Takribani watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati basi walilokuwa wakisafiria lilipopigwa na bomu lililotegwa katika barabara ya Arabia katika Kaunty ya Mandera nchini Kenya.
Basi hilo lilikuwa njiani kuelekea katika mji wa Mandera uliopo mpakani mwa Kenya na Somalia Jumatano asubuhi lilipopigwa na kilipuzi kilichotegwa.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema basi hilo liliharibika vibaya baada ya kulipuka.
Picha zilizochukuliwa kutoka kwenye eneo la tukio zinaonesha basi hilo likiwa limepasuka vipande huku waathiriwa wakiwa wamelala chini.
Polisi imesema kuwa inahofia idadi ya majeruhi inaweza kuongezeka. Gavana wa ManderaAli Roba pia amethibitisha idadi ya vifo.
Shambulio hili linakuja siku moja tu baada ya maafisa wa usalama kuzima jaribio la wanamgambo wa al-Shabaablakushambulia kambiya polisi iliyopo katika eneo laLafey, katika Kaunty ya Mandera.
Inaaminiwa kuwa kundi hilohilo ndilo lililohusika na shambulio hili.
Comments
Post a Comment