USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:10-12

 

USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:10-12





USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-10
Miaka 6 iliyopita Kuna rafiki alikwenda kijijini kwa Bibi yake kusalimia..alivyofika kijijini akatembea na Mume wa mtu...mke wa mwenye Mume akamlogezea ukimwi.

Rafiki alianza kuumwa ilibidi aletwe dar kwa vipimo zaidi ..kila akipimwa hakuna kitu na hali inazidi kuwa mbaya..na uumwaji wake ni ule ule wa wagonjwa wa ukimwi..hali ikazidi kuwa mbaya hadi kufikia kuwa mtu wa kitandani tu..Mama yake mdogo akajiongeza akamleta mtaalam akaweka kambi nyumbani kwao week mbili..week ya tatu rafiki mzima hakuwa na hata dalili Kama alitoka kuumwa ule ugonjwa...uchawi upo jamani.

USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-11

Hii ilitokea Tanga wilaya M. Kuna mganga fulani alikua mganga akaona akatoe huduma za kiganga wilaya M akitokea wilaya K. Basi alifikia nyumba ya jamaa mmoja na kumueleza kwamba amekuja hapo kutoa huduma kama kuna mwenye tatizo lolote aje. Basi mganga akapewa chakula akala na kupewa mahali pa kulala. Muda kufika akaenda kulala na mikoba yake. Kulipokucha adibuhi mganga alijikuta yuko nyumbani kwake wilaya K na mke wake na mikoba yake

USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-12

Miaka ya nyuma tunatoka mererani usiku wa manane tuko na pikipiki almaarufu baja tullikutakana na moto mkubwa ukiwa umetanda barabarani kama vile unavuka ,tulikuwa sita tukajishauri sana lakini kwasababu tulikuwa wengi tulipata ujasiri wa kupita ila cha kushangaza tulivuka na hatukuungua wala kuhisi chochote kuangalia nyuma baada ya kuvuka moto uko vile vile

Niliwahi kutongoza mtoto wa ustadh mmoja kama mchepuko , mzee wake akanistukia , akaniacha tu ,ila balaa kila nikienda kupiga ,kitu hakisimami hadi tunatoka ila nikienda sehemu zingine napiga kama kawaida

 FUATILIA MUENDELEZO WA VISA HIVI A:1-30, B:1-30, C:1-30

Comments