- Get link
- X
- Other Apps
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis hapo jana ameongoza ibada ya Jumapili ya Matawi, katika kanisa la Mtakatifu Petro Basilica likiwa tupu kabisa kutokana na vizuizi vya kukabiliana na virusi vya corona.
Katika ibada hiyo inayofanyika kwa namna hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo Papa amewataka watu kujisogeza karibu katika kuwasaidia masikini na wagonjwa.
Katika nyakati za kabla ya janga la corona, Jumapili ya Matawi, ambayo inaashiria mwanzo wa Wiki Takatifu kwa Wakatoliki kuelekea siku ya Pasaka, maelfu ya watu wakiwa wameshika matawi mikononi walikuwa wakishiriki ibada hiyo ya wazi katika kanisa hilo Mtakatifu Basilica.
Comments
Post a Comment