USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:13-15
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-13
Mwaka 2008 nafanya kazi Makambako kwenye mradi wa UKIMWI! Sikumoja mchana wa saa nane tulikua ofisini kama watatu hivi, nakumbuka nje jua lilikua Kali sana, ile nyumba ilikua na madirisha makubwa Na geti kubwa nje! Gahfla geti likagongwa na akaingia mwanamke mnene mrefu wastani amevaa gauni jekundu na handbag! Basi tukawa tunasubiri agonge sasa mlango wa ofisi aingie! Dakika kadhaa zikapita, kimya! Tukaulizana, mgeni kaishia wapi?
Nikatoka nje, hakuna MTU, nikazunguka jengo zima hakuna MTU! Nikarudi ndani nikawaambia mwenzangu, dah sitakaa nisahau
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-14
Kijiji kimoja mkoa X, mzee mmoja alipowaona kuku wa jirani wanashambulia mahindi shambani mwake akaamua kuwatimua kwa kuwapiga na mawe.
Alipoamka asubuhi akajikuta mguu mmoja umetoka uko pembeni hakuna damu wala nini, akiwa katika taharuki nini afanye akalala tena kuamka kesho yake mguu wa pili pia umetoka uko pembeni.
Mpaka leo huyo jamaa yuko na ameshakuwa mzee haelewi nini kilimkuta anatumia wheel chair, uchawi upo.
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-15
Kuna vijana wawili walipiga paka wa ostadhi mmoja hivi..mwenye paka akapata taarifa akawaambia waombe msamaha..kijana mmoja alikubali mmoja akagoma..yule aliyegoma alianza kutokwa na majipu mwilini wazazi wake wakamsihi akaombe msamaha lakini bado aligoma..kilichomkuta ni kupoteza maisha...yule mzee ni mchawi akikutaka uwe mpenzi wake ni dk 0 tu..
Tukio lingine Kuna kijana alijisaidia kubwa nyuma ya nyumba ya huyo mzee ostadhi alivyofika kwake akakuta ile kubwa ipo kitandani kwake.
FUATILIA MUENDELEZO WA VISA HIVI A:1-30, B:1-30, C:1-30
Comments
Post a Comment