NYUMA YANGU

             NYUMA YANGU  1

Mtunzi __ Ruvuly De Finisher
         

__ UTANGULIZI 
   Mtaani nilipewa majina mengi sana wengi wanapenda kuniita "Mtoto wa mtaani " kutokana na kuniona nipo mtaani muda wote nikikusanya uchafu katika Nyumba mbalimbali lakini wengine walipenda kuniita "Cha Nguvu " kutokana na uwezo mkubwa niliokuwa nauonyesha mbele ya watu pindi nipatapo kazi ngumu, Nilitambulika hivyo katika mitaa mingi lakini hakuna aliyejua ukweli kuhusu Maisha yangu nami sikuhitaji kuweka wazi historia inayohusu maisha yangu. Ukweli nilifanya kazi kwa bidii sana kwa sababu lengo langu lilikuwa ni kupata Fedha ili nimpatie Mama kwaajili ya  kuendelea kuishi nyumbani.

__ SONGA NAYO 
Niliendelea kuishi hivyo na nilijitahidi sana kulinda Furaha niliyokuwa naipata toka kwa watu wa rika mbalimbali, Hakika Mtaani nilipata Marafiki wengi sana kutokana na Ucheshi pamoja na Heshima niliyojaliwa na Mungu. Watu wengi walipenda kuwa karibu yangu muda wote, kwa sababu vituko vyangu vilifuta mawazo ya watu wengi, kwani walipata furaha kubwa sana kutoka kwangu hali iliyowafanya Wengi wao walijikuta wanashikilia mbavu zao wakidai zinawauma kwa kucheka mno.

Lakini pindi niliporudi Nyumbani nilijikuta naipoteza Furaha yote na kuikaribisha huzuni yenye majonzi ndani yake, Kwani nilipofika Nyumbani nilikuwa mtumwa kwa Ndugu zangu mbali na utumwa Baba na Mama hawakupenda kuniona Mazingira ya nyumbani, Sikuweza kujua ni kwanini Familia yangu hainipendi, Japokuwa nilionesha upendo wa juu sana kwao. Pamoja na kukabidhi fedha zote nilizopata mtaani lakini bado thamani yangu haikuonekana mbele yao .

Sikujali hilo nilivumilia kuishi hivyo nikiwa naamini kwamba siku zote Mzazi huwa hakosei, japo kilichoniumiza zaidi ni kitendo cha kulipia Chakula na Makazi kama mtu wa nje ya Familia , Hali hiyo iliniumiza zaidi nikashindwa kuvumilia ikabidi nimfuate Mama nikaomba kuzungumza nae, Cha ajabau Mama akakubali nizungumze nae, ilikuwa ajabu sana kwani sikuwahi kupewa nafasi kama hiyo tangu nilipoanza kujitambua , Nilifarijika kidogo Moyoni mwangu, kisha nikapiga magoti mbele yake kwa heshima ya juu nikasema : Mama nashukuru kwa nafasi hii pia naomba unisamehe sana kama nitakuwa ninakosea kwa swali nitalokuuliza Mama yangu .

Mama alinitazama kwa muda mrefu alafu akanijibu : Zungumza shida yako haraka nina mengi ya kufanya . 

Wakati huo alikuwa anatengeneza mboga kwa ajili ya chakula .

Nilifumba macho nikashusha pumzi alafu nikasema : Mama hivi nimekukosea nini Mimi ? Umetuzaa watoto sita wenzangu wote wanaishi kwa furaha, pia mmewapeleka shule lakini cha kushangaza Mimi mmenitenga , Shule sijaenda hadi umri huu, Mmenigeuza mtumwa ndani ya Nyumba hii kinachoniuma zaidi Mama yangu ni suala la kufua nguo za wadogo zangu wa kike yaani nafua nguo hadi za ndani kweli? Daah Mama 😧 naumia sana Mama naumia, nimewakosea nini Mimi ? Isitoshe ndani ya nyumba hii siwezi kula wala kulala pasipo kutoa pesa ninazo omba mtaani alafu Mimi sio ombaomba Mama kwa sababu ninyi wazazi wangu sio masikini , Baba ni mwanajeshi, wewe Mama ni Hakimu kwanini Mimi naishi kama ombaomba mtaani kwanini Mama yangu ?😣

Mama alinicheka sana kitendo hicho kiliniuma mno kwa sababu sikufikiria kama Mama anaweza kufurahia Mimi kuishi Maisha ya kuwa  ombaomba mtaani , Baada ya kucheka zaidi Mama akaniambia : Nisikilize Nurdin kwakua umeshakuwa mkubwa leo nahitaji kukueleza ukweli , Kwanza tambua Mimi sio Mama yako mzazi .

Mungu wangu nilistuka sana kusikia Mama ananikana kwamba Mimi sio mtoto wake , Nafsi iliniuma kupita kiasi nikajikuta nadondosha Chozi mbele yake, Lakini Mama hakuona thamani ya chozi langu akaendelea kusema akiwa amejawa na furaha : Sasa unalia nini ? Kukueleza ukweli ndiyo unalia , huo ndio ukweli Nurdin mimi sio Mama yako , nimekulea tu, Mama yako alikuwa mfanyakazi wangu wa ndani ( House girl ) Ujinga alioufanya Mama yako Nurdin ni kukuzaa wewe na Mume wangu, Nurdin Mama yako alinisaliti Kwa kufanya mapenzi na Mume wangu hatimae akakuzaa wewe, kwa kitendo hicho niliumia mno na ndio maana nikaamua kumfungia ndani ya chumba kile , 🏠 

Niligeuka na kuangalia Chumba hicho alafu nikarudisha Macho upande wake nikiwa sielewi anachoniambia, Mama aliendelea kusema : Umekiona chumba kile basi ndani yake ndipo yupo Mama yako mzazi na unajua kwanini unanipa Fedha hizi kila siku ? Najua hujui basi tambua leo Fedha hizi ndizo zinasababisha Mama yako aendelea kuishi laaa sivyo angelikuwa ameshakufa kwa njaa Kali muda mrefu,  kwahiyo jipongeze kwa kulinda Maisha ya Mama yako kwa miaka zaidi ya ishirini ( 20 years ) nahisi kwa sasa umejua ulichotaka kujua na kuanzia kesho unatakiwa ulete Fedha mara mbili ya unazoleta kwa ajili yako na ajili ya Mama yako umenielewa Nurdin ?

Nilihisi kuchanganyikiwa baada ya kusikia maneno hayo , Kichwa kiliniuma sana nilishikwa na Hasira zaidi nikajikuta nimesimama nikiwa na jaziba nikamsogelea Mama kisha nikamuuliza kwa sauti ya juu : Mama yangu anakosa gani hadi umempatia adhabu kali kama hiyo , Yaani umemfungia ndani zaidi ya Miaka ishirini kwa kosa la kupata ujauzito toka kwa Mume wako , Kwanini hujanipatia Adhabu hiyo Mimi, Nakuuliza kwanini ?

Mama alisimama akachukua kiti alichokuwa amekalia akanipiga kichwani nilipata maumivu makali sana , Ghafla nilihisi kizunguzungu nikaishiwa nguvu nikadondoka chini, Nilipokuwa chini Mama alimwita Baba , Baba alipofika alinivamia na kuendelea kunipiga bila huruma. Baada ya kunipiga sana Baba alimchukua Mama wakaingia ndani, Nilipata maumivu makali sana damu zilikuwa zinatoka kichwani kwa wingi , nilitamani nitoke nje ili niombe msaada lakini nilikosa nguvu.

Niliendelea kukaa nje hadi majira ya usiku pasipo kupewa msaada wowote, Yalipofika majira ya saa sita usiku nilijitahidi nikasimama japokuwa nilikuwa na maumivu makali mno , Nilisogea taratibu hadi katika chumba ambao Mama aliniambia ndani yake yupo Mama yangu mzazi, nilipofika nilishika kitasa cha mlango nikaona kufuli nilishindwa nifanyaje ili nifungue mlango Ghafla mlango mkubwa ulifunguliwa nikajificha nyuma ya chumba hicho .

Baada ya kujificha nilimuona Baba na Mama wakitoka nje wakiwa wameshika kamba pamoja na Kisu , walipofika nje walinitafuta sana lakini hawakunipata , Baba akamwambia Mama kwa sauti ya ukali : Mke wangu umekosea sana kumueleza Nurdin Ukweli kuhusu Mama yake na hapa hayupo inakuaje si atatuvurugia huyu ?

Nilimuona Mama anashika mikono kichwani na kusema : Daah ni kweli mume wangu sasa tufanyaje kuhusu Maua nahofu Nurdin anaweza kuwa kaenda kituo cha polisi .

Baba alisimama kwa muda kidogo alafu akasema : Hakuna kingine zaidi ya kumchinja Maua na kumzika usiku huu huu unajua Maua anafahamu siri kubwa kuhusu Maisha yetu kwahiyo lazima afe kwa sababu hatujui Nurdin kaenda wapi huenda kaenda kituo cha polisi .

Mama akajibu : Basi fanya hivyo Mume wangu tumchinje Maua haraka.

Mama aliingia ndani akatoka na ufunguo mkononi , wakafungua mlango Baba akaingia ndani akatoka nje akiwa amemshika nywele na kumburuza Mwanamke mmoja aliyekuwa amechakaa mno, Mama alimpatia Baba kamba wakafunga Mwanamke yule kisha Baba akachukua kisu alafu akamtemea mate Mwanamke huyo na kumwambia : Ulikuwa Mrembo sana Maua ukaringa na kunitukana leo hii upo wapi Maua hahahaha sali sala yako ya mwisho kwa maana leo huponi.

Baada ya kuzungumza maneno hayo Baba alishika kichwa cha Mwanamke aliyekuwa anamwita Maua na .............

__ ITAENDELE


Comments