KILICHONITOKEA BAADA YA KUBAKWA NA KAKA YANGU - 3

 

KILICHONITOKEA BAADA YA KUBAKWA NA KAKA YANGU - 3

 



Simulizi : Kilichonitokea Baada Ya Kubakwa Na Kaka Yangu

Sehemu Ya Tatu (3)



Yule mgeni alipata huzuni na kumuuliza mama mkubwa kama alichokisema kilikuwa kweli, akamwambia hakuwa na sababu ya kumuongopea kwenye suala la kifo, alijongea kwa mama mkubwa na kumkumbatia akaanza kulia na kumpa pole.


Alipomaliza kumpa pole alihamia kwangu, licha ya kwamba nilikuwa binti mkubwa alinipakata na kunipa pole, kwa dakika kadhaa nyumba ya mama mkubwa iligubikwa na vilio lakini baadaye tulinyamaza.


Baada ya kunyamaza, yule mama alimuuliza mama mkubwa sababu za kifo cha mama, alimfahamisha kwamba kilitokana na ajali.


Taarifa hiyo ilimhuzunisha sana yule mama akatupa pole na kusema kama angepata taarifa za msiba wa mama tungeungana naye kwenda Mpanda.


Baada ya kutufariji kwa muda, yule mama alifungua mkoba wake na kutoa pochi ndogo ambayo aliifungua na kutoa shilingi 20,000, elfu kumi alinipatia na kumi nyingine alimpatia mama mkubwa kama pole.


Hakuishia hapo, alifungua begi lingine akatoa kitenge kimoja akampatia mama mkubwa, mimi alinipatia gauni zuri sana ambalo alisema alikuwa ameliandaa kama zawadi yangu.





Baada ya kumshukuru, alitoa kitenge kingine akanipatia na kusema alikuwa kamletea mama lakini kwa kuwa hakuwepo kitakuwa changu.


Nikiwa nimeshika zawadi hizo, nilijikuta natiririkwa na machozi jambo lililowafanya mama mkubwa na rafiki yake kupata kibarua cha kunisihi ninyamaze.


Nilipotulia, yule mama aliniambia maneno ya faraja kwamba nisilie sana badala yake niwe namuombea mama huko aliko apumzike kwa amani kwani licha ya sisi kumpenda lakini Mungu alimpenda sana akaamua kumchukua.


Nilimshukuru kwa maneno hayo ya faraja, mama mkubwa aliandaa chakula, tulipokula yule mama alituaga kwamba anakwenda kufuatialia mizigo yake angerejea kulala pale nyumbani.


Jioni alirejea akiwa kanunua mahitaji mbalimbali ya nyumbani, katika maongezi yaliyojiri usiku, alimuomba mama mkubwa kama hatajali aondoke nami kwenda nyumbani kwake Shinyanga.


“Nipe muda wa kufikiria jambo hilo kwani siyo la kulifanya haraka,” Dorcas anasema mama mkubwa alimwambia rafiki yake.


Kufuatia kuambiwa hivyo, yule mama mwenye upendo alimwuliza kufikiria nini wakati naye alikuwa sawa na mama yake na alihitaji kunifariji kwa kufiwa na mama.


Mama mkubwa alimfahamisha kwamba alikuwa sahihi lakini akumbuke nilikuwa mtoto wa watu hivyo kuniruhusu tu kwenda Shinyanga bila hata ndugu yeyote wa mama kufahamu isingekuwa vizuri.


Mama mkubwa alipotoa kauli hiyo, yule mama alimwelewa na kusema awasiliane na ndugu wa mama atakaporejea tena Mbeya angeondoka nami.


Kwa upande wangu, nilifurahi sana kuhamia Shinyanga bila kujua kama huko ndiko ungekuwa mwanzo wa mateso yaliyobadilisha kabisa maisha yangu.


Usiku huo tulizungumza mambo mengi ambapo yule mama wa Shinyanga alitusimulia jinsi anavyoishi vizuri na familia yake na kwamba siku ambayo ningefika kwake angejisikia faraja sana.

Kulipokucha, niliwaaga mama zangu hao nikaenda shuleni na niliporejea alasiri mama mkubwa alinifahamisha kwamba rafiki yake aliondoka kuelekea Tabora.


Mama aliniambia kuwa, yule mama alikuwa na upendo sana ambapo nilimuunga mkono kisha aliniuliza kama nilikuwa tayari kwenda kuishi naye Shinyanga.


Kwa kuwa bado sikukomaa sana akili, nilimwambia nilikuwa tayari akacheka na kunieleza akiwasiliana na mjomba wangu akimruhusu nitakwenda Shinyanga.

Wiki moja tangu tulipozungumza na mama mkubwa kuhusu safari ya kwenda Shinyanga, nilianza kuugua tumbo ambalo halikuwa la kawaida.


Kufuatia maradhi hayo, nilipelekwa hospitali ambapo nilifanyiwa vipimo jambo la kushangaza sikupata nafuu.

Ugonjwa huo ulikwenda sambamba na kuweweseka usiku na kupiga mayowe jambo lililomchanganya sana mama mkubwa ambaye aliamua kunipeleka kwa yule mganga wa Songwe.


Aliamua kunipeleka huko kwa sababu alikuwa anaamini sana mambo ya kishirikina, tulipofika kama kawaida yule mganga alituambia kwamba ugonjwa wangu ulikuwa wa kurogwa.


Hata hivyo, kabla ya kuendelea kunitibu alimuuliza mama mkubwa mbona mama hakuwepo, swali hilo lilisababisha ukimya wa sekunde kadhaa ndipo alimuomba samahani kwa kutomfahamisha.


Mganga huyo alipouliza kufahamishwa kitu gani, mama mkubwa alimweleza kwamba mama alikwishatangulia mbele za haki, mganga akashtuka.


Kwa kuwa nilikuwa nimekumbushwa kifo cha mama, nilijikuta natiririkwa na machozi ndipo mama na yule mganga wakaanza kunibembeleza ninyamaze.


Niliponyamaza, mganga aliyekuwa ameguswa sana na kifo cha mama alimwuliza mama mkubwa kilichomsibu mama, akamwelezea kila kitu lakini cha kushangaza akasema kifo chake hakikuwa bure.


“Kwa maelezo yako kuhusu kifo cha mwenzako na jinsi huyu binti anavyoumwa siyo bure, ngoja niwaulize wakubwa,” Dorcas alimkariri yule mganga.


Baada ya kutoa kauli hiyo, mama mkubwa alimuunga mkono na kusema ndiyo maana alifunga safari kumfuata ndipo yule mganga alivaa zana zake za kazi na kukaa sehemu aliyokuwa akifanyia kazi yake.

Akiwa hapo alishika matunguri, usinga akawa anazungumza maneno ambayo hatukuyafahamu kisha akatikisa kichwa na kusema kwamba yule mbaya wetu alipanga kutumaliza.


Aliongeza kuwa, hata kifo cha mama kilisababishwa na yule mama mbaya wetu kwa kushirikiana na wenzake aliowaalika kutoka mbali kisha akasema apewe ruhusa ya kumuadhibu.


Kwa kuwa mama aliyekuwa akipinga kulipa kisasi hakuwepo, mama mkubwa alikubali mganga akasema mtu anayefikia hatua ya kuua watu bila sababu naye anapaswa kuuawa bila huruma.


Baada ya mganga kutoa kauli hiyo alisema kwa kuwa nilifika kwake angenipatia dawa ambayo ingeniponya ndipo alivua nguo za kazi akamuita mkewe aliyekuwa akianika mbona ya majani iliyokuwa imetwangwa.


Alipofika alimpa maelekezo ya kutengeneza dawa kisha aliomba amwite msaidizi wake, kijana huyo alipofika alimwambia amchinje kuku mweusi ambaye angechanganywa na dawa.


Baada ya saa moja dawa iliyochanganywa kwenye supu ya kuku ililetwa kwenye bakuli kubwa, mganga huyo alimimina supu na baadhi ya kitoweo kwenye bakuli tatu.


Alipofanya hivyo, bakuli moja alimpatia mama mkubwa, lingine mimi na iliyobaki ilikuwa yake akatuambia dawa ilikuwa tayari hivyo tunywe, naye akawa anakunywa iliyokuwa kwenye bakuli lake.

Tulipomaliza, mkewe alikuja na dawa nyingine iliyokuwa kwenye chupa akamkambidhi mumewe ambaye alianimbia ninywe kwa muda wa siku tatu mara tatu.


Baada ya kutupa maelezo hayo, alitufahamisha kwamba zisingepita siku nyingi tungepata taarifa kuhusiana na mchawi aliyekuwa akitusumbua ambaye alipanga pia kuniondoa duniani.


Mganga alipotoa kauli hiyo, mama mkubwa alifurahi sana na baada ya kumaliza mambo yaliyotupeleka kule tulimuaga mganga huku nikiwa nimepata nafuu kwa kiasi kikubwa.


Tulipofika nyumbani hali yangu iliendelea vizuri na baada ya ya siku mbili nilikuwa nimepona kabisa lakini sikujua kama yule mama mchawi alikuwa akinifuatilia.


Baada ya kuanza shule nikiwa buheri wa afya, tukiwa tumemaliza wiki moja asubuhi wakati nakunywa chai mama mmoja ambaye alikuwa rafiki wa mama mkubwa alifika nyumbani na kutupa taarifa ya msiba.


Kwa kuwa mama huyo hakutueleza ulikuwa msiba wa nani, mama mkubwa alimwuliza ndipo alitufahamisha kuhusu kifo cha ghafla cha yule mama tuliyehisi alikuwa akituchezea.


Mama mkubwa ambaye moyoni alifurahishwa na taarifa hiyo alijifanya kusikitika na kumuuliza mleta taarifa kilichomsibu mpaka akafariki dunia ambapo alisema alianguka akiwa msalani.

Baada ya kumpa taarifa mama mkubwa, mama huyo alituaga kwamba anakwenda kumpatia taarifa mwenyekiti wa kikundi chao cha kusaidiana ambacho marehemu alikuwa mwanachama pia.


Alipoondoka, mama mkubwa aliniambia mtenda ubaya hulipwa kwa ubaya kwani mganga aliamua kumuadhibu yule mama mchawi kwa maovu aliyotufanyia.

Siku hiyo mama mkubwa alifurahi, alihudhuria kwenye msiba maisha yakaendelea kwa amani bila kusumbuliwa na maradhi na mambo mengine.


Kufuatia hali yangu kuwa nzuri, mama mkubwa alinunua sukari, sabuni na mafuta ya kula kisha akaenda kumsalimia yule mganga.


Aliporejea jioni, aliniambia kwamba mganga alifurahi sana kumuona na alimfahamisha kwamba alikasirishwa sana na kitendo cha yule mama kumfuata kichawi kwa lengo la kummaliza.


Mama mkubwa alinieleza kuwa, mganga huyo aliamua kumuwekea mtego na siku ambayo mama huyo alikwenda Songwe kwa yule mganga kichawi alikutana na kombora lililommaliza.





Siku hiyo tulizungumza mambo mengi na mama mkubwa ambaye alikuwa akinipenda sana kisha tulilala na kesho yake nilikwenda shuleni, hata hivyo mara kwa mara nilikuwa naifikiria safari ya Shinyanga.


Miezi miwili baadaye, siku ya Ijumaa niliporejea nyumbani kutoka shuleni nilimkuta yule rafiki wa mama mkubwa, aliponiona alifurahi sana na kuniambia ujio wake alikuwa kanifuata.


Nilifurahi sana kusikia taarifa hiyo na mama mkubwa alibaini nilifurahishwa akiwa anacheka aliniuliza kama nilikuwa tayari kwenda Shinyanga nikamkubalia.


Katika maongezi yaliyojiri baada ya kupata chakula, yule mama wa Shinyanga alimwambia mama atafurahi sana kama angeondoka nami kwenda kwake na kuongeza kuwa aliamini hakukuwa na kikwazo kufuatia mama kuwaambia ndugu zangu.


Mama mkubwa alimfahamisha kwamba ingawa hakuwaambia mjomba hakuona tatizo, yule mama alifurahi sana kusikia hivyo.


“Kwa kweli nimefurahi kusikia hivyo, hata wanangu wanahamu ya kukuona Dorcas kwani mara kwa mara huwa ninawapa habari zako,” Dorcas anasema yule mama alimwambia.


Kwa kuwa sikuchukuliwa uhamisho, yule mama alisema anakwenda Malawi ambako angekaa wiki moja hivyo alimuomba mama anichukulie uhamisho ambapo alimweleza jina la shule ambayo ningehamia.


Kutokana mara kwa mara yule mama kupendelea kufikia hoteli, kabla ya kwenda kulala mjini alimpatia mama shilingi 20, 000 kisha alituaga akaelekea mjini.


Siku iliyofuata alikwenda Malawi na baada ya kupita siku sita alirejea na kukuta mama kishachukua uhamisho, alifurahi sana na siku iliyofuata alfajiri tuliondoka Mbeya kuelekea jijini Dar es Salaam alikotueleza alifuata mzigo wa biashara.


Tulipofika jijini Dar es Salaam mazingira yalikuwa tofauti na Mbeya nikawa nashangaa kila nilichokiona wakiwemo watu wengi, magari na uwingi wa nyumba.

Ingawa mama huyo alinifahamisha kuwa Dar alikuwa na ndugu zake, hatukufikia kwa mtu badala yake tulifikia katika hoteli moja iliyopo karibu na stendi ya mabasi yaendayo mikoani.


Kutokana na uchovu baada ya kuoga na kula tulilala na kesho yake asubuhi tulikwenda Kariakoo, huko nilizidi kulishangaa Jiji la Dar jinsi lilivyokuwa na watu wengi, majumba ya ghorofa nk.


Kabla ya kuanza kufanya manunuzi, tulikwenda katika benki moja ambapo mama huyo alichukua fedha tukaanza kuingia madukani ambako alinunua nguo za akina mama, watoto,mashuka na mablanketi kadhaa nami alininunulia viatu, nguo za ndani, magauni matatu.


Baada ya kuzunguka sana tukiwa na mizigo yetu tuliingia katika hoteli moja tukala kisha alikodi gari tukarudi hotelini Ubungo kwa ajili ya kupumzika, jioni tulikwenda kwa ndugu yake aliyekuwa akiishi Kimara.


Tulikaa huko hadi usiku na baada ya kula tulirudi hoteli ambapo tulilala na alfajiri tuliondoka Dar kuelekea Shinyanga ambako tulifika saa tatu na nusu usiku.


Tulipofika stendi tulipokelewa na kijana mmoja aliyekuwa na gari dogo, baada ya salamu alipakiza mizigo yote ndani ya gari tukaelekea nyumbani kwa mama huyo eneo la Majengo


Siku hiyo nilifurahi sana kubadili eneo la kuishi kwani sikuwahi kufika Shinyanga zaidi ya kuisikia tu, wenyeji wetu nao walifurahi sana kutuona.


Mama alinitambulisha kwa dada mmoja niliyemkuta pale nyumbani, msichana mmoja ambaye alisema alikuwa mwanaye aliyeitwa Emmy na kijana ambaye alisema alikuwa ni mtoto wa kaka yake.


Alinitambulisha pia kwa wenyeji wangu hao kisha alinifahamisha kwamba mwanaye aitwaye Evance alikuwa masomoni katika chuo kikuu kimoja kilichopo jijini Dar .


Kama unavyofahamu mtu anapokuwa mgeni anavyokuwa mgeni kwa kila jambo, nami ilinichukua siku kadhaa kuzoeana na wenyeji wangu na mazingira.


Baada ya kukaa nyumbani siku nne, ndipo mama huyo ambaye nilimchukulia kama mama yangu mzazi alinipeleka shule iitwayo Town School bila kujua huko Shinyanga ndiko ungekuwa mwanzo wa kuharibikiwa kimaisha.


Nilifurahi sana kuhamia katika shule hiyo kwani niliweza kupata marafiki ambao walinipenda, kutokana na uwezo wangu mzuri darasani hata walimu hasa wa darasa letu alikuwa akinipenda pia.


Maisha yaliendelea bila kujua masaibu yaliyokuwa mbele yangu na laiti kama ningejua wala nisingekubali kuhamia Shinyanga, kwa ujumla nyumbani kwa yule mama sikupungukiwa na kitu.


Ninaposema sikupungukiwa na kitu namaanisha alikuwa akininunulia nguo, viatu na kwa upande wa chakula nilikula kila kilicholiwa pale nyumbani tofauti na familia zingine zinavyofanya hasa kwa watu ambao siyo wanafamilia wa damu.


Kwa kuwa nilihamia Shinyanga mwezi wa kumi ilipofika Desemba mwanzoni tulifunga shuleni kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.


Wakati huo mama wa Shinganya alikwenda Mbeya mara mbili ambapo alikuwa akinieleza kuwa mama mkubwa alikuwa akiendelea vizuri na alikuwa akinisalimia.


Kufuatia kufunga shule, Evance mtoto wa kiume pekee wa mama huyo aliyekuwa akisoma chuo jijini Dar es Salaam alifika na kunikuta ambapo mama alimtambulisha.


“Evance huyu ndiye Dorcas niliyekuwa nakupa habari zake mara kwa mara, Dorcas huyu ndiye kaka yako Evance niliyekwambia anasoma jijini Dar es Salaam,” Dorcas anasema yule mama alimtambulisha kwa mwanaye.


Baada ya kutambulishwa, Evance ambaye wakati huo alikuwa mwaka wa kwanza chuoni kwao alinikaribisha kwa furaha na kusema alifurahi kupata dada mwingine kwenye familia yao.


Evance aliyeambiwa kwamba nilikuwa nina maendeleo mazuri shuleni alinipongeza na kusema anapenda sana watu wanaopenda kujisomea na kufanya vizuri shuleni kama mimi.


Nilimshukuru ndipo aliniambia kwa kipindi ambacho atakuwa pale nyumbani atautumia muda huo kunifundisha masomo mbalimbali, nilifurahi sana kusikia hivyo.


Maisha yaliendelea huku nikiwa na furaha na kaka Evance ambaye nilimchukulia kama kaka yangu wa damu akiwa karibu nami kwa kila jambo hususan kunifundisha mambo mbalimbali yahusuyo masomo.


Likizo ilikuwa nzuri sana na Januari tulifungua shule ambapo niliingia rasmi darasa la saba, nilifurahia sana hatua hiyo na wiki mbili baadaye kaka Evance alikwenda kuendelea na chuo Dar.


Nakumbuka baada ya kufungua shule sikukaa muda mrefu nilivunja ungo, mama alinifundisha namna nilivyopaswa kuwa msafi na mambo mengine yanayotuhusu wanawake tukiwa katika hedhi.


Kama kawaida, aliendelea kunijali na kuhakikisha kila mwezi ananinunulia vifaa vinavyohitajika kipindi cha hedhi, yaani alinijali mno hadi nilijisikia raha!


Nikiwa katika kipindi hicho nilianza kunawiri na kuonekana mrembo na kuwa na shepu nzuri ya kike ambapo vijana wengi walikuwa wakinisifia kwamba nilikuwa mzuri.


Kwa kuelewa jambo hilo, mama aliniketisha chini na kunisihi niwe makini na wavulana wasije kunirubuni na kuanza kushiriki mambo ya mapenzi.


Haukishia hapo alinipa mfano wa wasichana ambao walipata mimba wakiwa shuleni na kuharibu maisha yao, nilimshukuru mama kwa ‘darasa’ hilo.


Licha ya kupewa tahadhari hiyo na mama, kwa kuwa nilikuwa napitia kipindi cha ukubwa nilikuwa napata hisia za mapenzi lakini nilikuwa nikijizuia kwa kuwa bize na kazi za nyumbani.


Kadiri siku zlivyokuwa zikisonga, kuna baadhi ya walimu wakawa wakinisifia na yupo mmoja akaanzisha tabia ya kuniita ofisini na kunipa zawadi ya madaftari na kusema alifanya hivyo kwa sababu nilikuwa nafanya vizuri katika masomo yangu.


Mwalimu huyo ambaye niligundua nia yake, kuna wakati alikuwa akinipa fedha ambazo nilizikataa, kwa ujumla nami nilijijua nilikuwa mrembo haswa kwani hata wasichana wenzangu pia walinisifia.





Niliendelea na masomo huku nikikwepa vishawishi vya wanaume hadi tulipofunga shule likizo ya pasaka, kwa kuwa ilikuwa fupi kaka Evance hakuja Shinyanga.


Baada ya sikukuu hiyo, tulifungua shule ambapo niliendelea na masomo hadi ulipofika mwezi wa tano mwishoni tulifunga kwa ajili ya likizo ya mwezi mmoja na wiki moja.


Wakati huo, kaka Evance naye alikuja likizo ya miezi mitatu kama sijakosea, aliponiona aliniambia kwamba nilikuwa nimekuwa mdada, nikamwambia ndiyo akaishia kucheka.


Kaka alifurahi sana alipoona matokeo ya mitihani niliyofanya ambapo alinisifia, nilimshukuru kwani kwa sehemu msaada wake ndiyo uliosababisha pia nifanye vizuri.


Kama ilivyokuwa likizo ya awali, hakuacha kunifundisha na kuwa karibu namI ambapo alinieleza nikikutana na jambo lolote gumu katika masomo nimwambie ili anisaidie.


Baada ya kukaa nyumbani wiki mbili, alifanikiwa kupata kibarua kwenye mradi mmoja wa Wazungu uliokuwa ukishughulika na masuala ya mazingira na maji.


Kufuatia kupata kibarua hicho akawa anatoka nyumbani asubuhi na kurejea jioni, mama alifurahi sana na kuniambia nifuate nyao za kaka yangu kwani kusoma lilikuwa jambo zuri ndiyo maana hata kabla hajamaliza chuo aliweza kupata kazi.


Nilimwambia mama nitajitahidi kuwa kama kaka Evance, mama alifurahi sana kusikia hivyo, nakumbuka kaka alipopata mshahara wake wa kwanza, sehemu ya fedha alizolipwa alimpatia mama, akanininua viatu mimi na mdogo wake Emmy ambaye hakupenda sana sababu alikuwa hapendi shule.


Niliendelea na masomo na kaka aliendelea na kazi hadi muda wake wa kurudi chuoni ulipowadia aliaga alikokuwa akifanyia kazi na suku mbili baadaye alikwenda Dar es Salaam kuendelea na masomo.


Ilipofika Oktoba mwishoni tulifanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba na kwa jinsi nilivyokuwa nimejiandaa nilikuwa najua matokeo yatakapotoka nitakuwa miongoni mwa wanafunzi watakaofaulu.


Kaka aliporokuja nyumbani wakati wa Sikukuu ya Chrismasi na Mwaka Mpya alinuliza kama nilitafaulu, ningemwambia ilikuwa lazima, akafurahi sana.


Kama nilivyokuwa nategemea, matokeo yalipotoa nilikuwa nimefaulu, kila mmoja alifurahi sana na kunipongeza, nilimshukuru sana kaka Evance kwa msaada wake ulionmiwezesha kufaulu.


Ilipofika Januari nilianza masomo ya sekondari katika shule iliyopo mkoani humo, kaka aliniambia japo alikuwa mbali atajitahidi kunitafutia vitabu na kunitumia.


Wakati nikiwa kidato cha kwanza katika shule hiyo ya kutwa, bado niliendelea kusumbuliwa na wanaume kutokana na uzuri wangu kwani nikiwa kama binti niliyekua nilikuwa najipenda sana.


Pamoja na kusumbuliwa na wanaume wakiwemo wenye fedha zao, sikuzuzuka nikaendelea na msimamo wangu jambo ambalo lilimfurahisha sana mama.


Marafiki zangu ambao hawakuwa watulivu walikuwa wakinicheka kufuatia kutokuwa na mpenzi kama walivyokuwa wao lakini hawakuweza kubadili msimamo wangu.


Kutokana na msimamo huo, akina mama wengi walinitolea mfano kwa watoto wao kwamba waniige jinsi nilivyokuwa, kwa ujumla nilikuwa najisikia vizuri sana kusifiwa.


Kama kawaida, tulipofika katikati tulifunga shule kwa likizo ambapo kaka Evance alikuja Shinyanga kwa mapumziko marefu, aliponiona alifurahi sana.


Kama ilivyokuwa awali akawa yupo karibu nami latika kunifundisha na wakati mwingine alikuwa akinisubiri tule pamoja, alikuwa akinipenda sana.


Tofauti na wakati nilipokuwa nasoma shule ya msingi ambapo alikuwa akinifundisha masomo nisiyoyaelewa sebuleni wakati mwingine nje ya nyumba, akawa anapenda kuniita chumbani kwake.


Awali nilikuwa nahofu lakini kwa vile nilimchukulia kama kaka yangu wa damu, sikuwa na wasiwasi nikawa naingia ambapo alikuwa akinifundisha kusoma na namna ya kutumia laptop yake.


Kadiri siku zilivyokuwa zinasonga akawa anaonesha dalili za mapenzi ndipo kengele ya tahadhari ililia kichwani mwangu nikaanza kumkwepa kila aliponiambia nikajisomee chumbani kwake nikawa najifanya nipo bize au kumwambia tukae sebuleni.


Niliendelea na msimamo wangu hadi aliporudi chuoni, nami nikaendelea na masomo lakini mara kwa mara alipokuwa akimpigia simu mama aliomba wanipatie simu ili aweze kuongea nami.


Maisha yaliendelea hadi tulipofunga tena shule kwa ajili ya likizo ya Desemba ambapo kaka Evance alikuja Shinyanga kwa ajili ya Sikukuu ya Krisamsi na Mwaka Mpya, wakati huo mama alikuwa anaendelea na biashara zake za kusafiri.


Nakumbuka wakati wa likizo hiyo, pale nyumbani watu walisafiri kwenda kijijini nilibaki mimi, mdogo wa Evance, mama na Evance.


Kama ilivyokuwa kawaida yake, Evance mara kwa mara alikuwa akipenda kuwa na mimi na hata marafiki zake waligundua hilo wakaanza kumsema vibaya lakini hakujali.


Kaka aliendelea kuwa karibu na mimi kunifundisha masomo na namna ya kutumia laptop yake ambapo alisema ilikuwa muhimu sana kujua namna ya kuitumia.


Mara kwa mara alikuwa akiniita chumbani kwake akawa ananifundisha baadhi ya proglamu, kuna siku alifanya kitu kilichonishangaza sana.


Siku hiyo akiwa ananifundisha alifungua folda lillokuwa na watu waliokuwa wakifanya mapenzi, alipobaini nimeziona picha zile aliniambia nisijali kwani kwenye kompyua kuna mambo mengi na kwa kuwa nilikuwa mkubwa ninapojisikia niwe nafungua folda lile kwa ajili ya kujifunza mambo ya mapenzi.


Licha ya kutopendezwa na kitendo kile sikutaka kumuonesha kwamba nilichukia, nilimwambia sawa lakini moyoni niliapa kutofanya hivyo.


Tangu siku hiyo kila alipokuwa akinifundisha akawa anafungu mafolda ya picha za wanaume waliokuwa utupu au kukumbatiana na wasichana ndipo nikagundua hakuwa na nia njema.


Siku moja pale nyumbani waliondoka wote nikabaki peke yangu, nilipomaliza kupika kaka alirejea na mfuko wa rambo akaniita sebuleni kisha kunikabidhi na kuniambia aliniletea zawadi nzuri sana.


Niliupokea mfuko huo na kumuuliza ni zawadi gani aliyoniletea, akacheka na kuniambia ni zawadi ya kawaida ila anaaamini nitaipenda, nilimshukuru nikauweka ule mfuko juu ya meza ndogo iliyokuwa pembeni ya sofa.


Baada ya kuuweka pale, kaka aliniambia hapakuwa sehemu sahihi na kuniomba niende nayo chumbani kwangu kisha nikaiangalie zawadi hiyo.


Alipotoa kauli hiyo, nilimwambia kwa kuwa aliniletea zawadi asiwe na shaka nitaingalia kwa wakati wangu lakini kaka alisisitiza niende nikaingalie chumbani kwangu.


Kuepusha kuona sikumheshimu niliuchukua ule mfuko na kwenda nayo chumbani kwangu lakini sijui kwa nini sikuwa na haraka ya kutaka kujua ni zawadi gani kaka aliniletea, niliuweka ule mfuko kitandani nikatoka.


Nilipofika sebuleni, kaka alitabasamu na kuniuliza kama nilipenda zawadi aliyoniletea nikamwambia nimeuweka tu mfuko kitandani bila kuiangalia.


Aliniuliza kama sikufurahi yeye kuniletea zawadi nikamwambia nilifurahia lakini kwa kuwa ilikuwa yangu ningeiangalia muda wowote nitakaopenda mimi.


Baada ya kumwambia hivyo, ghafla alipoteza uchangamfu nigagundua nilimkwaza nikamuuliza kwa nini alipenda niiangalie ile zawadi muda ule!


Nilipomwambia hivyo alisema hakuamini kama ningemfanyia vile kwa sababu kawaida ya mtu yeyote anapoletewa zawadi huwa na shauku ya kuiona lakini mimi sikufanya hivyo.


Kumtoa shaka nilimwambia aondoe shaka nitaiangalia na kumshukuru tena kwa kuniletea zawadi hiyo, yaani nashindwa kuelewa kwa nini sikuwa na shauku ya kuiangalia.


Kufuatia kumweleza hivyo, kaka alibaki akiniangalia kisha alinieleza kwamba nitakapoingalia nimwambie kama niliipenda, nikamwambia asiwe na shaka ndipo akawasha TV akaanza kuangalia.


Wakati kaka akiangalia runinga, nikiwa nimeketi kwenye sofa ambalo lilikuwa kushoto kwake nikawa najiuliza ni zawadi gania aliyoniletea aliyokuwa akinilamisha kuiangalia.


Baada ya kujiuliza niliamka na kwenda chumbani kwangu nikaufungua ule mfuko, nikakuta ndani kuna kitu kama nguo kikiwa kimefungwa kwenye mfuko wa khaki nikaufungua.




Nilishangaa kuona kuna chupi tatu nzuri sana za rangi nyeupe, maziwa na pinki pia kulikuwa na vitambaa vyeupe vinne, nikajiuliza kaka kuniletea zawadi ya aina ile alikuwa na maana gani.


Ukweli nguo hizo za ndani zilikuwa nzuri sana tofauti na nilizokuwanazo lakini bado nilijiuliza kwa nini kaka yangu aniletee nguo hizo nyeti, nikazirudisha kwenye mfuko kisha nikauweka ndani ya begi langu.


Niliamua kuziweka kwenye begi kuhofia kama mama angeziona angeniuliza nilizitoa wapi, hata kama ningemwambia niletewa na kaka asingenielewa na kuniambia kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea baina yetu.


Baada ya kuziweka nilikwenda sebuleni na kumkuta kaka akiangalia runinga, alipogeuka na kuniona alijua nilikwenda kuangalia zawadi aliyoniletea, akaniuliza kama niliipenda zawadi hiyo.


Kufuatia kuniuliza hivyo, nilimuuliza akiwa kama kaka yangu kwa nini aliamua kuninunulia nguo za ndani badala ya kuniletea zawadi nyingine kama madaftari nk.


Kaka alicheka na kunieleza hakukuwa na ubaya kwa kaka kumnunulia dada yake nguo nzuri za ndani ili apendeze, nikamwambia alikosea sana hivyo nitamkabidhi zawadi zake.


Nilipomwambia hivyo, aliniambia niache ushamba kwani hakukuwa na ubaya wa kaka kumnunulia nguo za ndani dada yake kuonesha anavyompenda na kumjali.


Wakati tunaendelea na mazungumzo, mama alifika hivyo tulibadili maongezi ndipo mama alituuliza kuhusu habari za pale nyumbani tukamwambia zilikuwa nzuri sana.


Hata hivyo, mama aliyeonekana kuwa na haraka alituambia alifuata hela ambapo aliingia chumbani kwake hakukaa sana akatuaga kwamba anakwenda kumuona mtu mmoja.


Baada ya mama kuondoka, kaka aliendelea kuniambia kwamba alinishangaa sana badala ua kumshukuru kwa zawadi nzuri aliyoniletea badala yake nilimwambia alikosea.


Kwa kuwa sikuwa na amani moyoni juu ya zawadi alizoniletea, nilimwambia asubiri niende nikamchukulie zawadi zake ili akampatie mtu mwingine yeyote.


Alipoona nataka kuinuka alinizuia na kuniomba msamaha ambapo alisema kama sikupendezwa na zawadi nizipokee tu na kwamba siku nyingine hata kuniletea zawadi za aina hiyo.


Kufuatia kuniomba msamaha niligundua alielewa kwamba sikufurahishwa na zawadi zake na kwa kumheshimu nilimwambia yalikwisha na kuahidi kuzitumia.


“Hapo dada yangu umenifurahisha sana, hivyo ndivyo unavyotakiwa kuwa, nashukuru kwa kuzikubali zawadi nilizokuletea,” Dorcas anasema kaka yake alimwambia.


Baada ya kumaliza tofauti zetu kuhusu zawadi, niliendelea na majukumu yangu huku kaka akiwa anaangalia TV na wakati mwingine kunifuata jikoni na kunisemesha hadi mama na wengine walioondoka waliporejea.


Kama kawaida yetu usiku baada ya kupata chakula na kupiga stori za hapa na pale kila mmoja alikwenda kulala, hata hivyo nikiwa nimejilaza kitandani nautafuta usingizi, nikawa najiuliza maswali mengi kuhusu dalili za mapenzi alizoanza kunionesha kaka Evance.


Hata hivyo, kwa kujiamini nilijua hata angefanyaje asingeweza kunirubuni kwa vile nilikuwa najitambua na isitoshe pale nyumbani muda mwingi palikuwa na watu.


Licha ya Emmy aliyekuwa akisoma Tabora kunipita kidogo umri, sikuwa napenda kumshirikisha sana mambo yangu ya ndani ndiyo maana hata zile zawadi alizoniletea kaka sikumwambia.


Sikufanya hivyo kuhofia angehisi huenda nilikuwa nina uhusiano naye wa kimapenzi hivyo kumwambia mama na kuleta balaa jambo ambalo sikutaka litokee.


Kutokana na hofu niliyokuwanayo, niliamua kutozivaa zile nguo za ndani kwa sababu angeniuliza nilipata wapi fedha za kununua nguo zile za kisasa au angemuuliza mama iweje aninunulie mimi na kumuacha yeye.


Nilipanga kuzivaa nguo hizo nitakapoenda Mbeya kwani mama mkubwa angejua nilinunuliwa na rafiki yake, baada ya kupita kama siku mbili hivi nikiwa jikoni napika kaka Evance huku akichekacheka alinifuata na kuniuliza kama chupi alizoniletea zilinitosha na kunipendeza.


Kufuatia swali hilo, nilishindwa kumjibu nikabaki kumwangalia ndipo aliniita, nilipoitika aliniuliza mbona sikumjibu swali lake badala yake nilibaki nikimwangalia tu!


Ingawa nilizijaribisha zile nguo na kunitosha, kuepusha usumbufu wake nilimshukuru na kumwambia hazikuwa na tatizo na kuhusu kunipendeza au kutonipendeza ilikuwa siri yangu, akacheka sana na kusema; “Wewe Dorcas una majibu ya mkato sana!”


Alipotoa kauli hiyo, Emmy ambaye alikuwa chumbani aliingia jikoni ndipo tulibadili mada na kuzungumza mambo mengine, Emmy aliniuliza kama nilinunua matunda ya kutengeneza juisi nikamwambia sikununua.


Baada ya kumjibu hivyo aliniomba nimpatie fedha za kununulia matunda, nilipompa alielekea sokoni na kuniacha nikiwa na kaka ambaye aliniuliza kwa nini nilikuwa na majibu ya mkato!


Nilimjibu kwamba nilimjibu kawaida tu akasema sikumjibu sawa aliniponiuliza kama zile nguo zilinipendeza au la, kwa kuwa niliona ananisumbua nilimwambia zilinipendeza.


“Hapo umenijibu vizuri, sasa ungenijibu hivyo tangu awali unafikiri ningekusumbua?” Dorcas anasema kaka yake alimwambia.


Alipotoa kauli hiyo nilimwambia yalikuwa yameisha ila nilimkanya asirudie tena kuniletea zawadi kama zile kwa sababu nilikuwa namheshimu kama kaka yangu.

Cha ajabu licha ya kuonesha kwamba sikupendezwa na alichonifanyia alicheka tu, nikamuacha na kwenda chumbani kwangu.


Maisha yaliendelea nakumbuka Jumapili iliyofuata pale nyumbani waliondoka wote kwenda Kijiji cha Ndembezi kuwasalimia ndugu wengine, kaka naye alipotoka kanisani hakurudi nyumbani.


Kufuatia pale nyumbani kutulia, baada ya kula nilichukua madaftari yangu na kuanza kujisomea lakini sikumaliza hata dakika thelathini kaka alirejea.


Aliponikuta najisomea alinisifia sana na kuniambia kwamba tena ilikuwa afadhali alirudi mapema hivyo angenifundisha kutumia laptop yake.


Baada ya kuniambia hivyo aliniuliza kama nilikuwa nimekula nikamwambia tayari nilikula muda mrefu ndipo akaingia chumbani kwake akabadili nguo na kuvaa bukta na fulana.


Alipobadili akaja sebuleni akanywa maji kisha akasema twende akanifundishe namna ya kutumia laptop yake, awali niligoma lakini akanibembeleza sana kwamba alichotaka kunifundisha kilikuwa muhimu.


Alipoona nasita alibeba madaftari yangu na kwenda nayo chumbani kwake kisha akanifuata, sijui ilikuwaje nikaamua kwenda bila kujua alikuwa na nia gani.


Tulipofika chumbani kwake, ambapo tayari alikuwa kishawasha kompyua yake mpakato na kuiweka juu ya meza ndogo iliyokuwa mbele ya kitanda wote tulikaa kitandani kwa sababu hakukuwa na kiti wala stuli.


Baada ya kukaa, akaiwasha laptop na kunifundisha kidogo, nikamuona akiwa na wasiwasi ndipo aliniuliza kama siku ile nilikuwa nimevaa moja ya nguo za ndani alizoninunulia.


Nilipomwuliza kwa nini aliniuliza vile, akacheka na kuniambia alitaka aone jinsi ilivyonipendeza, nikamwuliza kwa hasira alitaka kufanya nini?


Huku akiwa anacheka akaniambia alitaka kuona kama ilikuwa inanipendeza, nikamwuliza mbona alinivunjia heshima wakati nilikuwa namheshimu?


Nilipomwambia hivyo alisema hata yeye aliniheshimu na ili kumuonesha nilikuwa namheshimu nimuoneshe nguo hiyo, nikakataa nikashangaa kanishika na kuniambia kama nilikuwa sitaki kufanya hivyo angeniangalia kwa nguvu.


Baada ya kunishika tukaanza kuvutana huku nikijitahidi kujitoa mwilini mwake lakini alinizidi nguvu akanilaza kitandani, kwa kuwa nyumba yetu ilijitenga hata nilipojaribu kupiga mayowe ya kuomba msaada hakuna aliyesikia.


Hata hivyo kuhakikisha anatimiza lengo lake akiwa amenibana akaniziba mdomoni kwa kutumia taulo kisha alifanikiwa kuipandisha juu sketi niliyovaa na kuichana nguo yangu ya ndani.



ITAENDELEA

Comments