Wanajeshi watatu wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa leo Jumatatu asubuhi katika shambulio dhidi ya vituo viwili vya jeshi kaskazini mwa Côte d'Ivoire, vyanzo vitano vya jeshi vimebaini.
Washambuliaji wawili wamepigwa risasi na kuuawa na wengine wanne walikamatwa, vyanzo hivyo vimeongeza
Hata hivyo hakua kudi ambalo limedai kuhusika a shambulio hilo.
Chanzo kimoja kimesema kuwa washambuliaji walitokea nchi jirani ya Burkina Faso, taarifa ambayo haikuweza kuthibitishwa.
Kulingana na vyanzo hivi vya jeshi, wanajeshi wawili wameuawa katika shambulio dhidi ya kambi ya kijeshi ya Kafolo, karibu na mpaka na Burkina Faso na kami amayo ililengwa na shambulio lillilogharimu maisha ya wanajeshi kumi na tatu wa Cote d'Ivoire mnamo mwezi Juni 2020
Comments
Post a Comment