SIO KILA MSALABA NI KANISA
Mambo yalikuwa shaghalabaghala pale ndani mke wangu alikuwa ana wiki mbili tangu aondoke zake baada ya kukorofishana nae na kisha kumpiga, aliposema anaenda kwao nilidhani anatania na atarudi kesho yake sasa siku kumi na nne zilikuwa zimemezwa na kalenda. Nyumba ilikuwa chafu sana, vyombo alivyoviacha vilikuwa vichafu vilevile, nguo niliyokuwa nimevaa ndio pekee iliyokuwa safi nyingnezo mh! najua mimi
."Ama kweli nyumba bila mwanamke haijakamilika" nilijisemea kwa sauti ya chni iliyojaa mikwaruzo nikiwa nakuu vifungu vya wimbo wa mke mwema wa Bony Mwaitege!! kwani ni muda mrefu nilikuwa sijaongea lolote juu ya hali hiyo.
Nilikuwa kwenye hiyo hiyo sebule chafu naangalia luninga kupoteza muda kwani ilikuwa ni siku ya mapumziko hatukwenda kazini. Siku ilionekana kuwa ndefu sana na niliichukia ile nyumba nilihisi ni kubwa kuliko mimi, nilitamani kumpigia simu mke wangu na kumwomba msamaha lakini nikaona kama nitakuwa najishusha sana.
"Oya Jimmy! umelala nini?" ilikuwa sauti kutokea mlango iliyonikatili kausingizi kalikoanza kunipitia, alikuwa mshkaji wangu wa siku nyingi David Lymo lakini wengi walipendelea kumwita D.Castle kutokana na kupendelea sana kunywa bia aina ya Castle.
"Sijalala wala nini karibu kaka" nilimkaribisha huku nikijinyoosha mwili wangu palepale kwenye kochi.
"Mh? hiyo nyumba mi sina la kusema ila Suzy alikuwa na umuhimu wake tena sana" aliniambia David mi nikatikisa kichwa kukubaliana nae. Ilikuwa tayari saa kumi na mbili jion Davy alikuwa amekuja kwa minajiri ya kunipa ofa ya chakula cha usiku na mimi sikuwa na kipingamizi.
Nilijiandaa kisha nikavaa nguo ile ile tukaondoka
* * *
Majira ya saa tatu usiku meza yetu ilikuwa imechafuka sana, makopo ya Castle, Kilimanjaro na Balimi yalikuwa tupu na mengine hayajafunguliwa tulikuwa tumemaliza kilo kadhaa za nyama choma, lugha ya kiingereza ilichukua mkondo wake ishara kwamba tayari pombe imevuruga vichwa vyetu.
Sijui katika pombe hizi za kisasa walitia kamusi ya kiingereza ama vipi. Maana tayari lugha ilikuwa imebadilika.
Siku ya jumapili ndani ya Lango la Jiji ni usiku wa taarabu na hadi milindimo inaanza sisi bado tulikuwa ndani, sijawahi kucheza taarabu lakini pombe ilinituma kwenda kumtunza dada mmoja aliyenivutia uchezaji wake, kwa staili ambazo sijui zilipotoka nilijikuta nyuma ya wowowo lake mikono yangu kwenye kiuno chake, weee! asikudanganye mtu pombe chanzo cha uasherati yaani alipokuwa akijisogeza kwangu eti mi najenga picha kitandani na Suz wangu basi namsogelea kwa nguvu najibana kwake ilimradi nivute hisia kingono zaidi, hapo tayari nimemwangushia elfu thelathini za kitanzania.
"Twende tukapumzike nilimwambia kwa utani"
"Ni wewe tu na roho yako kaka" alinijibu, hata sikuamini kama ingekuwa rahisi hivyo bila hata kukumbuka nilimwacha Davy mezani nikatokomea bila kuaga, huyo ndani ya Tax hadi Mikumi inn hapo hapo Magomeni tayari kwa kujipunguzia machungu ya kuondoka Suzy.
Nilikuwa nimelewa sana lakini nilijua kilichofuata pale, nikampapasa kama dakika tano, kiheleni hadi kitovuni mtoto wa kiume nikajipa sifa nimeopoa kitu, taratibu nikaanza kumwondoa nguo lakini akanizuia akazima taa kwanza, nikasema hapo safi sana maana ule mwanga kama ulikuwa unaninyima uhuru vile.
Aliporejea tayari alikuwa amenisaidia zoezi la kutoa nguo,
"Mh! amejuaje huwa mi mvivu wa kuwavua nguo? Viumbe hawa?" nilijiuliza huku nikishusha pensi yangu ya kijesh nikabakiwa na 'vest'.
Nikaanza kuzigandamiza shanga zake kiunoni ili kuleta raha ya mchezo zaidi. Akawa anahema nikajua tayari ameingia ninapopataka. Nikausogeza mdomo wake nikaanza kumnyonya ulimi akazidi kuhema. Ulimi wake ulinisisimua zaidi nikatamani zaidi kuendelea. Nikamminyaminya mbavuni akazidi kuhema.
"Ngoja nipime lita halafu mchezo uanze nahitaji kujua kama ni bwawa au kisima" nikajiwazia huku nikiupeleka mkono wangu wa kulia kunako mambo zake, mwanzoni nilidhani ni shanga kubwa mh! lakini nilivyopapasa zaidi nikagundua dizaini flani kama tunafanana. Shanga gani hiyo imefungwa ikaachwa inaning’inia?? Nikajiuliza!!! Nikapapasa vizuri zaidi.
Nani kakwambia nyama choma inakata pombe, mshtuko peke yake ndo dawa ya pombe hata iwe gongo ama mataputapu. Sikujali lile giza niliruka uchi uchi nikachanganya mlango ulipo nikakutana na ukuta 'paa' nikajibamiza kichwa kisha nikatua chini kwa kishndo, hapo tayari nikawa nimepoteza uelekeo sikujua wapi ulipo mlango na yule mtu yupo wapi. Nikiwa pale chini mara taa ikawashwa nikaishiwa nguvu zaidi. Nilichoamini ndio hichi kinatokea. Kumbe nimenyonya mdomo wa dume. Nikataharuki. Nilitaka kupiga kelele lakini nikaona noma. Nikajilazimisha kutapika!! Hakuna kilichotoka.
"Kwani vipi mpenzi"lile dume likaniuliza nikapigwa na bumbuwazi. Kidume kinaniita mpenzi!!!
"KUMBE SHOGA!" nikajibu kwa sauti ya chinichini iliyojaa uoga huku nikitetemeka kama vile nimeona mzimu. Sikuamini kabisa yule mtu niliyetegemea kuwa ni mwanamke sasa amekuwa dume, nilikuaga nasikia tu kuwa kuna mashoga sasa nilikuwa nalo chumbani tena nikiwa nimelipapasa limelainika.
"Ndio kwani ulidhani mkeo mie" likanijibu. Naamini sikufa ila nilizimia.
NILIPOZINDUKA nilikuwa na usemi mmoja tu kuwa
“SIO KILA MSALABA UNAMAANISHA MAHALI HAPO KUNA KANISA MISALABA MINGINE INAWAKILISHA MAKABURI!!!”
Comments
Post a Comment