Rais wa zamani wa Madagascar Didier Ignace Ratsiraka amefariki akiwa na umri wa 84, rais wa nchi hiyo ametangaza.
“Jumapili tarehe 28 Machi, 2021, rais wa zamani, Admirali Didier Ignace Ratsiraka alifariki akiwa na miaka 84.
“Wamadagascar wamempoteza mzalendo,” Rais Andry Rajoelina aliandika katika Twitter.
Rais ametuma salamu za rambimbi kwa jamaazake, jamii ya majeshi na raia wa Madagascar.
Rais huyo wa zamani alifariki katika hospitali ya kijeshi ya Soavinandriana iliyopo mji mkuu, Antananarivo, ambako alikua akipokea matibabi tangu tarehe 22 mwezi huu wa Machi.
Bw. Ratsiraka, ambaye aliingia madarakani akiwa afisa wa ngazi ya chini wa jeshi la majini mwaka 1975, aliongoza Madagascar mwaka 1991 na baadae tena kuanzia mwaka 1996 hadi 2002.
Baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2002, aliondoka nchini huma na kwenda Ufaransa na kurejea nyumbani miaka tisa baadae.
Comments
Post a Comment