Sababu za mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa

 

Sababu za mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa

changamoto ya hamu yatendo la ndoa kwa wanawake

Nini kinapeleka Wanawake Kukosa hamu ya Tendo la Ndoa?

Nimekuwa Napata kesi nyingi sana kutoka kwa akina mama hasa  wenye umri kuanzia miaka 25 na kuendelea  wakihitaji msaada kwenye ndoa zao kuhusu dawa ya kukosa hamu ya tendo la ndoa baada ya kujifungua au kabla ya kujifungua, maana hawafurahii tendo la ndoa kama vile inavotakiwa. Tatizo linazidi kuongezeka kwa kasi na wengi hawafahamu chanzo cha tatizo hili hivo inakuwa vigumu kulitibu. Leo tutaongelea chanzo cha tatizo na jinsi ya kuepuka na kulitibu ili uendelee kufurahia unyumba.

Zifuatazo ni sababu za Maumivu wakati wa Tendo la ndoa zinazoletekeza Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa  kwa Mwanamke.

  1. Kuvimba kwa kuta za uke kutokana na kushambuliwa na fangasi au bakteria. Kuta hizi huanza kuwa na vijitundu vidogo vidogo na kadiri muda unavyokwenda bila kutibiwa, vitundu hivi huongezeka ukubwa na kuwa kama vidonda na hatimaye kuta za uke kuanza kumomonyoka na hali hii huondoa kabisa hamu ya kushiriki tendo.
  2. Matatizo ya shingo ya kizazi kutokana na maambukizi ya fangasi maeneo hayo. Kutoka kwa mbegu za kiume muda mfupi  au saa kadhaa baada ya tendo ni dalili kuu ya tatizo hili. Pia mwanaume anapogonga shingo hii ya kizazi wakati wa tendo la ndoa mwanamke huwa kama anatoneshwa kidonda. Hali hii ya mbegu kurudi nje husababisha mwanamke kutoshika ujauzito.
  3. Uvimbe kwenye mji wa mimba/mfuko wa uzazi . Uvimbe huu kitaalam hujulikana kwa majina mengi lakini fibrod ni maarufu zaidi. Huanza kama mbegu ndogo ya mchicha na hukua kama boga kubwa. Mwanamke huongezeka ukubwa wa tumbo na baadaye huonekana kama ana mimba kubwa na watu hushangaa kwa nini hajifungui kipindi chote.
  4. Maumivu wakati wa tendo hasa chini ya kitovu huashiria tatizo kwenye mirija ya uzazi. Yawezekana ikawa ni tatizo la mirija ya uzazi kujaa maji machafu kutokana na kuzaliana kwa vimelea sana eneo hilo

Kitu hiki husababisha mirija ya uzazi kuziba kwani maji haya huwa mazito, kitu ambacho husababisha mayai ya uzazi na mbegu za kiume kushindwa kupenya.

Kutoshika mimba (ugumba) kwa mwanamke aliye kwenye ndoa au uhusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja na anasikia maumivu ya aina hii ni kiashiria kikubwa cha tatizo hili.

Kumbuka matatizo ya uzazi unayokutana nayo kama maumivu makali kipindi cha hedhi, ugumba, kukosa hamu ya tendo la ndoa baada ya kujifungua ama kabla ya kujifungua , kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa, kuvurugika kwa hedhi, uzito mkubwa na kitambi  siyo kitu ulichoumbiwa, bali ni matokeo ya maisha unayoishi .

Kwa kifupi matatizo yote haya chanzo chake kikubwa ni kuvurugika kwa homoni za kike au hormonal imbalance. Matatizo haya siyo kwamba ni mabadiliko ya vinasaba kutokana na umri, ila ni matokeo ya mpangilio mbovu wa vichocheo ama homoni zako na hasa homoni za uzazi. Hivo utakubaliana nami kwamba wanawake hawajaumbiwa kupata shida hizi zote hata kama umri wako umeenda, unahitaji kuendelea kufurahia tendo la ndoa. Sawazisha mpangilio wako wa homoni na matatizo yote haya utakuwa umeyakimbiza.

Dalili zifuatazo zinaonesha una Mvurugiko wa Homoni.

Hivo unatakiwa kutumia dalili hizi kujifanyia uchambuzi wewe mwenyewe bila hata kufanya vipimo hospitali tayari utagundua kuwa una tatizo kwenye vichocheo ama homoni zako

  1. Uzito kupungua ama kuongezeka bila mpangilio
  2. Tumbo kujaa gesi na kuhisi umeshiba mda mwingi
  3. Maumivu ya kichwa na kujuskia haupo kwenye mood nzuri
  4. Kupata msongo wa mawazo mara kwa mara
  5. Ugumba ama kutoshika mimba kwa kipindi kirefu
  6. Kukosa hamu ya tendo la ndoa ama kupata maumivu makali wakati wat endo la ndoa
  7. Kuhisi mwili umechoka mara kwa mara
  8. Kuota ndevu na nywele kifuani
  9. Kupungua kwa uwezo wa kumbukumbu
  10. Kutokwa jasho jingi usiku na
  11. Ngozi kukakamaa
  12. Kukosa usingizi
  13. Uvimbe kwenye mfuko wa mimba

Baada ya kujifanyia upembuzi juu ya tatizo lako sasa tuangalie nini cha kufanya ili uweze kutibu dalili hizi kuanzia leo ukiwa nyumbani kwako.

Nataka nikwabie mpenzi msomaji na unayefatilia makala hizi kwa makini, kwamba vitu tunavyoweka tumboni vianchangia karibu 80% ya kuvurugika kwa mpangilio wa homoni zako. Unatakiwa kuwa mvumilivu maana kusawazisha homoni ni kitu endelevu na kinachukua kuda kutokana na kwamba unajenga tabia mpya kwenye mwili wako. Hivo hatua ya kwanza katika kupangilia lishe na mlo wako ni

Comments