NYUMA YANGU 2

              NYUMA YANGU   2

Mtunzi __ Ruvuly De Finisher 


Mama alimpatia Baba kamba wakafunga Mwanamke yule kisha Baba akachukua kisu alafu akamtemea mate Mwanamke huyo na kumwambia : Ulikuwa Mrembo sana Maua ukaringa na kunitukana leo hii upo wapi Maua hahahaha sali sala yako ya mwisho kwa maana leo huponi.

Baada ya kuzungumza maneno hayo Baba alishika kichwa cha Mwanamke aliyekuwa anamwita Maua na.....

Baba alishika kichwa cha Mwanamke aliyekuwa anaitwa MAUA alipotaka kumchinja nilipatwa na nguvu za ajabu nikatoka sehemu niliyokuwa nimejificha kwa mwendo wa kasi sana nikafanikiwa kufika sehemu waliyokuwepo kabla Baba hajamchinja Mwanamke yule, Muda huo huo nilijikuta nimepata ujasili wa ajabu nikashika kisu alichokuwa ameshika Baba upande wa makali, nilipata maumivu makali kutokana na sehemu niliyoishika lakini sikujali hilo , Damu zilinitoka kwa wingi sana Kutokana na makali ya kisu nilichokuwa nimekishika, Cha ajabu Baba alicheka sana alafu akasema : Maua hakika Damu ni nzito kuliko maji unamuona mtoto wako kajitoa sadaka kwa ajili ya kusaidia Maisha yako hahaha .


Baada ya maneno hayo Baba aligeuka na kunitazama kisha na kuniambia : Nisikilize Nurdin hata kama umefanikiwa kuziwia kisu hiki ili nisimchinje Mama yako lakini bado hujafanikiwa, leo lazima Mama yako apoteze Maisha .


Nilikuwa siamini alichoniambia mwanzo Mama lakini baada ya Baba kunithibitishia Kutokana na maneno yake aliyokuwa anamwambia Mwanamke aliyetaka kumchinja, Hapo ndipo nilipoamini kweli Maua ndiye Mama yangu Mzazi, Moyo wangu ulishikwa na Simanzi , Roho iliniuma mno nilimtazama Mwanamke aliyesadikika ni Mama yangu nilimuona anatetemeka na kujikunyata kwa hofu na woga, wakati huo Upepo wenye baridi ndani yake ulizidi kuvuma kwa kasi sana , Baba aliendelea kucheka, kicheko cha Baba kilinipatia hasira mno  nikamnyanganya kisu Baba alafu nikamsukuma mbali sana.


Baada ya kumsukuma Baba nilipiga magoti mbele ya Mama yangu mzazi kwa Mara ya kwanza Macho yangu yaliyatazama Macho ya Mama yangu mzazi ( Maua ) Sura ya Mama ilikuwa imejawa na hofu pamoja na simanzi kubwa , Ghafla Mama ( Maua ) alinishika mkono akiwa anatetemeka, ghafla Mama akaanza kuzungusha kichwa huku na huko wakati huo alikuwa anasema : Askari nisaidie wanataka kuniua wamemchukua mwanangu hao alafu wanataka kunizulumu Mali zangu nisaidie askari nisaidie , hii nyumba ni mali yangu , Namtaka mwanangu Mimi nisaidie askari hao ni wauaji nisaidie .


Ilionesha akili ya Mama yangu haipo sawa, Wakati huo nilimsikia Baba anawaita Ndugu zangu ;

   " Hamza njooni nyote tumshungulikie huyu mjinga "


Yalikuwa maneno ya Baba akiwaita Ndugu zangu muda huo Baba alifuata kipande cha chuma kilichokuwa jikoni, Nilistuka na kupata wasiwasi kwakua nilikuwa na nguvu hafifu , niliamini sitoweza kupambana na familia nzima ikabidi nimbebe Mama yangu na kukimbia nae, nilifanikiwa kutoka nje ya nyumba lakini nyuma yangu nilifukuzwa na watoto wa Baba wakiwa wameshika silaha mbalimbali , Nilimuomba sana Mungu anisaidie nisichoke ili niweze kuokoa Maisha ya Mama yangu pamoja na maisha yangu .


Nilikimbia kwa muda mrefu kwa bahati nzuri nikakutana na askari wanaolinda na kutembea usiku ( Askari wa Doria ) Niliwaomba msaada kwa kuwaambia nafukuzwa na watu wabaya , Askari hao waliwafuata Watoto wa Baba na kuanza kuwakimbiza , Nilitumia nafasi hiyo nikaondoka na Mama yangu, Muda wote Mama aliendelea kulalamika akiomba msaada kwa Askari. Nilikimbia zaidi nikajikuta nimechoka sana nikasimama na kutazama huku na huko, Upande wangu wa kushoto niliona kichaka , nikakifuata kichaka hicho nikahisi huenda kingeweza kunisaidia hata kwa kujificha ili kuokoa maisha yetu .


Nilipofika katika kichaka hicho ilibidi nimlaze Mama nikavua shati langu nikamfunika, Baada ya kumlaza chini Mama nilijaribu kumtuliza kwa kumbembeleza kama mtoto hatimae Mama akalala , Nilitumia muda huo kuitazama Vizuri sura ya Mama yangu, baada ya kuitazama Vizuri sura ya Mama nilifarijika mno , Muda huo huo nilisikia sauti ya Msichana ikiomba msaada nilistuka mno nikasimama na kujiandaa kupambana na chochote kitachotokea , Kwa mbali nilimuona mtu anakuja upande niliokuwepo, ilibidi nijifiche na kumtazama Vizuri.


Mtu huyo alisogea zaidi alipofika karibu ndipo nilipogundua kuwa ni Msichana kutokana na mbaramwezi ilivyokuwa inatoa mwangaza mkali, Msichana huyo alisogea karibu zaidi nikashangaa kumuona ametapakaa damu kwa wingi, hususa sehemu za miguu. Msichana huyo alikuwa amebeba mtoto katika mikono yake, Cha ajabu Msichana huyo alimtupa mtoto chini alafu akakimbia , Nilitoka kichakani na kumkimbiza yule Msichana lakini baada ya kupiga hatua chache nyuma yangu nilisikia sauti ya mtoto aliyetupwa ikilia kwa uchungu , Ndani ya sauti ya mtoto nilisikia sauti ya ngurumo ya wanyama wakali nilisimama Mapigo ya moyo yalikwenda kwa kasi sana , nywele zilinisisimka nikageuka na kumtazama upande aliokuwepo mtoto sikuamini kumuona Yule mtoto amezungukwa na Mbwa mwitu wengi sana, Ilikuwa ajabu sana kuwaona Mbwa mwitu eneo la mjini Ghafla mbwa mmoja akambeba mtoto na kukimbia nae ...


 


Ndani ya sauti ya mtoto nilisikia sauti ya ngurumo ya wanyama wakali nilisimama Mapigo ya moyo yalikwenda kwa kasi sana , nywele zilinisisimka nikageuka na kumtazama upande aliokuwepo mtoto sikuamini kumuona Yule mtoto amezungukwa na Mbwa mwitu wengi sana, Ilikuwa ajabu sana kuwaona Mbwa mwitu eneo la mjini Ghafla mbwa mmoja akambeba mtoto na kukimbia nae ghafla Mbwa mmoja akambeba mtoto na kukimbia nae nilirudi kwa kasi mno nikaanza kumkimbiza mbwa aliyembeba mtoto , Nilijitahidi kukimbia sana lakini sikuweza kuimudu kasi ya Mbwa huyo kwa sababu Mwendo wake ulikuwa mkali mno, baada ya kukimbia sana niliishiwa pumzi, Miguu ikachoka sana ikabidi nisimame nikabaki namuangalia Mtoto akiwa katika mdomo wa Mbwa akizidi kutokomea , Roho iliniuma sana kwa kushindwa kusaidia maisha ya mtoto yule, nilikaa chini nikiwa naisikia sauti ya mtoto ikipotea polepole .

Sauti ya mtoto ilifutika kabisa katika masikio yangu nilipatwa na huzuni kubwa moyoni mwangu kwani nilitambua huo ndio utakuwa mwisho wa mtoto yule, Baada ya kukaa chini kwa muda mrefu nilikumbuka nimemuacha Mama sehemu ambayo sio salama ikabidi nisimame ili nirudi sehemu niliyomuacha Mama lakini cha ajabu wakati nimesimama nilisikia sauti ya mtoto kwa Mara nyingine , sauti ya mtoto ilisikika kwa kasi kubwa ikisogea upande niliyokuwepo ghafla kwa umbali kiasi niliwaona mbwa wengi wakija kwa kasi mno, katika kundi hilo kubwa la mbwa nilimuona Yule Mbwa bado akiwa na mtoto mdomoni, Nilijipanga bila woga nikamvamia mbwa yule , Kwa bahati nzuri Mbwa alimtupa mtoto alafu wakatawanyika na kukimbia hovyo.

Nilimuokota mtoto akiwa ametapakaa damu mwili mzima, wakati huo mtoto alikuwa analia sana. Baada ya kumpata Mtoto nilirudi eneo nililomuacha Mama nikamkuta Mama yupo salama amelala nilimshukuru sana Mungu, nikajaribu kumtuliza mtoto japo ilionesha alikuwa na maumivu makali sana, Nilimbeleza mtoto hadi majira ya Asubuhi lakini bado mtoto aliendelea kulia, Kwa bahati nzuri mtaa niliokuwepo nilikuwa naufahamu nilimchukua Mama nikambeba mgongoni nikamfunga vizuri alafu nikambeba mtoto katika mikono yangu nikaingia mtaani nikaomba msaada wa pesa toka kwa watu mbalimbali niliowazoea, Baadhi ya watu walinisaidia wengine walinicheka na kunitukana .

Baada ya masaa kadhaa kupita nilibahatika kupata kiasi kidogo cha fedha , nikamnunulia Mama chakula kiasi kilichobaki nikakitunza kisha nikaenda hospital , Nilipofika hospital kila mtu alinishangaa nikamshusha Mama toka mgongoni, baada ya kumshusha Mama nilijikuta nimerowa kwa mikojo , Nilijua mtoto ndiye aliyekojoa lakini nilipojikagua vizuri nilitambua Mama ndiye alikuwa amenikojolea nilipokuwa nimembeba, Mama alipokuwa chini pale hospital bado aliendelea kukojoa , Mkojo alioutoa ulisambaa sehemu kubwa aliyokuwa amekaa Ghafla Nesi mmoja akaja akaona hali hiyo akasema kwa sauti ya juu : He  hee heee ! Wewe Mama mjinga nini unakojoa hapa inamaana choo hukiona , Pumbafu kabisa sasa utadeki hapa nasema safisha haraka mshenzi wewe .

Niliumia sana kwa kauli mbovu alizokuwa anatoa Nesi yule nikamjibu : Dada samahani sana Mama yangu sio mjinga wala mpumbafu amepatwa na matatizo ya kidunia tu, Hapo alipo akili zake sio nzuri na ndio maana nipo hapa laiti angelikuwa mzima asingenikojolea kama hivi unavyoniona, Dada Mimi nitasafisha hapa hata usijali Dada yangu .

Yule nesi alinitazama kwa dharau na kunibia : Sikiliza wewe ombaomba hospital hii haihitaji watu wachafu kama ninyi angalia ulivyo Nguo zako zimechakaa chakaa minywele kama chizi unanuka mikojo , Mtoto wako huyo sijui mdogo wako katapakaa Damu Mwili mzima anapiga kelele hovyo , Sasa sikia wewe mjinga Nakupa dakika kumi mtoe Mama yako nje alafu safisha hapa haraka.

Roho iliniuma zaidi Jazba ilinitawala lakini nikatulia kwakuwa nilifahamu sehemu ile ndio msaada wa pekee kwa Mama yangu pamoja na Mtoto niliyemsaidia toka katika mdomo wa Mbwa, nikawasogelea watu waliokuja kutibiwa ili niwaombe wanisaidie kumbeba mtoto ili nifanye usafi lakini wote walinikimbia wakiwa wameziba pua zao, Wengine walisema kwamba natoa harufu mbaya nisiwasogelee , ikabidi nimuweke mtoto chini nikamwambia na kusema moyoni : Vumilia mdogo wangu najua nikikubeba mgongoni utaumia zaidi , nahitaji nisafishe sehemu aliyochafua Bibi yako sawa Mtoto mzuri usilie eee .

Ilikuwa ajabu sana Mtoto aliacha kulia papo hapo, Nikavua suruali nikabaki na bukta , nikaitandika vizuri suruali yangu alafu nikamlaza mtoto, Nikamchukua Mama nikampeleka nje alafu nikarudi ndani nikasafisha vizuri wakati nafanya usafi alikuja Daktari upande wa mbele yangu nikamuona anamnyanyua mtoto alafu akatazama huku na huko na kusema : Mtoto wa nani huyu ?

Nilimsogelea Daktari nikamjibu : Kaka samahani huyu mtoto ni wangu nimemuweka hapo chini kwa sababu nipo nafanya usafi, Mama yangu amekojoa hapa kwa bahati mbaya kwa sababu ni mgonjwa wa akili .

Daktari alihudhunika sana akanishika bega na kuniambia : Oooh pole sana mdogo wangu Mama wa mtoto huyu yupo wapi? na kwanini hamjamkata kitovu Mtoto huyu alipozaliwa hivi unajua madhara yake ?

Nilimsimulia Daktari yote kuhusu mtoto yule , Daktari alinipongeza sana akaniahidi atanisaidia matibabu ya mtoto pamoja na Mama yangu bila malipo yeyote , Nilifurahi sana nikapiga magoti mbele yake nikiwa namshukuru , Daktari akaniambia : Usipige magoti kijana mshukuru Mungu kwa ushujaa na wema wako aliokujalia hiyo ni hazina bora sana na unastahili pongezi Mama yako huyo mgonjwa yupo wapi ?

Nilimjibu : Yupo hapo nje Kaka yangu ?

Daktari akaniambia : Mfuate Mama yako kisha njoo nae chumba namba 21 utanikuta fanya haraka sawa .

Nilitoka nje haraka haraka nikamfuata Mama nikiwa na furaha sana lakini nilipofika nje nilistuka mno kutokumuona Mama eneo niliyomuacha nilichanganyikiwa mno nikatazama huku na huko kwa mbali nilimuona Mama ameshikwa na watu wawili watu hao walikuwa wanamvuta kwa nguvu .........

__ ITAENDELE


__ ITAENDELE


Comments