CHANZO CHA UKAVU UKENI



Nini kinasababisha ukavu ukeni? Uke umeumbwa kwa mashavu yenye kuta zenye tishu laini sana. Na kufunikwa na majimaji yenye utelezi ili kusaidia mbegu za kiume kuogelea vizuri na kurutubisha yai wakati wa tendo la ndoa.

Uteute huu pia ni kilainishi cha uke kupunguza msuguano wakati wa tendo la ndoa.

Kadiri mwanamke anavozeeka mabadiliko ya uzalishaji wa vichocheo ama homoni vinapelekea kuta za uke kusinyaa na kuwa dhaifu. Kuta zikisinyaa maana yake seli zinazozalisha uteute zinapungua na hivo kupelekea ukavu ukeni.

Mabadiliko ya homoni ndio sababu kubwa inayokufanya uwe na uke mkavu


Nini Madhara ya Ukavu Ukeni?


~ Kukauka kwa uke wako kunaweza kusababisha madhara kama

~ kuhisi hali ya kuungua ndani ya uke

~kukosa hamu ya tendo la ndoa

~ Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

~ kutokwa damu baada ya tendo kutokana na msuguano

- kuugua UTI kurahisi na kuwa sugu

- muwasho ukeni na

-kuvimba kuta za uke.


Nini Kinapelekea Ukavu ukeni?

Kupungua kwa homoni ya estrogen ndipo chanzo kikubwa cha ukavu ukeni. Wanawake wote hupungua uzalishaji wa estrogen kadiri wanavozeeka na kukaribia kukoma hedhi yaani menopause.

Menopause siyo chanzo pekee kwani kuna vitu vingine vinavyopelekea uwe na uke mkavu. Mambo mengine yanayopunguza uzalishaji wa estrogen ni pamoja na


> kunyonyesha

> kuvuta sigara

> kuzaa

> upasuaji kuondoa mifuko ya mayai(ovary)

> stress kupita kiasi

> mazozi makali sana

> sonona

magonjwa ya kinga na

baadhi ya tiba kama chemotherapy na radiotherapy


Lini Unatakiwa Kumwona Daktari?

Ni mara chache sana ukavu wa uke iwe ni kiashiria cha tatizo kubwa la kiafya. Muhimu ni kutafuta ufumbuzi wa daktari endapo tatizo lako limechukua muda mrefu . Endapo usipotibia mapema ukavu wa uke unaweza kusababisha kumeguka kwa kuta za uke.


Matibabu ya Tatizo la Ukavu Ukeni

Kuna aina nyingi za tiba ambazo waweza kuzipata famasi ya karibu yako ili kulainisha uke. Tiba hizi zinakuwa kwenye mfumo wa jelly mfano KY jelly ni maarufu sana.

Hakikisha unatumia vilainishi vya maji siyo vya mafuta. Vilainihsi hivi visiwe na manukato wala kemikali hatarishi.

Kamwe usitumie mate kama kilainishi wakati wa tendo la ndoa kwani unaweza kupata maambukizi ya bakteria. Usitumie mafuta ya kujipaka kama kilainishi kwani utaharibu kuta za uke.


Nawezaje Kuzuia tatizo hili kujitokeza mara kwa mara

kunywa maji ya kutosha kila siku

usitumie sabuni wa marashi ukeni

ongea na mwenzi wako kuhusu tatizo ili akuvumilie wakati unatafuta tiba.


Kupata tiba kamili wasiliana nasi kwa simu 0678367707

Comments