HUYU NDIE WAZIRI WA TANZANIA ALIE UKATAA UWAZIRI NA KWENDA VITANI

 :


Moja kati ya mashujaa waliokwenda kupigana vita Uganda dhidi ya Idd Amin Dada alikuwa ni Meja Jenerali 'MUHIDDIN KIMARIO'(marehemu kwa sasa). Wakati Idd Amin anavamia eneo la Kagera na kuishusha bendera ya Tanzania na kuipandisha bendera ya Uganda, Muhiddin Kimario alikua waziri wa Mambo ya ndani na ni miongoni mwa mawaziri wawili tu waliowahi kudumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitano katika historia ya Tanzania.  


Mwaka 1978 alitumwa na Mwl. Nyerere kwenda Mwanza kwenda kuwaaga Wanajeshi ambao walikuwa wanakwenda kupigana vita mkoani Kagera, kumng'oa Idd Amin Dada. Wakati Muhiddin akitoa hotuba yake ndani ya uwanja wa Nyamagana ghafla aliamua kujivua uwaziri na kuungana na wanajeshi hao kwenda kupigana vita hivyo, wakati akichukua maamuzi hayo alisema kuwa.        


 "Mkuu Wa Mkoa ninaomba ufikishe taarifa hii kwa Mh. Rais kuwa ninajivua uwaziri  na ninaamua kurudi Jeshini na wenzangu leo, kwenda kumshikisha adabu Amini.".       

Huyo ndio alikua Muhiddin Kimario ambae alivaa uzalendo wa Taifa hili.


Alikuwa tayari kuacha cheo chake kwaajiri ya kupigania Taifa hili.


Ni kiongozi gani kwa sasa ambae anaweza kufanya alichofanya Meja Jenerali Muhiddin Kimario, kukubari  kuacha wadhifa mkubwa wa uwaziri na kuingia Vitani, sehemu hatarishi?

Comments