Njia sahihi ya kuosha uke wako hii hapa acheni kujisugua na vidole ni hatari
Leo tunapeana elimu ili uelewe mambo muhimu ambayo unatakiwa kuzingatia katika kuuweka uke wako katika mazingira ambayo ni salama kuepuka madhara ya kujitakia.
Ninaposema madhara ya kujitakia ni yale ambayo wewe binafsi unayasababisha.
Hivi karibuni kumekua na malalamiko mengi toka kwa wasichana kutopata ujauzito na wengine kutofurahia pale wanaposhiriki tendo la ndoa.
Wanawake wengi hasa wenye umri kati ya miaka 18-45 wamekua wakikumbwa na matatizo mbalimbali ya uzazi bila kujua kwamba kwa namna moja ama nyingine wao wenyewe ndio chanzo cha matatizo hayo.
Yapo matatizo mengine ni ya kitaalamu lakini mengine tunayasababisha sisi wenyewe, hivyo ni muhimu tukawa makini na afya zetu.
Wapo ambao huwa wanajifanya ni wataalamu ya kuosha uchi huku akiwaelekeza wenzake kwamba unaingiza vidole ndani ya uke na kuuosha na wengine hadi kuingizaa vitu vya kuosha. Hii ni hatari kwa afya yako.
Kama wewe ni miongoni mwa hao mnaofanya hivyo naomba uache mara moja utajisababishia madhara makubwa katika uke wako.
Tabia ya kuosha sehemu za ndani ya uke kwa kutumia viosheo maalumu vinavyopatikana madukani au supermarket mbali mbali.
Hapana hii ni tofauti na ule unawaji wa kawaida au uoshaji wa kawaida unapokwenda kuoga,haijakatazwa kuosha uke wako kwa maji ya uvuguvugu kwakua hiyo ni salama na haina matatizo kiafya.
Vagina douching ni kule kutumia sabuni za maji au maji maalumu ambayo yanakua yamechanganywa na iodine,vinegar na magadi na kuyaingiza ndani ya uke, Hii ni hatari kwa afya ya uke wako.
Njia bora ya kujisafisha ni kutumia maji ya uvuguvugu pale unapooga kwa kusafisha sehemu za nje na sio ndani ya uke kwakua inaelezwa kwamba uke hua unajisafisha wenyewe kwa kutoa kitu kinachoitwa mucous ambayo ina control damu na uchafu mbali mbali ndani ya uke.
Wanawake wenzangu acheni mambo ya uswahili uchi unajiosha wenyewe kitaalamu, achene kuingiza vitu katika uke ili uoshe huko ni kujiingizia bakteria na kuruhusu magonjwa kuingia kwa urahisi kila wakati.
Najua unafahamu kipi kinatakiwa kiingie na kipi kisiingie kwenye njia yako ya uzazi (ukeni) uume na vifaa vya hedhi sio tatizo kiafya ila kumekua na tabia kwa baadhi ya wanawake kutumia ndizi na vitu vinavyofanana na hivyo katika kile kinacho aminika kujiridhisha pale anapokua mbali na mwenzi wake.
Kama hujawahi kufanya tafadhari usijaribu na kama unafanya acha mara moja vitu hivi husababisha vaginal irritation ni maumivu katika uke na michubuko ambayo itakufanya usifurahie tendo la ndoa.
Hayo ni mambo ya ya kuzingatia na kutothubutu hata kujaribu kuyafanya kwa ajili ya kulinda afya ya uzazi na kutoharibu Uke wako
Comments
Post a Comment