NJIA RAHISI YA KUPATA MIMBA HARAKA KWA MWANAMKE



1. Kufanya tendo la ndoa mara kwa mara, angalau siku tatu kwa wiki, ikiwezekana on alternate days.

2. Tumia ovulation prediction kit, hiki ni kifaa ambacho kitakusaidia kujua wakati hasa mwanamke ameengua yai na ndio kipindi ambacho mwanamke ana uwezo wa kushika mimba akikutana na mumewe. Ni rahisi kutumia.

3. Fanya tendo la ndoa kabla ya kuengua yai (kabla ya ovulation), huongeza uwezekano wa kushika mimba kuliko kusubiria ovulation au kufanya baada ya ovulation. Kutaneni siku mbili au tatu kabla ya ovulation. Ukitumia ovulation test kit, mkutane kuanzia siku itakapokuwa positive kwani huwa inapredict ovulation kutokea 48 hrs after it tests positive.

4. Usitegemee njia ya kalenda kutabiri uenguaji yai, njia hii kwa kiasi fulani huweza kuwasaidia wale wenye mzunguko wa siku 28, lakini pia haina uhakika wa 100%, wengi wa wanawake hawaengui yai siku ya 14 ya mzunguko wa hedhi, kwa hiyo kutegemea kalenda kutakuchelewesha kupata ujauzito.

5. Unapotaka kushika mimba, acha au punguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya pombe, sigara au dawa za kulevya.

6. Unapotaka kupata mimba, tendo la ndoa liwe kitu 'enjoyable' na sio tendo 'mechanical' kwa ajili ya kutafuta mtoto. Plan a romantic evening or try something different to spice things up. How you are feeling sexually may increase your chances of getting pregnancy. For women a better orgasm may help pull the sperms into the uterus and for men a better orgasm may increase their sperm count.

7. Kufanya mapenzi katika mtindo (style) ambayo itafanya mbegu za kiume zikae kwa muda mrefu ukeni na hivyo nyingi kupanda kuingia kwenye kizazi na kwenda kurutubisha yai. 'missionary position' ni nzuri zaidi, ambapo mwanaume anakuwa juu, epuka positions za mwanamke kuwa juu kwani hufanya mbegu zimwagike kwa gravity. Jaribu pia kuweka mto chini ya kiuno ili kukiinua na kufanya mbegu ziingie ndani kwa urahisi zaidi.


Kumbuka kuna asilimia 10 - 25 ya couples ambazo zina matatizo ya infertility lakini vipimo havionyeshi tatizo, inaweza kuwa namna ya kufanya mapenzi ndio ikawa shida, jaribu njia hizo 7 juu.


Je, ninahitaji kufika kileleni kupata mimba?

Ni dhahiri, kwamba ni muhimu sana kwa mpenzi wako kufikia kileleni ikiwa mnajaribu kupata mtoto. Hakuna ushahidi, hata hivyo, kwamba unahitaji kufika kileleni kupata mimba.
Kwa mwanamke kufika kileleni, jambo la kufurahia na kuridhika. Haina msaada wowote katika kufikisha manii kwenye yai. Mibano milaini ya mji wa mimba inaweza kusaidia mbegu ya kiume kusafiri kwa uhakika, lakini hii hutokea bila hata kufika kileleni
Kwa hiyo, sio muhimu sana kufikia kileleni ili kupata mimba.
Je kuna mikao yeyote inayoweza kutusaidia kuzaa mtoto wa kiume au wa kike?
Hakuna ushaidi, inasemekana kufanya tendo la ndoa mwanamke kuwa juu itapelekea kuzaa mtoto wa kike, ila mwanaume akiwa juu wakati wat endo hili inapelekea mtoto wa kiume kuzaliwa.


Je, nijilaze baada ya tendo?

Manii yanaweza kukaa ndani ya uke wako na maeneo ya karibu na kizazi zaidi kuliko ukinyanyuka mara baada ya tendo. Hata hivyo, mamilioni ya manii hutolewa na kiungo kimoja cha mwanaume, hivyo basi lazima ziwe nyingi katika uke wako hata ukisimama mara tu baada ya tendo.
Kama una muda wa kutosha, ni vema kukaa kitandani mpaka baada ya nusus saa baada ya kufanya mapenzi.

Jaribu kulala kwa mgongo, na mapaja yako yakiwa yamenyanyuliwa juu yam to ili kuhimiza manii kusafiri kwa wepesi kwenda kwenye yai. Usijaribu kufanya hivi kama mshauri wako wa afya alikushauri ukojoe mara baada ya kufanya tendo.
Ujanja mwingine kwa wanawake ni kulala kwa mgongo na kuchochea(cycling) miguu yako juu kwa dakika chache baada ya tendo.

Jambo la muhimu la kukumbuka ukiwa unajaribu kupata mimba, ni kwamba kufanya tendo la ndoa mara kwa mara inaweza kusaidia. Kufanya tendo kila siku mbili mpaka tatu inaongeza nafasi ya kupata mimba ndani ya mwaka, ukilinganisha na kufanya mapenzi mara moja tu kwa wiki.

Ikiwa umejaribu kupata mtoto kwa mwaka au zaidi bila mafanikio, muone mshauri wako wa afya. Ikiwa wewe una umri wa miaka 36 au zaidi au hauna hedhi ya kawaida, unaweza kufanya miadi hata mapema

Comments