USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:7-9

 

USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:7-9





USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-7

Yuko dogo mmoja alikua anasoma B sekondary. Alikua anamchukua mke wa mtu. Mtu mwenyewe alikua nje ya nchi kimasomo. Ndugu zake msomi hawakupendezewa shemeji Yao aliwe na student. Kuna siku dogo wakapanga na bibie wakapeane penzi kwenye minazi. Enzi hizo gesti wanaingia wenye pesa zao.

Dogo alikua dent hana pesa. Basi kweli muda kufika mke akafika na mechi ikaanza bila refa. Dogo akapakua mzigo kufika kileleni utamu Ulipozidi ni kawaida mtu kufunga macho. Basi dogo wakati anafyatua risasi alimkumbatia mke wa mtu kisawasawa huku amefunga macho. Ile kumaliza na kufumbua macho akajikuta alikua anafanya mapenzi na kisiki cha mnazi na sio mtu. Dogo kutoka pale hakurudi shuleni. Alipanda basi la Dar na kuacha shule. Sidhani kama alisharudi wilaya ya B.


 USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-8

Kuna jamaa angu alifumaniwa na mke wake,ugomvi ulikua mkubwa kiasi ya kwamba mwanamke alishaanza kufungasha mizigo yake aondoke,jamaa alichofanya alimpgia mtalaam wake simu aisee,baada ya masaa 5 mwanamke amesahau kila kitu,hali ikawa shwari 


USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-9


Kisa cha kwanza ambacho kinanivutia hadi leo ilikua mwaka 1998, Niko na jamaa yangu, Tunatokea Shule ya Wasichana Kifungilo tunarudi shuleni kwetu Magamba Secondary (now Sebastian Kolowa University)! Usafiri miaka ile usafiri ulikua wa shida sana, tukawa tunasubiri usafiri pale Lukozi, SAA Tisa au kumi hivi jioni. Mvua ikaanza kunyesha, wenyeji wakasema kuwa Mvua haitanyesha kwa kuwa Mzee Fulani yuko shambani kwake anauza mapeasi yake.

Ghafla yule Mzee akawa anapita, aiseee seriously kwa Mara ya kwanza tangu nizaliwe sijawahi kuona MTU hanyeshewi na mvua! Yaani mvua inanyesha lakini yeye hanyeshewi kabisa

FUATILIA MUENDELEZO WA VISA HIVI A:1-30, B:1-30, C:1-30  

Comments