MAMBO 8 MUHIMU KUHUSU MBEGU ZA KIUME

Kuhusu Mbegu Za Kiume





1.NAMBA
Kila siku mwanaume huzalisha mamilioni ya mbegu za kiume huku akitoa zaidi ya mbegu milioni 280 kila anapofika kileleni.
-
2.UWEZO WA KUTUNGA MIMBA
Kwa mujibu wa taarifa ya National Infertility Association,mwanamme mwenye uwezo wa kumpa ujauzito mwanamke anatakiwa awe na wastani wa mbegu milioni 40-300 kwa kila millilitre.Kinyume cha hapo inakuwa ni vigumu sana kwa mwanamme huyu kutungisha ujauzito.
-
3. KASI
Mbegu hizi huogelea kwa kasi kubwa sana baada ya kutolewa zikilitafuta yai kwenye mirija ya fallopio.Mbegu hizi hutumia wastani wa dakika 8-68 tu hadi kulifikia yai baaada ya kumwagwa kwake
-
4.WASTANI WA KUPONA NI 1%
Japokuwa zaidi ya mbegu milioni 280 hutolewa kila baada ya kufika kileleni,ni wastani wa 1% tu ya mbegu hizi ndizo huweza kuhimili mapambano na changamoto zilizopo kwenye mfumo wa uzazi wa mwanamke huku 99% zikifa.Asilimia hii moja ndiyo huamua utungwaji wa ujauzito .
-
5.HUTANGULIZA MAJIMAJI
Kabla mwanamme hajatoa mbegu kamili,majimaji hutangulia kwanza ili kuandaa mazingira mazuri ya kuogelea pindi zitakapotolewa.Bila uwepo wa kitendo hiki,mbegu zote zingekufa mara moja baada tu ya kutolewa
-
6.AFYA YAKE
Wanaume wanaokula vyakula hasa vya haraha haraka mitaani visivyo na virutubisho muhimu (Junk food),wavuta sigara pamoja na watumia madawa ya kulevya huzalisha mbegu chache zilizo na afya duni.Ikitokea mbegu hizi zimerutubisha yai,uwezekano wa kuharibika kwa ujauzito ama kuzaa mtoto mwenye matatizo katika baadhi ya viungo vya mwili ni mkubwa sana
-
7.ATHARI ZA MAISHA BINAFSI
Kasi,namba na uwezo wa mbegu hizi kurutubisha yai hutegemea tabia ya mhusika.Pombe,madawa ya kulevya,sigara,vyakula,miale mikali ya mwanga kama laptops na wifi huleta madhara kwa mbegu hizi
-
8.MUDA WA KUKOMAA
Japo kila siku mwanaume hutengeneza mbegu za kiume,huzichukua walau miezi miwili na nusu mbegu hizi ili ziweze kukomaa vizuri.Hii inatoa maana kuwa,mbegu zilizo na uwezo wa kurutubisha yai ambazo mwanamme hutoa anapofika kileleni huwa zimetengenezwa miezi mitatu iliyopita.Zile ambazo hazijafikia umri huu huendelea kukomazwa hadi pale zitakapokuwa tayari.
Maoni ,tiba na ushauri tupigie au tuma sms 0678367707

Comments