Mafuta ya lavender au mrujuani ni moja ya mafuta yanayotumika zaidi kwenye kundi la (essential oil) lakini faida zake ziligunduliwa kwa zaidi ya miaka 2500 iliyopita. Kutokana na uwezo mkubwa kama kiondoa sumu na kupambana na bakteria mafuta haya ya lavenda yamewea kutumika kwa afya ya ngozi na pia kama tiba kwa karne nyingi sasa.
Hapo zamani wamisri walitumia mafuta ya lavender kama pafyum na pia kuhifadhia maiti zisiharibike (mummification), ambapo inasemekana kwamba harufu ya mafuta ya lavender iligundulika kuendelea kuwepo kwenye kaburi la farao kwa zaidi ya miaka elfu 3 tangu kufariki kwake.
Kwa upande mwingine warumi walitumia mafuta ya lavenda kwa ajili ya marashi ya kuogea, kupikia na kusafisha hewa. Kwenye biblia pia mafuta ya lavender inafahamika kwamba yalitumika kwenye kutibu na kutakasa. Kwa siku za hivi karibuni mafuta ya lavender yamekuwa yakitumika kwenye njia hizi.
• Kupunguza msongo wa mawazo (pasipo kumeza vidonge)
• Kulinda mwili dhidi dalili mbaya za kisukari
• Kuimarisha uwezo wa ubongo
• Kuimarisha usingizi
• Kurudisha ngozi nyororo na kuondoa chunusi
• Kupunguza kasi ya uzee na
• Kupunguza maumivu
Kutokana na faida nyingi zilizopo kwenye mafuta ya lavender, nashauri ununue uwe nayo nyumbani muda wote. Utafiti tayari umeshagundua uzuri wa mmea huu wa lavender.
Zifatazo ni Faida 7 za Kutumia Mafuta ya Lavender (mrujuani)
1.Kutibu Majeraha ya Moto na ya Kukatwa.
Kutokana na uwezo wake wa kudhibiti ukuaji wa bakteria, mafuta la lavender yamekuwa yakitumika kuzuia maambuzi ya vimelea n magonjwa mbalimbali. Tafiti zinaonesha kwamba majeraha ya moto na kukatwa na kitu chenye ncha kali hupona haraka zaidi endapo utapaka mafuta ya lavenda.
2.Kuimarisha Afya ya Ngozi na Ukuaji wa Nywele.
Matumizi ya mafuta ya lavenda kwa kupakaa kwenye ngozi huzuia chunusi na matatizo mengine ya ngozi kama madoa, na pia kupunguza kasi ya kuzeeka kwa ngozi.
3.Kupunguza Maumivu ya Kichwa.
Kama wewe ni mmoja ya mamilioni ya watu wanaoteseka na maumivu ya kichwa kila siku, mafuta ya lavender yanaweza kuwa mwarobaini wako. Ni moja ya mafuta mazuri kutibu maumivu ya kichwa.
4.Mafuta ya lavender yanaimarisha Usingizi mnono.
Mafuta ya lavender ukilinganisha na dawa za kuleta usingizi haina madhara ya kiafya. itaimarisha utimamu wa mwili kwa ujumla.
5.Kutibu dalili za kisukari.
Mwaka 2014 watafiti nchini tunisia waligundua kwamba mafuta ya lavender yanawaweza kupunguza dalili zifuatazo za mgonjwa wa kisukari
Kupanda kwa sukari kwenye damu
Kuongezeka kwa uzito
Kupungua kwa uwezo wa figo na ini
kwa wagonjwa wa kisukari pakaa mafuta ya lavender kwenye shingo na kwenye kifua. Pia vuta hewa yake
6.Kupunguza maumivu ya mwili.
Tafiti mbalimbali zimegundua kwamba mafuta ya lavender husadia kutibu maumivu ya mwili kama ikitumia ipasavyo. Tunaweza kuiita hii ni natural painkiller. Chukua mafuta yako kisha tumia kitambaa laini au pamba kusugua mahali penye maumivu.
7.Kuimarisha mood yako na Kupunguza Msongo wa Mawazo.
Kwa miaka ya hivi karibuni mafuta ya lavender yamekuwa ni kitu adimu na cha kuaminika zaidi kutokana na uwezo wake kukukinga dhidi ya matatizo ya neva.
Usimeze tena vidonge vya famasi kuleta usingizi ama kuondoa msongo wa mawazo maana vina madhara makubwa, tumia mafuta haya halisi.
Kupata mafuta haya wasiliana nasi 0678367707. Utapata popote ulipo huduma yetu karibuni sana
Comments
Post a Comment