HOMA YA INI/HEPATITIS 🕳

 



🕳Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo vikishaingia mwilini hushambulia ini kabla ya kugeuka maradhi sugu.


~ Virusi hivyo vinaitwa *Hepatitis Virus* (Vipo vya aina nne yani Hepatitis A, B, C na D) .ila B na C Ndiyo hatari Zaidi.


🕳Virusi hivyo husambazwa kwa njia ya damu au majimaji mengine ya mwilini, mfano mate au jasho. 


~ Watu takriban 1,000,000 wanapoteza maisha duniani kote kutokana na Ugonjwa wa Homa ya Ini ( *Hepatitis* ).


🕳 Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye Kifo.


🕳Katika maeneo hatari zaidi duniani, Virusi vya *Hepatitis B* (HBV) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususan nyakati za utotoni.


🕳Kama ilivyo kwa Ukimwi, Virusi vya *Homa ya Ini* pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damChanjo. *Njia kuu za maambukizi* :-


-Kujamiana bila kinga

-Kunyonyana ndimi 'denda'

-Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua.

-Kuchangia damu isiyo salama

-Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k

-Kuchangia miswaki

-kuchangia taulo na mwenye ugonjwa huo.

-kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.


🕳Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa virusi hivyo ni hatari kuliko hata vya Ukimwi kwa sababu vinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu ( *Yaani nje ya mfumo wa damu* ) kwa siku saba. 


~ Virusi vya Ukimwi (VVU) havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.


🕳Kutokana na usugu wa HBV, maana yake ni kwamba kama kirusi kipo kwenye ngozi, kitaendelea kuwa hai kwa siku saba na katika kipindi hicho mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya damu au jasho.


🕳Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia mwilini, hupevuka ndani ya siku 75, hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya siku 30 hadi 180. Ndani ya siku 30 mpaka 60, mtu mwenye HBV anaweza kugundulika ikiwa atapimwa.


🕳Mtu mwenye *Homa ya Ini* ana wastani mdogo wa kuishi kuliko mwenye Ukimwi. Kwa maana hiyo, mwenye maambukizi ya Virusi vya Homa ya Ini hufariki dunia haraka kuliko mwenye VVU.


🕳Dalili za Ugonjwa wa HOMA YA INI na Jinsi Unavyoambukizwa ( *Ugonjwa huu ni hatari kuliko UKIMWI* ).


🕳Watu wengi hawaonyeshi dalili yoyote. Kwa maana hiyo mtu anaweza kuishi na HBV na kusababisha maambukizi kwa wengine bila kugundulika.


🕳Hata hivyo, watu wengine husumbuliwa na homa kali na dalili ambazo hudumu kwa wiki kadhaa. Dalili hizo ni:


-Uchovu.

-Kichefu,chefu.

-Mwili kuwa dhaifu.

-Homa kali.

-Kupoteza hamu ya kula.

-Kupungua Uzito.

-Maumivu makali ya tumbo upande wa Sehemu ini lilipo.

-Macho na ngozi kuwa vya njano kupita kiasi.

-Mkojo mweusi.


🕳Kwa wagonjwa wengine, Virusi vya Hepatitis B hukua hadi kusababisha ini kuharibika kabisa ( *cirrhosis of the liver* ) au saratani ya ini ( *liver cancer* ).


• Ili Kuepuka Maambukizi Ya Ugonjwa huu wa *Homa Ya Ini* / *Hepatitis* Unaweza Kuchukua tahadhali Zifuatazo :-


- Pata Chanjo

- Tumia kinga wakati wa kujamiana.

- acha kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k

- Epuka Kuchangia miswaki

- Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu.

- Usishiriki Kuchangia damu isiyo salama.


🕳Asilimia 80-90 ya watoto wachanga ambao huambukizwa katika kipindi cha mwaka wa kwanza tangu kuzaliwa, Homa ya Ini hukua mpaka kufikia kuwa sugu na hatimaye kifo.


🕳Asilimia 30-50 ambao huambukizwa kabla ya kufikisha umri wa miaka sita, Hepatitis B hukua mpaka kuwa sugu na baadaye ni kifo.


🕳Asilimia 90 ya watu wazima wanaopata HBV, virusi hivyo hutoweka ndani ya miezi sita. Yaani uimara wa ini husababisha virusi hivyo kupotea.


🕳Asilimia tano kushuka chini ya watu wazima wanaopata maambukizi ya HBV, virusi hivyo vya Hepatitis B kugeuka sugu na hatimaye kifo.


🕳Asilimia 15-25 ya watu wazima ambao walipata maambukizi utotoni na hatimaye Hepatitis B kuwa sugu, hufariki dunia kutokana na matokeo ya ini kuharibika kabisa au kwa saratani ya ini.


🕳Homa Ya Ini Ikipatiwa Matibabu Sahihi Ya Mapema Kabla Ya Ini Kuharibika Sana Inatibika 90%.


° Kwa Msaada Zaidi na Haraka Wa Matibabu Ya Magonjwa Mbali Mbali Kwa Njia za Kisasa Zaidi ~ Tafadhali : Wasiliana Nasi Kupitia Simu namba Call/WhatsApp: 0678 36 77 07

(..Share Kwa Kujali,Wengine Wapate Elimu

Comments