CUF YAENDELEA KUWALILIA MASHEIKH WA UAMSHO

 



Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la CUF- Chama Cha Wananchi limetoa wito kwa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan na vyombo vyake kuhakikisha Masheikh wa Uamsho wanatendewa haki katika Kesi iliyodumu kwa miaka nane (8) sasa. Akiongea na Waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa CUF-Chama Cha Wananchi alisisitiza kwamba mazingira ya kesi hii ambayo upelelezi wake umekaa muda mrefu sana na kuzalisha shaka juu ya haki kutendeka na hilo linaongeza uhitaji wa Uwazi katika kuendesha Kesi hiyo

Comments

Post a Comment