USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:19-21
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-19
WANAODHANI HAKUNA UCHAWI , HAYAJAWAKUTA;
Miaka michache iliyopita nilikwenda RUKWA wilaya ya Nkasi nikiongozana na wenzangu tukiwa na watu Dr Livingstone Expedition waliokuwa wanafuatikia njia aliyotumia Dr Livingston toka Ujiji Kigoma hadi Zambia alipopata umauti.
Tulupofika kijiji kimoja kinaitwa Ntuchi (Nakikumbuka kwa tukio hili) tulikutana na kisa cha kustaajabisha kilichowakuta Maafisa toka Wizara ya Elimu Dsm waliokwenda kukagua shule za Sekondari Nyanda za juu na walipofika kwenye shule hiyo wakakutana na malalamiko ya Walimu juu ya vitendo vya kishirikina wanavyofanyiwa na wenyeji.
Maafisa wale wakawaita viongozi wa kijiji na wazee maarufu kuwakemea sana huku wakitishia kuwaondoa walimu wote endapo vitendo hivyo vitajirudia. Baada ya kumaliza kukemea jambo hilo wakiwa ofisini, walipotoka nje wakakuta gari lao halina upepo kwenye tairi zote 4, wakabaki wanashangaa. Walimuuliza dereva kimetokea nini naye akabaki anashangaa maana hajaona mtu yeyote akitoa upepo.
Walimwita fundi aangalie lakini kila alipojaribu kujaza upepo haukuingia. Walilazimika kuita baadhi ya wazee wakawaomba radhi na ghafla tairi zikawa na upepo kama awali. Waliapa kutorudi mkoa ule na sisi tukaendelea na safari yetu huku tukiwa na hofu kubwa.
Maafisa wale kama wamo humu JF watashuhudia tukio hili.
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-20
Kuna mkaka alimaliza form 6 miaka hiyo ya 84
Akatafutiwa kazi lkn kila akiwa kazini akiandika mikono haiandiki inakuwa km mtoto wa miaka 2 au mmoja jinsi anavyojichorea hovyo,lkn akiwa home kwao au mishe za kikawaida sio za kazi anaandika vzr,basi ameishia kuwa fundi mafriji
Kuna mdada kipindi hicho sasa mmama,alikuwa amelala chumbani kwake karibu na dirisha akahisi kitu nje akachungulia na kumuona mtu mrefuuuu kavaa nguo nyeupe,kila akijitahidi aone sura yake yule mtu anazidi kurefuka,alikuwa amepata tungi mbona liliisha na kulala fasta
Mmama mwingine alikuwa anachelewa kurudi kazini na kuondoka mapema,saa 7 usiku akaamua kufua nguo zake,alikua anafulia uwani kwake,ghafula akahisi mwili na mywele kusisimuka,na kuhisi km mtu kamsimamia,kuinua shingo hamna mtu,lkn kamba inatingishika sana km mtu anaitingisha,akaamka na kuanza kusali
Akaingia ndani akasali sana,maana yeye ni kama mlokole,akaomba mpk kutetemeka,usingizi ukampitia km dk 10,akaota anampigana na mwanamke jirani yake,akajiona kucha zake zimekua na kuziingiza ndani ya macho ya huyo mwanamke,mwisho mwanamke akauimia na kukimbia.
Baada ya siku 3 akapata taarifa huyo mama anaumwa sana mpk kapelekwa kwa ndg zake
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-21
Kuna kisa kimoja nilikisikia kuna jamaa alikuwa anahutubia wananchi akiwa juu ya gari lake,mara moshi ukaanza kufuka ukimzugnguka
FUATILIA MUENDELEZO WA VISA HIVI A:1-30, B:1-30, C:1-30
Comments
Post a Comment