USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A:28-30
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-28
Mwaka 2014 maeneo ya Boko, mimi na dada zangu watatu tunatoka zetu viwanja saa tisa usiku kwa mbele hivi tunaona mtu kalala katikati ya barabara mmh dada aliyekua anaendesha akasita alitaka asimame, dada mwingine akamwambia kwa sauti kubwa "pita juu yake bila hivyo wote unatuua", basi akapita juu na wote ndani ya gari tulihisi kabisa matairi yamekanyaga mtu, tulivyopita mbele kidogo tukageuka kuangalia huyo mtu vipi ajabu hatukuona kitu yaan road nyeupeee, basi story zilikata hakuna mtu aliongea hadi tunafika home.
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A-29
Siku moja zamani sana tuliharibikiwa na bus maeneo fluni panaitwa makuyuni Arusha tukiwa tunatoka Dodoma tunaelekea Moshi kwa Bus enzi hizo ni mabus yalikuwa ni ya kampuni ya Rali hakuna mabasi mengine.
Kipindi hicho barabara ni mbovu sana gari inachukuwa siku mbili kufika Moshi.
Ikabidi konda na abiria mmoja wafuate spear Dodoma nayo ilichuwa siku mbili.
Ilibidi wazazi waniojiongeze tutafute nyumba za jirani ili angalau tupate huduma kama chakula, kuoga na kadhalika wazee na familia zingine walifanya hivyo pia.
Kutoka hapo kwenye bus mpaka kwenye nyumba ni umbali wa kama kilometa tano hivi tukakuta nyumba mbili tu lakini tunashukuru nyumba tuliofika tukawaeleza shida zetu walituelewa ambapo walikuwa wanaishi watu wawili tu kijana mmoja na mke wake ambaye alikuwa mrembo kweli wengi tulishangaa kwanini waliamua kuishi porini ili hali kwa muonekano walikuwa ni watu wastaarabu sana.
Basi baada ya wazazi wetu kupokelewa wakaanza mandalizi ya kupika na mambo mengine sisi watoto mimi na mdogo wangu na watoto wawili wa familia moja tulienda kucheza eneo fulani kama shamba hivi lakini kulikuwa na mteremko unaelekea kwenye mto hivi pembeni ya ya huo mto kulikuwa na ndizi mbivu basi tukazikimbilia tukazichuma tukaanza kula.
Kwakuwa ule mto haukuwa na maji tukavuka upande wapili hapo tuliona matunda ambayo siyakumbuki ni matunda gani lakini yalikuwa matamu sana.
Baadaye tukaona kijumba kidogo cha udongo kimeezekwa kwa nyasi tukaenda mpaka kwenye hicho kijumba tukamkuta bibi mzee sana anachuma mboga karibu na nyumba yake tukasalimia tukamweleza sikumbuki nini lakini akatuletea mziwa tukanywa.
Mara kukawa na wingu zito sana na radi baada ya dakika kumi mvua ilinyesha kunyesha tukaanza kukimbia nilibidi nimemshika mdogo wangu mkono alikuwa analia sana na mdogo wake na yule mwenzetu naye alikuwa analia sana, basi yule bibi alituzuia tusiondoke mpaka mvua itakatike ila mimi na na mdogo wangu tuliondoka na kuwaacha wenzetu tukaelekea mtoni ili tuvuke ngambo ya pili tuondoke ajabu ngambo ya pili tulimuona yule Bibi na fimbo yake amekunja uso anaonyesha ishara ya tukivuka tutaipata daa tulitetemeka sana huku dogo analia vibaya sana bibi anatunyooshea ile fimbo turudi.
Nyuma ya yule bibi tukaona kwa mbali mwanga wa tochi na sauti za watu kama wanaongea ndiyo kumbe mzee wanatutafuta.
Yule bibi kuona watu wanakuja akaja upande wetu huku akivuka mto huku anatembea kwa kuinama na fimbo yake tukampisha tukanza kumuita mzee huku tunatetemeka na dogo analia tumeloa chakari mzee alivyotuona walipatatwa na hofu sana wakatuuliza yaliotokea tukawaambia wenzetu wapo kwa bibi mmoja kule juu mwenyeji wetu na wazee waliwafuata kwa yule bibi huku mwenyeji akisema huyu bibi ni mchawi sana asije wazuru watoto wakakimbia kufika pale wakawakuta wapo ndani kwa yule bibi wanaota moto lakini wamejikunyata wamelegea sana hawajiwezi huku huyo bibi akiwa amejilaza kwenye kitanda chake anatamka sijui maneno gani.
Yule mwenyeji nasikia akamkoromea sana huyo bibi akamwambia lolote litakalo walata hawa watoto tunakumaliza ndiyo ikiwa salama yao.
Kufika pale kwa mwenyeji wetu hapo ni usiku kama saa 2:30 kunagiza tunawahadithia kilichotokea mh..wazazi waliogopa sana tukagombezwa sana lakini tunashukuru mpaka leo tupo salama ingawa mwenzetu mmoja alishatangulia kufa .
Hayo ndiyo nakumbula lakini ilikuwa siku mbaya sana na sitaisahau maishani.
USHUHUDA WA KWELI WA KICHAWI A- 30
FUATILIA MUENDELEZO WA VISA HIVI A:1-30, B:1-30, C:1-30 NA KADHALIKA
Comments
Post a Comment