UCHAWI UPO USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:1-3

 

UCHAWI UPO USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:1-3



USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-1
Wakuu habari zenu, ni matumaini yangu kuwa hamjambo.

Leo nataka kuweka ushuhuda wangu kwa niliyoyashuhudia live juu ya nguvu za giza, kwa wasioamini nadhani uzi huu hautakuwa na thamani kwao, kama na wewe unao ushuhuda usisahau kushea nasi.

1. Ushuhuda wangu unaanzia mwaka 1992 nikiwa nafundisha shule X wilaya ya Sengerema, kuna mwalimu nilikuwa nafundisha naye kituo kimoja.

Siku hiyo kuna kamvua kalinyesha sana, baada ya kupungua mwalimu mwenzangu alimuagiza mtoto wake wa kiume aliyekuwa akisoma darasa la kwanza kwenda kuchuma maharage shambani.

Bahati mbaya mtoto akiwa shambani aligongwa/aliumwa na nyoka na kupeleka kifo, tulifanya taratibu za mazishi na kumsitiri mtoto huyo.

Cha kushangaza mwaka 2008 mtoto huyo alionekana akiwa uchi na nywele ndefu sana alikuja moja kwa moja nyumbani na kupitiliza ndani nyumbani kwao, alikuwa ameshakuwa baba mzima, nywele zilikuwa ndefu sana pamoja na mikono iliyofikia usawa wa magoti.

Watu walistaajabu sana lakini hakudumu sana alifariki baada ya kukaa uraiani kwa wiki mbili.

2. Ushuhuda wangu bado unabaki huko huko Sengerema katika kijiji cha Bubandwamhela.

Nikiwa nafundisha shule X, kuna binti kijijini aliyekuwa akisoma darasa la saba aliugua ghafla baada ya kutoka shuleni.

Wazazi wake walipompeleka hospitali daktari aliwaambia mtoto hana ugonjwa, wazazi waliamua kujiongeza na kumpeleka kwa mganga wa jadi.

Cha kushangaza kesho yake shangazi ya binti alikutwa kwa mganga akiwa uchi, huku akiweweseka na akili zimemruka, shangazi mtu alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi lakini kwa kuwa serikali haiamini ushirikina aliachiwa huru, lakini hadi leo hii alishakuwa chizi. Binti yeye alipona kabisa.

3. Kisa cha tatu na mwisho ni hiki kilichotokea Liwale shule ya sekondari X nikiwa na walimu wenzangu ambao tulikuwa tunasoma chuo cha SAUT-Mtwara.

Tulipangiwa field katika wilaya ya Liwale ilikuwa mwaka 2009, mwanachuo mwenzetu akiwa zamu siku hiyo alikumbana na mtoto ambaye kwao iliaminika kuwa bibi yake alikuwa mtaalamu wa mambo ya giza.

Mwanafunzi huyo alichelewa kufika shule, mwalimu alipotaka kumuadhibu aligoma, wakasumbuana sana mwisho wa siku akamuadhibu yakaisha, jioni tukiwa uwanjani tunafanya mazoezi yule mwanachuo mwenzangu alianguka na kupoteza fahamu, ikawa jumla hadi kifo.

Kama na wewe umewahi kukutana/kushuhudia live ushirikina share nasi kisa chako watu tupate ilimu.

Mungu ni mwema siku zote.



 USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-2


Kisa kingine nilikisikia kilitokea maeneo ya sumbawanga

Kuna mzee wamakamo alikua ni tajiri sana, pesa zake haweki benk na hata akienda kufanya manunuzi hua haweki kwenye wallet kuzistiri zisionekane yeye hua anazishikilia tu kama wanafunzi wanavyoshika vitini vyao mikononi

Siku moja kuna kosi la majambazi lilijipanga kwenda kumvamia

Walimkuta yuko nyumbani kwake ameshikilia pesa akipata upepo kwenye garden yake

Wakamnyooshea bastola na kumwambia atulie kimya kisha atoe kila kitu alichonacho

Yule mzee akachukua zile pesa akazibana kwenye kwapa lake huku akitetemeka kwa woga

majambazi wakamsisitiza kua anyanyue mikono juu, mzee akatii amri kwa kunyanyua mikono juu kisha pesa alizozibana kwapani zikaanguka chini majambazi wakaziokota

Wakamwambia tena "toa kila kitu ulichonacho"

Round hii unaambiwa mzee alichomoa kichwa chake akakishika mkononi halafu kile kichwa kikiwa mkononi kikatoa sauti ikisema "sina chochote jamani nina kichwa tu hapa"

 

 USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-3

 Nawasilisha kama ilivyosimuliwa :

Kuna mwalimu Shule X, huko kanda ya ziwa, aliamka saa tisa usiku kuwahi usafiri asubiri gari kwenda mjini, kijiji cha ndani huko mkoa mpya uliopo ziwani.

Akasubiri gari na baada ya mda likaja, akasimamisha na kuingia. Gari ikaondoka, kakaa baada ya mda kumcheki abiria mwenzake kainama, akahisi labda ni usingz, lakini alipocheki waliopo nyuma pia dizaini kila mtu kainama. Akaona isiwe shida akamsemesha jamaa kainama tu kwa siti yake.

Sasa na yeye akatulia, gari imeenda lakini ghfla kama kausingz kakamwingia, akshtuka ghafla ni saa kumi na mbili asubuh na amesimama pale pale alipokuwa saa tisa kituoni.

Akapanic, kachukua baiskeli hadi wilayani hakurudi tena, ikabidi afisa elimu aende kule na timu yake kuongea na waalimu na wananchi ila jamaa hakuweza kukubali kurudi kituoni. In short walimpa uhamisho.

Nyingine mwalimu kapangiwa kituo Shule X huko kanda ya nyonyo. Kama ujuavyo vita ya kugombea mwalim binti mpya kati ya wanakijiji na wafanyakazi wenzake. Kumbe akawa kawakatalia, ikawa nongwa!

Siku moja anaosha ndizi kamaliza vizuri kwa sufuria, ghafla kikashuka kinyesi kingi kika replace ndizi zote, kinyesi fresh kinatoa hadi Moshi. Madam yule alikimbia kwenda kwa Bro nae ni mwalimu jirani Yake. Hakurudi tena kwa ile nyumba anaogopa.

Nina visa kama 10 kidogo ila mzembe kuhadithia.

Haya Mambo yapo kanda ya Nyonyo hasa kwa tuliokulia Bush huwa hata hatutetereki.

FUATILIA MUENDELEZO WA VISA HIVI A:1-30, B:1-30, C:1-30

Comments