USHUHUDA WA KWELI WA KICHAlWI A:4-6
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-4
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-5
2010 nipo ndani ya fuso, natokea Ifakara kwenda dsm. Kufika Maseyu mida kama saa 8 usiku dereva akapaki, akasema amechoka anapumzika kidogo. Akatuambia saa 10 tumwamshe tuanze safari.
Sijui kama ni uchawi au ni nini, tulipitiwa na usingizi mzito, na wote, tulikuwa watatu tuliota ndoto ya aina moja. TUNAPIGA MECHI. tumejipiga mabao wote, kuangali saa ni dk 20 tu zimepita. Nilichowaeleza wenzangu ndio walichoota. Mwanamke niloyeota namgonga ndio huyo huyo wenzangu walikuwa wakiota wanamgona.
Niliota vipele vya baridi kwa uoga. Tukaondoka kuendelea na safari. Tangu siku hiyo sipandi tena malori ya mzigo yanayosafiri usiku.
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-6
Nishawahi sikia kisa kinachohusishwa na uchawi
Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri
Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma
Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma
Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea
Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge
si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.
wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.
Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele
Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
FUATILIA MUENDELEZO WA VISA HIVI A:1-30, B:1-30, C:1-30
Comments
Post a Comment