USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:16-18
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-16
Nakumbuka kipindi hicho nikiwa na umri wa miaka 6. Usiku wa saa saba, mkojo ukanibana sawa sawa, ikabidi nimwamshe Mamdogo anitoe nje ili nitoe hiyo haja ndogo
Kwasababu Mamdogo alikuwa na usingizi kwa kutosha, ikabidi anipige biti la hatari na kufoka sana. Tukatoka, yeye akasimama mlangoni mie nikasogea kama mita nne hivi ili nijisaidie. Zile kelele za mother kufoka usiku akiwa mlangoni, tulisikia sauti ya kike kutoka nyuma ya jiko ikisema "MUACHE AKOJOE NAWEWE". Hahahahah!!! Sikutambua Mamdogo kaingia ndani sangapi maana kugeuka nyuma sioni mtu mlangoni. Kwakuwa nilikuwa mdogo niliendelea na haja yangu then nikarudi ndani......
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-17
Nipo Njombe huku!! Kuna mwanafunzi alikuwa anafanya mtihani kabla hajamaliza mkono ukaanza kuvimba ghafla hivyo ikashindikana kumalizia mtihani huo! Ikabidi tuwasiliane na Mzazi wake akasema tusimpeleke popote anakuja mwenyewe basi wakaja hapo shuleni na mchungaji baada ya maombi kama dakika 5 tu mkono ulijirudi na kuweza kuandika vizuuuuuuri! Daaa Kweli uchawi upo!! TUMWOMBE MUNGU DAIMA!!
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-18
Mwaka 1989 nilikwenda kijiji cha jirani nikanywa pombe sana.Nilipokuwa narudi nikapita sehemu ambayo inasifika kwa mauza uza nikawa mbishi vile nimelewa siogopi.
Nikafika kichaka flani nikasikia nywele zimesimama nikahisi joto kali sana nikasikia harufu ya marashi mara ukawaka mwanga mkali pombe yote ikaisha.
Kesho yake nikamuhadithia bibi yangu akaniambia bahati yako pale kulikuwa na jini lipenda dini liivyoona unanuka pombe likaona ngoja huyu mchafu aende zake.
FUATILIA MUENDELEZO WA VISA HIVI A:1-30, B:1-30, C:1-30
Comments
Post a Comment