JE TUPO WENYEWE KWENYE ULIMWENGU? S02, Ep6 (Nyayo za Wageni Kutoka Sayari Ya Mbali - Egypt )
Na salim Msang
Mapiramidi matatu ndani ya Geza.
Bado tukiwa tunamtafuta mwandishi wa kazi hizi katika maeneo ya Marekani ya Kusini, tunakutana na kitu ambacho tumepata kukiona na kukusikia huku kwetu Afrika, Piramidi, kwenye eneo hili kuna mapiramidi kadhaa, lakini kuna matatu yanayo vutia zaidi ambayo mwonekano wake hautofautiani na ule wa mapiramidi matatu ya Gaza.
Turudi Egypt kidogo ambako kuna maandishi mengi kuhusu piramidi kubwa la Gaza tutafute kama tutapata chochote kitu kuhusu kazi hizi za maajabu halafu tutarudi Peru kwenye haya mapiramidi matatu kabla hatujatoka nje ya dunia na kuitembelea sayari ya Mars ambako nako eti kuna Piramidi.
Daima majengo hayo ya Gaza yamekuwa yaki washangaza wanasayansi, hasa kutokana na ukamilifu wa muundo wake ambao unathibitisha utumikaji wa elimu kubwa ya mahesabu na elimu ya maumbo.
Kamwe hayakujengwa kama makaburi ya Mafarao kama wanavyo tufundisha katika mitaala yao, wala hayakujengwa na Mafarao wenyewe, wala watumwa, bali ni hazina waliyo irithi, wameirithi kutoka wapi, hilo ndilo swali tunalo litafutia jibu katika mtiririko wa posti hizi.
Uyakinifu wa mahesabu yaliyotumika kusimamisha kuta za Pyramid, hata kwa theluthi ya sekunde haikubaliki kwamba, eti yalijengwa na watumwa walioshinikizwa kwa adhabu na viboko, bali ni kazi ya kitaalam ambayo taaluma yetu ya leo ya ujenzi, ikishirikiana na mahesabu, elimu ya nyota na vifaa tulivyo navyo hatujaweza kutengeneza nakala (copy) ya mfano wa jengo hilo.
Kamwe hayakujengwa kama makaburi ya Mafarao kama wanavyo tufundisha katika mitaala yao, wala hayakujengwa na Mafarao wenyewe, wala watumwa, bali ni hazina waliyo irithi, wameirithi kutoka wapi, hilo ndilo swali tunalo litafutia jibu katika mtiririko wa posti hizi.
Ndani ya Pyramid kuna vyumba (vyemba) vilivyo jengwa juu, chini ya pyramid, kuna milango kama huo hapo kwenye picha ambao haujulikani unafunguliwaje na ndani ya chumba hicho kuna nini? Maduara meusi unayo ona ni matobo ambayo kamera imepenyezwa kuona kuna nini ndani. Walichoona ni mlango mwingne kama huo. Hakuna kibali kilichotolewa kuendelea kufanya utafiti kujua kuna nini ndani. Ni kipi tunacho ogopa?
Uwanda wa Gaza, nyumbani kwa Great Sphinx, na nyumbani kwa mapiramidi makubwa matatu ya Egypt, kwa kila hali ujenzi huo wakale ni fumbo kwenye sanaa ya ujenzi wa zama zetu, fumbo ambalo teknolojia yetu haijafikiriwa kulifumbua. Hii ni kwa sababu ni vichache sana vinavyo fahamika kuhusiana na mapiramidi hayo.
Mapiramidi hayo matatu makubwa yanahusishwa na makaburi ya mafirauni watatu, yaani Khufu, Khafre na Menkaure ingawa hakuna mwili wala alama yoyote ya ustaarabu wa Egypt wa zama hizo iliyo pata kupatikana ndani ya maumbo hayo ambayo kama ilivyo michoro na mapiramidi ya Nazca nayo mjengaji wake hajulikani ni nani.
Muonekano wa Great Pyramid

Khufu, Khafre na Menkaure
Katika Great Piramidi kuna alama ya mfalme Khufu ambayo inalenga kuashiria kuwa yeye ndiye mjenzi wa kazi ile au walau kazi ile ilifanyika katika zama zake, lakini utafiti unaonesha kuwa alama hiyo iliwekwa makusudi mwaka 1837 na mtu aliyeitwa Howard Vyse.
Mengi yamesemwa kuhusu jamaa huyu kuamua kuipa nguvu ile nadharia ya kuwa Khufu ndiye mjenzi wa kazi ile kwa kuweka alama yake kwenye ukuta wa Great Pyramid. Hata hivyo lilokubwa ni kuwa Howard Vyese si wa kwanza kuingia ndani ya Pyramid na kutoa hadithi zake, na alama hizi za Khufu zimeonakana katika vyemba vinne vilivyo gunduliwa na Howard na alama hizo hakuzitaja popote katika maandishi yake mpaka siku ya pili alipokwenda na mtu mwingine katika vyemba hivyo.
Mwaka 1765 mtu aliyeitwa Davison alipogundua kuwepo kwa vyemba hivyo hakuona wala kutaja kwenye kazi zake jina la Khufu . Hivyo jina hilo lililenga kumpa mfalme sifa isiyo yake. Lakini katika mtirirko wa sura hii tutakuja kuona kuwa Piramidi zilikuwepo hata kabla ya kuja binaadam, lakini ni kazi ya nani hiyo ndiyo jukumu letu kwa sasa kumtafuta mjenzi wa kazi hizi za maajabu.
Jina la mfalme Khufu liliwekwa hapo kwa kughushi ili ionekane kanakwamba yeye ndiye muhusika wa ujenzi huo au ulifanyika katika zama zake.
Mengi yamesemwa kuhusu jamaa huyu kuamua kuipa nguvu ile nadharia ya kuwa Khufu ndiye mjenzi wa kazi ile kwa kuweka alama yake kwenye ukuta wa Great Pyramid. Hata hivyo lilokubwa ni kuwa Howard Vyese si wa kwanza kuingia ndani ya Pyramid na kutoa hadithi zake, na alama hizi za Khufu zimeonakana katika vyemba vinne vilivyo gunduliwa na Howard na alama hizo hakuzitaja popote katika maandishi yake mpaka siku ya pili alipokwenda na mtu mwingine katika vyemba hivyo.
Mwaka 1765 mtu aliyeitwa Davison alipogundua kuwepo kwa vyemba hivyo hakuona wala kutaja kwenye kazi zake jina la Khufu . Hivyo jina hilo lililenga kumpa mfalme sifa isiyo yake. Lakini katika mtirirko wa sura hii tutakuja kuona kuwa Piramidi zilikuwepo hata kabla ya kuja binaadam, lakini ni kazi ya nani hiyo ndiyo jukumu letu kwa sasa kumtafuta mjenzi wa kazi hizi za maajabu.
Baadhi a vyemba ndani ya Pyramid. Ustadi na maarifa yaliyo tumika kuvichonga vyemba hivyo, bado unavitia soni vyombo nza zana za kwenye zama zetu katika ujenzi na uchimbaji.
Uzito wa jengo hilo unakaribia kufikia tani milioni 6! Leo hii kwa teknolojia tuliyo nayo, na maendeleo katika fani ya ujenzi, mahesabu na elimu ya nyota bado itahitajika maajabu kusimamisha jengo mfano wa hili. Great Pyramid linafahamika kuwa ndiyo jengo kubwa, bora zaidi duniani na lililojengwa kwa mahesabu na vipimo yakinifu.
Ni vigumu kukubaliana na wanahistoria wanao dai kuwa majengo hayo yalijengwa na mafirauni watatu walio tajwa hapo juu. Mawe mengine ni makubwa mno ambayo teknolojia tuliyo nayo haiwezi kuyanyanyua,achilia mbali binaadam wa kawaida, ndani ya mapiramidi hayo, wajenzi wake wamechimba, njia, vyumba na korido za haja kuelekea chini ya aridhi na kufunikwa na mawe mazito mfano wa mlango ambayo mingine mpaka hivi leo haijaweza kufunguliwa(watu fulani hawataki vyemba hivyo vifunguliwe).
Mapande ya mawe yalitumika kama matofali hayafahamiki waliyatolea wapi, kwani eneo hilo halina asili ya kuwa na mawe hayo zaidi ya mchanga, na wala hakuna alama ya kuonesha kuwa mawe hayo yaliburuzwa kutoka sehemu yoyote ile, mawe hayo makubwa yakanyanyuliwa na kupangwa kwa ustadi na maarifa makuu na kuunganishwa kiasi kwamba huwezi hata kupenyeza wembe baina ya mawe mawili.
Bado unafikiri kuwa mawe hayo makubwa yalikokotwa na watumwa na kupangwa moja juu ya jingine na kutengeneza Pyramid, ambopo jiwe lenye uzito mdogo kwenye jengo hilo linakadiriwa kufikia tani 20.
Mapande ya mawe yalitumika kama matofali hayafahamiki waliyatolea wapi, kwani eneo hilo halina asili ya kuwa na mawe hayo zaidi ya mchanga, na wala hakuna alama ya kuonesha kuwa mawe hayo yaliburuzwa kutoka sehemu yoyote ile, mawe hayo makubwa yakanyanyuliwa na kupangwa kwa ustadi na maarifa makuu na kuunganishwa kiasi kwamba huwezi hata kupenyeza wembe baina ya mawe mawili.
Historia wanayo tufundisha ni kama kwenye hiyo picha hapo. Lakini inashindwa kujibu maswali ya msingi kabisa kama vipi waliweza kuburuza jiwe lenye uzito wa tani 20? Hakuna eneo lolote kuzunguka Egypt ambako imeonekana kuwa ndipo mawe hayo mazito yalichimbwa. Hakuna alama yeyote au zana yeyote iliyopatikana ambayo inaweza kunasibishwa na ujenzi au wajenzi wake. Ni kifaa gani kilitumika kunyanyua mawe mengine yanayofikia tani 200?
Aina ya tabaka la aridhi mahali pa ujenzi wa mapiramidi hayo ni lile eneo linajulikana kuwa na mawe aina ya diorite, kwa wataalam wa tabaka la aridhi, mawe na mchanga aina hii ya mawe ndiyo mawe magumu mno kwenye uso wa aridhi, hutumika kujengea barabara kabla ya kuweka lami. Ni katika aridhi ya aina hii ambapo chini ya mapiramidi ndiko utakuta njia, korido na vyumba kadha na ambavyo vingine milango yake bado haijaweza kufunguliwa.
Uwanda wa Gaza
Muandishi wa kitabu cha Fingerprints of the gods bwana Graham Hancock,anasema kuwa,
“Hakukuwa na teknolijia ambayo ilipata kujulikana kwenye Egypt ya kale kwamba ina uwezo wa kufanya kazi za namna hii, na wala si katika zama zetu ambapo tutapata mhunzi wa kufanya kazi ya aina hii...”
Ikiwa hata kwenye teknolojia ya leo hatuwezi kufanya kopi ya kazi ile, ni vipi tuseme ilejengwa na watumwa, waliolazimishwa kwa mijeledi, ni vipi tuseme ilifanyika kibususa?
Kusema kwamba Pyramid zilitengenezwa kwa zana duni na watu wenye maarifa duni kama wanavyo sisitiza. Ni sawa na kusema mtoto mchanga anaweza kutengeneza engine ya ndege!!!!!
Chini ya aridhi ndani ya mapiramidi mamia ya mita kadhaa kwenda chini utakutana na korido hizo zilizo chongwa vizuri na kwa usatadi mkubwa na hata kutengeneza pembe ya nyuzi 90. Aina hii ya teknolojia ndiyo kwanza inapatika katika zama zetu.
Maajabu na maswali yasiyo jibika kuhusu Pyramid.
Karibu ndani ya Great Pyramid.
Lakini ukishangaa hili kwa nini usishangae barabara za kurushia ndege zinazo patikana Nazca, Peru ambapo sisi tulizigundua kwenye karne ya ishirini baada ya ndege kuanza kurushwa kupita eneo hilo!
Kuna mengi ya kujaza vitabu kuhusu malighafi na teknolojia iliyotumika,kusimamisha majengo hayo, ili kufanya somo liwe rahisi tuhamie kwenye kitu kingine, na hapa na zungumzia eneo lililochaguliwa kwa ajili ya ujenzi wa mapiramidi haya.
Majengo haya yapo kwenye degree 30 ya latitude ambayo iko sawa na dakika 3 za arc kwenye true north. Arc ni sawa na 1/360 ya mzunguko wa duara zima. Ambayo hugawanywa kwa dakika 60 ambapo kila dakika moja ni sawa na 1/21600 ya mzunguko wa duara zima, kwa sekunde 60 kila sekunde moja ni sawa na 1/1296000 ya mzunguko wa duara zima. Hii ina tuonesha kuwa viumbe hao walikuwa na uwezowa kupima latitude na longitude kwa usahihi kabisa.
Ni mwaka 1761 ndiyo tumeanza kutumia mistari hii ya kufikirika, na kabla ya hapo safari za kupitia kwenye maji zilikuwa za mashaka makubwa.

Ukilipima Great Pyramid kutoka kwenye kitako chake kuelekea mpaka juu unapata ni sawa na Pi ( π ) 3.14. Aina hii ya mahesabu yaani, Pi ( π ) haikuwa ikifahamika mpaka pale wa Giriki walipoanza kuitumia karne ya 3 BC nao hawana maelezo ya kueleweka kuwa waliitoa wapi, ni ajabu kuwa urefu wa Great Pyramid kutoka kwenye kitako chake ni sawa na futi 481.3949 ambao una wiana na mzunguko wa kwenye kitako chake yaani futi 3023.16, hesabu ambayo unaweza kuipata kwenye mzunguko wa duara lolote kuwiana na kipenyo chake. Uwiano huo uko hivi 2pi (481.3949×2×3.14= 3023.16). Kwa kutumia skeli ya 1:43,200 kwenye kipenyo cha dunia yetu na kipenyo cha Great Pyramid, kisha tukazidisha skeli hiyo na urefu wa Grat Pyramid kutoka kwenye kitako kwenda juu, yaani 481.3949×43200=3938.685. Hii namba tuliyopata yaani 3938.685 kwa makadirio machache ya pungufu ya maili 11 ni sawa na kipenyo sahihi cha dunia yetu ambacho ni maili 3949. Na hivyo hivyo ukichukua kitako cha jengo hilo ambacho tulipata ni futi 3023.16 ukazidisha na ile skeli yetu ya 1:43200, utapata 24734.94 ambayo nayo kwa makadirio machache ya pungufu ya maili 170 ni sawa na mzunguko wa duara la dunia yetu ambao ni maili 24902.
Kumbuka pungufu ya maili 11 na au maili 170 kwenye skeli yetu ni kitu kidogo mno, yaani ni sawa na tofauti ya vipimo vya sehemu ya nchi kwenye piramidi zima. Hapa unajiuliza swali moja. Je viumbe hawa walikuwa wakifahamu vipimo vya duara la dunia na kipenyo chake?
Kwanini yana wiana sana na nyota za angani?
Mundo wa Great Pyramid una siri kubwa kuhusu elimu ya nyota. Jengo hilo lina kile kinacho julikana kama shaft ambazo wachunguzi wengi walidhani ziliwekwa kwa sababu ya kuingiza mwanga ndani ya jengo hilo, lakini zina kazi kubwa zaidi ya kuingiza mwanga.
Kila shaft inaonekana kulenga nyota maalum inapo pita kwenye meridian. Kutoka kwenye Queen Chamber, shaft ya kaskazini iliyo lala kwenye engo ya nyuzi 39 imelenga nyota ya Kochab na mara nyingine hutamkwa kama Kocab na zaidi ni maarufu kama Beta Ursa Minor ni nyota ya pili kati ya nyota zinazo ng’ara sana kwenye kikundi cha nyota za Kaskazini zinazo julikana kama Little Bear. Shafti ya upande wa kusini kwenye Queen Chamber ambayo iko kwenye engo ya nyuzi 39 na dakika 30 imelenga nyota ya Sirius inayo patikana kwenye kikundi cha nyota za Alpha Canis Major, hii ni nyota inayo ng’ara kushinda nyota zote angani.
Hatukujua na bado hatujui kazi za shafti hizo, hivyo jibu rahisi ikawa ziliwekwa ili kupitisha hewa, je ni kweli?
Kila shaft inaonekana kulenga nyota maalum inapo pita kwenye meridian. Kutoka kwenye Queen Chamber, shaft ya kaskazini iliyo lala kwenye engo ya nyuzi 39 imelenga nyota ya Kochab na mara nyingine hutamkwa kama Kocab na zaidi ni maarufu kama Beta Ursa Minor ni nyota ya pili kati ya nyota zinazo ng’ara sana kwenye kikundi cha nyota za Kaskazini zinazo julikana kama Little Bear. Shafti ya upande wa kusini kwenye Queen Chamber ambayo iko kwenye engo ya nyuzi 39 na dakika 30 imelenga nyota ya Sirius inayo patikana kwenye kikundi cha nyota za Alpha Canis Major, hii ni nyota inayo ng’ara kushinda nyota zote angani.
Je yalijengwa kwa ajili ya kufuatilia mambo ya angani, je watumwa walikuwa wanajua kile kilichopo nje ya galaxy ya milk way? Bado unafikiri Mapiramidi yalijengwa na watumwa wasio jua kuvaa nguo na waliyo kokota mawe hayo kwa kamba? Fikiri tena.
Kutoka kwenye King Chamber, shaft ya kaskazini iko kwenye engo ya nyuzi 32 na dakika 28 imelenga nyota ya Thuban iliyo kwenye kikundi cha Alpha Draconis. Shafti ya kusini kwenye King Chamber iko kwenye engo ya nyuzi 45 na dakika 14 ina lenga nyota ya Al Nitak iliyopo kwenye kikundi cha nyota cha Zeta Orionis, ni nyota ya tano kwa mng’aro na pia ni moja ya nyota tatu zilizo chini kwenye kikundi hicho.
Vipi walijua juu ya uwepo wa nyota hizo, na eneo zilipo kwa vipimo sahihi, wakati sayari ya 12 kwenye milk way tumeigundua kwenye karne ya 19. Ni kweli hii ilikuwa ni kazi ya watumwa kwa ajili ya makaburi ya wafalme?
Shafti hizo nne kwa msaada wa kompyuta zinaweza kutuonesha nafasi za kila nyota mahala zilipokuwa mara ya kwanza wakati ujenzi wa piramid ulipo kamilika, kwani hakuna shaka muelekeo wa shafti hizo ulilenga eneo zilipo kuwepo nyota hizo. Kumbuka nyota hizo ziko nje ya Milk Way, yaani nje ya mfumo wetu wa Jua.
Zipo kwenye njia ambayo Jua letu, mwezi, na sayari nyingine tano ukiacha dunia yetu zinapo pita, nyota hizo zipo karibu na njia ya nyota kubwa tunayoiitwa Jua na sayari za Mercury, Venus, Mars, Jupiter, na Saturn pamoja na mwezi wa sayari yetu. Mzunguko wa jua kuzunguka nyota hizo huu unachukua muda mrefu wa miaka 25,950 kukamilika. Inachukua miaka 12,960 kwa nyota hizo kuteremka kutoka juu kuja chini na miaka mingine 12,960 kurudi juu kutokea chini.
Kutambua ni wapi zilipo nyota hizo si kazi ya kibususa, ni kazi ya kitafiti na mahesabu ya hali ya juu, vipi watumwa waliosimamiwa na mijeledi waliweza kuyatambua mahesabu hayo na kusimamisha jengo lenye uwiano na nyota hizo kwa usahihi wake.
Zipo kwenye njia ambayo Jua letu, mwezi, na sayari nyingine tano ukiacha dunia yetu zinapo pita, nyota hizo zipo karibu na njia ya nyota kubwa tunayoiitwa Jua na sayari za Mercury, Venus, Mars, Jupiter, na Saturn pamoja na mwezi wa sayari yetu. Mzunguko wa jua kuzunguka nyota hizo huu unachukua muda mrefu wa miaka 25,950 kukamilika. Inachukua miaka 12,960 kwa nyota hizo kuteremka kutoka juu kuja chini na miaka mingine 12,960 kurudi juu kutokea chini.
Safari ya milenia kadhaa.
Ukitizama mpangilio wa mapiramidi matatu ya Misri yamepangwa kwenye utaratibu ambao unawiana na nyota tatu zilizoko kwenye kundi la Orion. Great Pyramid na lile la pili kwa ukubwa yako kwenye nyuzi 45 kusini mashariki.
Wakati lile la tatu liko upande wa mashariki. Muonekano huo ndiyo muonekano wa nyota tatu angani kwenye kundi la Orion , ni kama wajenzi wake walikopi muonekano wa nyota hizo. Nyota mbili za mwanzo yaani Al Nitak na Al Nilam zimejipanga moja kwa moja kama piramidi kubwa la kwanza na lile linalofuatia, na nyota ya tatu Mintaka imekaa kuelekea mashariki kulingana na muhimili uliwekwa na nyota mbili za mwanzo.
Copy 'n' Paste from above so high to deep below Geza.
Kazi hii ni kazi ya kizazi kipi au viumbe gani katika zama zipi. Ni vipi waliweka alama hii inayoonekana ni ya milele kwenye macho yetu?
Kwa msaada wa kompyuta simulesheni iliyotengenezwa maalum kwa kazi kama hizi ikisaidiana na picha za satelaiti tunarudi nyuma mpaka mwaka 10500 KK ambapo ndipo wakati hasa ujenzi huo yakinifu ulifanyika. Tunasema ndipo wakati ujenzi huu ulifanyika kwa sababu uwiano wa moja kwa moja bila kukosea baina ya piramidi na shafti zake ulilinganisha na nyota nilizo zitaja hapo juu, uwiano huu haukupatikana kokote katika historia ila mwaka 10500BC.
Hivyo zama hizo zilizo gandishwa katika aridhi ya Misri kwa mfumo wa piramidi, yani mwaka 10500 ndicho kipindi nyota hizo zilikuwa zikianza safari yake ya kutoka chini kwenda juu safari ambayo itakamilika mwaka 2500AD kabla ya kuanza tena safari ya kushuka chini kwa mara nyingine. Kikundi hichi cha nyota kipo mashariki mwa Milk Way, na aridhini wajenzi wasiyo fahamika wakayalaza Mapiramidi yale mashariki wa mto Nile. Nivigumu mno kuelezea uwiano huu umetokea kwa nasibu.
Inamaana majengo hayo hayakujengwa mwaka 2500 KK kama tunavyo fundishwa ispokuwa 10500 KK, ni nani alikuwepo zama hizo? Binadam anakadiriwa kufika hapa duniani miaka 4000 KK iliyopita, ni nani huyo aliyekuwepo 10500 KK?
Hivyo zama hizo zilizo gandishwa katika aridhi ya Misri kwa mfumo wa piramidi, yani mwaka 10500 ndicho kipindi nyota hizo zilikuwa zikianza safari yake ya kutoka chini kwenda juu safari ambayo itakamilika mwaka 2500AD kabla ya kuanza tena safari ya kushuka chini kwa mara nyingine. Kikundi hichi cha nyota kipo mashariki mwa Milk Way, na aridhini wajenzi wasiyo fahamika wakayalaza Mapiramidi yale mashariki wa mto Nile. Nivigumu mno kuelezea uwiano huu umetokea kwa nasibu.
As above so below, only in 10500 BC was the alignment of three brightest stars was reflected perfectly to the three Pyramid on Geza plateau.
Bado tukiwa hapo kwenye aridhi ya Egypt, aridhi ya mapiramidi, kuna kitu kingine ambacho ni vigumu kukidharau na kukifumbia macho, unapotokeza kwenye aridhi hii ya Egypt kabla hujayafikia mapiramidi, upande wa mashariki utakutana na kitu hicho, kikutazama na macho mawili, hayaangalii kushoto wala kulia, ni kama mlinzi anayetizama mlango ambao anajua punde utafunguliwa na hapaswi kutizama pembeni kabla ya hapo, Sphinx.
Kichwa cha mtu lakini mwili ni wa simba, limelala kwenye aridhi hii, macho yake yanatizama mashariki. Kama walivyo elezea uwongo kuhusu mapiramidi, ndivyo wanavyo endelea kufundisha uwongo wao kuhusu Sphinx kwamba na lenyewe ni moja ya kazi za waegypt wa zama flani, ni kazi ya mfalme fulani wa Egypt.
Lakini hakuna ushahidi wenye mashiko kuhusiana na dai lao hilo, ispokuwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba Sphinx lilikuwepo hapo hata kabla ya mapiramidi yenyewe, ni la kale kushinda historia ya binadam mwenyewe.
Watu kutoka nje ya Egypty walipoliona kwa mara ya kwanza, mwili wake wote ulikuwa umefunikwa na mchanga ispokuwa kichwa chake, ni kama unatazamana na zimwi linalotoka chini ya aridhi.
Lakini hakuna ushahidi wenye mashiko kuhusiana na dai lao hilo, ispokuwa kuna ushahidi wa kutosha kwamba Sphinx lilikuwepo hapo hata kabla ya mapiramidi yenyewe, ni la kale kushinda historia ya binadam mwenyewe.
Yu wapi mjenzi wake, kwa malengo yapi au kwa sababu zipi aliamua kulitengeneza sphinix.
Kama yalivyo mapiramidi yale Sphinx nayo ni alama ya nyota maarufu ya Leo, au nyota ya Simba iliyoko katika kundi la nyota kumi na mbili maarufu kama Zodiac. Nyota hizi tunaweza kuzichukulia sawa na masaa 12.
Muhimili wa dunia yetu unafanya kazi ya kuhama kutoka kwenye nyota moja kwenda nyingine, au kazi ya kutoka kwenye nyumba moja ya Zoadic kwenda kwenye nyingine kwa muda wa miaka 25,920 mpaka 25,925, unapokamilika mzunguko huu dunia yetu inapambana na mabadiliko makubwa ambayo nitayazungumzia hivi punde.
Hivyo alama 12 za Zoadic ni kama masaa kumi na mbili na kama yalivyo mapiramidi, Sphinx nalo lililenga kugandisha katika aridhi ya Egypt moja ya alama ya Zoadic au moja ya lisaa katika masaa 12 ya Zoadic kwenye aridhi ya Egypt. Hivyo basi ni lini Sphinx liliwekwa rasmi katika aridhi hiyo hapana shaka itakuwa ni kipindi ambacho jua lilikuwa likichomoza nyuma ya alama ya Leo (Simba).
Mjenzi wa Sphinix alifahamu juu ya nyota za Zodiaki? Na juu ya nyota ya Leo, alifahamu elimu ya nyota nje ya milk way? Na alifahamu ni lini nyota ya Leo inakuwa sambamba na uwanda wa Gaza? Je alikuwa mnajimu aliyebobea kwenye mahesabu na elimu ya nyota au mtumwa?
Muhimili wa dunia yetu unafanya kazi ya kuhama kutoka kwenye nyota moja kwenda nyingine, au kazi ya kutoka kwenye nyumba moja ya Zoadic kwenda kwenye nyingine kwa muda wa miaka 25,920 mpaka 25,925, unapokamilika mzunguko huu dunia yetu inapambana na mabadiliko makubwa ambayo nitayazungumzia hivi punde.
Najua umefundishwa juu ya dunia kulizunguka jua, dunia kujizungusha kwenye mhimili wake, na pia jua kuzunguka. Lakini najua hili la mhimili wa dunia kuzunguka nyota ya Zodiak ni geni kwako. Tulia upate darsa.
Wakati nguvu za jua zinaivuta dunia upande wake na nguvu za mwezi zinaivuta dunia upande wake, muhimili wa dunia ulio lala nyuzi 23.5 kuelekea njia ya dunia kulizunguka jua taratibu,kwa taratibu mno unajizungusha kwenda kinyume na njia hiyo ya dunia kulizunguka jua na kufuata kwa taratibu sana kuelekea katika vikundi vya nyota vilivyoko katika great cirlce, mzunguko huu unaitwa Precessional cycle ambao unaichukua dunia miaka 25920 kukamilisha kuzipitia nyumba zote 12 zilizoko katika zodiac.
Mchoro huu unaonesha mhimili wa dunia kwenye safari yake ndefu ya miaka 25,920.
Mtu aliyekuwepo duniani anapolitizama jua linapo chomoza asubuhi kwa zama tofauti na kwa vipindi tofauti atagundua kuwa jua halichomozi katika sehemu moja miaka yote, bali linahama kutegemea na kituo lililopo kwenye kikundi flani cha nyota katika ujumla wa safari yake hiyo.
Mchoro unaonesha mhimili wa dunia katika nukta mbili za zama mbili tofauti.
Muhimili wa dunia kule uliko elekea na ambao taratibu sana na wenyewe unahama kwenye muelekeo zilizopo nyota hizo za angani unatufanya tudhani kuwa jua linachomozea sehemu moja, lakini mhimili huo unapo kuwa umekamilisha sehemu kubwa ya mzunguko wake tuna anza kuona tofauti ya vitu mbalimbali ikiwemo nafasi ya jua kuwa lilipokuwa likichomozea kabla sipo linapo
chomozea sasa.
The big Clock in the Sky, unajua sasa hivi ni saa ngapi? Sasa hivi ni PISCES NA NUSU. I like that clock!!
Hivyo katika safari hiyo ndefu kuna kipindi jua lilikuwa likichomozea nyuma ya kikundi cha nyota ya Leo kama inavyo julikana kwa watu wa fani ya mambo ya nyota na baadae mpaka inamaliza vikundi vyote na kisha inaanza upya tena.
Our Heavenly Clock is ticking.
Ikiwa binadam wa kwanza kukanyaga dunia hii tunamuweka kwenye kipindi cha baina ya miaka ya 6900 mpaka 6000 KK. Hii inamaana kuwa binadam alingia kwenye zama za Germin, au kipindi ambacho jua linachomozea kwenye kikundi cha nyota cha Germin. Hii inamaanisha kuwa tangu binadam wa kwanza akanyage aridhi hii, mpaka leo hii ni kama tumeishi masaa manne na nusu tu!!!!
Hatukuwepo wakati jua linachomoza nyuma ya nyota za kikundi cha Leo, ni nani aliyekuwepo zama hizo na kuliweka Sphinx hapo.
Muhimili wa dunia kwa kuchukua njia ya mzunguko tofauti na ambayo unazunguka kuifata great cycle ndiyo inayo iwezesha dunia kuhimili nguvu za mvutano za jua na mwezi bila kutoka kwenye muhimili wake kwa miaka bilioni 4.2 tangu ilipo anza kufanya mzunguko huo. Kwa sababu muhimili wa dunia unavutika kuifuata great cycle ambayo imeundwa na vikundi 12 vya nyota tofauti tofauti, hivyo zama hadi zama muhimili huo nao utakuwa sambamba na kikundi flani cha nyota moja baada ya kingine kutoka kaskazini mwa great cycle na baadae kusini mwa great cycle mpaka ikamilishe mzunguko huo, na wakati mwingine mhimili huo utakuwa ukilenga anga tupu pale unapokuwa kwenye daraja la kuvuka kutoka kikundi kimoja kwenda kingine.
Katika zama zetu leo jua linachomoza baina ya Pisces na Aquarius. Kwa maneno mengine mhimili wa dunia umelenga anga tupu, kutokana na kwamba tuko kwenye kivuko tunamalizia zama za Pisces na muda si mrefu tutaingia kwenye zama za Aquarius, hivyo tuko kati na kati. Ama new age na au zama mpya.
As the above, so below.
Hivyo basi Sphinx ilijengwa kutizama jua lilipokuwa likichomoza nyuma ya nyota ya Leo kitu ambacho kilitokea maelfu ya miaka nyuma hata kabla binaadam hajakanyaga nyumba hii inayoitwa dunia. Ajabu sana ukizitumia nyumba 12 za zoadic kama masaa 12, utashangaa kuona kuwa binadam tuna masaa machache sana tangu tulipoingia kwenye nyumba hii inayo itwa dunia, kifupi hatuna zaidi ya masaa manne tangu binadam wa kwanza akanyage nyumba hii.
Tuna masaa mangapi kabla hatujafutika.
Tuna masaa mangapi kabla hatujafutika.
Nisiwachoshe, msinichoshe, ngoja niweke pause kidogo hapa ... tutaendelea next time....
Comments
Post a Comment