Ulaji wa mayai na faida zake mwilini

 

Ulaji wa mayai na faida zake mwilini


mayai pic

Mayai ni chakula muhimu katika mwili wa binadamu na yana virutubisho na madini mengi yenye faida.

Mayai yana protini, vitamini A, D, B na B12 na madini ya lutein na zeaxanthin yanayoweza kuzuia mtu kupata matatizo ya macho atakapozeeka.

Kama ulikuwa hujui! Mayai yana kemikali iitwayo choline ambayo ni muhimu kwa ukuaji na afya ya ubongo wa mtoto tumboni na ndio maana mwanamke mjamzito anashauriwa kutumia yai moja hadi mawili kwa siku.

Narcisa Lihepanyama ni Ofisa Elimu Kilimo na Mifugo, Wilaya ya Kisarawe anasema kutokana na mayai kuwa na protini nyingi, ndio sababu wataalamu wa masuala ya lishe wanashauri walau kula yai moja kwa siku.

“Ni vyema ukala yai moja asubuhi wakati wa kifungua kinywa ili kujipatia virutubisho muhimu ambavyo huwezi kuvipata katika vyakula vingine,” anasema Lihepanyama.

Pia, anasema watu wanakosa madini na virutubisho muhimu ambavyo havipatikani katika vyakula vingine bila wao kujua au kutokuwa na mfumo mzuri wa kupangilia ulaji lishe bora. Hata hivyo, ulaji wa yai moja kwa siku kunaweza kuwasaidia watoto wadogo wenye utapiamlo kuongeza urefu kulingana na utafiti uliwahi kufanywa huko Ecuador.

Utafiti uliofanywa na Shirika la Chakula Duniani (FAO) mwaka 2011, unaeleza kuwa ulaji wa mayai kwa mtu mmoja kwa mwaka ni wastani wa mayai 106 tu, huku idadi inayotakiwa kuliwa na mtu mzima ni mayai 300 kwa mwaka.

Pia, ulaji wa mayai utakusadia kulinda macho, huondoa sumu na husaidia kuongeza nuru ya macho kutokana na kuwepo kwa kemikali za leutin -*na zeaxanthin.

Faida nyingine ni kwamba, mayai yana kaisi kikubwa cha kingi cha Omega-3, ambayo husaidia kupunguza mafuta yapatikanayo katika damu yaani ‘triglycerides’. Makala haya yameandikwa na mwandishi wa gazeti hli Hadija Jumanne

Comments