibembeleza kwa muda nilinyamaza ndipo nikawasilimulia kila kitu kuhusu yule paka na mama aliyekuwa akinikaba.


Baada ya kuwaeleza hivyo, mama alianza kulia na kusema kama baba yangu angekuwepo yote yaliyokuwa yakinitokea yasingetokea, nami nikaanza kulia.






Baada ya kuwaeleza hivyo, mama alianza kulia na kusema kama baba yangu angekuwepo yote yaliyokuwa yakinitokea yasingetokea, nami nikaanza kulia.


Kufuatia mama kulia, mama mkubwa alimsihi na kumwambia hata kama baba angekuwepo mambo hayo yangetokea kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa tabia ya wachawi.


Licha ya mama mkubwa kutoa kauli hiyo, mama alisisitiza kwamba anaamini baba asingekubalia nichezewe namna ile akaendelea kulia jambo lililonifanya name niungane naye.


Mama mkubwa alifanya kazi ya ziada kutunyamazisha, tukiwa tumetulia alimwambia mama Jumamosi twende tena kwa yule mganga wa Songwe tukamwelezee kilichotokea.

“Kwa hali ilivyo lazima twende tukamuone,” mama alimwambia mama mkubwa.


Baada ya kupata chakula, niliondoka na akina mama kwenda kwenye biashara zao ambapo tulirejea nyumbani saa 12 jioni, tuliendelea na mambo mengine kisha tulilala.


Usiku wa siku hiyo tulilala vizuri hadi kulipokucha ambapo nilijiandaa na kwenda shuleni, nikiwa shuluni baadhi ya walimu waliniuliza kuhusu maendeleo yangu niliwaambia yalikuwa mazuri.

Alasili niliporejea nyumbani, nilimkuta mama akiwa amelala akilalamika maumivu ya tumbo na juu ya meza ndogo palikuwa na vidonge.


Nilipouliza alianza kusumbuliwa na tumbo muda gani mama mkubwa alinifahamisha kwamba lilianza kumuuma ghafla wakiwa sokoni kwenye biashara zao.


Kitendo cha mama kuumwa kilinikosesha raha, licha ya maradha kadhaa kupenda kwenda kucheza na wenzangu baada ya kutoka shuleni, siku hiyo sikutoka kabisa.

Mama alisumbuliwa na tumbo hilo kwa siku mbili, ilipofika Jumamosi tulikwenda kwa yule mganga, alipoangalia kupitia zana zake alibaini mama alitupiwa kitu tumboni.


Mganga huyo alitufahamisha kwamba yule mama mchawi ndiye aliyfanya hivyo na kuongeza kwamba bila ya kutuchanjia dawa mimi au mama tungekuwa tumepoteza maisha.


Aliongeza kuwa siku niliyotokewa nap aka alikuwa yeye na alipanga kunimaliza lakini alishindwa na baadaye alinifuata nyumbani nikiwa nimelala lakini pia alishindwa kunidhuru.


Mganga huyo aliwauliza akina mama amfanye nini mchawi yule ambaye alipanga kutuletea madhara makubwa, mama mkubwa aliomba kama anaweza amamalize kabisa lakini mama alipinga.


Mganga hakuwa na la kufanya, alimpatia mama dawa ambayo alisema akinywa atatapika na kitu alichorushiwa kitatoka na atakuwa mzima.


Baada ya kufika nyumbani, mama alichemsha dawa aliyopewa ilipopoa alikunywa kikombe kizima, hakumaliza dakika tano alianza kuharisha na kutapika mpaka akaishiwa nguvu.


Alipomaliza mama mkubwa alimpikia uji, alipokunywa alianza kutapika na kuanza kusema shingoni kulikuwa na kitu kikimkaba akaanza kutapika tena ndipo kilitoka kitambaa cheusi kilichofungwa.


Mama mkubwa alipokifungua, wote tulipigwa butwaa kuona ndani mkiwa na mchele, maharage, unga na njugu mawe, jambo hilo lilitushangaza na kuamini kweli duniani kulikuwa na uchawi.


Mama mkubwa alichukua zile nafaka na kitambaa na kwenda kuvichoma moto nje, tangu hapo mama aliacha kulalamika kupata maumivu zaidi kilichomkabili ni mwili kuishiwa nguvu.


Kama alivyofanya awali alimpikia uji akaweka limao, mama alipokunywa hakutapika tena, siku iliyofuata asubuhi na mapema alituambia kwamba aliota ndoto kwamba baba yangu alikuwa Nkasi hivyo alitaka kwenda kumtafuta kwani aliumia sana mimi kuendelea kuteseka bila kumuona baba yangu.


Licha ya mama mkubwa kumshauri kwamba ndoto zilikuwa ndoto tu asiende kwani angepoteza muda wake na kwamba ipo siku baba angejitokeza kama huko alikokuwa alikuwa hai lakini mama alisema atakwenda Nkasi.


Kwa kuwa alikuwa na fedha, baada ya maandalizi ya siku mbili aliondoka kuelekea Rukwa na kuniacha na mama mkubwa, tangu alipoondoka sikupatwa na tatizo lolote.


Wiki mbili baadaye, tulipata taarifa ya kuhuzunisha kuhusu kifo cha mama kilichotokana na ajali ya gali, siku hiyo nililia sana, kwa upande wa mama mkubwa aliishia kuzungumza peke yake na kusema kifo cha mama kilikuwa na mkono wa mtu.


Ukweli sitakaa nisahau siku hiyo ambayo kila ninapoikumbuka huwa nalia, baada ya taarifa hiyo tuliondoka na mama mkubwa na kwenda Mpanda kwa babu.


Nilipofika nilipokelewa vizuri na ukoo wa mama ambao siyo mkubwa sana na baada ya wiki moja mama mkubwa aliwaaga tayari kwa kurejea Mbeya.


Hata hivyo, bibi na mjomba wangu mmoja walimuomba mama mkubwa aniache kule kijijini lakini alikataa na kuwaeleza kwa kuwa rafiki yake alifariki dunia yeye atanilea na kunisomesha hivyo wasiwe na wasiwasi.


Baada ya kuwaeleza hivyo, hawakuwa na kipingamizi ndipo tuliondoka na mama mkubwa tukarudi Mbeya kuendelea na maisha ya upweke.


Siku za mwanzo nilikuwa katika wakati mgumu sana lakini kwa kuwa binadamu tunasahau kadiri siku zilivyosonga mbele nilizoea na kumchukulia mama mkubwa kama mama yangu mzazi.


Wakati huo nilikuwa sielewi kama katika maisha yangu ningekumbwa na masaibu ambayo yangenifanya niichukie dunia na kutamani kumfuata mama yangu.


Baada ya kurejea kutoka msibani, nilikaa mwezi mmoja bila kupata tatizo lolote, siku moja usiku nikiwa nimelala nilishtuka usingizini nikakiona kimvuli cha mtu kikiwa kimesimama pembeni ya mlango.


Kutokana na uwoga niliokuwanao nikaamua kumwita mama mkubwa lakini katika hali ambayo mpaka leo nashindwa kuielewa sauti haikutoka, ghala nikashtikiwa nakabwa shingoni huku mtu aliyenikaba akisem nitamtambua.


Kila nilipojitahidi kumwita mama nilishindwa ndipo nikaanza kumuomba Mungu kimoyomoyo na kusema; Mungu nisaidie, Mungu nisaidie, niliendelea kusema hivyo ndipo yule mtu akaniacha na kutoa msonyo.


“Leo ningekuuliza mbali mweu wewe na ipo siku nitafanikiwa eti unamuita Mungu wako, nani ambaye hana Mungu,” mtu huyo alitoa kauli hiyo na kutoweka.


Baada ya kutoweka, nilimuita mama mkubwa ambaye alikuja chumbani kwangu na kunikuta nalia, aliponiuliza sababu nilimweleza kila kitu, nikahamia chumbani kwake.


Kulipokucha alinifahamisha kwamba alivumilia sana vitimbi vilivyokuwa vikitokea kwenye ile nyumba na kusema kodi yake ikiisha angetafuta nyumba sehemu nyingine.


Nilimshukuru sana kwa uamuzi huo, baada ya kujiandaa nilikwenda shuleni ambapo muda mwingi nilikuwa namuwaza mama na kujiuliza hivi ni lini nitaacha kusumbuliwa na wachawi ili nami nilale kwa amani!


Nakumbuka siku ya Jumamosi nikiwa nyumbani alifika yule mama rafiki yake mama mkubwa wa Shinyanga, mama mkubwa alipomkea kwa furaha.


Baada ya salamu, alimwuliza mama mkubwa mama alikuwa wapi, badala ya kumjibu mama mkubwa alinitazama usoni kisha akamtazama yule mgeni na kuishia kuguna.


Mgeni alipomuuliza sababu za kuguna alimwambia basi tu, alipotoa kauli hiyo nikajikuta natiririkwa na machozi na kuanza kujifuta kwa kutumia viganja.


Kitendo hicho kilimshtua yule mama akamwuliza sababu za kulia ndipo alimfahamisha kwamba mama alifariki dunia na kulia kwangu kulisababishwa na kumkumbusha msiba wa mama.


ITAENDELEA

Comments