Madhara ya Kula Nyama ya Nguruwe (Kitimoto)

 

NGURUWE ni mnyama anayeliwa kwa asilimia 38 ya watu wote duniani, lakini nyama yake ina madhara makubwa kuliko faida.  Leo tutaangalia kuhusu madhara yake japokuwa kuna faida chache ambazo tutaziandika pia.


HASARA YA KULA NYAMA YA NGURUWE

Kuna hasara za kitaalamu za kula nyama hii. Kwanza watumiaji wanapaswa kujua kuwa nyama ya nguruwe ina sumu ya carcin-ogen ambayo inasababisha kansa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO) na The International Agency for Research on Cancer.

 

Utafiti huo ukaonesha kuwa ukila kila siku gramu 50 ya nyama ya nguruwe, basi uwezekano wa wewe kupata kansa unaongezeka kwa asilimia 18.

 

Nyama ya nguruwe inasababisha Swine Flu kwa binadamu; hivi ni virusi vinavyosababisha mafua kwa binadamu. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Centers for Disease Control and Prevention inaonesha influenza virus H1N1 na H3N2 wanatoka kwenye nyama ya nguruwe.

 

Imeripotiwa kuwa virusi hivyo viliwahi kusababisha maradhi ya mlipuko wa ugonjwa huo nchini Marekani. Nyama ya nguruwe pia ina minyoo wajulikanao kwa jina la trichinella worm, ambao hawa ni vigumu sana kuweza kufa kwa nyuzi joto hata la 100C.

 

Utafiti uliofanyika 1998 na WHO ulionesha kuwa nyama ya nguruwe iliyopikwa kwa nyuzi joto la 104C, asilimia 52.37 na trichinella worm wanabaki kuwa hai. Minyoo hao wakiingia katika mwili wa binadamu, husababisha ugonjwa ujulikanao kwa jina la trichinosis; ambao huwa na dalili kama ifuatavyo:

 

Homa kali sana, kichwa kuuma, kukosa nguvu, maumivu ya nyama za mwili, macho kuwa rangi ya pink (conjunctivitis), kuvimba uso na kope, kudhuriwa na mwanga. Madhara mengine ya nyama ya nguruwe ni kwamba ina virus aina ya Hepatitis E virus (HEV); ambavyo husababisha homa ya ini aina E.

 

Wadudu wengine waliomo kwenye nyama ya nguruwe ni; Nipah virus, Menangle virus, Viruses katika kundi Paramyxoviridae wadudu wote hao huwa wanaleta madhara kwa mwili wa binadamu. Mbaya zaidi ni kwamba nyama ya nguruwe husababisha maradhi ambayo yana ukinzani (resistance) na dawa za kuua bakteria (Anti bayotiki).

 

Nyama ya nguruwe pia ina minyoo aina ya Taenia solium. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), wanasema; minyoo hii unaweza kuipata ikiwa hautapika vizuri nyama hiyo ya nguruwe iliyoathirika (infected).

 

Minyoo hii ikiingia katika mwili wa binadamu husababisha matatizo ya mfumo wa fahamu (central nervous system), kitaalamu neurocysticercosis na husababisha kifafa. Asilimia 30 ya wagonjwa wenye kifafa huwa ni wale ambao hushambuliwa na minyoo hii ipatikanayo kwenye nyama ya nguruwe isiyoivishwa itakiwavyo.

 

Imethibitika kuwa watu milioni 50 duniani wanaopata kifafa, huwa ni walaji wazuri wa nyama ya nguruwe, ama kwa kula nyama yenyewe au kwa kula soseji za nyama hiyo. Hata hivyo, kuna faida ya kula nyama ya nguruwe japokuwa hazishindi hasara za kutumia nyama hiyo.

 

Faida yake ni kwamba hupatikana vitamini muhimu katika mwili wa binadamu; ambavyo ni B1, B6 and B12. Walaji hupata madini ya chuma, ambayo husaidia kuimarisha mifupa pia nyama ya nguruwe inaimarisha ngozi yako na kuifanya iwe laini.

 

Nyama ya nguruwe ina magnesium kwa wingi ambayo ina faida katika mwili wa binadamu kwani ina protini ya kutosha, ambayo husaidia ulinzi wa mwili. Nyama ya nguruwe pia ina mafuta ambayo hufanya mwili kupata nguvu.

 

Lakini ukweli ni kwamba hata wanyama wengine kama vile nyama ya ng’ombe, mbuzi, kondoo, nyama zao zina virutubisho hivyo. Swali langu kwako wewe msomaji wa nakala haya; nani anayepika nyama huku akipima joto limefika ngapi?

 

Tahadhari, sana ulaji wa nyama ya nguruwe kwa sababu madhara yake ni makubwa kuliko faida yake! Kwa maswali na ushauri, wasiliana nami kwa simu hizo hapo juu

Comments